Pages

Friday, May 17, 2019

CHEKA KWA TANI YAKO ILA USIVUNJE MBAVU

Kichekesho: mchagga na pesa

Mchaga mmoja alipata ajali alipozinduka pale hospitali akauliza “nipo wapi hapa?”

Nesi akajibu,”umepata ajali, hapa upo hospitali. Bahati mbaya umekatika mkono.”

Mchaga Mgonjwa: Na je saa yangu ipo wapi ya Rolex?

Nesi: Ipo mzee, Mkeo na watoto wapo hapa kukufariji.

Mchaga Mgonjwa: Yeuwi… Wamefunga duka?
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Kichekesho cha Kimombo na Meseji za Kimapenzi

Njemba moja wa mjini alitumiwa meseji na rafiki yake wa kiume ambaye kwa bahati mbaya hakuhifadhi namba yake ya simu yake kwenye simkadi yake. Kutokana na urefu wa meseji ikashindwa kuonekana yote mwishoni ikaandika

‘some text missing…’

kwa vile jamaa kimombo hakishuki hivyo maneno ya mwisho hakuelewa maana yake lakini akahisi litakuwa neno la kimapenzi miss you kutoka kwa mchumba wake

Ili naye aonekane mjanja na anakijua kimombo akajibu hivi,

“some text missing too dear”



Kumbe ile message ilitoka kwa rafiki yake wa kiume

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Angalia ndoto nyingine zilivyo na Majanga

Ndoto zingine bwana usiombe zikupate Mimi usiku wa kuamkia Leo nikiwa nimelala nimeota naendesha gari Yangu aina ya BMW mpya Mara gafla ikakwama kwenye tope .hivyo ikabidi nishuke ili kuisukuma loh! Yani kudadeki ile kuamka nikakuta nimesukuma kitanda hadi sebleni Daaa ilinisikitisha sana jiangalie sana sese hivi ndio narudisha kitanda chumbani .angalizo angalia ndoto unazo ota unaweza kuota upo baharini ukaamka unajikukuta unaogelea kwenye Jaba la Maji shauri yako.

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚

---------------------------------------------------------------------------------------------------------------

 Angalia huyu mwanamke mwenye wivu kwa mumewe alivyoumbuka, Mme wake kamuweza kweli

Mke: Hivi mume wangu una wanawake wangapi huko nje?

Mume: Kama nywele za kichwa changu.

Mke akachukua nguo zake akaondoka, Kufika njiani akakumbuka mumewe alikuwa na kipara Akaanza kurudi kwa mumewe.

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚

--------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Angalia nilivyookoa maisha ya mtu leo

Nmeokoa maisha ya mtu asubuhi ya leo huwezi amini.Nmekutana na ombaomba nikamuuliza atajisikiaje nikimpa sh.30,000/-

Akasema ATAKUFA kwa furaha.Nikaondoka bila kumpa ili ASIFE.πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚

---------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Wazo la asubuh - penzi la kuku

Wazo la asubui
πŸ™ˆPenzi la kuku sekunde 2 ila vifaranga kibao.Lakini binadamu masaa kibao mtoto 1 au 2. Sasa binadam na kuku nani JEMBE? Ukimwona JOGOO popote piga SALUTI!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ukinuna poa tu!!!!!πŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒ
πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚

------------------------------------------------------------------------------------------------------

 Huyu mgeni wa huyu jamaa ni shida



*Pale unapokuwa umefulia sana…Mgeni anakutembelea Maskani kwako….Unaamua Kuchukua Ile Sh 600 iliyobaki na kwenda Dukani Kumnunulia Soda Unaondoka na Chupa Mbili Unanunua Fanta Moja kwaajil ya Mgeni na Ile Chupa ya Sprite Unaijaza Maji ili Ukirudi Uweze kumpa Kampani Mgeni……Unafika Seblen Unampa Ile soda ya Fanta Mgeni anakuambia Fanta huwa situmii Nipe hiyo sprite …..Bwana….Bwana. …Bwana….Weee* πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +