Pages

Thursday, May 16, 2019

ATHARI ZA KUANGALIA PICHA ZA NGONO

ATHARI ZA KUANGALIA PICHA ZA NGONO

Wanadam tumeumbwa na kiu ya kutafuta burudani za aina mbali mbali mbali ndoo maana wasanii wa muziki na sinema wanatajirika sana.Picha za kuangalia watu wanaoshiriki tendo la ndoa zimekuwa nyingi sana na kuwavuta wengi bila kujua madhara ya kuangalia picha hizo.Pale mtu anapoangalia picha za ngono pole pole ataanza kuzoea na kupendelea mitindo na mambo yanayofanywa katika picha hizo na hata mambo ambayo alikuwa hayapendi atajikuta ameanza kuyapenda. Utafiti mmoja umeonyesha kuwa kuna watu ambao baada ya kuzoea picha za kawaida wakajikuta wameanza kutamani kufanya mapenzi na wanyama. Mimi mwenyewe nimeshuhudia hilo baada ya mama mmoja kunipigia simu kuwa mume wake ameanza kufanya mapenzi na wanyama. Hivyo inatokana na kwamba pale mtu anapoangalia kitu kwa muda mrefu inafikia hatua akili yake inakiona kama kitu cha kawaida kwa kuwa walizoe msisimko mkubwa wa mwanzonii na sasa msisimko h uo unakuwa umepungua baada ya kuangalia picha hizo kwa muda fulani.

        Hatari kubwa kwa watumiaji wa picha za ngono ni kujikuta wamepoteza hamu ya tendo la ndoa katika hali ya kawaida. Jambo lingine ni kuiga mambo ambayo ni machafu sana kwa kuwa katika picha hizo unaona watu wanaonekana kufurahia mambo hayo machafu. Kwa mfano, kesi ya watu kutaka kufanya mapenzi kinyume na maumbile imeongezeka sana kwa wanaume na wanawake. Mbaya zaidi kwa mtu alieangalia picha hizo kwa muda mrefu atapata shida kuendelea kuvutiwa na muonakano wa mpenzi alie nae kwa muda mrefu. Kwa maneno mengine itafikia hatua anamuona mke au mume wake anaboa. Utafiti uliofuatilia ndoa 200 toka 2006 hadi 2012 ulithibitisha kuwa katika ndoa ambapo mwanaume anaangalia picha za ngono mara 1 au zaidi kwa siku zinakuwa na migogoro mingi zikilinganishwa na zile zisizokuwa na tatizo hilo. Katika ndoa zenye tatizo hilo kosa dogo lilileta migogoro mikubwa, kulaumiana kwingi, kutoelewana  kwingi na kuleta makosa ya zamani kumkandamiza mwingine.

        Mwanamke au mwanaume anaeangalia picha hizo za ngono atalinganisha mambo anayofanyiwa na mke wake na yale anayoyaona katika picha hizo na lazima mpenzi wake ataonekana kuwa na mapungufu katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya mitindo anayotumia, ukubwa au upana na urefu wa maumbile, nguvu au kasi ya utendaji na utundu mwingine katika kucheza ngoma ya wakubwa. Kwa kuwa lazima mmoja ataonekana na mapungufu na yule anaeona mapungufu hayo atakosa ujasiri wa kumuambia mwenzie na hivyo mvuto na hisia kupungua. Hisia zinapopungua na hali hiyo kujirudia rudia chuki inaanza kurudi kwa pole pole na penzi kunyauka. Ukweli wa jambo hilo ulionekana katika utafiti miongoni mwa makahaba ambapo asilimia 80 ya makahaba walishuhudia wateja wao kuwaonyesha mitindo toka kwenye picha za ngono, mitindo ambayo wateja hao walitaka kuitumia katika kucheza ngoma ya wakubwa na makahaba hao.

        Watu wanaoiga mambo wanayoyaona kwenye picha za ngono hawajui kuwa wengi wa wahusika wamelazimishwa kushiriki picha hizo, na haikuwa hiyari yao kufanya hivyo. Kutokana na kutokujua hilo wengine wanashangaa kuona wapenzi hawapo tayari kujaribu mambo mapya yanayopendekezwa na wapenzi wao na hivyo kuleta mvutano kati yao. Kutokana na hali hiyo tafiti nyingi zimeonyesha wazi kuwa watu walioangalia picha za ngono ndoa zao zinakosa furaha na nyingine kuvunjika. Naweza kusema kuwa kuvunjika kwingi kwa mahusiano kabla ya ndoa yanasababishwa na hali hiyo.

        Mbaya zaidi kuliko zote ni kwamba uangaliaji wa picha za ngono kunachangia katika kupunguza nguvu za kiume kwa wanaume wengi, na kwa wanawake zinachangia kupunguza hamu ya tendo la ndoa. Mtu anapokumbatiwa, kupigwa mabusu mengi au kufanya tendo la ndoa na mtu mwingine kuna kiasi fulani cha kichocheo cha DOPAMINE kinacho miminwa kwenye ubongo kupitia mzunguko wa damu na kumfanya mtu afurahie tendo la ndoa. Ila kiasi hicho kikizidi kipimo alichopanga muumbaji wetu inasababisha matatizo . Mtu anapoangalia picha za ngono yanatokea mafuriko ya kichocheo hicho cha DOPAMINE na inasababisha vipokeaji vya hisia katika mishipa ya fahamu (Receptors) kushindwa kufanya kazi na kuwa butu. Japokuwa ubongo utaendelea kuleta kichocheo cha hisia tamu cha DOPAMINE mtu anashindwa kupata msisimko na hivyo kushindwa kuwa na nguvu za kiume za kutosha, na kwa mwanamke kutokuwa na hisia hata mwanaume ajitahidi vipi kumwandaa.

Hapo unaweza kuona jinsi ndoa inavyoweza kuvunjika, mwanaume hana nguvu za kutosha na mwanamke ana hamu lakini mwanaume hana ujanja, inaleta mvutano.

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +