ILIPOISHIA
“Nabii wewe ume tumwa na Mungu kweli kuja kueneza neno lake hapa duniani?”
Swali la raisi Mtenzi likamstua sana nabii Sanga, akahisi haja ndogo ina kwenda kumtoka.
“Ndi….io muheshimiwa raisi”
“Una uhakika?”
“Ndio muheshimiwa”
“Kama kweli Mungu ana kutumia wewe, imekuwaje ukamashawishi kijana wangu mtiifu kumuachia mtuhumiwa aliye shirikiana na mke wako katika kukuteka kwako na pia mtuhumiwa huyo amekuibia mke wako. Eheeee?”
Nabii Sanga akashindwa kabisa kuuzuia mkono wake, ambao taratibu umeeanza kulowanisha boksa yake huku ukilowanisha suruali yake na ukaanza kuchuruzika kwenye miguu yake na kumwagika chini na kuanza kusambaa taratibu kwenye sakafu ya chumba hicho.
kwa maombi yake.
ENDELEA
Mlinzi wa raisi aliyomo ndani ya chumba hicho aliweza kuhushudia mkojo wa nabii Sanga jinsi unavyo sambaa katika chumba hicho.
“Ha….a…a….apaa…..ana”
Nabii Sanga aliendelea kubabaika kwa woga.
“Unataka kuniambia kwamba mke wako hajahusika katika kukuteka wewe?”
Nabii Sanga akazidi kuchanganyikiwa hakutarajia kwamba ujio wake wa Ikulu una weza kumuweka katika wakati mgumu kama huo.
“Mzee zungumza, huwa mimi sina utani na wakosaji na haijalishi nina kujua au sikufahamu. Una cheo gani au huna, na pia mimi nikikosea huwa nina baba makosa yangu, ndio maana mwanangu wa kwanza aliuwawa na Karata kutokana alikuwa ni jambazi na mimi ndio niliye toa amri ya kuuwawa kwake. Haya niambie mke wako ame husika au hajahusika?”
“Amehusika”
Nabii Sanga alizungumza huku mwili mzima ukiwa una mtetemeka.
“Ana takiwa kulipa kutokana na makosa yake aliyo yafanya. Inakuwaje penzi la kijana tu limpagawishe hadi kuamua kuku saliti. Ila kabla sijatuma watu wa kwenda kumkamata, ni kwa nini uliamua kumsamehe mke wako ikiwa ni muhalifu na ukazidi kwenda mbali sana na ukaamua kumsamehe mtuhumiwa wako?”
“Mungu baba ametuambia tusamehe saba mara sabani. Ni kweli kama binadamu mwenye nyongo na hasira, nilitamani kumuona yule kijana ana uwawa kikatili sana. Ila nilitafakari sana kuhusiana na maamuzi yangu, nikahisi kwamba damu ya kijana yule ita nililia mikononi mwangu. Kutokana mimi ndio mtendewa sikuona haja ya kuidhulumu roho ya yule kijana, nikaona ni heri akaondoka nchini Tanzania ili nisimuone”
Nabii Sanga alizungumza kwa kujikaza sana. Raisi Chinas akaka kwenye kiti alicho toka kunyanyuka muda mfupi ulio pita. Akachungulia chini ya meza hiyo na kuona mkojo ukiwa umesambaa chini na akagundua kwamba ume toka kwa nabii Sanga. Kitendo hicho kina muashiria kwamba mtumishi huyo ni muoga. Akamtazama nabii Sanga kwa sekunde kadhaa kisha akatabasamu.
“Mzee una moyo wa ajabu, sijawahi kukutana na binadamu mwenye moyo kama wako. So unataka kuniambia kwamba mtuhumiwa uli mtorosha?”
“Hapan sijamtorosha, ila niliomba aweze kuachiwa huru na kijana hapa. Natambua aliyo yafanya ni nje ya taratibu ya kazi yake, ila nina kuomba uweze kumsamehe na msalaba wake nipo tayari kuubeba mimi”
“Una uhakika?”
“Asilimia mia moja muheshimiwa”
“Mfungue pingu Karata. Msako wako wa kumtangaza Tomas kwenye vyombo vya habari ukatishe mara moja na atafutwe kimya kimya”
“Nashukuru sana muheshimiwa. Nashukuru sana”
RPC Karata alizungunmza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana. RPC Karata akafunguliwa pingu na mlinzi wa raisi na kutoka chumbani humo.
“Nipe siri ya kuwa na moyo kama huo wako”
“Ni kumjua MUNGU tu muheshimiwa raisi”
“Mimi mbona nina soma biblia, nina sali sana ila sijawahi kusamehe kwa namna uliyo fanya wewe”
Raisi Chinas Mtenzi alizungumza kwa upole huku akimtazama nabii Sanga
“Unajua nilipo sikia kwamba ulitoa hadi amri mwanao auwawe kutokana ni jambazi, kidogo nime stuka sana. Ina bidi tufanye maombi kwa ajili ya hiyo hali. Kwa kiongozi mkubwa kama wewe wa nchi, ukishindwa kuzuia hasira yako na ukawa ni mtu wa kukasirika sana, ipo siku uta iingiza nchi katika matatizo makubwa”
Nabii Sanga alizungumza kwa kujiamini sana kwani tayari amesha upata udhaifu wa raisi Chinas Mtenzi.
“Ni kweli, una jua kuna kupindi nina jikuta nina hasira hadi nina tamani kuachia madaraka, ila washauri wangu huwa wana pambana sana na hasira yangu hadi nina badilisha maamuzi yangu”
“Ohooo pole sana muheshimiwa raisi. Kama unaweza kuniruhusu kufanya mauombi kwa ajili yako niambie nifanye”
“Ahaa nipo tayari pia, nahitaji tutoke kwenye chumba hichi, ukabadilishe nguo kisha tufanye maombi. Mpeleke nabii Sanga kwa fundi wa suti, muambie ashoneshe suti ndani ya lisaa awe amesha maliza”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Nabii Sanga akaongozana na mlinzi huyo hadi katika ofisi ya mshonaji mkuu wa suti za raisi na wasaidizi wake katika ikulu hiyo. Nabii Sanga akachagua kitambaa anacho hitaji kushonewa na staili ya suti anayo ihitaji kisha ikaanza kushonwa huku akiisibiria hapo. Mshonaji huyooo mwenye kipaji kikubwa na kasi ya ajabu katika kazi yake ya ushanaji, ndani ya muda mchache akamaliza kushona suti hiyo na nabii Sanga akakabidhiwa ikiwa tayari imesha kamilika.
“Unaweza kuivaa tu mzee, hakuna haja ya kijaribu”
“Kila kitu kipo sawa”
“Ndio mzee”
“Aisee una kasi kubwa sana”
“Nashukuru sana mzee”
Nabii Sanga akaonyeshwa chumba cha kubadilishia nguo, ndani ya chuma hicho akakuta bafu. Akaoga kwa haraka kisha akaivaa suti hiyo. Hakika hapakuwa na sehemu ambayo ime kosewa au kuubana mwili wake. Vipimo vyote alivyo vifanya fundi huyo vime kaa vizuri sana kwenye suti yake. Nabii Sanga akatoka chumbani hapo na mmoja kwa kwa moja akaepelekwa eneo analo ishi raisi Chinas na familia yake ndani ya ikulu hiyo hiyo. Akamkuta mke wa raisi Chinas, wakasalimiana kwa furaha na bahati nzuri wana fahamiana.
“Karibu sana mtumishi, ni muda mrefu sana hatujaonana”
“Ni kweli, ila muna endeleaje na familia?”
“Ahaa Mungu ana saidia, majukumu ndio hayo yameongezeka. Kipindi kile nilikuwa huru kwenda sehemu yoyote mwenyewe, ila kwa sasa hadi uongozane na ving’ora”
“Ahahaa ila ndio hivyo Mungu ame kupandisha kutoka chini kwenda juu”
“Ni kweli”
Raisi Chinas akaingia sebleni hapo.
“Samahani mtumishi nimechelewa kufika”
Samahani hiyo ikamfanya mke wa raisi kushangaa kwani katika kipindi cha maisha yake hajawahi kumsikia mume wake akimuomba mtu wa kawaida sahamani zaidi ya mama yake mzazi tu.
“Hakuna shaka mzee”
“Mama Lily nabii hapa amekuja kuongoza maombi. Hivyo kama kuna wengine humo waite waje kujumuika nasi”
“Wametoka”
“Sawa, nabii Sanga unaweza kuanza maombi, kidogo nime kimbia ofisini”
Nabii Sanga akaanzisha ibada hiyo fupi kwa nyimbo za kuabudu kisha akaanzisha mauombi. Ndani ya muda mfupi raisi Chinas akaanza kuanguka chini huku akigaraga gara kana kwamba mtu mwenye ugonjwa wa kifafa. Nabii Sanga hakuiogopa hiyo hali zaidi ya kuendelea kusali na kuyakemea mapepo mengi sana yaliyomo ndani ya mwili wa raisi Chinas.
“Tokaaaaa kwa jina la Yesu”
Nabii Sanga alizidisha kukuemeea na ndani ya robo saa mapepo hayo yote yakatoka mwili mwa raisi Chinas. Wakasaidiana na mke wake na kumnyanyua huku raisi Chinas akionekana mwili wake kumuishia nguvu.
“Muheshimiwa una jisikiaje?”
“Ehee?”
“Una jisikiaje?”
“Nahijhisi mwili ni mwepesi sana”
“Kweli?”
“Ndio na huwa nina sumbuliwa na maumivu ya mgonga na hata asubuhi ya leo nilichoma sindano ya kupunguza maumivu, ila maumivu hayo yote yametoweka”
“Hakika Mungu amefanya muujiza wake. Una jua hatua uliyo kuw aumefikia, ilibaki kidogo sana uiingize nchi kwenye vita. Sasa ni wakati wa kwenda kusawazisha tofauti na baadhi ya viongozi ambao ume pishana nao kutokana na kauli zako ambazo ziliwaumiza na wengine kuanza kukuwazia mambo mabaya”
“Nimekuelewa nabii. Hakika nilikuwa sipendi kushauriwana wala nilikuwa simsikilizi mtu wa aina yoyote, ila hali ya chuki ndani yangu naona ime toweka pia”
“Mungu ni mwema”
“Hakika Mungu alikuwa na makusudi yake ya kukutanisha. Nabii uta rudishwa nyumbani na endapo utakuwa na haja yoyote ya msaada wangu basi nina kuomba uweze kuwasiliana nami”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Raisi Chinas akampatia nabii Sanga namba yake ya simu kisha naye akachukua namba ya nabii Sanga. Wakapiga picha kadhaa kwa pamoja, kisha wakatoka nje, nabii Sanga akapewa walinzi wa kumrudisha nyumbani kwake huku raisi Chinas akielekea kwenye mkutano na balozi kutoka nchini Ujerumani, huku moyoni mwake akijiona ni mtu mpya na mwenye furaha kubwa sana tofauti na siku za nyuma.
***
Magreth akawakaribisha mafundi wa kufunga kamera katika nyumba yake. Akawapa maelezo ambayo nabii Sanga aliyatoa na kazi ikaanza mara moja. Simu yake ikaanza kuita na kukuta ni nabii Sanga.
“Vipi mafundi wamefika”
“Ndio mpenzi upo wapi?”
“Nipo njiani nina kuja hapa”
“Sawa, nikuandalie chakula kwa maana sasa ni mchana”
“Kama huto jali fanya hivyo”
“Sawa mpenzi wangu”
Magreth akakata simu na kuanza kupiga chakula aina ya biriani. Akapika chakula kingi ili mafundi hao nao waweze kupata chakula. Nabii Sanga akafika nyumbani hapo na kuanza kumuadisia Magreth safari yake hiyo ya Ikulu.
“Hongere sana”
“Nashukuru, yaani hapa nina furaha nime kuwa mtu wa karibu sasa na raisi. Yaani ni kama muujiza sikutegemea”
“Kweli Mungu ni mwema”
“Mafundi wana endeleaje na kazi?”
“Kama unavyo ona wana zidi kufanya kazi”
Nabii Sanga akamfwata fundi mkuu na kuendelea kumumpa maelekezo anayo yahitaji yaweze kufanyika. Hadi inafika majira ya jioni mafundi hao wakawa wame maliza kazi ya kufunga kamera hizo na kuanza kuwapa mafunzo nabii Sanga na Magreth jinsi ya kuzitumia kwa kupitia simu zao za mkoni. Maelekezo hayo yalipo isha kwa pamoja wakajumuika na kupata chakula cha usiku. Kisha nabii Sanga akafanya maliopo ya kazi hiyo kwa njia ya mtandao. Mafundi hao wakaondoka na kuwaacha nabii Sanga na Magreth ambao hawakuwa na jambo jengine la kufanya zaidi ya kupeana burudani ya penzi moto moto.
“Kwa hiyo utaondoka na kuanicha peke yangu mwenzi mzima?
Magreth alimuuliza nabii Sanga kwa sauti ya upole mara baada ya kumaliza mtanange huo.
“Yaa hakuna jinsi, ila hakikisha hicho kiasi cha pesa nilicho kuachia una fungua biashara”
“Sawa nitafungua mgahawa nina imani hadi una rudi basi nitakuwa mbali sana kibiashara”
“Kweli, acha nirudi nyumbani nijiandae kwa safari kwa maana inanibidi kuondoka asubuhi”
“Sawa mpenzi wangu”
Nabii Sanga akaagana na Magreth na kuondoka eneo hilo. Nabii Sanga akafika nyumbani kwake na kupokelewa kwa mabaha mazito na mke wake.
“Mbona ume chelewa mume wangu”
“Nisamehe kwa kweli. Yanai leo nina habari njema”
“Habari gani tena mume wangu”
“Nimetoka ikulu kumfanyia maombi muheshimiwa raisi”
“Weeee!!! Acha kunitania mume wangu”
“Haki ya Mungu na ushahidi wa picha huu hapa”
Nabii Sanga akaanza kumuonyesha mke wake picha alizo piga ikulu na raisi.
“Yaani yule mzee alikuwa na mapepo, huwezi amini ameanguka”
“Sema kweli?”
“Hoo yaani, tena unajua jambo lililo nipeleka pale ni lakowako”
“Lipi?”
“La kuniteka, RPC alibanwa kwa kutishiwa kufukuzwa kazi, hakuwa na jinsi kijana wa watu akaamua kufunguka kila kitu, yaani nilikuwa nipo sehemu, sijui hata walijuaje nipo sehemu hiyo. Walinzi kama kumi hivi walikuja kunichukua mzoga mzoga hadi nikahisi kuchanganyikiwa, ila namshukuru Mungu kile nilicho kuwa nimekifikiria hakikuwa hicho”
“Ohoo Mungu. Kwahiyo raisi ametambua kwmaba mimi ndio nime kuteka?”
“Ndio ila kwa jinsi nilivyo muombea basi amekuwa mtu wangu wa karibu sana. Sasa nina imani ile biashara ambayo uliniambia jana tuna kwenda kuifanya”
“Sasa mume wnagu hembu niambie. ALihitaji kufanya nini?”
“Alitaka kutuma walinzi wake waje kukukamata ila kwa bahati mbaya au nzuri niliweza kumshawishi kwa neno la Mungu, akalainika basi nikaliua soo lako juu kwa juu”
“Waacha weee, na hii suti?”
“Nimeshonewa huko huko ikulu yaani mke wangu hapa nina bonge moja la furaha.”
“Sawa mume wangu, nimekata tiketi za saa moja asubuhi, hivyo saa kumi na mbili ina bidi tuwe uwanja wa ndege”
“Sawa mke wangu hilo haina shida”
Nabii Sanga alizungumza kwa furaha sana kwani ukaribu wake na raisi hakika utaanza kumsaidia kupitisha biashara zake haramu ambazo zina endelea kumuingizia kipato kikubwa sana cha pesa.
***
Levina na Tomas wakafika uwanaja wa ndege majira ya saa moja usiku. Kwabahati mbaya wakakutana na tangazo katika shirika la ndege walilo likata, kwamba ndege ime pata itilafu hivyo wana ombwa waweze kusubiria hadi pale ndege itakapo tengemaa ndipo safari ianze.
“Yaani haya mashirika ya nchi yana kera sana”
Tomas alizungumza huku akikaa kwenye moja ya kiti kilichopo kwenye eneo la abiria wanao subiria kuondoka nchini Tanzania.
“Maswala ya itilafu ni kawaida katika kila kitu, ndio maana hata wewe kuna kipindi una umwa. Hivyo acha kulalamika”
“Hata kama, sasa kwa nini wasilete ndege nyingine”
“Una hisi ndege ni mabasi mpenzi wangu, kwamba likiharibika basi hili lina letwa jengine na kufualisha abiria. Hembu kuwa mpole, au hupendi kukaa na mimi hapa na una naka uwahi kuondoka”
“Napenda”
“Sasa mbona una kuwa hivyo. Wewe tulia, ndege ikifaa, mutanangaziwa na muta ondoka”
Levina aliendelea kumtuliza Tomas mwenye uchu wa kuondoka nchini Tanzania. Masaa yakazidi kuyoyoma hadi saa kumi na mbili alfajiri ndipo walipo anza kutangaziwa kwamba ndege yao ipo tayari kwa ajili ya safari.
“Waseng** sana hawa”
Tomas alizungumza huku akiwa amekasiraka sana. Levina akatabasamu tu, kwani Tomas amekereka sana. Wakanyanyuka kwenye viti hivyo na wakakumbatiana kwa muda kidogo huku kila mmoja akiwa na hiasi kali za mapenzi.
“Jichunge na ujilinde Tomas”
“Usijali mpenzi wangu. Tambua kwamba nina kupenda sana”
“Hata mimi nina kupend……..Tom ona kule”
Levina alizungumza huku akimuachia Tomas, wakageuka nyuma na kumuona nabii Sanga na mke wake wakiwa miongoni mwa abiria walipo hapo uwanja wa ndege huku wakionekana kusoma soma baadhi ya matangazo yaliyopo uwanjani hapo jambo lililo mfanya Tomas kuanza kujawa na chuki dhidi yao kwani wao ndio wana mfanya sasa hivi kuishi katika sura ambayo sio yake.
ITAENDELEA
Haya sasa TOMAS amewaona maadui zake nao wakiwa ni miongoni mwa watu wanao odoka nchini Tanzania ni nini atakacho kifanya.? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 28.
Thursday, May 23, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments