Pages

Wednesday, May 22, 2019

AISIIIII……….U KILL ME 28........ ONLY 18+

ILIPOISHIA
“Jamani nisameheni, nimefanya yote kwa ajili ya familia yangu. Yote nimefanya kwa ajili ya mke wangu na mwangu aliyopo tumboni”
Lukas alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Akataka kunyanyuka nikamrudisha chini kwa kumpiga teke la kifuani, kitu kilicho mstua sana Latifa.
“Dany stopppppp. Huyu ni agent mwenzako”
“Lakini hawezi kufanya usaliti hata kama ni swala la familia”
“Mbona mimi umenishirikisha kwenye swala la nyaraka za mama yako, umeona uzito uliopo hapo kati ya kazi na familia?”
Latifa alizungumza kwa ukali jambo lililo nifanya nikae kimya huku ninamtazama kwa macho ya mshangao. Katika kuzubaa kwetu kwa haraka Lukas akasimama na kumpiga kabali Latifa na kumpokonya bastola yake na kumuwekea ya kichwa huku akinitazama na kutabasamu kwa dharau.

ENDELEA
“Luka…..”
Latifa alijaribu kupiga kelele ila Luka akamuongezea kumkaba shingo yake kwa mkono, huku bastola akiendelea kuiweka vizuri karibu kabisa na kichwa cha Latifa.
“Nyamaza wewe malaya”
“Luka hembu tulia kwanza tuyazungumze”
“Nyamaza na wewe kenge nini. Unahisi ulivyo kuwa unanitandika mangumi hapa nilikuwa siumii”
“Nalijua hilo?”
“Sasa nahitaji muniache niondoke, ukifanya chochote ninamuua Latifa hata kama ni rafiki yangu”
“Sawa sisi tunakuacha uendee, naomba umuachie Latifa kwanza”
“Noo siwezi kufanya ujinga wa aina hiyo”
Luka alizungumza huku taratibu akirudi nyuma nyuma huku akimburuta Latifa, anaye endelea kuushikilai mkono wa Luka usizidi kumkaba zaidi na zaidi.
Luka akakaribia karibu na ukuta ambao alikuwa amekusudia kuupanda hapo awali, akamsukumia Latifa kwangu, nikawahi kumdaka asianguke chini. Nikamshuhudia Luka akipanda ukuta huo na kuangukia upande wa pili na nikiasikia vishindo vyake vya kukimbia kuelekea anapo pajua yeye.
“Dany”
Latifa aliita kwa sauti ya chini huku akijiweka vizuri koo lake lililo kumbana na maswaibu ya kukabwa sana.
“Ina maana Luka ni msaliti kweli?”
“Kama ulivyo weza kuona”
“POLISIIII”
Tulisikia sauti kutokea getini, ikatubidi kugeuka kwa haraka, tukakutana na kundi kubwa la polisi, wapatao sita, huku mmoja wa polisi hao niliweza kumkumbuka kwa haraka ni yule polisi niliye weza kuonana naye nyumbani majira ya asubuhi.
“Mikono juu”
Mmoja alitoa sauti hiyo tukatii mimi na Latifa, kila askari aliweza kutunyooshea bunduki yake, kila mmoja akaonekana kushangaa mauaji yaliyo tendeka eneo hili kwa maana kumetapakaa maiti nyingi kila sehemu.
Askari hao wakatufwata na kutufunga pingu za mikono huku mikono yetu wakiwa wameirudisha kwa nyuma.
“Ninaomba nitoe kitambulisho changu”
Latifa alizungumza huku akiminyana na askari wa kiume aliye mshika mkono.
“Hakuna haja ya kitambulisho hapa, maelezo yote mutakwenda kuyatoa kituoni”
“Niachieni nyinyi, munajua mimi ni nani?”
“Hilo hatutaki kulijua tena kaa kimya, ukileta za kuongea ongea, tutakutandika makofi mtapisho sasa hivi”
Askari huyo aliendelea kuzungumza kwa kujiamini, askari wa kike ambaye nilikutana naye asubuhi akabaki akiendelea kunitazama pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote. Wakatutoa nje ya geti ya nyumba hii. Tukakuta wananchi wengi pamoja na waandishi wa habari wakiwa wamekushanyika wakishangaa tukio hili huku waandishi wa habari kazi yao ikiwa ni kupiga picha.
“Hamujui munadili na watu wa aina gani”
Nilimuambia askari aliye pembeni yangu huku akiwa na bunduki.
“Huo ni ujinga ambao sitaki kuusikia”
“Ahaaaa ehee”
Askari wa kike naye alitembea pembeni yangu huku kwa umakini akiwa anajaribu kutaka kuzungumza jambo ila anashindwa kuzungumza. Wakaniingiza kwenye gari aina ya defender, huku Latida naye akiingizwa katika gari nyingie. Katika defender hii wakaingia askari wanne akiwemo na askari wa kike yule ninaye fahamiana naye kwa kuonana. Akaka mbele yangu huku wazake wengine wakiwa wamesimama katika sehemu ya kuingilia, huku mitutu yao ya bunduki wakiwa wamishikilia vizuri.
Gari ya aliyo ingizwa Latifa taratibu ikaanza kuondoka cha kushangaza ikaeleka upande tofauti na upande ambao ninaelekea mimi. Askari huyu wa kike akanikonyeza kwa umakini mkubwa, hapa ndipo nikaanza kugundua ishara za askari huyo kwa mana ishara anazo anza kunionyesha ni ishara za kipelekezi ambazo si rahisi kwa askari polisi kuweza kuzifahamu. Ishara moja tuliyo zungumza kwa macho pasipo askari kugundua, ni kuutumia mguu wangu wa kulia. Nikaelewa ni nini anacho kimaanisha. Nikaupeleka mguu wangu wa kulia katikati ya mapaja yake na kugusa sehemu za siri. Kitendo hicho kikamkasirisha askari huyu wa kike, aliye ninasa kofi tizo hadi wezake wakashangaa.
“Mpumbau wewe unaidhalilisha kwa kunikanyaga sehemu zangu za siri ehee”
Alizungumza huku hasira ikizidi kumpanda, akaninasa ngumi nyingine nzito za kifua
“Afande Judith muache bwana”
“Awezi kunidhalilisha mimi nikamuacha hivi hivi”
Akanirukia na kunilaza chini, akaanza kunitandika makofi mfululizo huku askari wezake wakabaki wakiwa wamesimama, huku gari ikizidi kwenda kwa mwendo kasi, kutokana mikono yangu imefungwa pingu kwa nyuma sikuwa mnjanja wa kufanya chochote.
Afande Judithi, akanipiga kichwa cha pua na kunifanya nipanue mdomo, sikuamini nilipo muona akinitemea funguo ndogo ya pingu niliyo iwahi kuibana chini ya ulimi kabla sijaimeza. Akasimama na kunikalisha kitako huku nikivujwa damu.
“Pumbavu, huwa napenda waseng* kama nyinyi niwashuhulikie”
Afande Judithi alizungumza huku akihema, akanipa ishara moja ambayo nikaitekeleza ndani ya sekunde mbili kama si tatu. Nilijibenua kwa haraka na mikono yangu nikaileta mbele, ni jambo rahisi sana kwa mfanya mazoezi kufanya hivyo. Askari wakaanza kuchachawa huku akigeuza vitako vya bunduki zao wakitaka kunipiga navyo ila wakawa wamechelewa tena sana, kwani niliweza kujifungua pigu hizo kwa funguo aliyo nipatia afande Judithi.
Askari aliye shusha kitako chake cha bunduki ili anipige, nikakinyaka kwa haraka kisha nikampiga teke moja ala sehemu za siri lililo mfanya aiachia buduki yake hiyo aliyo kusudia kunipiga nayo. Nikaanza kuwashuhulikia askari hawa watatu wa kiume, nikashangaa kumuona afande Judithi akinisaidia kufanya hili. Askari aliyopo mbele anaye endesha gari alipo ona misukosuko na vishindo vilivyopo nyuma akafunga breki za gari. Kitendo cha askari huyo kuufungua mlango, akakutana na teke zito kutoka kwa afande Judithi aliye shuka pasipo hata kujua ameshukaje. Nikasikia askari huyo ambaye ni dereva akigugumia kwa maumivu makali. Askari wote watatu nikawa nimewaweka chini ya ulinzi mkali, hakuna askari aliye weza kufuruka hata mmoja, kila mmoja akawa na akaiz ya kuugulia maumivu yake. Kwa bahati nzuri eneo tulilo tulilopo hakuna watu wengi kwa mama ni moja ya njia ambayo pembeni kuna majumba ya kifahari na nimitaa iliyo tulia kabisa.
Nikashuka kwenye gari hili na kuanza kuwashusha askari hawa, kila mmoja nikamfunga pingu yake, na kuwaweka pembeni ya barabara. Afande Judith akamshusha askari huyu ambaye ni dereva akiwa amelegea sikujua hata amempiga kipigo cha aina gani kwa mana amelegea hata kusimama hawezi.
“Wapapase kaam wana simu za mawasiliano”
Afande Judith aliniagiza na kujikuta nikitii, nikaanza kumkagua mmoja baada ya mwengine, mmoja nikamkuta na simu ya thamani aina ya iphone six, huku mwengine akiwa na kijisimu aina ya nokia vyenye jina maarufu la Nokia Obama.
Nilipo hakikisha kwamba hakuna ambaye ana simu, bunduki zao nikazichukua na kuingia nazo upande wa dereva ambapo Afande Judith yupo ananisubiria. Afande Judithi akaliondoa gari kwa mwendo wa kasi huku akiwa kimya, akatatoa kitambaa cheupe kwenye mfuko wa suruali yeka ya kiaskari alio ivaa na kunikabidhi.
“Kifute damu”
Nikafanya hivyo kwa mana kuna michuruzo ya damu inanitoka puani mwangu.
“Pole sana kwa kuweza kukufanyia kile nilicho kufanyia kwenye gari”
“Asante ila ni kwa nini ulifanya vile?”
“Ahaa, jina langu alisi ninaitwa Babyanka Martin, ni mlinzi wa siri wa raisi. Mwenzi mmoja kabla alinituma kuja kuandaa dhiara yake na kuniingiza katika kikosi cha jeshi la polisi kwa jina la Judithi Ndauka”
“I…iii ina maana unafahamu kitu gani kinacho endelea?”
“Ndio natambua mpango wako mzima kwa maana raisi aliniagiza leo kuweza kukufwatilia na nilisha mpa ripoti kwamba wewe ni mtu safi na unaifanya kazi kama vile inavyo paswa”
“Ahaa sasa unafahamu raisi anakuja kwa njia gani?”
“Kama aliweza kunipa taarifa zako, basi tambua kwamba natambua kwamba anakuja kwa njia gani. Hato kuja kupitia njia ambayo wewe unaizungumzi, kwa mana yule aliye kamatwa naye ni miongoni mwa wavujisha siri”
“Nani, Latifa?”
“Ndio wale askari nao pia ni miongoni mwao, pale anapelekwa kwa mkuu wa mkoa kwenda kuzungumza kile kitu kinacho endelea. Nilisha wasiliana na raisi, atakuja kupitia njia ya helcoptar na tutakwenda kumpokea majira ya saa nane usiku katika eneo la Maranzara, lipo Pogwe kwenye moja ya kiwanja cha siri sana. Hapo ninapafahamu basi itatupasa saa saba kamili tuwepo pale”
“Sawa, sasa huoni kama itakuwa ni hatari kama tukitumia gari la polisi.”
“Hatuto tumia gari la posili, ninakupeleka nyumbani kwako, kuna mtu tayari amesha lichukua gari lako na kulipeleka kwa mbunge muheshimiwa Eddy”
“Umejuaje kama nimelichukua gari hilo kwa muheshimiwa Eddy?”
“Ndio maana nilikueleza hapo awali kwamba nilianza kukufwatilia siku nzima na ratiba na mizunguko yako yote niliweza kuifahamu”
“Mungu wangu…..?”
“Nini?”
“Kuna zile nyaraka zipo katika eneo lile tukio”
“Ahaa hizo nyaraka kwa sasa hazina umuhimu kwa sana kwa mana maamuzi yatatoka moja kwa moja kwa raisi”
“Mmmmm”
“Yaa”
“Sasa nikuite Babyanka au nikuite afande Judithi?”
“Ni vyema sana kama ukiniita afande Judithi, jina langu halisi huwa mara nyingi sipendi liweze kujulikana kwa watu”
“Sawa, naitwa Dany”
“Nashukuru kukufahamu, japo tayari nilisha weza kulifahamu jina lako”
Tukafika katika eneo la raskazoni kwenye moja ya nyumba ambayo imejitenga mbali sana na sehemu zilipo nyumba nyingine. Afande Judithi akashuka kwenye gari, akatembea kwa hatua za haraka hadi kwenye geti, akafungua na kuniomba niingize gari hilo ikanibidi kuhamia upande wa siti ya dereva. Taratibu nikaliingiza gari hilo katika eneo la nyumba hii nak umuacha Afande Judithi anafunga geti. Alipo maliza akatembea kwa mwendo wake wa haraka hadi sehemu nilipo simama.
“Karibu”
Alizungumza huku akitangulia mbele, akafungua mlango wa kuingilia ndani humo kwa kutumia namba za siri, ambazo ameminya minya kwenye batani nyingi zilizopo katika mlango huu. Mlango ukafunguka na sote tukaingia ndani, akawasha taa, hapo ndipo nilipo weza kupata fursa ya kuweza kuona kila kitu kilichopo hapa sebleni.
Haikuwa seble kama nilivyo jua mimi, ila ni sehemu yenye mitambo ya mawasiliano makubwa. Afande Judithi akawasha moja ya computer yenye kiooo kikubwa kiasi, akaanza kuminya minya batani za copture hiyo kwa kasi ya ajabu sana kisha akasimama mbele yake, hazikupita sekunde tano nikaona video ya raisi akiwa amesimama eneo hilo akiwa ndani yake.
“Muheshimiwa kijana Dany nimesha kutana naye”
“Upo naye hapo?”
“Ndio”
Afande Judithi akaniita kwa ishara nikasimama pemebeni yake.
“Asante sana kijana kwa kuweza kufanya kazi yako kwa uaminifu mkubwa sana”
“Asante muheshimiwa”
“Kama alivyo kueleza Babyanka, leo nitatumia njia hiyo, ila kesho kwenye msafara atakuwepo raisi huyu”
Akasimama mtu mwengine ambaye ametengenezewa sura kama raisi, akasimama pembeni ya raisi. Kusema kweli hakuna utofauti wowote na raisi, raisi huyo feki akasogea pembeni na kumuacha raisi aendelea kuzungumza na sisi.
“Ratiba ya viongozi wote ambao si waadilifu wa serikali yangu, nimeweza kuipata nawaahidi nikija huko nitahakikisha kwamba wote wanaweza kutumikia kile ambacho wamekipanda kwa muda mrefu”
“Sawa muheshimiwa”
“Tutaonana baadaya, na kuanzia sasa Babyanka, atakupatia mawasiliano ya kuwasiliana nami moja kwa moja”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Afande Judithi akazima computer hiyo kisha akanigeukia.
“Unatakiwa sasa ukaoge na kukupa vitendea kazi vyako. Njoo nikuonyeshe bafuni”
Nikaongozana na afande Judithi hadi katika bafu, akanionyesha kisha akatoka, taratibu nikaanza kuvua koti la suti kisha shati. Nikavua viatu pamoja na shati kisha nikasimama mbele ya kioo huku nikijitazama majeraha niliyo yapata usoni mwangu. Nikiwa nimesimama mbele ya kioo nikaona mlango wa bafu ukifunguliwa ikanibidi kugeuka na kumuona Banyanka akiingia bafuni hapa akiwa amevalia chupi na siridia, kwa jinsi umbo lake lilivyo la kirembo nikabaki nimeduwaa.
“Tuoge wote”
Babyanka alizungumza na kunifanya nibaki nikiwa nimekaa kimya nisijue nini cha kufanya, huku jogoo wangu akianza kuleta fujo za kutaka kusimama taratibu.
ITAENDELEA

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +