Pages

Friday, May 17, 2019

Mke kapewa mimba na shemeji yake

Mdau kanitumia hii, anaomba msaada wa mawazo, msaidieni. JAMANI hii ni habari ya kweli, na inanisumbua moyo sana. Nimeolewa na bwana wa kiarabu miaka 20 iliyopita, huyo bwana ana mke wake wa kiarabu aliyezaa naye watoto 6, mimi hajanizalisha. Tumetibiwa kila hospitali nchini na nje ya nchi lakini hakuna mtoto, Dk Kaisi amefanya kila njia lakini wapi. Hata hivyo huyu mume wangu wala hajawahi kunipigia kelele juu ya hilo,ameonyesha love kubwa sana. Miaka 10 iliyopita alimleta mdogo wake wa kiume ambae alikuwa anasoma Ulaya, ni kijana mzuri, msomi na ana bidii sana ya kazi , anamsaidia sana kaka yake kazi zake maana kaka yake ni tajiri sana tu. Siku moja katika maongezi naye nikamweleza shemeji yangu shida yangu ya kutozaa na nikamwambia kuwa Dk Kaisi anasema mume wangu mbegu zake haziwezi kunibebesha mimba. Tukajenga mazoea sana (mimi na shemeji yangu),disko tunaenda wote na mengi tu tukawa tunafanya pamoja. Miaka 6 iliyopita kaka yake akaenda kwa mke wake uarabuni nikabaki na shemeji ambae akawa msimamizi wa familia, bila ya ajizi nikamtolea uvivu nikamwambia kuwa naomba kuzaa naye, alisita sana na akaniuliza maswali mengi mno lakini hatimaye nikalala nae na nikabeba mimba na kuzaa mtoto wa kiume. Kaka yake hakujua maana alirudi baada ya miezi mitatu. Shemaji kwenye 6 kwa 6 ni eksipati (mtaalamu) sana yaani sijawahi kuona mwanaume mtamu kama yeye. Shemeji akapata kazi Marekani akaenda ila kila akirudi tunawasiliana tunaendeleza libeneke kama kawaida na hivi sasa nina mimba yake. Kinachonisikitisha ni kwamba shemeji anapokuwa kifuani ananiita mama watoto wangu nipe raha nami nampa raha, sasa naumia roho sana kuona nazaa na shemeji yangu na namsaliti mume wangu ambaye amenifanyia mengi mazuri. Je, nikaungame kwa mume wangu kwa kumwambia ukweli kuwa nazaa na mdogo wake

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +