Pages

Sunday, April 21, 2019

AISIIIII……….U KILL ME 06........ ONLY 18+

ILIPOISHIA
Nikapiga saluti na kugeuka, nikafika mlangoni na kukishika kitasa cha mlango huku dukuduku la kuhitaji kuzungumza kitu likiwa linanisumbua moyoni mwangu.
‘Potelea pote’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikigeuka na kumtazama K2 aliye nigeuzi mgongo wake akieleka kukaa kwenye kiti chake.
“Sikiliza, kuanzi leo. Nijue kama mfanyakazi wako na si mwanaume utakaye iona mbo** yangu ikiingia kwenye kum** yako. Jana ndio ilikuwa mwanzo na ndio itakuwa mwisho”
K2 akageuka na kustuka kusikia maneno hayo niliyo yazungumza, nikafungua mlango na kutoka kwa hasira, iliyo yafanya machozi yangu kutiririka hadi secretary akanishangaa.

ENDELEA
Nikajifuta machozi nikiwa kwenye kordo ya kuelekea kweye ofisi yatu. Nikaingia ndani ya ofisi wala sikumsalimi mfanyakazi yoyote jambo ambalo si kawaida kwa maana watu wamenizoea kwa ucheshi wangu kwa kila mmoja.
“K2 kasha fanya yake”
Rafiki yangu mmoja alizungumza huku akinitizama hadi nina kaa kwenye kiti changu. Kwa jinsi ninavyo jijua nikiwa na hasira macho yangu yanavyo kuwa nikaamini kila mmoja anauona wekundu wa macho yangu. Nikafumba macho huku nikiziba masikio, nikijaribu kushusha pumzi taratibu, ikiwa ni njia moja kupunguza hasira.
“Mambo vipi jamani”
Nilizungumza huku nikitabasamu na kuwafanya watu wote kuangua kicheko. Kila mmoja akaitikia alipo maliza kucheka.
“Munacheka nini sasa?”
“Ahaaa najua K2 kasha fanya yake”
“Ahaaa hakuna kitu kama hicho”
“Kwenda huko. Dany sikuwahi kukuona ukiwa na hasira ila leo nimekuona”
“Nilikuwa naigiza”
“Hahaaaaa, bongo movie umeileta humu ndani?”
“Si unajua siku moja moja kucheka inabidi nipaweke pembeni. Ehee niambie huyo bi mkora katoa kazi gani?”
“Kaka umepewa kazi ya kwenda kukusanya habari shirika la nyumba”
“Kuna nini tena”
Jumbe akaniletea faili na kuniwekea mezani. Nikalifungua na kuanza kupitia ukurasa mmoja hadi mwengine. Kazi iliyo kubwa ni kwenda kufwatilia mapato ya ujenzi wa nyumba zinazo jengwa Kigamboni, na inaonyesha kuna ubadhilifu wa pesa umefanyika. Nikalifunga faili hilo na kuliingiza kwenye droo yangu.
“Jamani baadaye”
“Poa poa Dany”
“Nyinyi hamtoke leo?”
“Ahaa sisi kila mtu ana kazi yake”
“Ahaaa poa poa”
Nikaelekea kwenye lifti, nikaingia na kushuka moja. Nikatoka nje ya jengo, nikatembea hadi barabarani, nikakodi bajaji iliyo nipelekea hadi katika ofisi za shirika la nyumba. Moja kwa moja nikaelekea sehemu ya mapokezi na kumkuta dada mmoja mweupe aliye valia sare nadhifu sana.
“Habari yako dada?”
“Safi, nikusaidie nini?”
“Ahaa naweza kuonana mkurugenzi?”
“Hapana mkurugenzi hayupo”
“Meneja?”
“Yupo kwenye kikao cha bodi”
“Muhasibu je?”
“Naye pia yupo kwenye kikao cha bodi”
“Na kinaisha saa ngapi?”
“Kusema kweli sijafahamu kinaisha saa ngapi kwa manaa wameingia muda si mrefu”
“Basi ngoja niwasubirie hapa”
“Sawa”
Nikakaa kwenye viti vilivyo eneo hilo la mapokezi. Nikaitoa simu yangu mfukoni na kukuta meseji ya K2. Nikaifungua na kukuta ikiwa imeandikwa ujumbe wa kuniomba msamaha kwa kilicho tokea ofisini. Nikajikuta nikiachia msunyo hadi sekretari akanitazama na kutabasamu.
Nikairudisha simu yangu mfukoni nikachukua gazeti lililopo pembeni na kuaza kulisoma, huku nikivuta vuta muda kuwasubiria viongozi hao ambao ninahitaji kuzungumza nao. Hadi inafika saa saba kamili hapakuwa na dalili yoyote ya viongozi hao kumaliza kikao chao.
“Kaka samani ninatoka, ninakwenda lunch”
“Hao viongozi bado wapo kwenye kikao”
“Ndio naona kikao leo kimekuwa kirefu sana”
“Sawa”
Secretary huyo akaondoka, nikabaki nikiwa nina tazama wafanyakazi wanao toka na wengine kuingia. Wazo la kwenda kupata chakula likanijia. Nikatoka nje ya ofisi hizo, nikatembea sehemu hadi kwenye mgahawa uliopo karibu sana na ofisi hizo. Nikakuta wafanyakazi wengi wa shirika hilo wakiwa wamejazana. Nikatazama tazama kila sehemu na kumuona yule secretary akiwa amekaa peke yake kwenye moja ya meza. Nikaenda hadi alipo kaa na kukaa kwenye kiti hicho.
“Umekuja na wewe?”
“Yaa naona njaa kidogo imeniamsha”
“Karibu mimi ndio nipo katikati”
Muhudumu akanifwata kwa ajili ya kunihudumia.
“Muna pronse?”
“Ndio, unahitaji wakavu au walio pikwa rosti?”
“Niletee wakavu pamoja na chipsi kavu”
“Sawa kaka”
“Na niletee juisi ya ukwaju”
Muhudumu akaondoka. Nikamtazama dada huyo jinsi anavyo kula chipsi yai aliyo iagiza, huku pembeni kukiwa na kuku aliye kaangwa vizuri.
“Hivi mgahawa huu chakula wanacho kipika ni kizuri?”
“Sanaa, yaani wafanyakazi karibi wote wa ofisi za hapa karibu tunakimbilia hapa wakati wa kula”
“Wee!!”
“Yaa, wewe ni mgeni kwani?”
“Yaa ni mgeni wa eneo hili”
“Wewe ofisi zako zipo wapi?”
“Ahaa zipo kariakoo”
“Ahaa unafanya kazi gani?”
“Nimfanya biashara wa duka tu. Sema leo nilikuwa na miadi ya kuonana na hao viongozi watatu sema nao wapo kwenye kikao”
Muhudumu akaniletea chakula nilicho muagiza pamoja na juisi. Nikaanza kula huku nikijaribu kumchunguza dada huyo, niliye ona ananifaa kwenye kazi yangu iliyo nileta hapo.
“Unaitwa nani?”
“Mimi?”
“Ndio?”
“Mery”
“Ok mimi ninaitwa Dany”
“Una jina zuri, nina mtoto wa kaka yangu naye anaitwa Dany basi ni mkorofi huyo”
“Hahaa mbona mimi sio mkorofi”
“Mmm sifahamu kwa sababu sijakaa na wewe”
“Sijui ninaweza kuipata namba yako ya simu?”
“Kusema kweli huwa sitoagi namba ya simu kwa mtu ambaye simfahamu?”
“Kwa nini?”
Hata kabala Mery hajajibu, jamaa mmoja mrefu mweusi aliye valia tisheti ya shirika hilo la nyumba akasimama pemeni ya meza yetu na kutuangalia wote wawili hususani Mery.
“Huyu nani?”
“Ni…..ni ni”
Mery alijing’ata ng’ata huku akionyesha dahiri kumuogopa jamaa huyo aliye nikazia macho baada ya kunitazama. Jamaa akachukua glasi yangu ya juisi na kunimwagia kichwani na kuwafanya watu karibia wote walio kuwepo kwenye mgahawa huo kushangaa.
“Mose, una fanya nini sasa?”
Merya akashushwa na kofi zito lililo mfanya arudi kukaa, mara baada ya kunyanyuka kidogo. Nikajikita nikitabsamua huku nikijipangusa uso wangu ulio jaa juisi hiyo ya ukwaju.
“Hivi wewe mseng** unapenda sana kuvamia mademu za watu si ndio?”
Jamaa alizungumza huku akinitazama kwa macho ya hasira. Nikashusha pumzi huku nikijaribu kuizuia hasira yangu.
“Wewe fala si ninakusemesha?”
Jamaa ambaye nilisikia jina lake kwamba anaitwa Mose alinishika tai na kuninyanyua kwa nguvu kwenye kiti nilicho kalia. Watu waliopo karibu na meza yetu wakanyanyuka na kujaribu kumshika huyo jamaa anaye itwa Mose.
“Muheshiwa acha hayo si unajua watu wengi”
“Niacheni nimuonyeshe huyu mjinga anakazi ya kuparamia paramia wanawake wa watu. Hapa mjini”
Mose alizungumza huku akiendelea kunikwida. Sikuzungumza chochote zidi ya kumtazama Mose anacho taka kukifanya. Watu wakafanikiwa kumtoa jamaa huyo mwilni mwangu na kujikuta akiondoka na vifungo vyangu viwili vya shati.
“Na wewe twende”
Mose akamshika mkono Mery na kuondoka naye. Nikawatazama jinsi wanavyo toka kwenye mlango wa mgahawa huo. Nikachukua waleti yangu na kwenye sehemu ya malipo na kumuuliza muhudumu aliye nihudumia.
“Una nidai pesa ngapi?”
“Elfu ishirini na tatu”
“Yule dada niliye kuwa nimekaa naye pale amelipia?”
“Hapana”
“Na yeye munamdai bei gani?”
“Elfu kumi na tisa”
Nikatoa elfu arobaini na tano na kumkabidhi muhudumu huyo. Kila nilipo pita ndani ya mgahawa huo watu walinitazama huku wengine wakionekana kunionea huruma.
“Ila Mose muonevu, yeye kakuta watu wemekaa tu anawakoromea”
“Ila yule siku atakuja kupata kidume mwenzake atampiga hadi afurahi”
“Kinacho upa ujeuri ni huo uhasibu wake”
Wadada wawili walio kuwa wamekaa kwenye meza ya karibu na malngoni nilidaka mazungumzo yao na nikawa nimepata pointi kwamba kumbe mose kumbe ndio muhasibu ambaye ninatakiwa kumfanyia upepelezi. Nikafungua mlango na kutoka moja kwa moja nikarudi katika jengo lao. Nikamkuta Mery akiwa anamwagikwa na machozi huku pembeni akiwepo msichana mwengine akionekana kumfariji.
“Mbona unalia?”
Nilizungumza na kumfanya Mery kunyanyua kichwa chake alicho kuwa amekiinamisha. Akastuka kuniona eneo hilo na kuanza kufuta machozi yake.
“Kaka ni vyema ukaondoka kwa maana Mose akikukuta hapa unaweza kumsababishia matatizo mengine Mery”
“Kwani ofisi ya huyo Mose ipo wapi?”
Dada huyo akataka kunielekeza ila Mery akamuwahi na kumzuia kwa kumshusha mkono wake alio kuwa ameunyanyua kwa kutaka kunielekeza ofisi hiyo ilipo.
“Dany tafadhali nakuomba uo……”
Mery alinyamaza gafla huku macho yakitazama kwenye lifti, nikageuka na kumuona Mose akitoka kwenye lifti hizo, akanitazama kwa macho makali huku akinifwata nilipo simama.
“Wewe mwana haramu umekuja hadi huku si ndio”
Mose alizungumza na kutaka kuniparamia, ila safari hii sikuhitaji kuwa fala tena kwa maana, kitendo cha kunisogelea nimuwasha ngumi sita za kasi zilizo tua katika sura yake na kumfanya ayumbe na kuanguka chini.
Kila mtu aliye kuwa katika eneo hilo akashangaa. Mose akaanza kujizoa zoa na kunyanyuka, akasimama wima japo kwa kuyumba, akajaribu kurusha ngumi ila zote nilizikwepa, nikamtisha kidogo aniachia sura, nikavuta ngumi moja kali kabla haijafika karibu na shingo yake nikauzuia mkono.
“Usirudie tena”
Mose alicho kikosea ni kunitukania mama yangu, hapo sana nikaweka ustaarabu pembeni na kuanza kumtembezea kichapo, hadi walinzi wanao linda eneo hilo wakaja kunikamata. Nikiwa katika kizuizi cha walinzi hao nikashangaa kuona gari ya polisi ikija eneo hilo.
“Mtuhumiwa mwenyewe huyu hapa”
Alizungumza mzee mmoja aliye valia suti ya kaki. Askari hao wakanisogelea wakiwa na bunduki zao.
“Nyoosha mikono, una haki ya kukaa kimya hadi pale utakapo fika kituoni kwa mahojiano”
Sikuwa mbishi, wakanifunga pingu za mikononi na kunipakiza kwenye gari lao na kuondoka eneo hilo.
“Afande ninaomba nimpigie mwanasheria wangu aje kituoni?”
Nilizungumza tukiwa njiani. Askari huyo hakuweza kunijibu chochote zaidi ya kunikata jicho baya. Tukafika kituo cha polisi. Wakanifungua pingu, wakaniamuru kuvua mkanda, viatu, kutoa waleti mfukoni. Nikafanya hivyo kitu lilicho mstusha askari aliye kuwa akinipapasa ni bastola yangu niliyo kuwa nimeichomeka kiunoni.
“Jamani huyu ni jambazi”
Askari huyo aliuzungumza kwa sauti ya juu na kuwafanya askari wengine wote kituoni kunitazama mimi huku wengine walio na bunduki kuninyooshea mimi, huku wakiniamuru kunyoosha mikono juu kwa ukali sana.
ITAENDELEA

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +