Pages

Sunday, May 19, 2019

Nilichokishuhudia mume wangu akifanya siamini jaman utamu wangu unaniponyoka

Naamini kwa uwezo wa Mungu mko wazima.

Napenda kuwashukuru sana kwa michango yenu ambayo huwa mnatoa humu mm ni mdau japo huwa siyo mchangiaji sana lakini siyo mara ya kwanza kuleta matatizo yangu hapa na mkanisaidia.

Kama utaweza kupitia topic zangu za nyuma utanielewa vizuri ila leo nimekuja na lingine.
Nimeolewa nina mtoto mmoja ana miaka 5 nimeolewa miaka 7 iliyopita, kipindi chote cha maisha yangu ya ndoa nimepitia mambo magumu sana kutokana na tabia ya ufataki aliyonayo mume wangu lakini mungu amenisaidia mpaka hapa nilipo.

Kama wiki 3 zilizopita kuna mtoto wa kike wa shangazi yake na mume wangu alikuja nyumbani kama kawaida huwa anakuja kutusalimia then anaondoka ila safari hii akawa amekaa sana nkamuuliza vpi unarudi au umekuja mjini kwa lengo gani akaniambia amechoka kukaa kijijini bora akae nyumbani anisaidie kazi za nyumbani nikamwambia sawa.

Tumekaa nikaona tuna shida ya mfanyakazi katika biashara yetu na yeye kwa elimu yake ndogo hiyo kazi anaiweza, basi nikamweleza mume nae akakubali tukaona kuliko akae nyumbani na kuna msichana wa kazi haina sababu, basi jana kaanza kazi na hiyo kazi anafanya hadi saa nne usiku then wanarudi na mjombaake ( yaani mume wangu).

Jana usiku saa nne nikiwa ndo nataka nijilaze kitandani nilisikia gari la mume wangu akiwa anarudi coz najua mlio wake, basi nikakaa kama dk 10 gari ipo nje nikajiuliza mbona hafungui geti aingize gari akili ikanijia labda anaongea na simu, nikalala zangu kama dk 20 mbele bado gari ipo silent nje, nikaamka nikatoka nje nikafungua geti taratibu nilishuhudia mume wangu akikisiana na huyo mtoto wa shangazi yake.

Niliishiwa nguvu nikamsogelea kuwaangalia vizuri binti akashtuka sana akataka kukimbia akashuka kwenye gari, nikamuuliza mnafanya nini hapa akaniambia wanafanya mahesabu nikamwambia mbona giza ebu leta hilo daftari la mahesabu mnalofanyia, akababaika akamuita yule binti akamwambia leta daftari akakimbia ndani chumbani kwake akajifungia akalala, nilistaajabu sana sikuamini nilichokiona, mume wangu akaingiza gari ndani akaja chumbani jasho linamtoka sikumsemesha wala kumuuliza chochote nikalala.

Leo asubuhi nilipoamka nikamwamsha yule binti nikamwambia ajiandae arudi kwao kajiandaa nikampa nauli nikamwambia asije tena nyumbani kwangu.

Wapendwa kichwa kinaniuma na kinachoniuma siyo kuwakuta katika hali ile ila roho inaniuma mume wangu alipofikia ukiangalia yule binti ni ndugu yake wa damu kabisa ana miaka 17 tu, mume wangu ana miaka 47 mtu mzima.

Nimefikiria cha kufanya nakosa sina wa kumueleza naogopa mume wangu ni kiongozi nikisema kwa watu ni aibu natamani nifungashe niende kwanza nyumbani kwetu kwani naishi mbali na wazazi labda huyu mume atabadilika nikiondoka au nifanye nini msaada wenu jamani.

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +