ILIPOISHIA
“Mama hajakuachia maagizo yangu?”
Nilimuuliza kwa sauti ya upole, huku jinni mahaba likiwa tayari limesha nivaa, taratibu mkonno wangu wa kushoto nikauweka juu ya paja lake, na kulitomasa taratibu kidogo, nikamuona Yudia akifumba macho kwa woga na tukio hili la ufumbaji wa macho lilisha nikutaga kwa Lucy.
“Eti mama hajakuachia maagizo yangu”
Nilizungumza huku nikianza kulipandisha gauni lake juu taratibu kuhakikisha kwamba nataja kuliacha paja lake wazi, ili nilione tena kwa mara ya pili ukiachilia nilivyo liona kwa mbali alipo kuwa anacheza mzika pale sebleni.
ENDELEA
Yudia alipoona kigauni chake maeneo ya mapajani ninazidi kukipandisha juu, kwa haraka akanyanyuka kitandani. Akasimama mita chache kutoka kwenye kitanda, huku nikiona dhairi mwili wake mzima unamtetemeka kwa woga.
“Chai tayari”
Yudia alizungumza na kutoka chumbani kwangu na kuniacha nikiwa najilaumu kwa tama zangu, na endapo atamueleza mama juu ya hisia zangu za wazi wazi nilizo muonyesha sifahamu itatokea nini. Nikashuka kitandani taratibu, nikafungua kabati langu la nguo na kutoa pensi kwenye begi langu la nguo, kisha nikatoa na shati kubwa kiasi, nilipo maliza kuzivaa nguo hizo nikatoka chumbani kwanu huku nikiwa nina maswali juu ya kitu gani ambacho Yudia atakifanya.
Nikafika sehemu ya kulia chakula, sikumuona Yudia zaidi chupa ya chai na sahani iliyo funikwa, zilizopo juu ya meza. Taratibu nikanawa mikono kwenye sinki la kunawia, maumivu ya viganja vyangu kwa sasa yamepungua kwa kiasi kikubwa na vinaelekea kupona. Nilipo maliza kunawa, nikafungua chupa ya chai pamoja na kufunua sahani hiyo iliyo jaa chapati za kusukuma na soseji zilizo kadhaa.
Taratibu nikaanza kula huku kichwa changu mara kwa mara kikigeuka pande zote mbili kutazama kama ninaweza kumuona Yudia.
Hadi nina maliza sikuweza kumuona hata akikatiza kueleka jikoni, moyo wangu ukaingia simanzi kubwa kuona kwamba uwepo wangu hapa ndani umeanza kumkosesha amani na raha mtoto wa watu.
‘Dany punguza tamaa’
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikielekea jikoni, sikumkuta. Wazo la kwenda kumuangalia chumbani kwake hilo ndilo lililo nijia kichwani mwangu, nikatoka jikoni na kuelekea kilipo chumba chake, ambacho kinatazamana na mlango wa chumba cha mama. Nikiwa karibi kabisa katika mlango huo, nikasikia miguno ya kimahaba ndani ya chumba hicho.
Mapigo ya moyo yakaanza kunidunda taratibu huku kajasho kakinimwagika. Kitu cha kwanza nilicho kiwaza ni kwa nini binti huyu amemamua kuleta mwanaume nyumbani kwetu, amejiamini nini.
Maswali hayo niliendelea kujiuliza huku nikinyata kwa utaratibu hadi mlangoni kwa nyudia. Nikajaribu kuusukuma ila nikakuta umefungwa kwa ndani.
“Ooooooaiaaasisssssss”
Kelele za Yudia zilizidi kuongezeka kiasi cha kuzidi kunichanganya, nikajaribu kuchungulia kwenye kitundu cha funguo, nikakutana na funguo iliyopo kwa ndnai. Nikataka kugonga ila mkono wa kulia ambao nilijiandaa kugonga mlango ukasita na kujikuta taratibu nikilitega sikio langu nisikilizie vizuri.
“Oohoo Pussy, kick my pussy”
Nilijihisi kuchanganyikiwa kwa maana kelele za Yudia ni za kumdatisha kila mwanaume, ila kitu kinacho niumiza zaidi inakuwaje mwanaume huyo anakuja tena nyumbani kwetu na kumla mfanyakazi wetu ikiwa kidume nipo mimi nipo humu humu ndani.
“Dirishani”
Nilijisema kimoyo moyo na kuanza kutembea kwa hatua za haraka ila za kunyata, nikatoka kabisa nje nakuzunguka upande wa nyuma kulipo na dirisa la Yudia. Taraibu nikaanza kunyata kulisogelea dirisha hili la kioo ambalo limefungwa vizuri ili kuzuia sauti kutoka kwa sana.
Taratibu nikasogeza macho yangu kuona ni kitu gani kinaendelea ndani ya chumba cha Yudia, ila nikakutana na pazia zito ambalo si rahisi kuweza kuona ndani, hata kama taa imezimwa.
“Pumbavu”
Nilijikuta nikizungumza huku nikiondoka kwa haya. Nikarudi sebleni na kukaa kwenye sofa ambalo, kama kuna mtu ambaye ameingizwa ndani humo akitaka kupita kwa lango wa uwani ni lazima nitamuona na hata akipita kwa mlango wa sebleni ndio kabisa nitamuona. Masaa madakika yakazidi kukatika hadi inatimu saa saba kasoro nikasikia mlango wa chumbani kwa Yudia ukifunguliwa. Nikajitega vizuri ili kuhakikisha ninamuona kidume huyo ambaye haogopi kuingia kwenye nyumba tena ya mkurugenzi wa jiji.
Nikamuona Yudia akiwa anatoka chumbani humo huku akiwa amevalia suruali nyeusi na tisheti nyeupe, nywele zake za kichwani ameziweka vizuri, huku kaarubu kazuri ka manukato aliyo jipulizia vikiitesa pua yangu.
“Yupo wapi?”
Nilijikuta nikiropoka huku nikimtazama Yudia anaye chupa na sahani mezani.
“Nani kaka Dany?”
Swali hilo la Yudia likanifanya ninyamaze kimya nisijue ni cha kumjibu.
“Ahaa hakuna kitu, kuna mambo nilikuwa ninayafikiria”
“Ok sawa”
Akabeba chupa mkono wa kushoto na sahani hizo mbili akazibeba mkono wa kulio. Kalio lake linavyo tingishika ndivyo jinsi linavyo nitia wendawazimu na kujikuta nikilaani mwanaume ambaye amekuja nyumbani kwetu na kumla mfanyakazi wetu.
“Mamaee hii zarau sasa”
Nilizidi kuzungumza maneno ya chini chini huku nikimtazama Yudia akimalizikia kuingia jikono. Mlio wa simu yangu unao itia chumbani kwangu, ndio ulio nifanya ninyanyuke na kuingia chumbani kwangum hata wazo la kulinda mwanaume ambaye amekuja kumfaidi Yudia likaniondoka kwa muda.
Nikaikuta simu yangu ikiwa juu ya kitanda, nikaichukua kwa haraka kabla haijakata nikaipokea na kuiweka sikioni kumsikiliza Hassani ni nini anazungumza.
“Dany niambiee kaaka”
“Savi haya vipi?”
“Ahaa nimesha ianaza safari nipo Segera hapa. Nipo na mtoto Lissa”
“Aisee wee jamaa una hatari”
“Hatari gani kaka?”
“Demu umekutana naye jana tu leo umembeba”
“Ahaa kaka, ngoja nitakucheki”
Nje nikasikia vishindo vya kama mtu anakimbia kwenye kordo, kwa haraka nifungua mlango huku simu yangu ikiwa sikioni. Nikamuona mtu akifunga mlango wa sebleni, kwa haraka nikakimbilia sebleni ila kabla sijatoka nikamuona Yudia akiwa jikoni, anaosha vyombo huku masikioni mwake amevaa earphone.
Sikumsemesha chochote zaidi ya kutaka kwenda kuwahi getini kuona ni nani aliye toka. Nikatoka nje kabisa na kukimbilia genitini kiwa peku peku. Nikafungua geti dogo na kutoka nje kuangalia ni nani, ila sikuona mtu wa aina yoyote akiwa anaonyesha dalili ya kutoka hapa nyumbani kwetu.
Nikafunga geti na kurudi sebleni, nikasimama kwa sekunde kadhaa kisha nikaelekea jikoni. Nikamkuta Yudia akiawa amefungua friji.
“Kuna mtu alikuwepo humu ndani ni nani?”
Nilizungumza kwa sauti nzito kidogo, Yudia hakunisikia kwa sababu hata mimi niliye simama nyuma yake ninasikia sauti ya mziki unao piga kwenye earphone zake. Nikachomoa earphone ya sikio la kulia na kumfanya kustuka na kugeuka nyuma kwa haraka.
“Nimekuuliza kuna mtu alikuwemo humu ndani ni nani?”
“Mtu…..!!?”
Yudia aliuliza kwa mshangao, akionekana kama ndio kwanza habari za mtu huyo anazisikia sasa hivi.
“Ndio kuna mtu ametoka humu ndani na kukimbilia nje”
“Ehee, kusema kweli kaka Dany mimi sijasikia kabisa”
“Utasikia saa ngapi wakati umeweka hiyo midude yako masikioni”
Nilizungumza kwa ukali, hadi Yudia akarudi nyuma kidogo kwa kuogopa. Moja kwa moja wazo langu nililo kuwa nikiliwaza kwamba kuna mwanaume ameingia ndani kwetu hapo ndipo likajitia tiki. Nikamtazama Yudia machoni kwa macho makali, kisha nikaachia msunyo na kutoka chumbani humu. Nikaingia ndani kwangu na kuufunga mlango kwa kuubamiza kwa nguvi.
“Fuck…..”
Nilijikuta hasira ikinipanda, huku kwa mbali nikijihisi wivu juu ya Yudia, japo simpendi kutoka moyoni, ila kitu cha mwanaume wan je kuingia ndani kwenu na kumburudisha dada wa kazi wenu na dada huyo amekubania ina uma sana.
‘Dany kuwa basi, atakupeleka wapi huyu msichana’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikikaa kitandani. Nikajikuta nikiwaza mambo mengi sana na kubwa zaidi ni jinsi mwanaume huyo alivyo ingia ndani kwenu na kumla Yudia, makelele yake ya mahaba yakaanza kujirudia rudia tena. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuvua shati na kulalam usingizi mzito ikanipitia na kulala fofofo.
“Heeee Dany ni nin hii?”
Niliisikia sauti ya mama ikizungumza karibu yangu kwa haraka nikayafumbua macho yangu na kumkuta mama akiwa amekaa pembeni yangu huku akilitazama jeraha langu la mgongoni huku sura yake akiwa amekikunja, si kwa kukasirika ila kwa uchungu wa kuliona jeraha hilo.
“Shikamoo mama”
“Marahab, huku mgongoni imekuwaj kuwaje mpaka ukaungua hivi?”
Sikuwa na jinsi zaidi ya kuanza kumsimulia mama kwa kila kitu ambacho kiliweza kutoka katika kusaidia kuiokoa nyumb yam zee Jongo.
“Kwa hiyo mwenyewe ulijifanya super mar?”
“Hapana mama si niliamua kusaidia maisha ya watu?”
“Ahaa mama usiseme hiyo, ila kupitia hilo pia nimepata likizo”
“Mjinga wewe, ungekufa ndio ungepeta likizo ya moja kwa moja ya kuzimu”
“Mama”
“Ngoja nimpigie daktari aje kukutibu, na jana umekuja hata kuzungumza, ukaenda matembezi”
Sioni ajabu kwa mama yangu kulalamika sana kwa mana nimesha mzoea kwa kulalamika kwake. Akatoa simu yake kwenye pochi na kuanza kuminya minya namba kwenye simu.
“Mama kile kimeo chako kipo wapi?”
Nilimuuliza mama kwa utani baada ya kuona amenunua simu aina ya Samsung Galax note 3.
“Kwani unaona mimi kila siku ni mtu wa kutumia vimeo”
Kauli ya mama akanifanya nicheke, akaanza kuzungumza na daktari huyo. Mazungumzo yao hayakuchukuam dakika nyingi akakata simu.
“Anakuja usitoke leo”
“Sitoki”
“Ngoja niaende chumbani kwangu nikaweka hii mizigo”
“Sawa mama”
Mama akachukua pochi yake na mfuko wa bluu, ambao unaonyesha kuna vitenge. Akatoka chumbani kwangu na kuniacha nikishuka kitandani, saa ya simu yangu inaonyesha saa kumi alasiri, nikatoka chumbani na kuelekea jikoni kunywa maji, nikamkuta Yudia ana kuna nazi.
Sikumsemesha kitu chochote zaidi ya kufungua friji na kumimina maji ya baridi kwenye glasi. Tukiwa hapo jikoni tukasikia sauti ya mama ikimuita Yudia kwa nguvu.
Yudia ambaye kwa sasa hajavaa earphone masikioni, akasimama kwa haraka na kueleka chumbani kwa mama.
“Ni nani ameingia chumbani kwangu?”
Sauti ya mama iliweza kunifikia hadi jikoni nilipo, ikanibidi kutoka jikoni na kusimama kwenye kordo nikatazama mlango wa mama ulio achwa wazi kidogo. Nikasikia sauti ya Yudia akijitetea kwamba aliingia asubuhi tu alipo kuwa anafanya usafi.
“Ohoo Mungu wangu jamani”
Kauli hiyo ya mama ikanistua kidogo na kujikuta nikielekea chumbanikwa mama na kuufungua mlango na kukuta kiji shelf cha chumba ambacho kimejengewa ukutani kikiwa kimevujwa. Huku baadhi ya vitu vikiwa vimeanguka chini ikiwemo vibunda vya pesa za kigeni ambazo ni dola za Marekani na Paun ya Uingereza.
“Mama kuna nini?”
“Kuna nyaraka za serikali ambazo ni muhimu sana, zimeibiwa. Sijui nitafanya nini mimi”
Mama alizungumza kwa unyonge huku machozi yakimlenga lenga mikono yake akiwa ameiweka kichwani, hapo ndipo taratibu nikaanza kupata picha ya mtu ambaye alitoka kasi na nilimuhisi kwamba ni mwaume wa Yudia kumbe sivyo hivyo ni mwanaume aliye kuja kuiba nyaraka muhimu za mama.
“Dany mwanangu unatakiwa kufanya kitu, la sivyo kazi sina mwanaungu”
Mama alizungumza huku machozi yakimwagika kitendo kilicho nifanya nijisikie vibaya sana moyoni mwangu.
ITAENDELEA
Monday, May 6, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments