Katika mahusiano, kujamiiana ni moja ya jambo linalohuisha penzi. Watu wengi wamekuwa wakigombana na wenza wao au wamechepuka kwa sababu tu wamenyimwa penzi.
Katika jamii nyingi duniani inaaminika kuwa mwanaume ndiye mwenye hamu kubwa ya kufanya mapenzi.
Wengine wamediriki hata kusema kuwa mwanaume huwaza mapenzi mara nyingi zaidi ya mwanamke. ndiyo ni kweli kwa kiasi fulani, lakini hili haithibitishi kuwa mwanamke hawi na hamu ya kujamiiana.
Wanawake huwa na hamu ya kujamiiana kama walivyo wanaume. Ila kutokana na jamii inavyowachukulia, wao kuwa wa kwanza kumwambia mwanaume kuwa wana hamu ya kujamiiana inawawia vigumu.
Jambo hili huwatesa sana, siyo wao tu, bali hata wanaume ambao hawajawajua vizuri wenza wao.
Hizi hapa ni faida za kuwa na mwenza mwenye hamu kubwa ya kufanya mapenzi.
Kamwe hatokudanganya
Wanawake wengi wamekuwa wakidanganya kuwa wamefikia kileleni ili tu kuwaridhisha wapenzi wao, jambo ambalo huwa si kweli.
Ukiwa na mwanamke mwenye hamu kubwa ya kufanya mapenzi, hatokudanganya, badala yake atakufundisha namna sahihi ya wewe kufanya ili wote mfike kileleni na mpate kufurahia tendo la kujamiiana.
Hatoogopa kukuanza
Ni kawaida kwa wanawake kuogopa kuanza kumueleza mwanaume kuwa wanataka kufanya mapenzi, badala yake hutumia ishara mbalimbali ambazo wakati mwingine huwa ni vigumu kwa baadhi ya wanaume kuwaelewa. Wasipoeleweka mwisho wa siku huishia kuugulia hisia zao.
Unapokuwa na mpenzi ambaye haogopi kukueleza wewe mwanaume kuwa ana hamu ya kujamiiana, ni jambo zuri na la kufurahia.
Kwani kwa namna hiyo anakurahisishia hata wewe kujiandaa na kumuandaa kwani akili yake tayari imeshajiweka katika hali ya kujamiiana. Hivyo itawafanya wote mfurahi na kuridhika na hii itaimarisha uhusiano wenu.
Huwa muwazi
Wanawake wengi wanapokuwa katika mahusiano, huogopa kuweka wazi mambo yanayowafurahisha, aina za ufanyaji wa mapenzi wanazozipendelea na hata sehemu ambazo wakishikwa wanasisimuka zaidi, kwa kuogopa kuonekana ‘malaya’. Hali hii huwafanya washindwe kufurahia kufanya mapenzi kwa kiwango na kutoridhika.
unapokuwa na mwenza ambaye ni muwazi, atakueleza na hatosita kukufundisha jambo jipya wewe mwanaume na mwisho wa siku wote mtaburudika na kulifurahia tendo.
Atakurahisishia kazi
kwa wanaume mnaelewa ni jinsi gani inavyokuwa vigumu kumuandaa mwanamke pasipo kumjua vyema. unashindwa kuelewa kama anafurahia ama anakerwa na unachomfanyia. kazi inakuwa kubwa na ngumu kwa wewe kuelewa ni kipi hasa umfanyie.
Lakini kama mpenzi wako amekuwa muwazi kwako, amekueleza mambo anayoyapendelea na yanayomfurahisha wakati mnajamiiana, basi kwako haitokuwa kazi kubwa. Badala yake utafurahia na utamridhisha sawa sawa.
No comments:
Write comments