Wachumba wakiwa wamekumbatiana. Picha/MAKTABA
Kwa Muhtasari
Wataalamu wa masuala wa mahaba wanasema kuwa yapo mambo mengi ambayo kila mwanamke anayetarajia kuolewa na kuwa na familia yake anahitajika kuwa nayo. Utafiti unaonyesha kuwa wanawake wanaojua kufanya marekebisho madogo ya vifaa vya nyumbani huwavutia wanaume.
JUZI kulikuwa na kisa cha mwanamke mjini Nyeri aliyemhadaa mume wake kuwa ametekwa nyara na akaja kupatwa na polisi akila raha na mwanamume mwingine. Ilidaiwa kuwa alimhadaa mumewe kuwa 'watekaji wake’ wanaitisha Sh500,000 kumbe ni yeye alitaka hela hizo. Ni jambo lililofanya watu kujikuna vichwa kuhusu aina ya wanawake wanaoolewa siku hizi.
Allan, mzaliwa wa Pwani mwenye umri wa miaka 28 anamtafuta mpenzi mwingine baada ya kumtema Liz, mrembo ambaye anasema alimpenda sana. Kulingana na Allan, Liz ni mwanamke ambaye kila mwanamume lazima atammezea mate na kupindua shingo atakapopishana naye njiani.
Hata hivyo licha ya umbo lake namba nane na sura ya kuvutia, Allan asema hawezi kumuoa Liz kwani anakosa ujuzi muhimu ambao mkewe lazima awe nao. Mapenzi ya wawili hawa yaliyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja hayajakuwa rahisi.
Kutojua kupika ni jambo kubwa lililomfanya Allan amteme Liz licha ya kwamba tayari alikuwa amemtambulisha kwa wazazi wake kama msichana aliyenuia kufunga pingu za maisha naye. Anasema katika mwaka huo mmoja hakuwahi kuonja chakula cha kipusa huyo. Kilichomuudhi zaidi ni kwamba Liz hakuwa na hamu ya kujifunza kupika.
“Nilijua kwamba Liz hajui kupika uhusiano wetu ulipokuwa umedumu kwa miezi mitatu. Wakati huo sikujali sana kwa sababu nilijua kwamba angejifunza. Hata hivyo juhudi zangu zote za kumfanya awe na hamu ya kujifunza mapishi ikiwemo kumjulisha kwa wazazi wangu, hazikufua dafu,” alisema Allan.
“Kila alipokuja kwangu, nilikuwa napika na nikimwambia aingie jikoni nimfunze anakataa katakata. Siku zote nilipoenda kwake nilipata amenunua chakula cha hotelini. Nilimpenda sana hasa kutokana na upole wake na ubabe wake kitandani lakini hayo hayakunitosha,” akaongeza.
Jambo jingine lililomuudhi Allan ni tabia ya Liz ya kutopenda kwenda kanisani. Allan asema kila Jumapili mpenziwe alikuwa na visingizio vipya vya kutoenda kanisani licha ya kwamba wote wawili ni wa dhehebu moja.
Afya nzuri
“Nataka wanangu wakue katika mazingira mazuri ya kumcha Mungu na pia wawe na afya nzuri. Sitafuti mwanamke mwenye sura nzuri bali ambaye anamuogopa Mungu na ambaye anajua mapishi hasa ya vyakula vya kipwani vya nazi,” alisema Allan.
Bila shaka kando na tabia nzuri, sura ya kupendeza au umbo lililoumbwa likaumbika, yapo mambo ambayo kila mwanamke anapaswa kuyajua au kuyafanya iwapo anataka kuitwa mke wa mtu. Siku hizi wanaume 'huwapiga msasa’ wanawake na kuhakikisha kwamba wanaafikia vigezo vyao kabla ya kuchukua uamuzi wa kuwaoa.
Vigezo hivi ndivyo vinavyotofautisha kama mwanamke huyo atafanywa kuwa 'chips funga’ yaani kifaa cha mwanamume cha kutosheleza hisia za mwili au atatawazwa kama mke rasmi.
Tuliwauliza Wakenya vigezo na ujuzi ambao wanatafuta kutoka kwa mwanamke na ingawa wengi wao walisema kuwa hulka njema ni jambo la kwanza wanaloangalia, vipo vigezo vingene kama dini, usafi, kujua kuvaa nadhifu, heshima, bidii, utu uzima, uvumilivu, uaaminifu na kadhalika. Bw Ali Petit, mkazi wa Hola, anasema mkewe lazima awe mcha Mungu.
“Kwanza mwanamke huangaliwa kama ameshika dini. Je sheria na kanuni za dini yake anazifuata? Mwanamke akiwa anamuogopa Mwenyezi Mungu ndio mnaweza kuishi vyema katika nyumba. Jambo la pili ni tabia. Je tabia zake ni zenye kuridhisha? Je heshima zake na utu wake anauchunga? Muhimu zaidi, tabia zako ziwe zinaambatana na zake,” alisema Bw Petit.
Naye Bw Samir Abdallah kutoka Zanzibar anasema mwanamke ambaye atamvutia ni yule mkweli na muaaminifu ingawa anasema ni jukumu la mwaname kuhakikisha kwamba mkewe anapendeza.
“Mawanke anafaa kujitunza kwa kuwa msafi na pia awe mwenye uwazi. Sitaha, heshima, muonekano mzuri kwa jamii ni juhudi yangu mimi mwenyewe kama mwanaume, kiongozi kwa mwanamke,” akasema.
Kupika
Bw Kipkoech Arap Too anasema mwanamke anapaswa awe wa kulinda siri, avae vizuri na wala sio minisketi hasa akiwa maeneo ya watu wengi, ajue kupika chakula kitamu, ajue jinsi ya kupanga uzazi, awe anafanya kazi kwa ustadi, asitamani maisha ya juu kuliko uwezo wa mumewe na awe na maongezi bora.
“Bila shaka mwanamke dhabiti ni yule aliye na uwezo wa kukimu familia nikiwa mbali, tena yapasa mwanamke alee watoto kwa bidii sana. Mwanamke asiye na kidomo anafaa sana kwa ndoa, yule asikiaye makosa yake na kurekebisha. La mwisho ni kuwa aonyeshe upendo kwa watoto wangu,” alisema Bw Too.
Naye Maureen Cheruiyot, mkazi wa Nairobi, anasema mwanake lazima awe na hulka njema, heshima kwa maulana, mumewe, kwake na kwa kila mtu. Pia awe na bidii, aonyeshe mapenzi kwa wazazi na ndugu wa mumewe na avae mavazi bora.
Wataalamu wa masuala wa mahaba wanasema kuwa yapo mambo mengi ambayo kila mwanamke anayetarajia kuolewa na kuwa na familia yake anahitajika kuwa nayo. Utafiti unaonyesha kuwa wanawake wanaojua kufanya marekebisho madogo ya vifaa vya nyumbani huwavutia wanaume.
Vigezo vingine muhimu ni kama kubadilisha mtoto nepi, kupika chakula kitamu, kujua kutumia vifaa vya kiteknolojia kama vile tarakilishi, kujua kufua, kupiga pasi na kuosha nyumba,kumfanya mtoto aburudike kwa zaidi ya dakika 10, kujua kushona kifungo na kadhalika.
Hata hivyo mwanasaikolojia Maurice Matheka anasema kuwa ingawa kuwa na vigezo hivi ni muhimu kwa kila mwanamke, dunia ya sasa imegeuka kwani kile kinachotafutwa na wanaume wengi wa sasa ni ngono na hasa mitindo mipya wanayoona kwenye majarida, kwenye video na wanayohadithiwa na marafiki zao.
“Ni kweli kwamba wanaume hutafuta mambo mengi sana kutoka kwa mwanamke lakini siku hizi ngono ndilo jambo muhimu sana katika ndoa nyingi na sio pesa wala tabia,” alisema Bw Matheka.
“Leo, mambo yamebadilika. Ingawa jamii inasema kuwa wanaume hutafuta mwanamke atakayekuwa mke, mama na mpishi mzuri, huo sasa ni upuzi kwa sababu wanaume wanapotoka nje, hawatoki kwa sababu ya mapishi. Wanatoka ili kutafuta ngono ambayo hawaipati nyumbani,” akasema.
Anawashauri wanaume wasiwaoe wanawake ambao hawawatoshelezi kitandani kwani hiyo ndiyo sababu itakayopelekea kuvunjika kwa ndoa yao. Aidha anawataka wanawake wasijifunge kufuata tabia ambazo jamii inawalazimisha.
“Wanawake wamelazimishwa na jamii kuwa na tabia ambazo wanaume hawazitaki. Wanaume wengi husema wanataka mke mwenye tabia na vigezo fulani lakini wengi wao hata wakiwa na mke kama huyo nyumbani bado watatoka nje kutafuta wanachokikosa. Nawashauri wanawake wabadilike na wakati,” akaeleza.
Wednesday, April 10, 2019
SIFA ZA MKE MZURI WA NDOA NA SIO WA KUTUMIKA KUTOMBWA TYU BHALI AWE NA SIFA HIZI
Posted by
NeverGoBack
on
12:32 PM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments