Pages

Friday, May 24, 2019

KWANINI UNASHINDWA KUISHI NA MWANAMKE AU MPENZI?

Habari wapenzi wasomaji wa makala zangu za mahusiano katika jamii hasa ya wanandoa,wachumba au wapenzi pamoja na mahusiano ya mtu na mtu, kikundi na mtu au jamii Fulani na jamii Fulani.nipo hapa kwa sababu yako.
Yawezekana umeachwa mara nyingi na wapenzi wako uliowahi kuwa nao na umekuwa mtu wa kubadilisha wapenzi kila siku sababu tu kila utakae kuwa nae anakumbia na wala sio kwamba hauwahudumii chumbani au lah .Hata uwe unapiga dudu balaah ikifika muda wa kusepa anasepa tu kama hujui jinsi ya kuishi nae. Je wajua sababu nini? Fanya yafuatayo
1:  Onyesha uhalisia wako tangu unaanza kumtongoza ili isije kupatia tabu mbeleni. Ikiwezekana zile sifa nzuri ambazo unahisi zitakupa credit ili kumpata kirahisi demu haupaswi kuzionesha mwanzoni. Jifanye mtu wa kawaida sana kwake hadi akuzoee kabisa. Baada ya kumpata na kuwa nae hapo unaweza kuwa unaonesha unavyoviliki hata benki akaunt ikiwezekana ni siku baada ya siku hii itamfanya taratibu aendelee kukupenda na kujenga imani nawe.hii itakusaidia kwani upendo na imani huwa haijengwi kwa siku moja. Ukianza na pesa, gari na majumba  mwanamke atakusoma kama mtu wa majigambo, mbinafsi na pia upo nae kwa sababu una kitu ,isitoshe tayari umemuanda kisaikolojia kuwa yupo kwako kwa  muda tu na kwa sababu ya gari yako au pesa zako au kiwanja chako ulichomuahidi na  akifanikisha tu anakimbia. Na  siku zote jaribu kumshirikisha baadhi ya vitu vyako hasa katika maamuzi.jaribu kujenga hoja za umiliki au umoja  kama vitu vyenu wote ili kuondoa ubinafsi kauli kama`` baby traffic wamekamata gari langu..au nimenunua nyumba yangu sehemu fulani´´. Hapo moja kwa moja anajiandaa kuondoka kwako kwani umeonesha upo pale kwa kumtumia tu. Anza kulinda penzi lako wakati unaanza tu kutongoza.
2:  Mwanamke siku zote anapenda vitu vidogo vidogo au zawadi ndogo ndogo sana ambazo zitaonesha kuwa unamjali na sio pesa pekee. Vitu kama chupi, sidiria, mafuta au parfume anayopendelea ,vinaweza vikawa na thamani kuliko hata hizo pesa zako kwani ndivyo vinavyoonesha utu wako kwake. Hata kama unataka kumpa pesa angalia mazingira ya kumpa pesa hiyo ,tafuta sababu mwenyewe ya kumpa pesa yako ili asione kama unamuhonga hiyo pesa. Akikuomba pesa yeye kama yeye sikiliza kwanza sababu na pima na uzito kama sababu haina mashiko mkatalie lakini chagua maneno(sababu) ya kumkatilia ,ukishindwa kabisa kumkatalia mpatie hela kidogo na onesha kuishiwa au hauna kabisa. Tumia lugha ya upole na uoneshe umeguswa na tatizo lake kwani tayari kama alikuja kimaslahi atachukia au hata kukununia. Wewe usijali ilimradi unaweza kumbembeleza na kuendelea kuwa nae.
3: Onyesha hisia zako pale inapobidi ili akujue au akusome tabia zako. Inapokubidi kuchukia unatakiwa uchukie na sehemu ya kuonesha hasira basi onyesha…hapa utaonesha mipaka yako ya utu wako yaani unampa onyo asivuke mipaka yake. Inapobidi kumsifia au  kufurahishwa basi furahi sana..hapa unaonesha jinsi gani unapendezwa nae na unamfurahia yeye . kwenye huzuni onyesha huzuni na mpe pole pale inapobidi.
4:Mwanamke siku zote anaishi kwa mazoea.basi hakikisha unamzoesha tabia ambayo utakuwa nayo kipindi chote cha mahusiano yenu. Hii itakusaidia kulinda penzi lako kwani mwanamke ni mtu mwenye wivu sana hasa katika mapenzi (mbinasi sana wa mapenzi). Mfano kama nyumbani huwa unarudi saa mbili usiku piga uwa urudi muda huo kila siku vinginevyo nyumbani patachimbika au kama amezoea chakula cha usiku uwe nae mezani fanya hivyo kulinda ratiba hiyo, vinginevyo ndiyo mpasuko unaanza kutokea. Hata kama umemzoesha kila wikiendi kumtoa basi mtoe vinginevyo unaharibu penzi. Mwanamke mwepesi sana kujishtukia au ana wivu sana (mbinafsi sana kwenye mapenzi) kwavo anaweza hisi anaibiwa tena atahisi mchepuko unafaidi zaidi kumbe mwanaume hauna hata wazo.
 Hadi hapo nadhani nitakuwa nimekusaidia kidigo kiasi chake kulinda penzi lako. Acha koment yako iwe swali, ushauri au maoni.
 By Waziri wa Mapenzi

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +