ILIPOISHIA
“Afande ninaomba nimpigie mwanasheria wangu aje kituoni?”
Nilizungumza tukiwa njiani. Askari huyo hakuweza kunijibu chochote zaidi ya kunikata jicho baya. Tukafika kituo cha polisi. Wakanifungua pingu, wakaniamuru kuvua mkanda, viatu, kutoa waleti mfukoni. Nikafanya hivyo kitu lilicho mstusha askari aliye kuwa akinipapasa ni bastola yangu niliyo kuwa nimeichomeka kiunoni.
“Jamani huyu ni jambazi”
Askari huyo aliuzungumza kwa sauti ya juu na kuwafanya askari wengine wote kituoni kunitazama mimi huku wengine walio na bunduki kuninyooshea mimi, huku wakiniamuru kunyoosha mikono juu kwa ukali sana.
ENDELEA
Nikafwata kama wanavyo hitaji, nikainyoosha mikono yangu juu huku nikimtazama askari aliye nichomoa bastola yangu.
“Piga magoti wewe mjinga”
Askari mwengine alisisitiza kwa sauti ya ukali, taratibu nikapiga magoti. Askari huyo akachuka waleti yangu na kuifungua, akaanza kuikagua vitambulisho vyangu. Nikamuona akistuka baada ya kutoa kitambulisho changu cha kazi. Akanitazama mara mbili mbili huku macho yakimtoka na jasho likimwagika.
“Kuna nini kinacho endelea hapa”
Nilisikia sauti ya kike, nyuma yangu. Ikanibidi kugeuka na kumkuta mkuu wa polisi ambaye ninamtambua ni rafiki wakaribu sana na K2 na mara nyingi niliweza kumuona akija ofisini kwetu.
“Mkuu kuna huyu kijana alifanya fujo, ndio tumemleta hapa kituoni”
Mwanamama huyo mrefu kwenda juu, aliye valia suruali ya kaki pamoja na shati la kaki, lenye nyota kadhaa kwenye bega lake, akazunguka na kuja kusimama mbele yangu.
“Mumegundua nini?”
Alimuuliza askari aliye shika kitambulisho changu. Askari huyo akaonekana kupata kigugumizi na kujikuta mkuu wake akikichukua kitambulisho hicho na kukikoma. Akanitazama kwa haraka kisha akayarudisha macho yake kwenye kitambulisho hicho.
“Nani aliwapa oda ya kwenda kumkamata?”
Askari wote wakaka kimya. Kila mmoja alimtazama mwenzake, mwanamama huyo kwa ishara akaniomba ninyanyuke juu. Nikannyanyuka na kuwafanya askari wote kuduwaa.
“Mrudishieni kila kitu chake, unatoa toa macho ya nini?”
Askari aliye chukua waleti na bastola yangu, akanirudishia huku mwili mzima ukimtemeka. Sikulijali juu ya woga nikachukua kila kitu changu, nikavaa mkanda pamoja na viatu vyangu.
“Samahani kijana, naomba tukayazungumze ofisini kwangu”
Mwana mama huyo alizungumza huku akinitazama. Nilipo maliza kufunga kamba za viatu vyangu, nikaongozana naye hadi kwenye ofisi yake iliyopo gorofani. Akanikaribisha kwenye kiti kilichopo mbele ya meza yake kisha yeye akaka kwenye kiti kilichopo nyuma ya meza yake hiyo yenye mafaili mengi pamoja na meza ya mezani na simu ya upepo.
“Samahani kwa usumbufu wa vijana wangu, naona walikuchukua pasipo kujua kwamba wewe ni nani”
“Kwa hilo halina tabu, ni vyema nikaondoka na kwenda kuripoti kazini kwangu kwamba kazi yangu iliziwa na vijana wako”
“Hapana hapana, wachukulie ni vijana wezako wale. Endapo wataingia kwenye tabu wengine ndio kwanza hata pesa ya serikali hawajaitafuna”
“Kwa hiyo na mimi nikafukuzwe kazi kwa ajili ya vijana wako, unatambua kabisa kazi yangu ilivyo na uhatari wa hali ya juu, ila bado vijana wako wakaamu kuniharibia ndio nini sasa”
Nilizungumza kwa kumkoromea mama huyo baada ya kugundua amingiwa na hofu kidogo.
“Basi ngoja niweza kuzungumza na bosi wako, ili kukukingia kifua, si unajua tena sote sisi ni watumishi wa uma na kazi yetu ni moja”
Mama huyo alizungumza huku akichomoa simu yake aina ya Samsung Galaxy note 3. Akaminya minya baadhi ya namba ambazo sikuziona na kuiweka simu yake sikioni huku akinitazama usoni.
“Shosti vipi?”
“Safi vipi”
Kutokana na simu hiyo kuwa na sauti kubwa kidogo niliweza kuisikia sauti ya K2, nikatamani kumpokonya simu mama huyo ila nikajikuta nikishindwa na kubaki nikiwa nimemkazia macho.
“Safi tu, bwana nina ombi moja”
‘Ombi gani?’
“Kuna kijana wako hapa alikamatwa na vijana wangu akiwa kwenye kazi yake wakidai alifanya vurugu kwenye moja ya ofisi sasa nikaona nikujulishe mapema isije akaja huko ukawajibisha”
‘Anaitwa nani?’
“Anaitwa Daniel Thamson Kajenge”
‘Mmmmm’
“Mbona unaguna sasa?”
‘Hapana, upo naye hapo au amesha ondoka?’
“Nipo naye hapa ofisini kwangu”
‘Hembu mpatie simu’
Mama huyo akanipatia simu yake, taratibu nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Hallo”
“Hivi Dany unachanganyikiwa siku hizi?”
K2 alizungumza kwa ukali na kunifanya nimtazama mama huyo kwa jicho la kuiba nikagundua anayafwatila mazungumzo yangu kwa umakini.
“Hapana mkuu”
“Ni kitu gani kilicho kupeleka huko kituani. Mbona uinafanya kazi zako kipuuzi kama sio professional aliye fuzu mafunzo eheee?”
“Hapana mkuu haito jitokeza tena”
“Au unahisi kukupa kum* yangu ndio kunakufanya uwe unakuwa mbovu kwenye kazi, mbona hapo nyuma ulkuwa unafanya kazi zako kwa umakini eheee?”
K2 alizidi kunifokea hadi mama huyo nikaamini anayasikia mazungumzo hayo. Nikaka kimya kwani sikujua cha kumjibu K2 ambaye tangu asubuhi alisha nivuruga.
“Sasa hiyo ripoti hadi inafika kesho saa moja asubuhi ninaihitaji ofisini kwangu. Sasa wewe kaa kaa na kuwaza kum* na mkund* wangu uone mwisho wake utakuwa ni nini. Utavuna upuuzi wako huo”
Simu ikakatwa, nikaishusha taratibu sikioni mwangu na kumkabidhi mwana mama huyo aliye baki akiwa amenikodolea macho.
“Hivi nilicho kisikia ni kweli au……?”
Mwana mama huyo alizungumza huku akiendelea kunikodolea macho yake. Sikuwa na kitu cha kumjibu zaidi ya kukaa kimya.
“Nakuomba niondoke tafadhali”
“Sawa unaweza kwenda”
Nikanyanyuka na kumuacha mwana mama huyo akinisindikiza kwa macho hadi natoka ofisini mwake. Nikashuka kwenye ngazi na kukutana na askari aliye kuwa akisoma kitambulisho changu cha kazi. Sikumsemesha kitu zaidi ya kumpita. Nikapita mapokezi kila askari akabaki akiwa amenikodolea macho. Moja kwa moja nikatoka kituoni. Kusema kweli akili yangu haikuwaza chohote zaidi ya kurudi nyumbani kwangu.
“Bosi nikupeleke wapi?”
Dereva mmoja wa pikipiki alisimama pembeni yangu huku akinitazama. Taratibu nikajikuta nikipanda pikipiki hiyo.
“Nipeleke Sinza kwa Remy”
“Sawa mkuu”
Dereva huyo mwenye pikipiki aina ya boksa akaanza safari. Hadi tunafika maeneo ya Sinza ndipo nikaanza kumuelekeza hadi mtaa ninao kaa. Nikamlipa kiasi alicho nitajia na kuingia ndani. Nikamkuta Mariam akiwa amekaa kwenye kibaraza anasikiliza miziki kwenye simu yake. Nikampita bila samu, na kwa jinsi shati lango lilivyo katika vifungo nahisi aliweza kujiuliza maswali.
Niakatiza kwenye kordo na kukutana na Asma akiwa anatoka kuoga, huku amejifunga tenga moja tu.
“Dany mambo?”
Asma alinisalimia huku akiwa na tabasamu pana usoni mkwa.
“Poa za kushinda?”
“Salama”
Sikutaka kukenua kenua meno, nikafika mlangoni mwangu. Nikafungua mlango na kuingia, nikaanza kuvua nguo moja baada ya nyingine hadi nikabakiwa na boksa. Nikawasha feni na kujitupa kitandani, kilia nikiwaza jinsi ya kuifanya kazi niliyo pewa na ofisi nikajiona nimevuruga mpangilio mzima.
“Ohooo Mungu wangu nisaidie”
Nilizungumza huku nikiwa nimetizama juu. Sikuwa na jibu la uhakika wa nini nifanye. Mazingira ya chumba changu nilivyo yaacha asubuhi kwa muda huu hayaniridhishi kabisa. Nikaanza kuifanya usafi wa kubadilisha mashuka na kuweka shuka jengine, nilipo maliza hapo nikahamia kwenye kufagi na kufuta futa vumbi kwenye meza ya Tv pamoja na redio yangu. Sikuishia hapo nikavaa pensi na tisheti nikatoka nje nikiwa na ndoo ndogo nikinga maji nusu na kurudi nayo chumbani kwangu na kuanza kudeki kila sehemu.
Nikamaliza kufanya usafi wangu huo, nikachukua nguo zangu zote chafu na kutoka nazo nje, nikiwa nimeziweka kwenye dishi langu. Nikaanza kufua, nikiwa ninaendelea kufua Asma akatoka akiwa amevalia suruali iliyo mbana makalio yake makubwa.
“Nakuona leo umeamua kuwa dobi”
“Yaa kidogo dogo si unajua maisha ya ubachela”
“Kweli ila unabidi ufanya uoe Dany, kazi ndogo ndogo kama hizo za kufua zitakuondokea”
“Ni kweli ila bado nipo nipo kwanza si unajua wanawake wa sanana ni pasua vichwa na wengine hatupendi mambo hayo ya kuumizwa kichwa”
Asma akachukua kidoga kilichopo eno hilo la uwani ambapo kuna jiko la wamama kupikia. Akakaa pembeni ya tanki kubwa la maji lililopo hapa nyumani kwetu.
“Ni kweli, lakini kwa sasa hata wanaume munapasua vichwa. Wanake wanawapenda ila hampendeki sijui kwa nini?”
“Sio wote. Hivi jana ilikuwaje kwa jamaa kwa maana ninaona alitaka kukua?”
“Yaani Dany kaka yangu mimi nimesha jichokea. Mwanaume hapendeki, mwanaume ana wivu nashindwa hata nimfananishe na kitu gani. Yaani unavyo niona hapa hata kwenda kwa majirani hataki. Kila kitu amenunua na kuweka ndani, ni mimi na Tv na Tv na mimi, nikichoke ni kulala tu”
“Kwa nini auakuwa hivyo, hakuamini au?”
“Kigezo chake kwamba mimi ni mzuri kwa hiyo nikitoka nje watu wataniiba”
“Hahaaa sasa jana ilikuwaje hadi akakupiga?”
“Jana unajua kisa cha kupigwa ni kwamba. Tulikuwa tunaangalia myereka ya kina Jonh Cena, sasa mimi nikasema John Cena ni mzuri ana kifua kikubwa, basi hapo ndipo ugomvi ukaanza. Akaanza kuseme ohooo sijui umalaya umezidi hadi ninawasifia wanaume kwenye Tv ohooo kimepanda kimeshuka. Sasa nikawa ninamjibu mwenzangu kama ninamtania kumbe akachukulia serious, ndio akaanza kunipiga na kutaka kunichoma na kisu”
Mazungumza ya Asma yakanifanya nicheke na kujikuta hata mawazo ya kazini kwangu yakikaa pembeni kwa maana kwatika maisha yangu sikuwahi kuona wivu wa namna hiyo.
“Yupo wapi sasa mume wako?”
“Kasafiri kaenda Arusha, kapeleka mzigo wa mafuta”
“Mzigo wa mafuta?”
“Ndio mume wangu ni dereva wa magari makubwa yale ya mafuta, siku nyingine hupeleka mafuta Rwanda, Burudi, Congo”
“Ahaaa, sasa jana ulivyo rudi chumbani hakukoroma?”
“Wee ana ubavu, akikoroma tu namwambia ninakuja kukugongea basi anakaa kimya”
Nikamaliza kusuuza nguo zangu, Asma akaniomba kunisaidia kwenda kuzianika. Sikuwa na hiyana nikamuachia kindoo nilicho jaza nguo hizo na mimi nikamalizia kuyafua mashuka yangu.
“Asante mwaya”
“Usijali kaka yangu, sasa ngoja mimi niandae chakula cha usiku”
“Nihesabu basi”
“Usijali, ila unakula ndizi nyama wewe”
“Ahaa hapo mbona umenifikisha”
“Basi ngoja niandae chap chap, si unajua muda umesonga”
“Poa”
Asma akaondoka na kuniacha nikiwa ninasuuza mashuka yangu. Nikamaliza shuhuli hiyo na kuzunguka nyuma ya nyumba kwneye kamba za kuanikia nguo, nikaanika mashuka yangu na kurudi sehemu nilipo kuwa ninafulia. Nikamwaga maji ya mapovu chooni na kuanza kuyasuuza mabeseni hayo.
“Nani amemwaga maji ya mapovu chooni?”
Mariam alizungumza huku akinitazama usoni, tambambua analifahamu jibu lake, ila anatafuta mbinu za kuzungumza na mimi. Sikujibu chochote zaidi ya kubeba mabeseni yangu yote na kurudi nayo chumbani kwangu. Nikayaweka chini ya uvungu na kujitupa kwenye sofa.
“K2 mamae ipo siku nitakuonyesha kwamba mimi mtoto wa mbwa”
Nilijikuta nikizungumza mazungumzo hayo huku nikikagua namba zilizo piga kwenye simu yangu kipindi nikiwa nipo nje ninafua, na namba ya K2 ni moja wapo.
‘Huyu ataniletea chakula kweli, au ana nizingua?’
Nilijiuliza swali hilo huku nikiwasha Tv kufwatilia taarifa ya habari ya saa mbili usiku inayo rushwa na kituo cha ITV.
Hadi taarifa ya habari inamalizika saa tatu kasoro Asma hakuleta chakula chochote. Nikataka kunyanyuka kwenye sofa ili nijiandae kwenda kununua chakula ila, mlango wangu ukagongwa.
“Nani?”
“Mimi”
Nikasikia sauti ya Asma, kwa haraka nikanyuka na kwenda kufungua mlango. Nikamkuta akiwa amesimama huku mkononi mwake ameshika ‘hotpot’ kubwa pamoja na sahani isiyo na chakula.
“Karibu ndani, si vyema kupeana chakula mlangoni”
Asma akatabasamu na kuingia ndani. Moja kwa moja akaelekea mezani na kuweka ‘hotpot’ hilo mezani pamoja na sahani hiyo.
“Chumba chako umekipangilia vizuri, unaweza kusema unaishi na mwanamke”
“Unajua usafi mimi nilifundishwa tangu kipindi nipo sekondari ya bodi, kwa hiyo nimekulia kwenye mazingira ya usafi safi hadi hapa nilipo”
“Kweli Dany, kuna waaume ukiingia vyumba vyao utatamani kukimbia kwa manaa vimepangiliwa vibaya kama stoo”
Asma alizungumza huku akipakua chakula hicho, kinacho nukia vizuri hadi nikajikuta utumbo wangu ukitetemeka kwa njaa na hamu ya kula chakula hicho.
“Oooho nimesahau kijiko”
“Usijali kijiko ninavyo”
“Umeviweka wapi?”
Nikamuenyesha kiji trei cha kuwekea vyombo, akachukua kijiko kimoja na kuja kukiweka kwenye sahani ya chakula. Kabla hatujazungumza chochote sote wawili tukaisikia sauti ya Jumaa huko nje.
“Mariam umemuona wapo Asma?”
Nikamuona Asma akihisi kuishiwa nguvu, kutoka chumbani kwangu akwa anatamani kutoka ila anashindwa atatoka vipi kwa maana chumba change ndio cha kwanza kabisa kwa upande wa uwani isitoshe endpo atatoka na kukutana na mume wake basi inaweza kuzuka kesi nyingine ya kufikiriana vibaya.
ITAENDELEA
HADITHI HII NI MAHUSUSI KWA WANA MAHUSIANO NA WATU WENYE UMRI JUU YA MIAKA KUMI NA NANE
Sunday, April 21, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments