Pages

Monday, May 20, 2019

INGIZA DUDU YOTE NDANI BABY SEHEMU YA 11

TOLEO LILILOPITAA............."mambo grace."nilimsalimu kicheshi.

"poa gao"aliitika kwa mapozi na kurembua.

"wow you look good."nilimsifia kidogo mana wanawake wanapenda kusifiwa.

"mmmh thank you."tuliendelea kuongea ni kamkumbusha jibu langu.

"vipi kuhusu jibu langu.?"niliuliza.

"aaaah gao nimejizuia nisikuambie ila nimeona bora ujue ukweli, sikufichi daaah mwenzako tayari nina mpenzi........."POROMOKAA NAYOOO... "GRACE kwanini hukunambia mapema nikajua ukweli v unanambia sasa."niliongea kwa upole kiasi kwamba machozi yananitoka, nikajipa kazi ya kupangusa machozi ili nisije chekwa.

"ooh sorry gao jaman niliogopa kukuambia najua unanipenda ila mwenzio tayari ninampenzi"alizidi kuniumiza na maneno yake. hakuna kitu kibaya katika kupenda kama pale umempenda mtu aje kukuambia anampenzi daaah nilichoka hata ujasiri wa kuendelea kuongea nikakosa,niliamka pale mkuku mkuku kiasi kwamba nikamshangaza hadi grace..

"gao waenda wapii jamani gao gao."aliita grace hapo sikusikia nikabeba begi langu na kuondoka nje ya darasa hata baadhi ya wanafunzi walishuhudia ninavyoondoka ila wengine hawakuniona kutokana na ufanyaji kazi za walimu.
Nilipotoka nje nilijiona ni kiumbe dhaifu mbele ya grace.

"mapenzi mapenzi nini daah.?"nilijisemea peke yangu,huku nikiachana na majengo ya kidato cha tatu ninachosomea, Hakika grace nilimpenda visivyokawaida kitendo cha kuniambia anampenzi tayari kiliniathiri mnoo,mpaka naona shule chungu.
Nilitembea upesi upesi nikiomba mungu nisikutane na mwalimu yoyote ili nitimize azima yangu, ya kuondoka eneo la shule. nilitembea mwendo wa hatua ndefu mwishowe nilifanikiwa kuachana na shule na kuanza kuelekea nyumbani mwendo wa kijeshi, njiani sikuacha kumkumbuka grace hasa taswira yake haikuacha kunijia mara mbili mbili,nikikumbua uzuri wake, upole na ucheshi nilianza kulia njiani kama mtoto.

"mamboo mbona unalia"ni sauti ya kike tena sauti nyororo kama ya mtoto mchanga.

"daaaah wee acha tu dada yangu."nilisema hukunikidondokwa na machozi na sauti ya kufina fina.

"au mwalimu kakucharaza viboko shule."alizidi nitia hasira akijua nimechapwa.

"bwanaaaaah sijachapwa niachee ondokaaaaaaaaa, aaaah"nilisema kwa jazba zote hasira yule mdada akaondoka na kuniacha natembea mwenyewe, nilifika mahali nikaona kulia sio sababu nilifuta machozi na leso yangu ya rangi nyeupe kisha nikaanza kuifata njia ndogo ya kuelekea nyumbani.
Nilitumia dakika kadhaa hadi kufika nyumbani, muda huo ilikuwa yapata saa mbili au tatu hiyo kutokana na jua kuwa la wastani sio la kuchoma,
Niliingia ndani moja kwa moja hata Ester alinishangaa.

"wewe mbona mapema leo umerudi kunani."alisema huku muda huo akiwa hata kudeki hajaanza ndio kwanza anapanga vitambaa kwenye mito na kufagia.

Alipoongea sikumjibu kitu chochote niliingia ndani kwangu na kuufunga mlango sanjari na kulitupa begi langu kando ya kitanda kisha nikakikaribia kitanda na kujilaza.
Nilisikia kugogwa kwa mlango ila sikujali ilikaa kimya tu, mpaka mgongaji akaacha pengine ni maumivu aliokuwa akiyapata pale anapogonga.
Nilijifanya kama sijui kilichotokea shule ilinimsahau grace hata taswira yake sikuivuta tena.

"daaah mapenzi kitu gani kama ipo ipo tu, ya nini nijiumize kisa mwanamke na wakati wapo wengi."nilisema na kuamka kitandani japo nilimpenda sana ila nilijivua tu pendo.
Nilikaa ndani muda mchache nikisubiri Ester amalize kufanya usafi, ndipo nikamkumbuka mdada wa jana alietaka kunigonga na gari lake bahati mbaya, akanipa hela pamoja na namba za simu, nilianza operesheni ya kuitafuta nguo niliyovalia jana mana ndio niliweka pesa aliyonipa nilitafuta hadi nikachoka kila nguo sio ndio nikakumbuka nguo chafu nilitia kwenye ndoo na ndio ile nguo ipo humo humo na ndoo ipo nje, nilifungua mlango haraka haraka na kutoka nje hadi kufika kwenye ndoo na kuanza kupekua nguo zangu hadi kuiona ile pesa hapo roho ikatulia nikarudi ndani wakati huu sikufunga mlango nikarudishia tu.
Nakuanza kuzihesabu zilikuwa noti za elfu kumi kumi zipo kumi na mbili yani laki na ishirini nilifurahi mnoo na kuziweka ndani ya begi langu la nguo,kisha nikaanza kuvua nguo zangu za shule na kiziweka juu ya enga iliyopo chumbani kwangu zilikuwa hazikuchafuka, wakati huo nikatoka hadi valandani Ester hayupo anaosha vyombo niligundua kutokana na kusikia mgongano wa sahani za dongo na vikombe.
nikakaa na kuiwasha tv siku hiyo sikupanga kurudi shule kabisa siku hiyo niliamua kupoteza muda kwa kutizama runinga,muda nao ukaanza kusogea mpaka kufika mchana Ester alikuwa busy muda wote mpaka mchana ndio akamaliza kupika na kutenga mezani nikaenda kula.

"wewe gao mbona leo mapema alafu ulikuwa haupo sawa nini shida."alisema ester.

"amna kawaida ondoa shaka."nilimtoa wasi wasi aliokuwa nao,akatulia hakuongea tena akaendelea na shughuli zake.
Na mimi nikaendelea na kula hadi kumaliza nikaelekea chumbani kwangu kulala.
Nilikaa kwanza nilipo kosa cha kufanya nikaamua nilale tu, kikapita kimya cha muda wa masaa kadhaa hadi kujakustuka tayari nilikuwa nimelala sana niliamka na kuelekea bafuni kuoga, niliingia nikaoga hadi nikamaliza nilingia chumbani kwangu nikavaa nguo zilizo nipendeza nikachukua na zile pesa kisha nikatoka valandani muda huo saa kumi na mbili giza ndio linaingia hakuna alierudi sii shangazi na wanae wala neema kutoka chuo,aliekuwepo ni ester tu.

"ester hivi hawajarudi tu."

"hawajarudi neema aliniambia atachelewa kurudi leo."

"na shangazi nae.?"niliuliza.

"yeye hajasema ila nilipoongea nae sijui alisema atapitia sehemu na wanae"

"sawa "niliitika nakuendelea kutizama tv, tayari nikamkumbuka mama imma akili yote ikahama kwake nilikaa pale hadi kufika saa mbili usiku nikamuaga ester na kutoka nje nikiwa na nia ya kwenda kwa mama imma.
Nilitembea hadi kufika katika eneo la boda boda nikapanda ilinipeleka kwa mama imma nilipanga nisifike kwetu sikutaka nikutane na baba nilimchukia mnoo.
Mwendesha boda boda alinifikisha hadi mitaa ya kule nyumbani kwa mama imma ambako ndio kwetu, sikuenda haraka haraka nilitembea kwanza mpaka kufika saa tatu nikijua kuwa imma atakuwa kalala, nikanyata hadi dirishani.

"mama imma,mama imma, mama imma,"niliita dirishani kwake.

"weee nani hapo dirishani."nisauti ya mama iliyonitisha mpaka nusu haja ndogo inimwagike tena kibaya zaidi yupo na shangazi....

Je?nini kitatokea hapo gao atagunduliwa au laaah mimi sijui ila tukutane sehemu ijayo.
Kama umeipenda story hii n unataka kuisoma mwanzo mwisho ni wakati wako kuisoma.

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +