ILIPOISHIA
“Mama kuna nini?”
“Kuna nyaraka za serikali ambazo ni muhimu sana, zimeibiwa. Sijui nitafanya nini mimi”
Mama alizungumza kwa unyonge huku machozi yakimlenga lenga mikono yake akiwa ameiweka kichwani, hapo ndipo taratibu nikaanza kupata picha ya mtu ambaye alitoka kasi na nilimuhisi kwamba ni mwaume wa Yudia kumbe sivyo hivyo ni mwanaume aliye kuja kuiba nyaraka muhimu za mama.
“Dany mwanangu unatakiwa kufanya kitu, la sivyo kazi sina mwanaungu”
Mama alizungumza huku machozi yakimwagika kitendo kilicho nifanya nijisikie vibaya sana moyoni mwangu.
ENDELEA
Kwa ishara nikamuomba Yudia kutoka chumbani kwa mama, naye akafanya hivyo akiwa katika hali ya woga. Taratibu nikamshika mama na kumkalisha kitandani kwake.
“Nitafanya nini mwanagu, mkataba huo ni muhimu na kesho kutwa raisi anakuja Tanga na anahitaji kuweza kuusaini”
Mama alizungumza machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake. Ikanibidi kukaza roho kama mtoto wa kiume kuto kulia mbele ya mama yangu kwa maana, machozi yake yanaufanya mwili wangu wote kusisimkwa na kujihisi na mimi ninaweza kudondosha chozi muda na wakati wowote.
“Kwani mama kuna kitu watu ambao una bifu bifu nao?”
Mama akakaa kimya kwa muda, kisha akatingisha kichwa kuashiria kwamba kuna watu ambao ana ugomvi nao.
“Ni kina nani hao?”
“Kuna huyu meya mpya, wao nina uhakika kwamba ndio wanao winda hizi nyaraka, wanataka kuziteketeza ili mpango wa ujenzi wa bandari mpya usifanikiwe”
“Na huyo meya ana kaa wapi?”
“Raskazoni kule”
“Ok ngoja nianze kuifanya hivyo kazi muda huu, ila nina kuomba usilie sawa mama yangu”
“Sawa”
Nikamfuta mama machozi kwa kitambaa chake, kisha nikanyanyuka na kutoka chumbani humo. Nikakutana na Yudia kwenye kordo akiwa kama ni mtu mwenye wasiwasi na kitu fulani, ila sikutaka kumsemesha chochote kwa maana mambo ya muhimu ya mama yamesha haribika. Tukiwa hapo kwenye kordo tukasikia sauti ya kungele ya getini ikiita. Yudia kwa haraka akaondoka na mimi nikaingia chumbani kwangu.
Nikafungua kabati na kutoa begi langu la nguo, nikaitoa bastola yangu, niliyo iweka chini kabisa ya nguo zangu, nikaitazama huku nikitoa magazine yake, nikaikuta ikiwa na risasi za kutosha na wala sijaitumia muda mrefu. Nikaiweka pembeni kisha nikatoa suruali yangu ya jinzi nikaiweka pembeni, nikiwa katika hatua hizo nikasikia mlango ukigongwa, kwa haraka nikaichukua basola yangu na kuirudisha ndani ya begi na kwa mwendo wa taratibu nikaelekea mlangoni na kuufungua.
“Kaka Dany daktari amesha fika”
“Nakuja”
Nikaufunga mlango mara baada ya Yudia kumaliza kunipatia ujumbe wake, nikalifunga begi vizuri na kutoka chumbani kwangu nikakutana na daktari ambaye mama alizungumza naye muda mchache ulio pita, nikamsalimia kutokna ni mzee wa makamo ya kina mama.
“Muheshimiwa yupo wapi?”
“Amejipumzisha mama, unaweza ukaanza kunihudumia tu”
“Ok sawa ninakuomba nione kidonda chako”
Taratibu nikavua shati na kumuonyesha daktari Kidonda hicho.
“Kimeanza kukauka”
Alizungumza, huku akikigusa gusa kwa juu. Akafungua kiji begi chake kidogo cha mkononi, akatoa kichupa kidogo pamoja na bomba la sindano lililo jipya kabisa.
“Nitakuchoma sindano ya kukikausha ndani ya siku mbili hizi kitakuwa kimepona kabisa”
“Ina maana na ngozi yake itarudi kama kawaida?”
“Hapana ngozi itarudi taratibu taratibu”
“Sawa”
Akachukua pamba na kuipaka dawa ya kusafishia, kwenye mshipa wa mkono wa kushoto. Alipo maliza kufanya hivyo akanichoma sindano hiyo yenye dawa ambayo nilisha wahi kuchomwa hospitalini juzi.
“Kijana unaonekana unafanya sana mazoezi”
“Kwa nini?”
“Mishipa yako imejitokeza kiurahisi ni tofauti sana na watu wengine mishipa yao kujitokeza ni kazi sana”
“Ahaaa, huwa na fanya sana mazoezi”
Daktari akachomoa sindano yake baada ya kuisukuma damu taratibu. Akanipatia pamba iliyo na dawa nikajiziba nayo katika eneo ambalo amenichoma sindano.
“Kesho asubuhi ukija Hospitalini kwangu nitakuchoma nyingine ya kumalizia”
“Sawa sawa hospitali yako ipo eneo gani?”
“Barabara ya pili pale”
“Ahaa ok asante”
Nikamuga daktari huyo na kuingia chumbani kwangu, nikafungua begi langu na kuitoa bastola kisha nikavua pensi na kuvaa jinzi, sikuona haja ya kulivua shati nililo livaa. Nikaichomeka bastola yangu kiunoni kwa nyuma na kutoka chumbani kwangu. Nikaingia jikoni kwa ajili ya kunywa maji kabla sijaanza upelelezi wangu wa kuifwatilia nyumba ya meya ambaye mama anamtilia mashaka.
Nikiwa hapo simu ya Yudia ikaingia mesiji, mwenyewe hakuwepo nikaona bora niichukue na ili kuifungua meseji hiyo niliyo hisi labda ni mtu ambaye ni bwana wake.
(Mambo yameharibika, kaeni kwa tahadhari mjulisheni na meya)
Meseji hiyo ameituma Yudia kwenda kwa mtu huyo aliye jibu ‘SAWA’. Nilijikuta nikianza kupata mashaka makubwa, kwa haraka nikaituma namba ya mtumaji wa meseji hiyo kwenye simu yangu, nilipo hakikisha kwamba nimemaliza kuituma. Nikaifuta meseji yake aliyo tuma na niliyo jitumia na simu ya Yudia nikairudisha sehemu nilipo itoa, nikatoka jikoni humo nikiwa nimejikausha na nikamkuta Yudia akingia kwenye mlango wa sebleni akitokea nje.
“Kuwa makini na mama”
“Sawa”
Nikataka kutoka ila ikanibidi kuelekea chumbani kwa mama. Nikagonga mlango wake, kwa sauti ya unyonge akaniruhusu kuingia. Nikaingia na kumkuta akiwa amelala kitandani amejikunyata huku akitazama makatuni kwenye Tv kubwa iliyopo ukutani mwake.
“Unajisikia kutoka leo mama”
“Hapana Dany, kichwa changu hakipo sawa”
“Basi nakuomba tuweze kutoka”
“Dany”
“Mama tafadhaki nakuomba tuweze kutoka, tazama kukaa kwako kwa huzuni kisukari inaweza kupanda”
Mama akanitazama kwa macho ya uchovu, kishwa kwa msaada wangu nikamnyanyua kitandani na kukaa kitako. Akashusha pumzi kidogo kisha akashusha miguu yake kitandani.
“Unataka twende wapi?”
“Sehemu yoyote japo kupunga upepo”
“Mmm”
“Ndio, jiandae basi”
“Sawa nipe dakika kumi”
“Poa”
Nikatoka chumbani kwake na kwenda kumsubiri sebeleni ila nikiwa kwenye kordo ambapo unaweza kuona mtu aliyopo jikoni nikamuona Yudia akikata simu baada ya kuhisi uwepo wangu na kujifanya yupo bize anaendelea na kazi zake. Sikutaka kumuonyesha labda kuna kitu ambacho nimesha kitilia mashaka juu yake. Nikapita zangu na kukaa jikoni huku nitoa simu yangu na kujaribu kukagua majina ya marafiki zangu. Nikaona jina la Joseph, rafiki yangu ninaye fanya naye kazi moja ila yupo kwenye kitengo cha mawasiliano ndani ya ikulu. Nikampigia namba yake iliyo anza kuita taratibu kisha ikapolewa.
“Dany Dany babaa niambie”
“Safi mwanangu, lete habari”
“Daaa safi kaka, nasikia upo likizo hata kupeana shavu?”
“Ndugu yangu shavu la wiki moja”
“Ahaaa wiki moja mbona ndefu sana”
“Yenyewe imekuja kimazabe zabe sikutegemea kabisa”
“Wacha wee”
“Sasa ndugu kuna meseji nitakutumia hapa, naomba unisaidie”
“Poa poa, ila Dany ukirudi nijie na wale samaki wadogo wadogo ulio kuja nao kipindi kile”
“Uono?”
“Ewalaaaa hao hao uwono”
“Poa nitakujia nao”
“Sawa ndugu yangu”
Nikakata simu na kumtumia Joseph namba niliyo ichukua kwenye simu ya Yudia, anisaidie kupata habari ya mtu huyo aliye tumiwa meseji ile. Sikukaa sana sebleni mama akatoka chumbani kwake akiwa amevalia vitenge vyake.
“Yudia pika wali leo”
“Sawa mama ndio ninapika”
“Ok sisi tunatoka uwe makini na getini, hakikisha haingii mtu”
“Sawa mama”
Tukatoka ndani, mama akanikadhidhi funguo ya gari, Yudia akatoka na kutufungulia geti. Tukaondoka taratibu katika eneo la nyumabi kwetu huku ukimya ukiwa umetawala.
“Mama Yudia umemtolea wapi?”
“Kwa nini?”
“Nakuuliza tu”
“Umesha anza tabia yako ya kuwatamani wadada wa kazi eheee”
“Hapana mama nia yangu sio hiyo”
“Kama sio hiyo kwa nini unamuulizia”
Sikutaka kumueleza mama juu ya kitu ninacho kihisi kwa Yudia, kwa maana ana onekana kumuamini sana msichana huyu.
“Hamna”
“Uache tabia yako, usije ukacheza cheza na watoto wa watu”
“Sawa mama”
Moja kwa moja tukaeleka kwenye hoteli ya Tanga beach Resort. Tukaa sehemu ya mapumziko, nikaagizia vinjwaji pamoja chakula kwa maana ninatambua mama hajapata chakula cha mchana.
Nikiwa katika harakati za kuanza kula, simu yangu ikaanza kuita nikaitoa simu yangu mfukoni na kukuta ni Joseph ndio anapika, nikaipokea na kuiweka sikioni.
“Jose”
“Naam kaka”
“Nipe ripoti”
“Ebwana huyu mtu uliye niambia niweze kumtafuta anatokea katika kikosi cha Al-Shabab na kwa sasa yupo hapo mkoani Tanga”
Maneno ya Joseph yakanifanya nisimame kwenye kiti na kuanza kutembea kusogea pembeni ili nizungumze vizuri na Joseph.
“Unasema Al-Shabab?”
“Ndio tena huyo ni mpelelezi wa Al-Shabab. Kwani kuna kitu gani kilicho tokea”
Nikamtazama mama alipo kaa kwenye kiti akiendelea kula, akanitazama nikatabasamu na sikuonyesha sura yoyote ya wasiwasi. Mama naye akatabasamu na kuendelea kula.
“Kuna ishu imetokea nyumbani kwa bi mkubwa. Kuna nyaraka zimeibiwa na ni muhimu sana, si unajua Magu kesho kutwa anakuja Tanga?”
“Ndio nalitambua hilo na makachero wamesha tumwa tangu majuzi”
“Sasa wanalitambua juu ya hawa makachero wa Al-Shabab?”
“Hapana wewe ndio wa kwanza kulitambua hili, hata mimi nimeshangaa sana”
“Ok poa nitumie picha yake, na full detail zake”
“Poa dakika moja”
“Na usimuambie yoyote, hapa nahisi kuna mtandao mkubwa wa viongozi wanajihusisha na watu hawa”
“Sawa kaka”
Nikakata simu na kurudi kwenye kiti. Mama akala kipande cha kuku licho kuwa amekishika mkononi, alipo kitafuna na kukimeza, akaniuliza swali.
“Yaani hadi sasa hivi unaogopa kuzungumza na wakwe zangu mbele yangu?”
“Ahaa mama mimi sina mchumba”
“Wewe Dany ninaye kujua, labda si mimi. Kesi za kipindi upo sekondari, una tembea na vijisichana vya watu unahisi sizikumbuki?”
Ikanibidi kutabasamu tu kwa maana mama amesha wahi kunifumania sana na wasichana kipindi cha uvulana wangu, na anatambua kwamba mwanaye nina nyote ya kupendwa na mabinti.
“Mama nikuulize kitu tena”
“Niulize”
“Yudia umemjuaje juaje?”
“Mmmmm, ameniletea rafiki yangu mmoja hivi amemtoa huko Lushoto”
“Ahaaa huyo rafiki yako ni nani?”
“Ninafanya naye kazi hapo Jiji”
“Ok, na je anasema Yudia ametokea katika family gani?”
“Baba yake na mama yake ni wakulima wa nyanya na viazi. Amefeli form four amekuja nyumbani kwangu basi ananisaidia kufanya fanya kazi”
“Ok, na ana muda gani pale nyumbani?”
“Kama miezi mitatu, huu unakwenda mwezi wa nne”
“Tangu aje nyumbani mgogoro wa wewe na huyo meye ulisha anza?”
“Yaaa ulisha anza. Mbona unaniuliza maswali mengi hivyo kuna kitu gani kinacho endelea?”
“Ni mapema sana kukizungumza kwa leo ila nitakuhitaji usirudi nyumbani leo hadi nizipate hizo nyaraka”
“Dany”
“Ndio mama hakuna usalama kabisa pale nyumbani, kuanzi hadi hapa ninapo zungumza, itabidi ubaki hapa hotelini hadi nitakapo pata nyaraka”
Nikaanza kumuona mama jinsi alivyo jawa na woga, kiasi kwamba hata kula akaacha kabisa. Akashusha pumzi huku akinitazama wakati huu, aliweza kunielewa kabisa kwamba kitu ninacho kizungumza kinatakiwa kwenda kama nilivyo sema.
“Na yule mtoto wa watu atabaki peke yake pale nyumbani?”
“Muache abaki peke yake ni mtu mzima anaweza kujilinda”
“Ila Dany kama kuna kitu kibaya kinacho endelea ni vyema ukanieleza”
Kabla sijamjibu mama kitu chochote macho yangu, yakawa yanamuangalia muhudumu wa kiume anaye kuja eneo nililo kaa na mama, huku mama akiwa amempa mgongo muhudumu huyo aliye beba sahani pana huku juu yake ina chupa ya whyne pamoja na glasi mbili na chini ya sahani hiyo kuna kitaulo kidogo cha kufutia mezani, ila ndani ya kitaulo kwa umakini sana nikaona bastola, iliyo fungwa kiwambo cha kuzuia risasi, kikiwa kimefungwa. Pasipo kusubiria aweze kutekeleza lengo ambalo linamleta mezani kwetu nikachomoa bastola yangu kiunoni na kumpiga risasi mbili za miguuni na kumfanya anguke, huku chupa, sahani, glasi na bastola yake vikiangukia pembeni. Ila mlio wa risasi bastola yangu ambayo sijaifunga kiwambo cha kuzuia sauti, ukawafanya watu walio kuwepo katika eneo hilo kutawanyika kwa woga, huku mama akiwa ameshikwa na bumbuazi akinitolea macho.
ITAENDELEA
Thursday, May 9, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Write comments