Pages

Monday, April 22, 2019

Huyu traffic noma, kweli ulevi mbaya


Trafik mlevi alisimamisha gari Mama akapaki pembeni akaona trafik anakuja akiwa anayumba! Alipofika akasema, "naomba leseni yako."
Mama akasachi mkoba Wake akatoa kioo kidogo cha kujtazama akampatia! Trafik akakiangalia kwa dakika 2
Akasema sasa si ungesema kama wewe ni trafik mwenzangu!
Haya nenda
Ulevi sio mzuri
πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚

-------------------------------------------------------------------------------

Analia kilichompata huyu jamaa baada ya kubadili jinsia yake kichawi


Jamaa alimpa ujauzito mwanafunzi akashtakiwa kumbe yule jamaa ana bibi yake mtaalam wamambo yetu ya Jadi…

Jamaa akaongea na bibi yake amuwekee jinsia ya kike ili akashinde Mahakamani na akitoka arudishiwe mambo yake kama kawaida.

Bibi akampachika jamaa jinsia ya kike alipofika mahakamani kuhojiwa akasema mi sijampa ujauzito kwasababu minina jinsia ya kike pia…!
Kwa kuthibitisha akajifunua nguo, basi jamaa akashinda kesi.

Jamaa akawa anarudi Home, lakini wakati anakaribia kufika akaona watu wengi wamejaa home wanalia akauliza kulikoni akaambiwa "Bibi amefariki"!

Vuta picha hapo…!!!

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚

---------------------------------------------------------------------------------------

Jinsi ya Kubana matumizi X-mass

Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.
πŸŽ€✨Marry Xmas & Happy new year.✨πŸŽ€
πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚

----------------------------------------------------------------------------------------------------------

V.gif Upendo wa kweli ni nini?
*Upendo wa kweli ni nini?*
*πŸ‘‰Upendo wa kweli ni pale mwanaume anapomfumania mwanamke wake na kisha kumwambia baby vaa nguo twende nyumbani*

*Kifo ni nini?*
*πŸ‘‰Kifo ni pale mwanamke anapokubali kwenda nyumbani na mwanaume yule.*

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Jamaa mpenda michepuko kapatikana
…Upo kazini umeacha familia yako nyumbani mara ghafla unapigiwa simu kutazama unakutana na no ngeni na kuamua kuipokea ndipo unakutana na Sauti ya msichana ya kuvutia lakin kabla hajasema shida yake anaamua kukata simu. Unashikwa na hamu ya kujua ni nani. Tamaa ya mchepuko inakujia ghafla na kuamua kuipiga ile no tena kwa mara nyingine inakuwa haipatikani.

Siku hiyo hiyo usiku ukiwa umelala chumba kimoja na mkeo meseji inaingia tena kwenye cm yako kwa ile namba iliyokupigia mchana ikikuomba umpigie kwa mida ule na kusisitiza kuwa ana hamu ya kukufahamu. kila ukimtumia meseji ya kumdanganya upo sehemu mbaya hasikii anakubipu mara nyingi. Uzalendo unakushinda, unamuangalia pembeni mkeo kalala fofofo kajifunika shuka hadi usoni. Unaamua kuondoka kwa kunyata mpaka sebuleni kwenda kuipiga Ile namba kwa lengo la Kumwambia kesho mkutane. Ile unafika sebuleni na kuanza kuipiga ile cm ndipo unakutana na sauti hii:- MUME WANGU ACHA MCHEPUKO, NILIKUWA NAKUPIMA TU RUDI TU CHUMBANI TULALE πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹ Hapo ndo utajua kwann bata hata ale kokoto anaharisha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Nilichokifanya jana baada ya kushuka kwenye basi Ubungo
Jana nateremka kwenye BASI UBUNGO nataka nichukue TEKSI hadi KIMARA naambiwa sh.15,000/=.
Wakati niponatafakari hiyo bei, nikasikia "Moro, Moro,Morogoro sh.6,000/="

Nikaamua nipande niende zangu MOROGORO.
Kwenda na kurudi sh.12,000/=.
Wakati wa kurudi nikamwmbia KONDA aniteremshe KIMARA.

SIPENDAGI UJINGA MIMI NA BEI ZA TEKSI.

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Muda mzuri wa kulipa mahari
Amini Nawaambieni
Hakuna Muda Mzuri wa Kulipa Mahari Kama Mwezi January. Baba Mkwe Anapokea Hata Buku Kumi…. πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜›πŸ˜πŸ˜›πŸ˜
πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Kweli shilingi yaua, Huyu jamaa kapatikana, angalia anachomjibu mke wake,
Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
"Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako na……..

Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia

"Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo".Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,"eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu "Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue".

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Dingi kauzu kuliko wote duniani ndiyo huyu hapa
Mtoto: Baba nitumie pesa ya matumizi huku shuleni hali ni mbaya sana la sivyo najinyonga.
Baba: Huku nyumbani hali ni mbaya kuliko huko shuleni kwahiyo kama unajinyonga utapunguza Bajeti, kopa Kamba dukani kwa Mangi nitalipa nikija kuchukua Maiti yako, Mungu akulaze mahali pema peponi Mwanangu…..
πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Huyu mke ni shida! Angalia anachokisema sasa
Jamaa kwa kuchoshwa na tabia ya mkewe iliyobadilika ghafla akaamua kumpleka kwa Padre ili amuelezee nini tatizo mambo yakawa hivi:

Padre: Mumeo analalamika umebadilika sana siku hizi nini tatizo?
Mke: Baba Padre tatizo ni hali ngumu ya maisha.. sio mimi
Padre:Fafanua..!

Mke:Unakuta asubuhi naenda kazini sina hela na inanibidi nichukue tax, nikifika kazini dereva anauliza unanilipa au tufanyeje? Me nachagua tufanyeje
Padre:tufanyeje ni nini?
Mke:kulala nae

Padre:Ooh endelea..!
Mke:Inafika wakati wa kula Sele akiniletea chakula nae anauliza unanilipa au tufanyeje? Me nachagua tufanyeje
Padre:Mmh aiseee..

Mke:Hata nkienda kwa dokta nae anauliza unanilipa au tufanyeje? Me nachagua tufanyeje
Padre:Duh..!!

Mke:hata wakati wa kurudi home nkichukua tax ni yale yale nachagua tufanyeje. ndo maana nkifika nyumbani sina hamu kabisa..

Padre: Aisee pole sana mwanangu, sasa tumwambie mumeo au tufanyeje??

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Mipango ya mke na mume ya pasaka
Mke: Unampango gani na pasaka hii mmewangu..
Mume: Nitafanya kama yesu..
Mke: Unamaanisha Nini?

Mume: Nitaondoka ijumaa na Kurudi j3..
Mke: Unanishangaza, kama utafanya hivi nami nitafanya kama Maria..
Mume: Unamaanisha Nini?
Mke: Nitapata mimba bila ya kuingingiliwa na wewe mume wangu..
Mume: 😳😳😳

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Huyu Jamaa kaona bora afe kuliko mke wake ajue Siri zake
Jamaa Mmoja Alimwambia Mke Wake Wasiliana Na Kitengo Cha Dharura Hospitali, Niko Taabani Nahisi Kama Ninakufa.
Mke Akamwambia Nipe Namba Yako Ya Siri Nifungue Simu Yako.
Mume AkasemaπŸ‘‰πŸ‘‰ Basi Acha Tu; Kila Nafsi Itaonja Mauti
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo
Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangi… kiberiti kikawaishia… wakamtuma mwenzao akatafute kingine… bangi lilikuwa limemkolea… akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweni…
MSHIKAJI: oyaaa wanangu eeeh… niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe …..
WENZAKE: baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.
πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Mjini shule. Soma hii
*MJINI SHULE*

Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.

Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!

Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsApp…!

_Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang'oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri._

_*Kisha nikaituma ile message*_

Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yake… Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.

*Akatuma message akiniuliza…*

_Hao wanawake unawajuwa, …mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweli…!_

Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaa…!

Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaa…! Akaniandikia message nyingine….

*…Nakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupe… Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuri…!*

Nami nikamjibu…

_Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipo…!_

Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdai…!

Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaa…. Kama sio mie!

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Kilichowakuta boss, mke wake na mfanyakazi wao
Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue.
Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika.
Ilikua ni bahati tu alimvizia na
kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua
anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali.
Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.

Boss: Bakariiii!
Bakari: Naam baba!
Boss: nani anakunywa wine yangu?
Bakari kimyaaaa hajibu kitu!
Boss: Bakariiiii !
Bakari: naam baba!
Boss: nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari kimyaaaaa!

Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.
Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari: baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.

Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.
Bakari:Babaa!
Boss: naam Bakari!
Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?

Boss kimyaaaa!
Bakari: Baba babaa!
Boss:ndio Bakari!
Bakari: Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?

Boss kimyaaaaaaa!
Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!

Mke wa Boss akaingilia kati
Mama: nyie msinitanie kabisa mnasemaje?
Bakari: kweli mama ukiwa jikoni husikii kitu nenda uone

Mama akaenda na Bakari akaanza

Bakari: mamaaaa!
Mama: abeee!
Bakari: hebu niambie hiyo mimba ni ya baba au yangu?
Mama kimya

Bakari: mamaaaa!
Mama: abeeee!
Bakari: hebu niambie ukweli hiyo mimba ni ya baba au yangu??
Mama kimya

Mama akatoka nje: kweli humu jikoni kuna tatizo nilikuwa nasikia jina tu

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Angalia hawa vichaa walichokifanya, Vichaa bwana, ni noma!
Vichaa walipanga kutoroka, wakakubaliana wamnyonge mlinzi watoroke!
Walipofika getini wakakuta geti lipo wazi na hakuna mlinzi, wakasema "Turudi mipango yote imevurugika…
πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Angalia kilichomkuta huyu msanii wa mziki na mashabiki wake
Msanii mmoja anaitwa ''KINYA'' alikuwa ana perfom jukwaan..!!!
Kawaida kila msanii lazima ajitambulishe, mfano:-
''YEAH NI TEMBA hapa au
YEAH NI CHEGE hapa…!!!

Yeye akasema: "YEAH NIKINYA HAPA…!!!"
Watu wakapiga kelele ''UTAZOAAA'' mwenyewe bwenge wee

JE, WEWE UNGEJITAMBULISHAJE NAITAJI JIBU LAKO TUONE♥

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Safari ni safari
*FUNDISHO : SAFARI NI SAFARI*
Maisha ni ya ajabu sana, wakati mwingine maisha ni mazuri na mwingine ni mabaya, katika maisha yetu tumeshapitia safari nyingi sana na za aina mbalimbali kwa nyakati mbalimbali. Lakin kiukweli kila safari ni safari tuu.
Japokua kila safari ina changamoto zake lakini mwisho wake ni ule ule , kila safari ina uzuri na upekee wake.
Vile vile kila safari ina ubaya wake, kwa mfano kila safari ina gharama yake kulingana na upekee wake.
Usiwe na wasiwasi na mashaka na aina ya safari ulionayo, jipe moyo utaimaliza na kupata ulichokitarajia. Haya ndio maisha na wote tunatakiwa tuyafurahie.
Ingawa kila mtu ana safari yake bado wote tunatakiwa tufurahie pamoja kwa safari tuliyo nayo. Hata Uwe Na safar ya aina gani wewe furahi tuu. Hii ni kwa sababu safari mwisho wake ni mmoja kwa wote burudani ni ile ile
Safari🍺 ni safari 🍺hata kama ni ya chupa au ya kopo mwisho wake πŸ’€πŸ’€
πŸ˜‹πŸ˜œπŸ˜œπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Ulijua ni nn??
πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Jinsi mzunguko wa elimu ulivyo
01.πŸ‘‰ Wale wanafunzi walioongoza
Mashuleni, wanaenda kwenye
Engineering na Medical school.

02.πŸ‘‰ Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa
wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.

03.πŸ‘‰ Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia
Siasa na kuwaongoza wote hapo juu.
Yaani wa kwanza na wa pili.

04.πŸ‘‰ Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu
wote hawana raha.

05.πŸ‘‰ Wale waliopata Zero na waliokataa
shule wanakuwa waganga wa kienyeji,
wote hapo juu watamtafuta huyu, pale
mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‰πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸƒπŸΏπŸƒπŸΏπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œ

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Soma hii, kama wewe ndio mzazi wa huyu msichana ungefanyaje?
Wewe ni mzazi mwanao anasoma kidato cha tatu mkoani umemsafirisha leo kwenda shule baada ya masaa matano ukasikia gari alilo panda mwanao limepata ajali wamekufa watu wote upo ktk harakati za kuandaa msiba,

mwanao anakupigia simu baba/mama mimi mzima sijafa mpenzi wangu ABDUL aliniambia nishuke Chalinze ili niwe nae kwa siku mbili alafu niende shule je, wewe mzazi unge mfanyaje mwanao?

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Kauli 10 mbaya za walimu darasani, unakumbuka ipi hapa?
Kauli 10 MBAYA za walimu darasani, unakumbuka ipi hapa??

1:Mkimaliza kuongea niambieni niendelee kufundisha

2:Baba yako kauza ng'ombe ili alete ng'ombe mwingine shule

3:Kama unajua kuliko mimi njoo ufundishe wewe

4:Ulikuja peke yako na utaondoka peke yako

5:Hata msiponisikiliza mshahara wangu uko pale pale

6:Baba yako anahangaika kulipa ada wewe unafanya utumbo tu

7:Hata nikeshe nafundisha wengine ni mizigo hawatoki na lolote

8:Tunavisaidia tu kwan vikifanikiwa mbelen hata salam vinatoa?

9:Bichwa kubwa ubongo nukta

10:Wengine hapa wamekuja kukua tu

SHARE NA MARAFIKI ZAKO WAKUMBUKE ENZI ZA SHULE KIDOGO

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
V.gif Mmasai alivyochafua Hali ya hewa kwenye mazishi
Mmasai alipewa kipaza sauti msibani ili aseme japo machache, mambo yakawa namna hii; "Musiba oyee; jenesa safii? Amependesa hajapendesa? Mwenye wifu akufe kama hii mutu hapa kwenye jenesa. Kwansa kabisa napenda kushukuru hii marehemu sababu ina upendo, nafanya sisi nakutana leo, nakula wali musuri, nakunywa bia, na maji ile nauswa kwa duka. Naomba keso ikufe ingine, tubaki hapa, tukule, tukunywe, mpaka siku ya munada" Musiba oyeeeee!!! Itikia basi, jamani

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +