Pages

Sunday, April 21, 2019

Penzi langu linavuja damu” 06........ ONLY 18+

Kufumba na kufumbua, miezi miwili ikapita. Hakika iliniuma sana. Kuna wakati hua najihisi huzuni . Maana kwa kipindi chote hicho, Haiba hakunitafuta kwa njia yoyote ile toka nilipompatia namba yangu ya simu. Nami sikua na uwezo wa kumafuta kwakua tu sikua na namba zake za simu.
“bora hata ningechukua namba zake yeye badala ya yeye kuchukua namba zangu mimi..... Hata sijui kwanini sikua na wazo hili hapo awali.” nilijisemea baada ya kumkumbuka. Lakini ndio hivyo tena, nilikua nimeshachelewa.

Wiki hiyo nilirejeshewa mswada wangu baada ya kuhaririwa vyema na kuambiwa kua hapo sasa naruhusiwa kuuchapa kama nahitaji kufanya hivyo.
Hakika hiyo ndiyo ilikua ndoto yangu, na kwakua nilipata pesa baada ya kupokea tuzo hiyo, nilifanya hivyo.

Umaarufu wa jina langu ukanifanya nichape idadi kubwa sana ya nakala za kitabu hicho Kwakua tayari nilikua nina uhakika wa soko.
Nilitenga miioni nne kwa ajili ya uchapaji wa kiabu hicho kilichoyabadilisha maisha yangu kama mzaha.
Kwa kudra za Mwenyezimungu kitabu cha SIKU 71 kikatoka.
Kwa juhudi zangu na mapenzi ya waandishi wenzangu na mashabiki zangu tulikitangaza haswa na watu wakakinunua kama njugu.

Nilitamani kumtumia Haiba nakala laini kama vile alivyoniomba. Lakini ilishindikana kwakua sikua na email yake.
“itakua alipoteza simu ile siku niliyompa namba zangu.... Angalau ningekua nalijua jina lake analotumia kwenye mitandao ya kijamii ningeweza kumtafuta.”
Niliongea maneno hayo baada ya kufungua facebook yangu na kuangalia ile akaunti yake ya zamani, ila picha yake ya mwisho ilipostiwa miaka mitano iliyopita.
Hiyo ilimaanisha kua akaunti hiyo haikua hai.

Niliamua kutulia huku nikifuatilia mauzo ya kitabu changu cha kwanza kuchapa nakala nyingi na kupata oda sehemu mbalimbali nchini Tanzania na nchi za jirani zinazotumia lugha ya kiswahili kama lugha ya mawasiliano.

Kwa msaada wa wafasiri nguli na wataalamu wa lugha, nilifanikiwa kukichapa kitabu cha SIKU 71 kwa lugha ya kiingereza.

Hiyo ikawa sababu yangu ya pili kwenda nchini Marekani baada ya kampuni moja ya usambazaji kuniomba iweze kusambaza vitabu vyangu nchini humo.

Niliamini inaweza kuwa furasa ya kuonana na Haiba kwa mara nyingine.
Nilipelekwa kwenye vituo vya Radio na televisheni mbalimbali nchini humo kukinadi kitabu changu ambacho kina tuzo kubwa iliyotolewa miezi kadhaa nchini humo. Nashukuru Wamarekani hawakuniangusha, Na hata Waafrika wanaojua kiswahilli na kingereza wanaoishi sehemu mbalimbali nchini humo nao walimiminika kwa wingi kununua kitabu changu ambacho kilizidi kunipa dira ya maisha bora kupitia maandishi yangu.

Siku, miezi hatimaye mwaka mzima ukapita bila kuonana na Haiba. Hata matumaini ya kuonana naye tena, yakapotea.

Kikubwa zaidi nilichobadili katika mfumo wa maisha yangu, ni kumsamehe mzazi mwenzangu na kuanza kuishi naye kama awali kabla hajachoka kuvumilia shida zangu.

Hata sijui nilikumbwa na jini gani. Maana licha ya kuirudisha familia ndani ili tuanze kula mmatunda ya kazi zangu ambazo kwa muda huo zilikua zinanilipa hasa, ila kiukweli kabisa bado nilikua namfikiria sana Haiba japo alikua mbali na upeo wa macho yangu.

**************
Baada ya kuunganisha familia yangu na kuishi nao pamoja, nilipanga kwenda nayo nchini Marekani kwa ajili ya mapumziko na kufurahi. Maana ilipita muda mrefu sana tukiwa haujatoka pamoja toka penzi lilipotushinda hapo awali.

Zilipita siku tatu tukitalii maeneo mbalimbali ya nchini humo. Ndipo nilipoamua kuwapeleka ukumbi wa sinema baada ya filamu moja maarufu iliyotangazwa muda mrefu kutoka siku hiyo.

Baada ya kuangalia filamu hiyo iliyotuvutia na kutoka nje ya jumba hilo la sinema, Ndipo nilipomuona msichana mmoja akipita mbele yangu akiwa na muonekano unaofanana kabisa na Haiba. Sikujali kama nilikua na mpenzi wangu karibu, ila nilichomoka eneo hilo na kumuwahi msichana huyo.
“Haiba.”
Niliamua kuita jina bila kumshika. Maana nilihofia kumfananisha halafu ikawa zahma tena mbele za watu.
Baada ya kulisikia jina hilo, aligeuka na kunitazama. Alivua miwani yake na kuachia tabasamu pana. Tabasamu ambalo nimezoea kuliona kwa Haiba peke yake.

Msichana huyo allikua Haiba mwenyewe kabisa. Wala sikumfananisha.Nilitamani kumkumbatia kwa hamaki niliyoipata baada ya kumuona msichana huyo, Ila mpenzi wangu pamoja na mtoto walishatufikia tulipo. Ikawa ngumu kufanya hivyo tena mbele ya mwanangu. Nilibaki nimeachia tabasamu tu bila kuongea kitu chochote.

Haiba alimtazama mpenzi wangu na mtoto ambaye nilifanana naye sana, hivyo bila maelezo yoyote yale, Haiba aliweza kufahamu kama tayari nina familia.
“Niambie Molito.”
Haiba alinisalimia huku akinioneshea tabasamu hafifu lililonipa tafsiri kua hakutarajia kile alichokiona.
“salama tu.” Nilijibu na kumtazama mpenzi wangu ambaye alijisogeza karibu kabisa na kunishika kama ukumbusho ili nisiisahau familia yangu kwa ajili ya huyo msichana mrembo.
“nimefurahi kukuona Molito. Kitambo kidogo.” Haiba aliongea huku macho yake yakionyesha wazi kua hayupo huru kuongea na mimi.
“hata mimi Haiba.... Mama Omary, naona kama tunakutenga hivi. Ila ngoja nikutambulishe ili uweze kumfahamu huyu msichana. huyu ni rifiki yangu anaitwa Haiba. Ni rafiki yangu wa muda sana toka mwaka elfu mbili na kumi huko.” nilitoa utambulisho wangu kwa mpenzi wangu ili aondoe shaka na ugeni huo nilio ukimbilia.
“Haiba...huyu ni mpenzi wangu na huyu ni mtoto wetu wa pekee kwa sasa. Anaitwa Omary.” nilikamilisha utambulisho wangu kwao na kumuangalia Haiba ambaye aliachia tabasamu kwa mara nyingine na macho yote yakaganda kwa mwanangu.
“umefanana sana na mwanao... Kweli una damu kali.” Haiba alitoa sifa na kunifanya na mimi nitabasamu.
“acha niwaache... Kuna mahali nawahi mara moja.” Haiba aliongea maneno hayo na kutaka kuondoka bila kusubiri niongee kitu chochote.

Hakika wazo lilinijia kua nahitaji kuwa na mawasiliano na Haiba. Sikujua kwanini hakunitafuta baada ya kumuachia namba zangu kule ukumbini. Ila siku hiyo ilinibidi nitoe simu yangu na kumpatia aandike namba zake. Aliandika namba kwenye simu yangu na kunikabidhi.
“kesho jioni nitawatembelea ili tuweze kuongea. Leo imekua ghafla sana. Kwahereni jamani.” Haiba aliongea maneno hayo na mimi kwa roho moja nikamruhusu aende.

Tulirudi hotelini. Omary na mama yake wakaenda kuchezea maji kwenye bwawa la kuogelea.
Ndipo nilipoona hiyo ni nafasi pekee ya kumpigia Haiba ili niweze kuongea naye. Maana kiukweli nilitamani sana kusikia mawili matatu kutoka kwake. Hasa kuhusu mahusiano yake baada ya kunitema na kukata mawasiliano na mimi. Nilitamani kujua kama ameshaanza kukumbuka chochote. Hata hapo Marekani amefikaje na anaishi kwanani.

Majibu ya kila swali ambalo nilijiuliza. Ni wazi wa kuyajibu alikua ni Haiba pekee.
Nilisimama kwenye vioo vikubwa vya chumba hicho na kuichungulia familia yangu huku nikipiga namba Haiba.
“namba unayopika kwa sasa haipatikani.....”
Nilifikiri ni utani au mitandao ya marekani nayo inasumbua kama Tanzania. Lakini baada ya kujaribu mara nne, ujumbe huo haukubadilika. Simu ya Haiba ilikua haipakani.

Nilipata wazo huenda namba hiyo ikawa kwenye mtandao wa whatsApp. Hata hiko haikuwepo pia.

Siku hiyo ilipita bila simu ya Haiba kupatikana. Siku ya pili aliyoahidi kufika ilipita pia bila Haiba kufika. Na namba aliyonipa haikupatikana.

Hatimaye wiki nzima ilipita na kurudi nchini bila kuonana na Haiba. Na namba aliyonipa haikupatikana hata kwa bahati mbaya.

Kiukweli hali hiyo ilinitesa kimawazo na kunifanya nishindwe kabisa kuelewa ni kitu gani kilichompata msichana huyo na kushindwa kuniamini kwa kunipatia namba yake anayoitumia kwa kipindi hicho.

Nilitamani kurudi nchini Mrekani ili nimtafute. Maana hisia zangu ziliniambia kua maamuzi ya Haiba kuninyima namba yake sio bure, huenda ana kitu nyuma ya pazia kinachomfanya ashindwe kukubali kuwa karibu na mimi tena.

Maana kama ana mume,kivyovyote ilikua ni wakati wake mzuri sasa wakunifahamisha ili na mimi niweze kumfahamu. Maana yeye familia yangu ameshaijua hivyo hatokua na mawazo ya mimi kumtongoza au kumtaka kimapenzi.

Wazo langu halikurudi nyuma, akili yangu ikanituma nirudi tena Nchini Marekani kumsaka Haiba.
“kuna wazungu wamenitumia Email, wanahitaji kufanya matangazo ya kibiashara na mimi. Hivyo natakiwa niende nchini Marekani nikaonane nao.”
Nilitumia njia hiyo ya uongo kwa ajili ya kwenda kumtafuta Haiba kwa uhuru zaidi.

Kwakua nilimwambia ni maswala ya kuendelea kutengeneza pesa huko niendapo, hakuweza kunihoji zaidi ya kuniuliza ni lini nitasafiri.
“ni safari ya haraka sana. Natumai nitaondoka na ndege ya kesho alfajiri.” nilitoa majibu hayo na jibu likawa ni kunitakia safari njema huko niendapo.

Nilikamilisha tararibu za safari na kuweza kusafiri kwa mara nyingine mpaka Marekani. Nia na madhumuni yangu ni kumtafuta Haiba ili nikifanikiwa kumpata, niweze kumuuliza maswali ambayo yalikua yananisumbua sana kwenye kichwa changu.

Nilifika kwenye ule mji niliofanikiwa kumuona mara ya mwisho na kuchukua hotel hapo. Nilijaribu kumsaka maeneo kadhaa ambayo hapo awali niliweza kuonana naye. Hata kujaribu kuuliza Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo kwa kuonyesha picha zetu ambazo nilikua nimezitunza kwenye simu yangu baada ya kupiga naye siku ya ugawaji wa tuzo.

Ilinichukua wiki nzima nikimtafuta Haiba bila mafanikio yoyote yale. Ndipo siku moja wakati nipo mgahawani nakunywa kahawa, akaingia Haiba pasi na kutarajia. Nilimfuata na mshtuko wake ulinifahamisha kuwa ni yeye hasa.
“habari.”
Nilifungua maongezi kwa kumsalimia.
“safi...” alijibu na kunitegea niendeleze maongezi.
“za kunipa namba ya pikipiki?” nilimkumbusha tukio lake alilonifanyia na kumfanya aanze kucheka.
“yaani unazidi kunionyeshea kua kile alichokifanya ulidhamiria... Sio haki kabisa.” nilianza kulalamika na kumfanya anyamaze kucheka. Alinitazama na kumsikiliza muhudumu aliyemfuata na kuagiza kinywaji alichokihitaji.
“hivi unadhani ni rahisi mimi kutoa namba zangu mbele ya mpenzi wako? Sikuhitaji unitafute kwakua sikuhitaji kumfanya yule mpenzi wako asiwe na amani juu yangu. Maana nilimuona alivyotufuata pale tuliposimama, alionesha wazi kutoniamini mimi hata kidogo licha ya kumtambulisha kama rafiki yako. Aliniangalia kama mdudu mbaya aliyekuja kumwaga sumu kwenye penzi lake. Nami sikutaka hilo litokee ndio maana sikuja kuwatembelea wala sikutaka unitafute.” Haiba alitoa maelezo yayo juu ya maamuzi yake ya kunipa namba ambayo sio sahihi na kupokea kinywaji chake kilicholetwa muda huo na muhudumu.
“tuachana na hayo... Nimekuja hapa Marekani kwa ajili yako. Na kama bahati tu kukuona hapa leo hii. Maana ni wiki sasa toka nifike hapa na sikufanikiwa kuonana na wewe kwa kipindi chote hicho.”

Nilamua kulifukia lile jambo la awali na kuamua kusema dhumuni langu hasa lililo nirudisha nchini Marekani.
“umekuja huku Marekani kwa ajili yangu?” alishtuka sana baada ya kuzisikiliza sentensi zangu na kunitazama usoni.
“Haiba, laiti kama ungekua unakumbuka chochote kuhusu mimi. Nadhani ungeweza kuelewa kwanini nakufuatilia Hivi. Ila ningependa uniambie chochote kuhusiana na maisha yako ya mahusiano.” niliongea maneno hayo na kumfanya Haiba anitazame kwa sekunde kadhaa na kunywa kinywaji chake.
“sijakuelewa.” alitoa jibu hilo na kuendelea kunitazama ili niweze kuamini kua kile nilichokiongea hakukieleweka na mrembo huyo.
“Namaanisha hivi... Una mpenzi au umeolewa?” niliamua kufafanua kiurahisi swali langu bila kupepesa macho.
Kabla ya kulijibu swali hilo, alinyanyua kinywaji chake taratibu na kunywa fundo moja kisha akanitazama usoni.
“sina mpenzi na wala sijaolewa.”
Jibu la Haiba lilinifanya nishtuke. Japo nilijizuia na kuufanya mshtuko huo uwe wa ndani kwa ndani. Sababu kubwa kabisa iliyomfanya Haiba aweze kunikataa hapo awali ni kwamba alidai kua ana mpenzi ambaye wanapendana sana. Hivyo hawezi kumuacha na kuwa na mimi. Hivyo ikawa mwisho wa mawasiliano yangu mimi na yeye.
“ina maana hawakufikia hatua ya kuoana? Au ndio hakumbuki hata kama aliolewa na huyo mvulana ama laa?”
Nilijiuliza mwenyewe huku nikiyagandisha macho yangu kwa Haiba kujaribu kuendelea kumsoma.
“inaelekea wewe ni bingwa wa kuwapiga vibuti eeh?” niliongea maneno hayo yaliyomfanya Haiba acheke.
“hapana.... Ni maamuzi tu. Nimeamua nisijihusishe na mahusiano ya mapenzi mpaka pale nitakapo pona kabisa na kurejewa na kumbukumbu zangu zote. Labda naweza kufikiria tena upya swala la mahusiano ya mapenzi.” Haiba alijibu na kunifanya na mimi kuinywa kahawa yangu ambayo ilishaanza kupoa kutokana na kuitelekeza muda mrefu.
“samahani Haiba kwa masawali yangu... Ila nahitaji kujua tu kama unakumbuka ulivyoweza kusafiri kutoka Tanzania hadi kufika huku Marekani.... Labda unaishi na nani kwa sasa.” Nilimuuliza maswali hayo yaliyomfanya Haiba anitazame na kunikagua kuanzia chini hadi juu kwa kushusha na kupandisha macho yake.
“bila shaka kazi yako nyingine ni upelelezi... Nachukia watu wanaofuatilia maisha yangu.”
Haba aliongea maneno hayo na kusimama.
Nilifikiri ulikua ni utani baada ya kuongea maneno hayo na kusimama, ila nilimuona akienda kulipia kinywaji chake na kuanza kuondoka.

Hapo ndipo nilipopata akili ya kusimama na kumuwahi kabla hajafungua mlango wa kutokea mgawani hapo. Nilipomfuata na kumshika mkono, aliniputa na kuniwekea ndita zipatazo kumi na moja kwenye paji la uso wake.
“kaka naomba fuata njia yako. Sihitaji ukaribu na wewe kwa njia yoyote ile. Naomba unikome na usinizoee kabisa.”
Haiba alitoa maneno hayo yaliyonifanya niwe mnyonge ghafla. Maana sikutegemea kama maswali yangu yangefikia hatua ya kumkera mrembo nimpendaye kiasi kile hadi kunikasirikia kupita kiasi.

Kwa ukali wa maneno yake aliyotamka mbele yangu tena kwa sauti sauti ya juu hadi watu wengine wakawa wanatuangalia, ilinibidi niwe mpole.
“naomba unisamehe kama kuna kauli yoyote ile iliyokukwaza. Ila kiukweli nilikua najaribu kuipa mazoezi akili yako huenda ukakumbuka chochote kati ya yaliyotokea nyuma.”
nilijitetea kwa sauti ndogo ili aweze kunisikiliza. Ila Haiba hakunijibu kitu chochote, aliishia kuniangalia kama adui yake niliye sababisha kumbukumbu zake kupotea au mimi ndiye mtu niliye wasababishia ajali yao iliyowapotezea uhai wazazi wake. Alifungua mlango na kuondoka.

Niliishiwa nguvu za kumfuata kwa mara nyingine, nilibaki namtazama tu.
Kiukweli niliumia sana. Nilikaa kwenye mgahawa ule kwa muda wa masaa mawili bila kufanya kitu chochote zaidi ya kuwaza vitu mbalimbali kuhusu Haiba.

Niliwaza toka siku ya kwanza namuona kwenye maisha yangu. Hakika alinivutia sana na kunifanya nitamani awe mama wa watoto wangu. Hakika sikuwahi kupenda kama nilivyotokea kumpenda Haiba.

Basi nilirudi Hotelini kwangu taratibu na kwenda kukaa kwenye moja ya viti vingi vilivokuwa nje ya bwawa kubwa la kuogelea.

Pindi nilipotazama kulia kwangu, nilimuona mtu anasoma kitabu cha siku 71, tena cha kiswahili.
Sikusita kunyanyuka na kumfuata. Nilimsalimia na kumfanya mtu huyo ashtuke na kujawa na furaha balaa baada ya kuniona.

Mshtuko wake na tabasamu lake vilionyesha wazi kwake kuona kama ngekewa kuniona.
Maana sura yangu ilikuwepo kwenye jalada la kitabu hicho.

Vile vile wakati nakinadi kitabu hicho huko nchini Marekani, nilitumia vipindi mbalimbali vya radio na televisheni. Hivyo niliamini ni rahisi kufahamika kwa mtu yeyote ambaye alishawishika kununua kitabu hicho.

Basi nilisalimiana na mtu huyo kwa lugha ya kiswahili. Hakika kiswahili chake kilikua fasaha kabisa kuashiria kua hata yeye ni mbongo kama mimi tu.
“shukurani sana kwa niungisha. Hakika nimefurahi kukutana na shabiki wa kitabu changu tena kutokea Afrika, nyumbani.” niliongea maneno hayo huku nikionyesha tabasamu lililofanana na maongezi yangu.
“yaani kuanzia nilipokisoma mpaka hapa nilipofikia, sitamani kabisa kukiacha. Hakika wewe ni mtunzi mahiri sana.” alinisifia.
“nashukuru sana ndugu yangu.”
“mimi naitwa Farahani... Ni Mtanzania kabisa kama ulivyobashiri. Sema nipo huku muda mrefu kidogo. Nina miaka mitano mpaka sasa. Hivyo nimejenga huku na nimeoa huku pia. Mishe zangu zote nafanya huku. Naweza sema kwa sasa maisha yangu naishi Marekani.” mtu huyo alijitambulisha kwangu na kufanya nimfahamu japo kwa muhtasari.
“nimefurahi sana kukufahamu ndugu Farahani.”
Kama unavyojua wabongo tunapokutana sehemu yoyote ile. Tuliongea kiswahili na sikusita kumpatia namba zangu za simu na nilimuahidi kumtembelea nyumbani kwake siku moja baada ya kunialika.

Aliniambia anaishi Philadelphia. Niliifurahia mualiko huo kwakua ni mji ambao sikuwahi kuukanyaga.
ITAENDELEA.....

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +