Pages

Tuesday, May 21, 2019

INGIZA DUDU YOTE NDANI BABY SEHEMU YA 12

TOLEO LILILOPITA....Nipo dirishani kwa mama imma nachungulia huku namuita,kumbe wakati huo mama nae ndio anatoka nje tena yupo na shangazi,mama alianza kuuliza baada kuona kimvuli cha mtu pale...

"wewe nani hapo "aliuliza nilikosa cha kumjibu tayari hata haja ndogo ilitaka kunimwagika......
JIACHIEEEE NAYOOOOO...
Nilisimama kama mti uliokauka unaongoja kukatwa au kidondoka,mama na shangazi walianza kunifata wakitaka kunijua mimi nani,kitendo hicho kiliperekea nichomokome haraka kama gari lililoko mwendo kasi na break kukatika, kitendo cha kukimbia ndio ikawa afadhali yangu mana ilikuwa kidogo mama anione.
Mbio nilizotoka nazo pale,zilienda kukomea karibu na barabara ya magari nikaanza kuhema juu juu mithili ya mwizi aliewaponyoka watu wenye hasira kali waliotaka kuuondosha uhai wake baada ya kuiba vyao.
Nilienda mpaka upande wa pikipiki nikapanda kurudi nyumbani,masaa machache tu ilinifikisha karibu na nyumbani nikashuka na kumlipa kisha akaondoka na mimi nikauendea mlango na kuingia ndani.

"mamboo gao watoka wapi.!"ni sauti ya neema akiniuliza,nikafikiria uongo wa kumdanganya.

"oooh nilikuwa juu hapo napiga misele tu."nilidanganya nae akakubali tukaa pamoja kwenye makochi tukipiga story na kucheka.
Dakika kadhaa shangazi akaingia na wanae wawili niliotambulishwa hapo awali kuwa ni doreen na careen.

"shikamoo kaka gao"walinisalimia kwa pamoja nami nikawaitikia kumbe walisha nijua tayari ujio wangu,nilimsalimu shangazi akaitika na kukaa kochini.

"Ester "aliita, shangazi.

"abeeeeh dada."

"niletee maji ya baridi"

"sawa dada alafu chakula tayari hamieni huku."alisema ester hapo wote tukaelekea meza ya kulia chakula,shangazi nae akapewa maji yake akaanza kunywa huku kila mmoja akijipakulia chakula chake mwenyewe kinachomtosha.

"haya mwanangu gao za tangu juzi.?"

"salama shangazi za huko utokapo."

"salama unapaonaje hapa nyumbani."

"pazuri shangazi."tulizidi kuongea na shangazi , huku vikisikika vijiko vinapo gonga sahani wakiwa kimya tu wapo busy na kutafuna,story za pamoja zikaanza.
Msimuliaji alikuwa careen alietusimulia kichekesho kilicho tuweka wote midomo wazi kwa vicheko,story ziliendelea hadi wote kumaliza kula kisha kila mtu akaelekea chumbani kwake kulala baada ya kutakiana usiku mwema.

Niliingia chumbani kwangu nikajiandaa kwa ajili ya kesho,niliweka kila kitu sawia kuanzia mavazi ya shule na vitu nyengine vihusivyo shule sanjari na kupaka kiwi viatu vyangu kisha nikajilaza kuitafuta kesho,kiza kilitawala.

Nilikuja kustuka kutokana na mlango kugongwa na jina langu kuitwa na sauti nilioinakiri kichwani alikuwa ni Ester akiniamsha.

"gao,gaooo, amka kumekucha muda wa shule huu."niliisikia kwa mbali kama mtu anae ninong'oneza,alizidi kuita mpaka nikaamka na kuitika ,huku najivuta vuta kwa uchovu nikijinyoosha mwili.
Nikachukua mswaki na kuvaa taulo nikielekea bafuni kuoga upesi upesi nikaingia na kujiandaa haraka kukimbizana na muda dakika tano zilitosha kunifanya nitakate kisha nikatoka na kuingia chumbani kwangu kujiandaa nilivaa sambamba na upakaji mafuta mpaka namaliza nikatoka na kumuaga shangazi tulieongozana akitokea ndani kuingia chooni nilimuaga kisha nikatoka nje na kuelekea shule.
njiani nilianza kukumbuka tukio la jana lililotokea kwangu lilizidi kuniumiza moyo,ila sina jinsi niliendelea na safari mpaka kufikia eneo la shule kengere maalum kwa ajili ya namba iligongwa nikaelekea eneo la kuhesabiliwa namba, baada ya kupata namba nikaelekea darasani siku hiyo ilikuwa ni zamu yangu katika usafi wa darasa hivyo sikufika kabisa katika eneo la nje,nilibaki darasani na usafi kuendeleaa nikiwa na wenzangu, tulimaliza kufanya usafi tayari na kukaa humo humo darasani.

"eheeeeee.!gaoo umekuja mwenyewe leo,nilisema utakuja hapa ni mtoni lazima uje kama si kunywa maji,utakuja kuchota kama si kuchota utakuja kufua."ni maneno aliyosema sir lusinde mkononi akiwa na viboko vyake hapo nilikuwa natetemeka kwa woga tu.

"Jana ni nani alikupa idhini ya kuondoka shule muda ule kabla ya kuruhusiwa."alinitandika swali ambalo lilikuwa gumu kujibika haswaaa,nilishimdwa kujibu nikawa namtizama tu.

"mbona hujibu ndio dharau au umekuwa asaivi."aliniambia,na kunisogelea karibu.

"hapana sir."

"hapana nini wewe mjeuri eeh ngoja nikuoneshe ujeuri leo,nifate ofisini."akitoa kauli na kuondoka,na mimi nilianza kuzuga zuga nikisita kwenda mana shughuli yake sio ya kitoto,sikumfata nilipoteza nuda kadhaa

"gaoo unaitwa na sir lusinde."alikuja mwanafunzi wa kidato cha kwanza niliemtambua kwa sale yake ya tofauti na mimi ambayo ni ya kidato cha kwanza yake rangi ya kaki na yangu kijivu kijivu,nilizidi kuchanganyikiwa kitendo cha kutuma mtu aniite ndio haswaa kilinitisha, niliganda ganda hadi kupata uamuzi nikamfata.

"wewe nimekuita saa ngapi,hadi utumiwe mtu ndio uje sio."alisema kwa jazba sir .

"haya lala chini lala chini."alinilaza chini kwa fimbo za bega mpaka nikalala,hapo alipata uwanja alianza niteremshia fimbo zisizo na idadi hata wiki zililipita tena kwa hasira hakuchapa sehemu yake alikuwa akinipiga kiunoni.

"aaaah sir sasa unanichapa wapi huku."

"unasemaje wewe umekuwa si ndio"aliniambia na kuendelea kunichapa,alinichapa fimbo za kutosha.

"sasa adhabu yako uhamishe kifusi cha udongo ujaze pale kifusi kikubwa mikokoteni mitatu."alisema maneno mfurulizo,alinipa kazi nzito ambayo sijawahi ifikiria kabla kama nitaifanya.

"nenda store kachukue chepe jembe na ndoo"

"sawa."nilijibu kifupi,nilienda nae mpaka store ajanikabidhisha vifaa na kunionesha eneo la kuchimba.

"haya chimba hapa ukajaze kifusi ole wako usaidiwe unaanza upya sehemu nyengine."aliniambia,daah nikifikilia mikokoteni mitatu ni udongo mwingi sana na itanichukua muda mrefu kumaliza,nilianza kuchimba na jembe ili kurahisisha nikitumia chepe.
kengere ya paredi iligongwa nikiwa pale pale mpaka wanaingia darasani nipo pale pale tu.
kazi ilikuwa ngumu upande wangu sijawahi ifanya ila nilitumia jinsia mwanaume yani uwanaume wangu kuifanya unajua mwanamke na mwanaume ni tofauti sana hivyo nilitumia nguvu za kiume kuifanya hiyo kazi kila mwanafunzi anapita hakuacha kunipa pole wengine wakiuliza kosa langu nililofanya ila sikuwa nikiwaambia, kazi ili hadi kubakisha mkokoteni mmoja na nusu hapo nimechoka tayari,nikauendea mti uliokaribu na eneo lile kujituliza tu.
Madamu alikuwa anakuja eneo hilo kwa mwendo wa madaha kiasi kwamba anaogopa kukanyaga chini,alikuwa akitokea nyumbani kuja shule,alinifikia na kunishika shavu.

"oooh gao i mis you upo wewe."aliniambia mkono mmoja akiwa kauweka shavuni kwangu,nilikosa cha kumjibu nikiomba aondoke tu pale ila haikuwa hivyo alizidi kuongea maneno ya ajabu.

"gao leo usiku nataka uje kwangu si utakuja eeh,nikuandalie nini."aliongea,mara ghafla sir lusinde akatokea eneo lile madam alipomuona akazuga............
ITAENDELEAA

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +