1. Sio Mahusiano yote huishia kwenye Ndoa. Baadhi ya Mahusiano yapo kwa sababu fulani, mengine ni ya msimu na baadhi hudumu mpaka Ndoa. Hivyo, kama mahusiano yako yamefeli, usisikitike, kulikuwa na sababu. Tambua hilo na jaribu kusonga mbele.
2. Usipende kwa Moyo wote, unavyopenda ondoka na akili yako pia. Mpende mtu uliyenae lakini jipende na wewe pia. Ujue mustakabali wako na muelekeo wa maisha yako. Usiwekeze kila kitu kwa mtu ambaye mmejuana ukubwani. Kuwa muangalifu.
3. Usivutiwe na mtu kwa fedha ama uzuri wake. Kama mtu huyo hakupendi na anazo sababu zake binafsi basi, uzuri wake au fedha zake haziwezi zikafanya mahusiano hayo yadumu.
4. Mapenzi pekee hayatoshi. Ila, maelewano, kuendana, hekima, uvumilivu na ustahimilivu ndivyo vitakavyofanya kuwe na mahusiano ama Ndoa imara.
5. Usijidanganye kwamba, inakubidi uwe na hisia za kumpenda mtu ndio umkubali au uwe nae kwenye mahusiano. Watu wengi wanafikiri wapo kwenye mahusiano yasiyofaa ama Ndoa isiyofaa kwa sababu tu hawawapendi walio nao, wasichojua ni kwamba mahusiano na Ndoa ni maamuzi zaidi kuliko hisia.
Unavyoamua kuwa na mtu, hisia za mapenzi hufuata baadae na hata unavyomchukia mtu, hisia zako zirakufanya uyaone makosa kila siku ya mtu uliyempenda hapo awali.
Kupenda ni maamuzi, sio hisia peke yake. Choose to love and the right feelings will follow.
No comments:
Write comments