Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo kubwa sana ambalo endapo halitatafutiwa ufumbuzi na muhusika linaweza kuyaathiri maisha yake kwa kiasi kikubwa sana. Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume, hii ni kulingana na utafiti uliofanyika.
Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Mwanaume anayekabiliwa na tatizo la ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume huonyesha dalili zifuatazo:-
1. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake barabara. Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika (rijali ) unaposimama, hutakiwa kuwa imara kama msumari, lakini kwa mwanaume anaye kabiliwa na tatizo hili uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na huweza kusinyaa wakati wowote. Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume. Mishipa ya uume ndio inayo ufanya uume usimame barabara. Mishipa hii inapokuwa imelegea, uume hauwezi kusimama barabara hata iweje.
2. Kukosa hamu ya tendo la ndoa: Hapa mwanaume anakuwa hana uwezo wa kutamani kufanya tendo la ndoa hata anapokuwa faragha na mke wake. Tatizo hili kwa kiasi kikubwa husababishwa na msongo wa mawazo.
3. Kutokuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara moja. Hapa mwanaume akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakuwa hana tena uwezo wa kurudia mshindo mwingine. Hali hii husababishwa na kutokuwa na msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya kwenye uume.
4. Kufika kileleni mapema
5. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha kabisa. Hali hii hutokea pindi tatizo la kutokuwepo kwa msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume, linapokuwa limekomaa. Na wakati mwingine, hali hii hutokea pindi vyanzo zaidi ya kimoja vya tatizo la kiume vinapo kuwa vimejitokeza kwa mtu mmoja.
6. Uume kusinyaa na kurudi ndani. Hapa uume wa mwanaume unakuwa umesinyaa na kurudi ndani. Uume huu unakuwa hauna uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa.
Kwa ufupi sana, mambo yafuatayo ndio vyanzo vikuu vya tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume:-
• Upigaji punyeto wa muda mrefu.
• Msongo wa mawazo.
• Ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu (pressure).
• Kupooza kwa mwili.
• Kuugua ugonjwa wa ngiri.
• Kuugua chango la kiume.
• Ulevi uliokithiri.
• Kuwa na wasiwasi wa kumudu kutekeleza tendo la ndoa.
• Woga wa kufanya tendo la ndoa.
• Uzoefu wa kukatisha tamaa wa siku za nyuma.
• Ulaji mbovu wa vyakula haswa vyenye mafuta mengi/kupita kiasi.
• Mazingira yasiyoridhisha wakati wa tendo la ndoa.
• matumizi ya madawa makali (hususani madawa ya kizungu) ya kuongeza nguvu za kiume, husababisha mishipa ya uume kulegea Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
• Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone.
• Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini.
Kutokuwa na nguvu za kiume huleta madhara na athari nyingi sana kwa muhusika. Baadhi ya athari hizo ni pamoja na:-
• Kuvunjika kwa mahusiano ya kimapenzi.
• Kuvunjika kwa ndoa.
• Kujiua: Baadhi ya wanaume hufikia uamuzi wa kujiua baada ya tatizo kuwa kubwa na kutumia dawa za aina mbalimbali bila mafanikio.
Friday, May 24, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments