Tatizo la usaliti limekuwa ni kubwa sana katika mapenzi. wengi wamekuwa wakilalamika kuhisi kusalitiwa na wapenzi wao.zamani wanaume ndio walikuwa wakiongiza katika usaliti kwa wake zao ,lakini utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa nao wanawake wamekuwa wasaliti katika ndoa zao Na hii ndio sababu iliyonifanya niandike sababu za usaliti katika mapenzi
Kutoridhika katika tendo la ndoa.
Ni dhahiri kuwa mmoja wapo asipotosheka kila mnapokutana ,nakama hiyo hali itaendelea bila ufumbuzi basi yule asiyeshiba katika hayo mapenzi atatafuta njia ya mkato(michepuko)
Kutopata mapenzi ya kweli katika ndoa hasa ikiwa Kijana/Binti alilazimishwa kuoa/kuolewa na mtu ambaye hakumpenda.-Wengine hawapata mapenzi ya kweli kwa sababu tu mwanaume au mwanamke hamjali, kitendo ambacho kinasababisha baadhi yao kuona kwamba suluhu pekee ni kwenda nje ya ndoa.
* TABIA YA UCHAFU WA MWILIU, kutojijali au kujipenda kwa mwanaume na mwanamke-
*Kutotosheka/kuridhika katika tendo la ndoa
*Ubize wa kazi kupita kiasi/Kusafiri (masomo
Kuna watu wako bize kila kukicha, wakati mwingine si kweli kwamba wako bize bali ni unafiki au labda kutojua namna ya kupangilia mambo. Wengine ni watu wa safari kila mara, hiyo ni mbaya kwa wanandoa.
*Tamaa ya mali na vitu vya thamani(utajiri wa haraka):
Kuna wengine wako tayari kufanya ngono hovyo ili wapate mali. Huu ni ujinga, badala ya mtu kufanya kazi, anafikiri kwamba njia rahisi ni kubabaikia wanaume wenye magari, wenye fedha ..
*Kujifunza mambo au mitindo mipya
-Wakati mwingine kuna wengine wanatoka nje ili kusaka miondoka mipya...kuna wengine wamekuwa waoga wa kusema ukweli kwa wenzi wao juu ya yale ambayo wanayataka, matokeo yake wanaona wafanye hiyo ‘dawa mbadala’.
*Kutopata tendo la ndoa muda mrefu,
labda kwa sababu mume ana matatizo au mke ana uja uzito mkubwa ama amejifungua n.k-Hata hivyo kitaalam kuna njia za kuridhishana si lazima tendo la ndoa la aina moja, bali wapenzi wanaweza kuchezeana na kila kitu kikawa chenye kuwafurahisha wote au kumfanya mwenzi wake afurahie
Wednesday, April 24, 2019
ZIJUE SABABU 7 ZA USALITI KATIKA MAPENZI (NDOA) ILI TUPUUNGUZE USALITI
Posted by
NeverGoBack
on
10:39 PM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments