Pages

Sunday, April 28, 2019

Ushauri nimeikuta mahali nikaona niwape na nyie mumshauri huyu mwenzeta



Mimi naitwa Najma.ni mwalimu wa shule ya msingi nipo dar maeneo ya Gongolamboto.Ninaishi na Mwanaume na nimezaa nae mtoto mmoja.
Tatizo nililolipata ni kuwa baada ya kuonana na huyu mwanaume ninayeishi nae hivi sasa,kuna maswali nilimuuliza kabla sijaamua ishi nae.
Nilimuuliza kama alishawahi kuoa..akanijibu ndio alishawahi kuoa na akabahatika kupata mtoto mmoja na huyo mwanamke.
Akaniambia pia bahati mbaya yule mtoto alifariki kwa ajali,na baadae akaachana na yule mwanamke.
Nikamuuliza kwahiyo hana mtoto??akanijibu ndio hana mtoto wowote. Kiukweli nilibaki njia panda maana umri wake ulionekana ni mkubwa.hivyo kusema hana mtoto nilishangaa.
Nilimkubalia ila nikamwambia Mimi Nina mtoto mmoja,akaridhika! nilimpeleka kwetu na yeye akanipeleka kwa baadhi ya ndugu zake,tukafunga ndoa "simpo" tu isiyo na gharama yoyote.tukaanza kuishi pamoja.
Nilipata ujauzito na nikajifungua mtoto wa kike.kwahiyo na Yule wangu aliyenikuta nae nikawa na watoto wawili.
Sasa wiki iliyopita narudi toka kazinii nakuta kuna ugeni nyumbani.alikuwa ni wakina mama wawili.mmoja akiwa na watoto watatu.
Wale wakina mama wakadai wanamuhitaji mume wangu. Nikasema wanaweza tu niambia shida yao.
Mmoja akasema yeye alikuwa ni mke wa mume wangu na hakuwahi kupewa taraka.akadai mume wangu kamtelekeza huko morogoro mwaka wa tatu sasa.
Akadai na wale watoto watatu kazaa na mume wangu.akadai kaja kuwaacha wale watoto ili nae mume wangu aonje utamu wa kulea.kiukweli nilichanganyikiwa.
Walimsubiri mume wangu hadi aliporudi.Mume wangu alishtuka kuwaona nusu akimbie.
Tulikaa kikao na mume wangu alikuwa hana la kusema.yule mwanamke aliwaacha wale watoto na wakaondoka zao.
Mpaka sasa hawa watoto ninao Mimi hapa kwangu.kiukweli nimechanganyikiwa..sio kwakuwa sitaki kuwalea watoto wa mwenzangu,ila kwanini mume wangu hakuniambia ukweli nijue!?
Nafikiria niachane nae nifanye maisha yangu.Naomba ushauri wako kaka Nurdin Nalinga.
Najma.

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +