Mojawapo ya kazi ngumu sana kwa mwanaume yoyote aliye kamilika ni kumtokea au kumtongoza msichana hadharani.Unakuwa unajaribu kumfanya mtu ambaye humjui sio tu kwamba akuone bali mfahamiane kwa undani zaidi.Unkuwa unakuwa na uoga wa kukataliwa lakini unajitahidikujikaza kwa ajili ya tukio hilo.Basi zifuatazo ni hatua ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kupata namba kirahisi kabisa.Basi nakuomba usome hizo hapo chini hatua kwa hatua bila hata kuacha hatua moja.
1.Mfanye msichana atambue uwepo wako:
Kama unataka kumtokea msichana kwenye watu wengi sana ,unatakiwa kuhakikisha kuwa msichana atakumbue uwepo wapo kwanza hata kama kuna watu wengi sana usiogope wala kuona aibu katika hatua hii.Mpe nafasi ya kutambua uwepo wapo.Unaweza kufanya hivi kwa kukamata macho yake,kwa maana ya kumwangalia,au kufanya kitu ambacho kitaweza kushika umakiniwake mfano unaweza kumpa ofa ya kumnunulia kituchochote mfano kinywaji baridi.Usiamke na kuanza kuomba namba ya simu hapo hapo moto unaweza kutokea,
2.Anza kwa kumsifia:
Njia nzuri ya kukamata hisia za msichana yoyote Yule ni kwa kumsifia kwanza .Msifie kwa sifa ambazo anazo na wala usimpake mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kumpa sifa zile ambazo hana,unawea kumwambia”umependeza” linaweza kuonekana kama neon la lawaida sana lakini lina maana kubwa sana kwa msichana yoyote Yule anavyoambiwa ivo.Unaweza kumpa sifa ambazo wengine wanaweza wasigundue.Saa nzuri,viatu au kitu chochote ambacho yeye anakipenda.
3.Anza kwa kuzungumza mazungumzo ya kawaida na makini sana:
Atakapo kuwa amegundua uwepo wako kwa wakati huo na umekuwa umeshasema kitu flani,ni mda sas wa kuanza mbadilishano wa maneno au mazungumzo ya moja kwa moja..Hakikisha unaepuka mazungumzo ya kisiasa au dini kwani mazungumzo kama haya yanaweza kuamsha hisia za msuguano mkali na kuwasha moto mkali wa mabishano,kitu ambachosio lengo lango la kukutana nae.Chagua topiki kama muziki,utamaduni au mambo yaliyopo kwa wakati huo hakikisha unakuwa mbunifu na hubishani nae hata kidogo,mkubalie kwa kilakitu anachokisema.
4. Hakikisha unakuwa mwanaume mchangamfu:
Kama ukifika hatua ya kumfanya afurahi au acheke,basi mpaka hapo utakuwa na kiatu cha dhahabu.Unachohitaji kukifanya ni kumalizia kwa umakini tu hakikisha unakuwa mchangamfu na mstaarabu kwa mambo yote baina yenu mnapokuwa mnazungumza
5.Mpe nafasi ya kuzungumza:
Watu wanapenda kuzungumza kuhusu mambo yao,kwa hiyo mpe nafasi ya kuzungumza akiwa anaongea hakikisha unamsikiliza kwa makini kasha jenga hoja kwa kumuuliza maswali mbalimbali,kitu kama hiki kitamfanya ahisi kuwa unania naye ya dhati,kwa kuwa umekuwa makini maye,lakini maswali yasizidi sana kama umefika polisi
6. Msifie mafanikio yake:
Anapokuwa akizungumza kuhusu mambo yake,anaweza akakuambia kuwa alisoma wapi au kuhusu kazi yake.Hii ni sehemu muhimu sana ambapo unaweza kusema kitu ambacho kitamfanya ajisikie kuwa na furaha sana kama anasoma kozi flani ngumu au yoyote unaweza ukamwambia kuwa umevutiwa na ubongo wake na malengo yake.Wachu wachache sana wanaambiwa maneno kama haya kuwa wanafanya vizuri.
7. Tafuta sababu nzuri ya kutaka namba yake:
Usikurupuke tu na kuruka,”naweza nikapata namba yako?”Lazima uwe na sababu ya msingi sana,hata kama sababu ya msingi umeificha moyoni subiria na kuwa mvumilivu.Sio kwamba mmezungumza na akacheka hakumaanishai kuwa atataka kuongea na wewe kesho.Kama una jiamini unaweza kumuomba kutoka aout siku nyingine.Kama huna uhakika acha na tafuta sababu nyingine kama ungetaka kujifunza zaidi kuhusu mambo flani,au kujadili nae maswala falani.Point hapa ni kwamba hakikisha huchagui sababu ya kijinga ili uweze kupata namba yake ubunifu mkubwa unahitajika.
8. Endelea na mazungumzo kasha sema kwaheri:
Sio kwa sababu umeshapata namba hakumaanishi kuwa umemaliza kazi yako.Endelea kuongea nae kwa muda zaidi hata kama namba zake unazo muache azungumze kuhusu yeye, hii iagarantee kuwa atapokea simu yako muda mwingine ukimpigia
Saturday, April 27, 2019
HIZI NDIZO MBINU 8 MUHIMU SANA ZA KUMFANYA MSICHANA AKUPE NAMBA YA SIMU,BASI SOMA HAPA KUFAHAMU
Posted by
NeverGoBack
on
8:39 AM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments