Kwa ufupi.
“… Jamani, mapepo ya zinaa yalinitesa sana kwa miaka mingi. Nakumbuka nilikuwa naingiliwa na mwanaume ambaye simjui, na nikiamka najikuta nimechafuka au wakati mwingine sichafukagi lakini nijikuta nipo hoi, utafikiri kweli nilikuwa kwenye tendo na mwanaume. Hali hii ilinisumbua kwa muda nami sikujua nini ni chanzo hasa. Kwa upande fulani ilipoanza hali hii kusema ukweli nilikuwa nahisi raha lakini baadae ilikuwa ni kero kupitiliza. Cha ajabu ni usiku tu ndio nilikuwa nikiingiliwa.
Nilikuwa nimeokoka tu, lakini nilikuwa sielewi kuona bado mwanaume akinifuatilia hali mimi nilishaachaga mambo ya kiuni zamani!!! Baadae Mungu alimtumia mtumishi wake, yale mapepo yakakemewa. Lakini yenyewe yakawa yanadai mikanda yake ya video za ngono X, nilizokuwa nazo bado chumbani mwangu. Unajua nilikuwa nina mikanda ya picha za uchafu za mapenzi, nilikuwa sijaitupa, lakini nilikuwa nimeokoka na kanisani naenda kama kawa! Kumbe mapepo yakadai mikanda hiyo, siku nilipoichoma moto ndipo na majini hayo yakaniachia lakini kwa maombezi makubwa kweli kweli…. ” Hayo ni maneno ya mwanamke mmoja aliyeokoka, akishuhudia jinsi alivyokuwa akiteswa na majini mahaba.
Ndugu yangu wewe unayesoma sasa ujumbe huu, nataka nikwambie; watu wengi wanasumbuliwa na majini / mapepo mahaba si wanawake si wanaume wote husumbuliwa nayo. Lakini wengi wenye kuteswa na majini mahaba ni wadada / wanawake, tena cha ajabu leo hii wanandoa ndio imekuwa shida sana! Hili ni janga la kimataifa!!! Sijui wewe kama upo salama katika hili.
“Pornography ” ni neno tunalolitumia kwa lugha ya kiingereza. Ninapozungumzia pornography nina maana picha za mapenzi ( sexual material) za video au za mnato zinazowekwa kwenye sinema / moves, majarida / magazines, matangazo / advertisements, n kwenye mitandao yakijamii / Internet n. K. Dunia inakoelekea ni pabaya sana, hata ilipo sasa ni mahali pabaya sana. Kwa maana dunia imefika inakushawishi ujiingize kwenye Pornography pasipo kujua ili shetani akunase vizuri, kwa mfano ebu angalia vipindi vinavyorushwa leo kwenye
Luninga ( TV) yako,asilimia 90 ni Pornography, katika muziki, tamthilia, matangazo. Inafika wakati hata mtu mzima leo huwezi kuangalia tv na watoto wako maana ni mambo machafu yametawala huko. Ebu angalia mwanamke anavyochorwa / anavyotazamwa, ni kwamba mwanamke anatazamwa kama chombo cha mapenzi hivyo, utakuta akilazimika awe uchi au nusu uchi katika matangazo au musiki tena cha ajabu hadi kwenye nyimbo za wokovu za leo hali ni hivyo hivyo wakati mwingine kwenye mahojiano kati ya mtangazaji na mwimbaji wa nyimbo za injili tunaona jinsi uvaaji wao wakuonesha maungo yao ya ndani yaani ni sawa tu nakusema “ nipo kwenye biashara nyingine pia, sasa uitazame, si unaiona mwenyewe, ukiinihitaji njoo inbox.. ” huyo sasa ni mtu ambaye anatuongoza kwenye nyimbo za ibada, sasa kama si mapepo ni nini?
Utafiti unaonesha;
30% ya shughuli zote za internet ni pornography ndio inayoangaliwa.
Watoto kuanzia miaka 11 wapo kwenye pornography.
Wakristo wanaume wanaangalia pornography kwenye kiwango /asilimia sawa cha wanaume wasio wakristo.
Wakristo wanawake wanaangalia kwenye kiwango cha chini kidogo ukilinganisha na wanawake wasio wa Kristo ( 15% wanawake wakristo kwa 30% kwa wanawake wasio wakristo)
Sasa hali inatisha!!!
Chanzo kikuu cha zinaa ni kuziangalia pornography, na ndio mzizi wa mapepo mahaba yanayokutesa hata sasa. Kumbuka, kitendo cha kuangalia video au picha za uchafu kinaaribu moyo wako, na picha au video haziondoki kwa wepesi kwenye moyo na kwenye akili zako. Video au picha zinanasa akili kwa haraka na hazitoki kwa haraka. Ninaweza kufananisha na muhuri unaopigwa mahali fulani, ni vigumu kuufuta ingawa unaweza kufuta muhuri. Ebu jiulize siku ya kwanza ulipoangalia pornography ulifanya nini baada ya hapo? Jiulize tena ; ijapokuwa ni muda mrefu tangu ulipokuwa ukiangalia video za ngono, Je video hizo zimetoka ndani yako leo? Ukweli ni kwamba hazijatoka kwenye akili hata sasa kwa maana unazikumbuk, kwa sababu tabia ya akili ya mwanadamu ni kushika tukio la video au picha kuliko maandishi au mafundisho.
Ebu fikiria, ni wanandoa wangapi walionaswa kwenye mapepo mahaba? kiasi kwamba mwanandoa anajikuta akilala na mwenzake, hisia zake zipo kwa yule aliyekuwa akimtazama na sio kwa mpenzi wake wa ndoa. Hiyo ni dalili ya kuvamiwa na pepo mahaba. Yaani ni hivi wewe mwanandoa unalala na mpenzi wako lakini huna hisia naye kabisa isipokuwa hisia zako zipo kwa yule mwingine uliyekuwa ukimtanzama kwenye picha za uchafu, kisha baada ya muda unahisi kama upo naye kitandani huku upo na mke / mume wako!!! Ni mapepo hayo! Na matokeo yake ni kuvunja ndoa yako, na kuvunja uhusiano wako na Mungu.
Video au picha za uchafu ni ibada ya sanamu!
Moja ya machukizo mbele za Mungu ni ibada za sanamu (1 Wakorintho 6:13) Lakini neno linasema tena“… ibada ya sanamu isiyo halali. “1 Petro 4:3. Uchafu wa namna hii ni sawa na kuutoa mwili wako na kumwabudu shetani kwa sababu sio matumizi halili ya mwili wako. Kitendo cha kuangalia tu, umeshiriki ibada ya sanamu kwa maana ni lazima utajikuta ukitamani kufanya kama ulivyoona! Na hapo utautumia mwili wako katika uchafu badala ya kuutumia kwa kumtukuza Mungu aliyekuumba.
Matokeo ya mapepo mahaba
Kushindwa kutulia kwenye ndoa ( kama si mwanandoa utakuwa balaa mtaani kwa uzinzi. Ikiwa umeokoka, shetani atakutoa kwenye wokovu kwa njia ya uzinzi usipofanyia kazi ipasavyo)
Kumchoka mwenzako wa ndoa kwa haraka ( huwezi kujisikia kuwa naye, kwa sababu umeolewa / umeoa na mtu wa kiroho. Ikiwa ni mwanamke ukiolewa na pepo, ujue halitakupa nafasi ya kumpenda mumeo maana wewe ni mali yake.
Kushindwa kuzaa / utasa. ( wakati mwingine pepo linafunga tumbo la mama, au kumfunga baba asiweze kuwa na nguvu ya uzazi)
Kuota mara kwa mara ukizini na mtu usiyemjua au unayemjua. N. K
Wewe unayeteswa na majini mahaba ebu jikague kama bado unazo pornography kwenye mikanda ya video yako. Kisha ukiona kweli bado hujatoka huko, ni lazima ufanye hatua kuanzia leo, tena sasa. Fanya ifuatavyo;
Mfuate mchungaji aliyopo karibu akuombee, au nipigie simu sasa tuombe.
Fanya maamuzi ya kuchoma moto video au picha za ngono.
Simama katika neno.
Kwa msaada zaidi wa ushauri, maombi ebu nipigie tuzungumze vizuri. Namba zangu zipo hapo juu kabisa.
UBARIKIWE.
Thursday, May 23, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments