Upungufu wa nguvu za kiume ni janga kubwa ambalo linazidi kuwakanganya wanaume wengi wa siku hizi. Wengi wanaokumbwa na matatizo haya hujaribu kutafuta kila mbinu ili kuhakikisha maisha yao ya mahusiano na wapenzi wao hayaishi.
Kuna mbinu tofauti tofauti ambazo zinatumiwa na matabibu kuhakikisha ya kuwa swala hili limekandamizwa. Kama ijulikanavyo kuna mbinu tofauti za kurudisha nguvu za kiume kwa mwanaume. Kuna kutumia dawa za hospitali ambazo zinaongeza testerone kwa mwili wako, na ile ambayo inapendwa sana na wengi ni kutumia vyakula asilia ambavyo vinatumika kurudisha mwili wako uwe na nguvu za ujana.
Hivi ni baadhi ya vyakula vinavyosaidia kurudisha nguvu za kiume:
Avacado
Parachichi
Mtini (figs)
Chaza wabichi (Uncooked Oyster)
Njugu karanga
Kitunguu thaumu
Chokoleti
Ndizi
Hii ni baadhi ya vyakula vinavyoaminika kurudhisha nguvu zako za kiume lakini swali ni je, iwapo nimerudisha nguvu zangu za kiume lakini sikufuata mambo ambayo nafaa kuyazingatia je nitafanikisha kudumisha mahusiano yangu na mpenzi wangu?
Hili swali ndio limenifanya kuja na sababu kuu ambazo zinachangia upungufu wa nguvu za kiume.
Kulingana na utafiti uliofanywa ni kuwa kati ya wanaume watano, mmoja anasumbuliwa na tatizo la upunguvu wa nguvu za kiume. Lakini kulingana na tamaduni na hadithi za kiafrika ni kuwa eti upungufu wa nguvu za kiume husababishwa na laana ya ukoo ama kurogwa. La hasha. Mtu yeyote yule anaweza kukumbwa na janga hili kama hatofuata mkondo mzuri wa maisha katika mahusiano.
Upungufu wa nguvu za kiume huletwa na matatizo yafuatayo:
1. Matatizo katika mahusiano
Swali ambalo unafaa kujiuliza ni je, mahusiano wewe na mpenzi wako yanafaa ama nikupotezeana? Je, unauaminifu kwa mpenzi wako? Mpenzi wako unamshuku?
Maswali kama haya ni muhimu katika kuchangia uwezo wako wa kufanya vyema katika tendo la ndoa. Iwapo unamwendea kinyume mpenzi wako basi fahamu ya kuwa hili ni shimo ambalo unajichimbia wewe mwenyewe bila kujifahamu.
Pia kuwa na uhusiano na mpenzi wako kwa muda mrefu bila kubadilisha mitindo tofauti ya mapenzi yenu kutachangia pakubwa kwako kupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa hivyo kuashiria ya kupoteza nguvu za kiume. Hebu wewe fikiria kila siku unakula chakula aina moja bila kubalisha aina nyingine. Mwisho itafikia mahala fulani utaishiwa na hamu.
So suluhisho hapa ni kufanya nini?
Badilisha mitindo yenu ya kufanya mapenzi- jeuza mitindo yenu ya kufanya mapenzi ili kufanya maisha yenu ya kufanya tendo la ndoa kuwa ya kusisimua
Usifanye ngono kama chakula- najua wengi wangetamani kufanya kila siku lakini ushajiuliza kwa nini kisu kikitumika kila wakati kinapoteza makali yake?
Msaprize mpenzi wako- katika maisha yenu, mwanamke anapenda kuona mabadiliko ya mara kwa mara kutoka kwako. Mfano leo umekuwa na tabia hii kesho nyingine. Kufanya hivi hakutamsaidia mpenzi wako kuwa na furaha na mapenzi yenu pekeake, bali inakusaidia na wewe kuondoa shida au matatizo yanayoweza kutokea katika mahusiano yenu.
2. Msongo wa mawazo, wasiwasi, uchovu
Iwapo maisha yako yanakumbwa na msongo wa mawazo, wasiwasi ama uchovu ujue unajichimbia kaburi wewe mwenyewe. Ikiwa unalalamika ya kuwa wakati unapofanya tendo la ndoa unakumbwa na uchovu ama wasiwasi wa kujishuku iwapo umemridhisha mpenzi wako au la, fahamu ya kuwa hii ni dalili moja wapo ya kukufanya kupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa ambapo itafikia mwishowe kupoteza nguvu za kiume.
So suluhisho ni nini?
Iwapo unahisi uchovu wakati wa kufanya ngono, inamaana ya kuwa hauna stamina ama hauna nguvu za kutosha za kutimiza mpango mzima hivyo ni lazima kwako ufanye mazoezi kwa kuingia gym.
Wasiwasi huletwa na kutojiamini. Iwapo utaweka akili yako kuamini ya kuwa hauwezi kumridhisha mpenzi wako, utakuwa ukijenga saikolojia ya kuwa hauwezi kutimiza matakwa ya mpenzi wako. So unachohitaji kufanya ni kujiamini na kupuuzia iwapo hauwezi kumridhisha mpenzi wako.
Msongo wa mawazo unaweza kuutatua kwa kula lishe bora na kujihusisha na maisha ambayo hayatakuwa yakikutatiza kiakili.
3. Huzuni/ depression
Huzuni ni tofauti kabisa na kutokuwa na raha, kuchoshwa ama kusumbuliwa na jambo kwa muda mfupi.
Huzuni ni ugonjwa ambao humkabidhi mhusika kwa muda mrefu, aidha miezi ama hata miaka. Hisia hizi zinaweza kukuathiri kwa muda mrefu na kuingilia hadi kwa maisha yako ya kawaida ikiwemo maisha yako ya kimapenzi.
Huzuni mara nyingi huletwa na mambo ambayo umepoteza tamaa ama kutojiskia na maisha ama kutofurahia na mambo ambayo zamani yalikuwa yakikufurahisha ama kukupendeza.
Pia kulingana na utafiti inasemekana ya kuwa baadhi ya madawa ya antidepressants ambayo hutumiwa huchangia pakubwa kufanya mtu kupoteza nguvu za kiume.
Mambo ya kufanya
Usijipe stress na maisha. Iwapo utakuwa kila wakati unakumbwa na misongo ya mawazo fahamu ya kuwa kutachangia pakubwa kwako kupoteza nguvu zako za kiume.
Madawa unayoyatumia kama antidepressants unafaa uyahakikishe kwa daktari ili ayaangalie kama yanafaa kwa matumizi ama la.
4. Dawa za kulevya na vinywaji
Wengi wanasahau ya kuwa vinywaji huchangia kupoteza nguvu za kiume. Usizidishe chupa 3-4 kwa siku kwa mwanaume. Kulingana na utafiti ni kuwa tembo linachangia pakubwa kwa wanaume kuishiwa na nguvu.
Pia dawa za kulevya zinachangia pakubwa kumharibu mwanaume. Miraa ikiwa moja wapo ya dawa za kulevya zinazochangia pakubwa kulemaza nguvu za kiume kwa mwanaume.
5. Kuzeeka
Pindi unapokuwa mkubwa ndipo unapopunguza hamu yako ya tendo la ndoa. Hii ni kwa sababu wakati unapozeeka, mwili wako unapunguza kiwango cha homoni za testerone ambazo zinatolewa kutoka kwa mwili wako. Pia magonjwa yanayohusiana na uzee ama matumizi ya dawa fulani zinachangia kwako kupunguza hamu ya tendo la ndoa.
Mambo ya kufanya
Hakikisha unaishi maisha yasiyokuwa na mawazo
Tumia baadhi ya vyakula ambayo vinaongeza nguvu za kiume
Fanya mazoezi kuimarisha misuli yako
6. Matatizo ya homoni
Tatizo hili haliko sana na mara nyingi halijaripotiwa kama kuwa sababu kuu ya mwanaume kupoteza hamu ya tendo la ndoa.
Tatizo hili linakuja wakati tezi (thyroid gland) inayopatikana nyuma ya shingo ya binadamu haifanyi kazi vile ipasavyo. Tatizo hili madhara yake kwa mwanaume ni kuingiwa na huzuni, kuongeza uzani wa mwili, na kuwa na uchovu wa mara kwa mara.
Mwisho la msingi ni kuwa iwapo unakumbwa na upunguvu wa nguvu za kiume usikimbilie dawa ambazo zinapatikana kwa maduka hivi hivi bali unafaa kupata ushauri nasaha kutoka kwa matabibu walioorodheshwa na serikali.
Wednesday, April 24, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments