Ni story inayo muhusu Lisa
Naitwa Lisa ni mzaliwa wa wilaya ya nyamagana katika jiji la mwanza,nilizaliwa mwaka 1989 katika hospitali ya Bugando. Katika familia yangu tumezaliwa wawili mimi na kaka yangu John. Na pia katika familia yetu tumelelewa katika dini. Pia katika familia yetu tuliishi kwa kutegemea kilimo. Hatukufanikiwa kuishi na wazazi wote kwani mzazi wetu mmoja alitangulia mbele ya haki mnamo mwaka 2005.Kipindi hicho sitokuja kusahau maana baba yetu alitutoka katika mazingira ya kutatanisha,siku hiyo ilikuwa ni juma pili asubuhi baba aliamka na kwenda shambani…. Mimi,mama na mdogo wangu John tulibaki nyumbani kumalizia majukum ya nyumban kwa asubuhi na baada ya hapo tukaelekea shamban kuungana na baba yetu. Tulipofika tulimuona ng’ambo ya pili akiendelea kulima,masaa machache yalipita mara ghafla tulisikia KELELE kisha akanyamaza kimya,wote tulishtuka na kuelekea alipokuwa,tulimkuta amelala kimya, kumbe ndo alikuwa ameshatutoka R.I.P BABA. Tulilia sana kwan hatukujua nini kilimpata baba yetu na kupelekea mauti yake kwani alikuwa mwenye afya njema siku hiyo. Basi tulifanya mipango ya mazishi ambayo haikuchukua mda sana yalikamilika huku tukisaidiwa na wanakijiji na baadhi ya ndugu zetu. Basi siku ilifuata tulimaliza shughuli ya mazishi kila mtu akarudi kuendelea na shughuli zake. Mama alikuwa mpweke sana kipindi hicho kwani alikuwa ni nguzo yetu na mboni yetu kwa kila kitu,kwani ndiye aliekuwa akitusomesha kwa bidii na kutusihi tusome kwa bidii kutokomeza ujinga. Baba alitutoka ghafla sana mimi na mdogo wangu John maana wakati huo ndio tulikuwa tukisubili matokeo ya darasa la 7. Matokeo yalikuja vizuri kwa mimi na mdogo wangu John tulikuwa tumefaulu kujiunga na kidato cha kwanza. Mama alipopata taarifa kwamba tumefauru kujiunga kidato cha kwanza mama…………………………………………… FATILIA SEHEM YA PILI
Wednesday, May 15, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments