Pages

Thursday, May 23, 2019

Simulizi ya kweli kuhusu madhara ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile

Nimeolewa nina mtoto mmoja, mme wangu anapenda sana kushika shika makalio yaani akiona niko mtupu tu basi bora anishike hata makalio aridhike, sikuogopa nilijua mwili wangu ni haki yake nikawa namuwachia, tukilala tu, anaweka mkono kwenye makalio ndio usingizi unampata alizowea hivyo.

Yaani hata tugombane vipi tukilala tu anaweka mkono wake kwenye makalio kwa juu kila nikishtuka nakuta mkono, ILA HAKUWAHI KUNIAMBIA HABARI ZA KIINGILIA KINYUME CHA MAUMBILE

Aliniheshimu sana wala hata sikuwahi kuhisi kama ana mtu nje yaani hata wazo sikuwa nalo maana unawezashinda na simu yake usione chochote, hata upekuwe vipi hukuti chochote, saa moja yupo nyumbani, weekend hatoki, yaani amani tupu, sasa kuna kipindi.

AKAANZA TATIZO LA KUTOSIMAMISHA
Ikawa akifika asubuhi anakuwa ha hamu kabisa, naamimi nakuwa na hamu sana, lakini inakuwa imesimama kidogo sana,basi naichezea naigusisha baadae kabisa ndio inasimama anaingiza, akiingiza unakuta katikati ya mapenzi inalala tena kwahiyo nakuwa sijakojoa yeye analalamika tu anaumia sana hasa sehemu za korodani.

Basi ilichutukua kama wiki kwa hali hiyo nikawa najitahidi kumset mind yake kuwa free nikawa namuuliza labda hali hii iliwahi mpata ujanani akasema hapana, nikawa namuuliza sasa inakuwaje unawaza nini isijekuwa una mawazo, akasema hapana sina mawazo nikamwambia haya niambie basi nini shida, twende hospitali akasema kesho nina dr, rafiki yangu Aga khan nitakwenda kumuona, basi ikaisha.

Kesho yake akaja na dawa kama ungaunga kwenye kakopo, nikamuuliza hii dawa ya hospitali kweli?

Akasema hapana kuna staff mwenzangu nae tatizo hili lilimpataga akanywa dawa hii ya kimasai, unamix na maji ya moto, alikunywa kichupa kile aliuziwa 120,000 alikunywa kikaisha uwezo wa kusimama ulikuwepo, lakini hafiki mwishoni inalala kabisa inakuwa ndogo.

Nikauliza au ni ngiri? akasema hapana.

Hali iliendela hivyo kuna siku nilishtuka sana nilikuwa nafua chupi nikatoa nimfulie na yeye, nikakuta vitu kama usaha umejaa kwenye chupi yake nilishtuka sana sikufua nikaiweka pembeni, nikamsubiri aliporudi nikamuliza huko chini unatoa nini?

Mimi ni mke wako natakiwa kujua uume wako unatoa nini maana ni mali yangu na haki yangu kwanini unaniogopa hata kama unaumwa tena ni vizuri mkeo akijua ajue anakuhudumiaje, niambie kweli, akasema mie sijui, naona tu kuna vitu vinatoka vyamoto vyeupe nikamuuliza vimeanza lini, akasema siku ya tatu leo.

Nikakumbuka kweli siku hizo zote chupi zake alifua mwenyewe nikamwambia sasa kwanini husemi, unakaa kimya, isijekuwa magonjwa ya zinaa akasema niyaote wapi mke wangu, nikamwambia twende hospitali aligoma kwenda na mimi, nilimsimulia rafiki yangu akaniambie niende nikapime mimi maana ushirikiano mme hana.

Nilienda regency nikapima nikaambiwa niko salama salmin sina chochote kile isipokuwa kuna kigozi waliniingiza wakasema kesho yake nifate majibu, nilirudi nikaambiwa kipimo kile pia kinaonyesha niko mzima nikasema asante Mungu.

Ilienda hivyo niliamua kumuacha maana hataki kushirikiana na mimi kabisa.

Kila nikiuliza anaficha ficha siku hiyo usiku nimelala nikasikia mtu analia, nikaamka nikakuta analia huku ameshika nyeti zake analia kwa uchungu sana.

Nilitazama saa ilikuwa saa sita, mie huwa siwezi kuendesha usiku, nikamuita rafiki yake akaja tukampakie hao hadi agakhan njia nzima analia hawezi hata kukaa wala kukunja kiuno yaani ilibidi nikae nyuma na yeye anilalie analia kama matoto, kwa mara ya kwanza nilishuhudia machozi yake na sauti ya kilio
nikajikuta namhurumia nalia na mimi.

Akaniambia mke wangu nishike huku, nipuulize, naumia nishike shike mama naumia analia sana, nikamwambia niambie basi.

Kama uliiba mke wa mtu twende ukaombe msamaha, ona sasa hueleweki unaamua nini, wakati huo imesimama mishipa yote imeonekana kuvimba yaani niliogopa sana, nilimvisha bukta laini tu maana chupi ingemuumiza sana.

Tulipokelewa akaingizwa kwa Daktari cha ajabu kufika pale akawa anataja jina la daktari anaemtaka yeye wakasema hayupo akanipa simu akaniambia chukua namba jina limeandikwa dokta...........................(jina la dokta kapuni yeye kataja mimi admin nimelificha) akasema yeye ndio anajua issue yangu, nikasema issue gani?

Akasema wewe mwambie huyo, wakati nataka kumpigia rafiki yake akasema mwambie hapatikani, anaficha nini huyu jamaa katika hali hii, nikamfata nikamwambia hapatikani yeye analia tu, yule dokta, mwingine akasema acha nikuhudumie mimi.

Akaingia nae chumba cha daktari, sijui ilikuwaje baadae nikaona tu anavutiwa kwenye kitanda anapelekwa wodini, nikaambiwa analazwa, dokta akaniita ofisini akaniuliza huyu ni nani yako, nikasema mme wangu.

Akasema okay, wa ndoa? nikasema ndio, akauliza mna watoto nikasema ndio, akasema okay wangapi, nikasema mmoja wa mwaka mmoja akasema okay, sasa wewe ni mtu mzima ukae hapo na naomba unijibu maswali yangu vizuri ili nijue nakusaidiaje, usiogope usinionee aibu, wewe na mumeo huwa mnafanya mapenzi kinyume na maumbile?

Nilishtuka nusu nianguke kwenye kiti, nikasema nini dr? akasema nakuuliza huwa anakufanya kinyume na maumbile? nikasema no akasema ugonjwa alionao umekuwa sugu na inaonyesha ni mchezo wake wa siku nyingi sana hadi kufikia hatu mbaya hivi.

Nikaanza kuvuja jasho, mwili ukaishiwa nguvu macho yakanitoka vinyweleo vikanisimama dr, aliona hali yangu imebadilika ghafla akaniambia tulia nijibu ili nikupime na wewe yawezekana unaumwa, haiwezekani hali hii iwe hivi kwake wewe ukawa mzima, nikasema no mimi hajawahi kunifanya nyuma wala kuniomba hiyo kitu.

Daktari naapa kwa Mungu mmoja na nimepima juzi juzi tu niko salama, akasema naomba nikupime na mimi, sikubisha akanipima, wakati vipimo vinashughulikiwa nikawa namuuliza sasa mme wangu mwisho wake unakuwa nini.

Akaniambia wagonjwa wa hivi tunawapokea sana siku hizi, sijui huu mchezo wameutoa wapi hata kuvaa condom wanasahau, hawajui madhara yake na ukiwaambiwa hawakuamini, sasa huyu wako kuna kipimo nimechukua, na pale tuliharibu wakati anaumwa hakutakiwa kufanya wala kujaribu hata kidogo alitakiwa apate matibabu mapema bila kufanya chochote kile mishipa imeziba, uchafu umeingia kwa ndani, kwahiyo watamfanyia operation ya kumpasua ili kusafisha na akitoka hapo uwezekano wa kupona ni mkubwa ila uhakika wa kusimamisha ni mdogo sana wamfanyie operation.

Nikasema dr kweli unahikia ni kwa ajili hiyo? akasema niko kwenye hii kazi zaidi ya miaka kumi, jinsi kulivyo na vinavyotoka ni dalili mojawapo kabisa hata sijachukua majibu ya vipimo, ila tulia, usimharakishe na maswali huyu anatakiwa kufanyiwa operation usiku huuhuu, hali yake sio nzuri, niliishiwa nguvu nilitamani nimfate kule chumbani nikamuulize huwa unamuingilia nani?

Kivile niliogopa sana nikaanza kulia sana nawaza anapasuliwaje halafu inakuwaje, nililia sana lakini shemeji yangu alinipa moyo kwamba tumuombee, niliomba tu mungu amsamehe ila amponye.

Sisi tulikuwa nje kwenye gari yaani sikuwa sawa kabisa, wakaanza kumuandaa hadi kufika saa kumi na mbili wakamuingiza kumfanyia, akatoka mida ya saa tatu.

Hajielewi kabisa, akalazwa, nikaitwa nikawa naelekezwa namna ya kumuhudumia.

Ilinipa ugumu sana kuwataarifu wengine maana wangejua kilichotokea kwake nikasema sisemi kwa mtu yeyote kama mme wangu anaumwa hata kwa mama yake sisemi ntauguza peke yangu akinifia tutajua mbele ya safari.

Hata rafiki yangu sikumwambia, ila yule shemu wangu niliwambia asiseme kokote nashukuru hadi leo hii sijasikia kokote.

Niliuguza mgonjwa wangu akapona kabisa ila aliambiwa haruhusiwi kufanya awe anatumia dawa na anarudi hospitali ili kuchekiwa akiwa tayari ndio watamwambia.

Nilishindwa kuvumilia kurudi hadi home ndio niulize, nikamuuliza hospitali, wewe unajua unaumwa nini, akasema ndio mke wangu ni uchafu umeziba nikamuuliza.

Jalala hilo? sema kinyesi ndio kimeziba ya hao unaowawafanya, sasa unaruhusiwa leo nakurudisha kwako salama salmin nakuacha mzima kabisa naondoka na mwanangu.

Siwezi kuishi na wewe hadi useme unamfanyaga nani?

Akasema hakuna kitu kama hicho, akakomaa nikasema poa dr, muongo, tuliruhusiwa hao hadi nyumbani, kufika nyumbani alijua natania, nilimuogesha mwanangu nikamwambia dada ajiandae, na mabegi ya nguo nikachukua funguo zangu, hao kwenye gari, nikamwambia naondoka.

Ukitaka nirudi sema kweli ulikuwa unamfanya nani, niliwasha gari na kuondoka zangu na mwanangu na dada wa kazi.

Nilikwenda kijichi kwa rafiki yangu, alipiga sana simu yangu sikupokea baadae mama yake akaanza kunipigia nikamwambia mama muulize sababu ya mimi kuondoka mwambie aseme mwenyewe kwako, mimi sisemi na niko serious, kweli sikusema nikakata simu, usiku kama saa nne akanipigia simu akasema yuko tayari kusema kweli, nirudi nikamwambia nitakuja asubuhi akakataa akasema nirudi usiku ule ule nikasema siwezi drive usiku mimi, akasema nichukue tax atalipa.

Nilizima simu nikalala kwa rafiki yangu asubuhi akapiga tena, nikaenda niliacha watoto na dada huko kijichi, nilipofika tu nikamkuta kaka peke yake, akaanza kulia anasema nimsamehe, mateso aliyopata huyu bwana yalimtosha alikua akikojoa kwenye mrija ulioingizwa huko chini, alikuwa analia kama mtoto, yaani alikonda ndani ya wiki alikuwa anateseka akianza kukojoa ananiita ananishika kwa nguvu anang'ata meno ndio anakojoa aliteseka vya kutosha aisee hadi nilimuhurumia.

Basi nilivyoenda akaanza kulia mke wangu nisamehe nikamwambia niambie ulifira nani akanitajia ni dada mmoja hivi, mfanyakazi wa bank(jina kapuni by admin).

Nikamuuliza ulianza lini?

Akasema siku nyingi, naomba nisamehe nilianza kabla sijakuoa hata wewe, ilia niliapia mke wangu nitamheshimu sitamvunjia heshima, ndio maana niliamua kufanya huko, nikamwambia uliniheshimu asante lakini hukuogopa magonjwa? heshima iko wapi hapo, je tungekutwa tumeathirika ungeniambia nini? mie mwenzio nishapima kila kitu mzima, haya wewe umepima? akasema nisamehe kwanza hatarudia na akirudia niondoke nilimhurumia kwakuwa nampenda sana, nikasema namsamehe na aibu nitamfichia ila huyo mwanamke nitamtafuta nimwambie tu aache.
Nilikubali kumsamehe kwa sharti la kutofanya chochote hadi akapime kwanza.

Tulikwenda hadi hospitali akapima alikutwa negative, wakati anajisubiria maana alikatazwa sex kabisa kwa kipindi hicho, utulikaa miezi mitatu bila kufanya chochote kile, tukarudi tena hospitali wakapima yuko negative, tukarudi home bado hakuruhusiwa kusex, ilifika miezi mitano kasoro nikaitwa na yeye hospitali tukaelekweza how can we sex kwa kipindi cha mwanzo kutuokana na hali yake.

Ilichukua muda sana kufanya kawaida mwanzoni alikuwa anaishia njiani au hakojoi kabisa, niliambiwa kwa upande wao madokta wamemaliza jamaa yako fresh kazi ni kwangu kumuandaa, kumuweka sawa ili aperform maana imeathiri hadi kichwa chake, nilikuwa na hasira sana mwanzoni, mwisho nilimhurumia kwakweli maana nampenda, nikawa najitahidi kumpa upendo wangu wote,namuweka karibu sana.

Ilisaidia sasa hivi yuko vizuri tunaenda kama kawaida na sasa niko na mimba, ya miezi mitano.

Back to the lady from bank,

Nilifunga safari hadi ofisini kwao, nikamuulizia nikamkuta, akaja kuniona, kabinti kazuri huwezi kuamini admin mdogomdogo mzuri sana anaonekana mstaarabu sana nilishangaa yeye ananijua mimi simjui, alishtuka kuniona nikahisi, ananijua nikamuuliza do you know me? akasema no oh yess nikamwambia yes or no! akasema yes ni mrs...................... nilishikwa hasira hapo hapo nilimuwasha kibao paaaaa!

Waliokuwepo karibu waliona, yule dada mwenyewe akanishika mkono tukaongelee nje maana wengi walikuwa hawajashtukia kila mtu yuko busy, waliona wachache waliokuwa karibu ila kuna staff mwenzie aliona.

Nikamwambia kwanini umemtesa hivi mme wangu, kwanini unampa makalio wako mchafu mme wangu hadi kummpa matatizo makubwa vile, kwanini usitulie ukapata wako mbona wewe bado mdogo sana, wakati tunaongea akawa anasema dada naomba tuongee jioni hapa ofisini watasikia nikamwambia nikitoka hapa naingia kuonana na bosii wako.

Nimwambie kaajiri mashetani humu, akatoka mdada mwingine, sie yule alietuona, akamuuliza .................... vipi kwema?

Nimeambiwa nitoke nje kuna mtu amekupiga nani? akasema hakuna alienipiga, nikamwambia mimi nimempiga njoo ujue sababu, yule binti nusu akimbie, akaniambia niko chini ya miguu yako naomba tuongee baadae.

Mwenzie akaja akaniuliza chanzo nikamwambia aseme mwenyewe binti alilia kama kapokea msiba, anasema tu nisamehe nitakutafuta nikamwambia.

Jioni unitafute mwenyewe ikibidi njoo kwangu maana unapajua, jiulize hapa nimefikaje, jina nimepataje, mnasahau kuwa hampendwi nyie mnachezewa tu, tazama sasa karudi kwangu kwa heshima na adabu zote, nimempokea mikono miwili, kanielekeza hadi kwenu hadi unapoishi hadi wazazi wako nimeelekezwa umeharibiwa makalio hayo, mie wangu uko na adabu zake namuhurumia atakaekuja kukuoa... nitafute mwenyewe, niliondoka kwa hasira sana nikaanza kulia kwenye gari, kweli alinipigia saa kumi na mbili akiulizia kama tunaweza kuonana sehemu nyingine sio nyumbani, nilikuwa na hasira nikasema nitamuua nipate kesi, nililia sana niakamwambia nitakutafuta niko mbali, sikumtafuta kama wiki hivi yeye ndio alikuwa akinitafuta na kunitext sms za kuomba radhi nimfichie ufirauni wake.

Niliingia kwenye maombi, nikaomba sana mungu anisamehe nami nawasamehe walionikosea, nilimwambia yule binti kwamba basi nimemsamehe, mme wangu nilisamehe, hadi leo niko nae.
Ni hayo tu,nimejisikia kushare na ninyi

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +