Pages

Friday, May 24, 2019

AISIIIII……….U KILL ME 31....... ONLY 18+

ILIPOISHIA
“Sawa mkuu”
Daktari akaongoza nyia, tukafika hadi kwenye chumba ambacho ndipo madkatari wote wanapotakiwa kufika kazini asubuhi wanasaini na pale wanapo toka wana saidi. Raisi akaanza kuligagua daftari hilo, nikaona akitingisha kichwa tu.
“Naombeni koti na mimi leo niwe daktari nikaaa humu kuangali jinsi wanavyo kuja, nyinyi nilindeni kwa nje”
“Sawa mkuu”
Raisi akapewa koti la kidaktari kisha sisi tukatoka nnje ya chumba hichi kuendelea kuimarisha ulinzi. Muda wa kufika ofisini kwa mfanyakazi wa serikali mwisho ni saa moja na nusu tena kwa wale wa mbali ila hadi inafika saa mbili asubuhi hakuna hata mmoja aliye fika, jambo lililo nifanya niwaze sijui ni kitu gani watakacho fanywa na raisi hawa madaktari.

ENDELEA
Tukaanza kuona makundi makundi ya madakatari wakija huku wakitembea kwa mwnedo wa taratibu wakipiga stori kama vile wanakwenda harusini. Hapakuwa NA Daktari aliye weza kustukia ni kitu gani ambacho kinaendelea kwa wakati huu. Hadi wanaingia ofisini humo, ndipo hapo wengine wakagundua kwamba vibarua vyao vipo hatiani kufutwa. Madaktari na manesi si chini ya thelathini wote wamekuja nje ya muda wa kufika ofisini kama mfanyakazi wa uma.
Kutokana na wingi wa wafanyakazi hao hatukucheza mbali na raisi, ambaye amewaitisha kikao cha dharura ndani ya ofisi hiyo hiyo japo wote wamesimama.
“Nasemea kuanzia sasa hivi ninavyo zungumza, kazi hamuna”
Sura za manesi na madaktari zikabadilika kila mmoja aliweza kuweka pozi lake, mwenye machozi kumlenga lenga, yalimlenga lenga. Mwenye machozi kumtoka yakamtoka.
“Nyinyi munakuja kazini kama hospitali hii ni ya baba zenu na mama zenu. Daktari mkuu hapa ni nani?”
Mzee mmoja mweusi na mfupi akanyoosha mkono wa kulia.
“Hii hospitali kila mwaka inapata ruzuku ya kiasi gani kutoka serikali kuu?”
“Bilioni tano mkuu”
“Bilioni tano hizo zinatumika katika kufanya nini?”
“Kupaka rangi majengo na…..naa…..naaaaa…..”
Daktari huyo akapatwa na kigugumizi kizito cha kujibu dhairi hawa wanaonekana ndio walaji wa pesa za serikali.
“Hembu huyu muwekeni ndani akajibu hili swala takukuru”
Mlinzi aliyekuja na raisi akamtoa daktari huyo na kumpeleka kwneye magari tulio kuja nayo. Raisi akatoa simu yake na kupiga namba anazo zijua yeye.
“Ndio muheshimiwa raisi”
Kila mmoja aliweza kuisikia sauti hiyo kwa manaa raisi ameweka simu yake, loud speaker.
“Una madaktari wangapi wanao ingia makazini wiki hii?”
“Zaidi ya elfu moja mia mbili”
“Hembu niletee madaktari mia moja hospitali ya Bombo hapa Tanga, hadi kesho sijamaliza ziara yangu hapa Tanga wawe wamesha fika”
“Sawa mkuu”
Raisi akakata simu na kuirudisha mfukoni mwake. Akawatazama madaktari hawa na wauguzi kwa macho ya ukali.
“Unajua munapo pewa dhamani na serikali ya kuahudumia watu wake basi musilete longolongo. Saa tatu nyinyi ndio munafika kazini kweli, mimi tangu saa kumi na moja nipo hapa. Nimekuta hospitali ovyo ovyo, ifike kipindi watanzania muelewe kwamba Hapa ni kazi tu na si kuishi kimazoea kama mulivyo kuwa mumezoea kuishi kimazoea”
Raisi baada ya kuzungumza hivyoa katokaka na sisi walinzi wake tukamfwata kwa nyuma. Mojo kwa moja tukaelekea naye kwenye gari zetu, nikamfungulia mlango, akapanda nikaingia upande wa dereva na kuondoka eneo la hospitali huku tukiacha watu ambao wamemuona raisi kila mmoja akiwa anazungumza lake.
“Nipelekeni soko la Ngamiani”
“Sawa muheshimwa”
Simu ya muheshimiwa ikaita, akaitoa mfukoni, akaipokea na kuiweka sikioni mwake.
“Ok”
“Nyinyi tu nendeni kwenye uwanja wa hapo Mkwakwani”
“Hawawezi kukujua, mimi naendeleza ziara yangu”
“Ulinzi uzidi kuimarishwa”
“Ok”
Raisi akakata simu, tukaelekea moja kwa moja kwenye soko la Ngamiani, mazingira ambayo tumekutana nayo hayakunistajabisha sana kwa maana ninalifahamu soko hili kwa uchafu. Wafanya biashara wakabaki wakiwa wamejawa na kigugumizi kwa maana wanatambua raisi yupo katika uwanja wa Mkwakwani kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ila wanamuona huku sokoni muda huu.
“Habari zenu?”
“Salama muheshimiwa”
“Naona bishara zinakwenda?”
“Zinakwendaje muheshimiwa, wakati watoza ushuru wakatoza bei kubwa kila siku bei inapanda”
Mfanya bishara mmoja alizungumza kwa sauti ya uchungu iliyo jaa gadhabu.
“Ehee, wanawatuza shilingi ngapi?”
“Muheshimiwa imtoka shilingi mia mbili hadi mia tano kwa kila kichwa kwenye hili soko”
“Na mbona mazingira ni machafu?”
“Ndio hapo sasa muheshimiwa, manispaa wanatunyanyasa sana, kwanza hawaji kufanya usafi, pili wanadai ushuru unapanda kwa ajili ya kodi unayo sema muheshimiwa”
Wafanya bishara hao wakatoa malalamiko yao kila mmoja kwa wakati wake, raisi hakusita kuyaandika malalamiko hayo kwenye kijikitabu chake cha kumbukumbu. Akawaaga wafanya bishara na tukaondoka katika soko hili.
“Hii Tanzania bwana, kiongozi wa juu anamuambukiza kiongozi wa chini madudu, huku nao wa chini wanafanya utumbo, ila mwaka huu watanijua mimi vizuri”
Raisi alizungumza huku tukiwa ndani ya gari, tukielekea kwenye gereza la Maweni. Ni ngumu sana kwa mtu kuweza kutambua kwamba raisi tupo naye sisi kwenye hizi gari mbili, huku gari la baba mkubwa, likitufwata kwa nyuma. Tukafika kwenye gereza la Maweni huku tukiwa na daktari mkuu. Akashuka mlinzi wa niliye kuwa naye ndani ya hili gari, akamfwata askari aliye simama kwenye nje ya kibanda kilichopo hapa getini cha kuingilia eneo la gereza hili. Akazungumza naye maneno mawili matatu, geti likafunguliwa, gari zetu zikaingia. Moja kwa moja tukaeleka katika ofisi ya mkuu wa gereza, kwa bahati nzuri tukamkuta.
Alipo muona rahisi, wasiwasi mwingi uliweza kumjaa, raisi akaachia tabasamu pana na kumsalimia mzee huyu aliye valia nguo za askari magareza.
“Mzee mbona una wasiwasi?”
“Kusema kweli muheshimiwa sijategemuea kama unaweza kuja eneo hili”
“Unaogopa?”
“Aaha hapana”
“Nahitaji kuonana na wafungwa wote nao nataka kusikia maoni yao”
“Sawa”
Mkuu wa gereza akatoa amri kwa kijana wake, aende akaandae mazingira ya raisi kuweza kuoana na raisi.
“Twende tu, hakuna haja ya kuandaa mazingira nahitaji kuona jinsi wafungwa wanavyo ishi”
Ikabidi kijana huyo ambaye nayepia ni askari magareza kusitisha safari yake hiyo ya kwenda kuandaa mazingira mazuri ila hata raisi akienda asione mabadiliko. Tukafika kwenye moja ya uwanja ambo ni maalumu kwa mazoezi ila kitu tulicho kikuta kila mmoja alishangaa, ikatubidi sote wanne kuweza kuchomoa bastola zetu na kuziweka tayari kwa lolote litakao tokea. Kwanza uwanja huu umelowana kwa maji mengi yaliyo sababisha tope jingi. Wafungwa zaidi ya mia moja, wanapigishwa mazoezi makali huku wakiwa na vijibukta tu, sura zoa wala huwezi kuziona vizuri kwa kujaa damu kwani askari gereza wanawapiga kwa vitako vya bunduki wale ambao wanaleta ubishi katika kutekeleza kile ambacho askari hao wamekiamrisha.
Raisi akamtazama mkuu huyu wa gereza ambaye mwili mzima unamtetemeka kwa woga kwa maana mafunzo wanayo yatoa hapa ni mafunzo ya kijeshi, ina maana kuna mpango mkubwa unao fanywa na wakuu hawa wa gereza kupitia wafunga hawa ambao hawawathamini kama binadamu.
“Hivi ni macho yangu au nina ota?”
Raisi alizungumza huku akiendelea kutazama wafungwa hao jinsi wanavyo pewa mazoezi makali, ata askari wanao fanyisha mazoezi hayo hawakuweza kujua ni kitu gani kinacho endela, wao kwa sifa wakazidi kuwashushia kipigo wafungwa hawa.
“Wanafanya mazoezi kwa ajili ya nini?”
“Ahaa….mu…mu….heshiii miwaaa. Unajuaa nini?”
“Nini?”
“Nchi hii kidogo ulinzi umeyumba yumba na sisi tunaandaa vijana wetu wame wakakamavu”
“Wakakamavu wafungwa, wamekuja huku muwafundishe maisha bora ya kuja kuishi uraiani, nyinyi mutafundisha waje kuwa majambazi. Amrisha watu wako kuacha zoezi hili mara moja”
Hapo ndipo nikamuona raisi akiwa amezungumza kwa kukasirika, huku akiiweka weka vizuri miwani yake sawa. Mzee huyo hata sauti haikumtoka, ikambidi kijana wake kumsaidia kutoa sauti ya ukali iyo wafanya askari magereza hao kuacha kile wanacho kuifanya. Wafungwa hawa miili yao imezohofika kwa njaa na mateso wanayo yapata. Askari magereza walio kuwa wanendesha mazoezi hayo walipo gundua kwamba raisi yupo hapa waliishiwa pozi kabisa kila mmoja alijihisi anavyo jisikia yeye.
“Nani ametoa hili agizo la kuwafundisha mazoezi ya kijeshi?”
“Ahaaa muhe…..”
“Sitaki kusikia muheshimiwa, ni nani ametoa agizo hili”
“Ni mkuu wa mko mzee”
“Ahaa yeye ndio anaye badilisha amri ya nchi?”
“Ahaaa”
Raisi akaanza kuelekea katika uwanja huu, mimi na Babyanka hatukumuacha kusonga mbele, bado bastola zetu zipo mikononi, na tukimtazama kila aliye karibu na raisi.
“Habari zenu”
“Sala..maa”
Wafungwa wachache waliweza kuitikia ila wengine walishindwa kasisa kufanya hivyo kutokana na kuchoka kwa kipogo kikali wanacho kipata.
“Munafundishwa juu ya nini?”
“Muheshimiwa bora yaani umekuja, sisi wengine humu tumefungwa kwa kesi za kusingiziwa, ila tumekuja huku tunakutana na mateso makali kama haya”
“Yana muda gani?”
“Miezi mitatu sasa, kuna wezetu wachache kila siku usi……”
Mfungwa aliye kaa karibu na mfungwa huyu anaye zungumza akamuwahi mwenzake na kumfunga mdomo kwa nguvu. Mfungwa huyo aliye zibwa mdomo akampiga mwenzake kisukusuku cha kifua na kusababisha vurumai kuanza kutokea, kati ya wafungwa hao, jambo lililo tufanya mimi na Babyanka kuchanganyikiwa tukitafuta ni jinsi gani tunaweza kumuokoa raisi kutoka katikati ta watu hawa wanao onekana kujawa na hasira kali sana.
ITAENDELEA

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +