Pages

Thursday, May 16, 2019

SHEMEJI INGIZA TARATIBU SEHEMU YA TATU

Alikuja mgeni na alipofika nyumbani hakumkuta mama kwani mama alikuwa kwenye mizunguko yake ya kutafta pesa kama ilivyo kila siku. Mgeni alinikuta mimi nyumbani nami nilimsihi amsubili mama kwani hiyo ndio ilikuwa mida yake ya kurudi nyumbani,mgeni alionekana mchangamfu sana na mwelewa kwani alinikubalia na tukamsubili mama,hatukuongea sana na mgeni mara mama aliingia……….! Mara tu mama alipomwona Yule mgeni alianza kulia nilihisi kuwa kidonda kimetoneshwa na kumwangalia sana mgeni huyo kadri alivyokuwa akimsogea, mgeni nae alikuwa akimfata aliko,nilitahamaki mda mrefu na kushangaa na kuona kama ni mchezo wa kuigiza. Sikuelewa kilichokuwa kikiendelea mda huo kwan mgeni nae aliangua kilio kikali sana na yalipopita masaa kadhaa wote walinyamaza na kila mmoja alimtazama mwenzake kwa jicho la huruma sana,
Mama ” Vainness huyu ni mwanangu wa pili na wa kwanza yupo shule mda ukifika utamwona anaitwa John ndo Yule ulie muacha akiwa mdogo sana, na huyu ndie nilikuwa na mimba yake,yeye anaitwa Lisa.
Vainness “Nashukuru na nimefurahi sana kumfaham kwani ni muda mrefu sana nimeondoka hapa nchini kuelekea masomoni,pia pole kwa msiba uliokukuta kwa kumpoteza mpendwa wako”
Mama “ Asante sana ndugu yangu kwani mpendwa wangu kaniacha kwenye njia ambayo sijui iko wapi kwani naona giza limetanda safarini”
Mama alipokuwa akiongea maneno yale machozi yalianza kumtoka nami nilimsogelea na kuanza kumbembeleza na kumfuta machozi.
Muda ulipita kidogo na mama aliacha kulia na mimi ilinibidi niingie jikoni kutayarisha chakula cha pamoja kwani mama hakupenda mgeni aondoke bila kupata chochote. Niliivisha chakula kile upesi kwani nilihitaji sana mgeni ale chakula nilichopika mimi,nilitayarisha meza na kuwakaribisha wote mezani kwaajili ya chakula. Wote walifika mezani kwa wakati na tukaanza kula chakula,wote waliendelea kupiga story na story walizokuwa wapiga nje kabla ya chakula. Katika mazungumzo yao mgeni alimgusia mama hiki kitu……………………………………………..………………………………………………………….!
FATILIA SEHEMU YA 4

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +