Pages

Thursday, May 23, 2019

SMS TAMU ZA KIMAHABA ,HAKIKA LAZIMA MPENZI WAKO AJE AKUTUNUKU UTAMU WA USIKU

Raha kwako naipata, hakika nimeridhika,
Kwako hakuna matata, moyo wangu umefika,
Usiku ninakuota, kwako naliwazika,
Siogopi kukupenda, hata watu wakisema.

Upendo uso kipimo, wewe nimekupatia,
Moyo unalo tuwamo, raha naipata pia,
Kwenye moyo wangu umo, raha yangu ya dunia,
Siogopi kukupenda, hata watu wakisema.

Wenye kusema waseme, waseme hadi wachoke,
Roho zao ziwaume, ziwaume wakereke,
Mioyoni ziwachome, wachomeke wakauke,
Siogopi kukupenda, hata watu wakisema.

Wenye wivu uwashike, uwashike uwagande,
Zaidi wahuzunike, wahuzunike wakonde,
Chakula kisiwashuke, wacha mie nikupende,
Siogopi kukupenda, hata watu wakisema.

Ni raha mwangu moyoni, wewe kuwa ndiwe wangu,
Nimezama furahani, rahani chini ya mbingu,
Sisi tumo mapenzini, tuache ya walimwengu,
Siogopi kukupenda, hata watu wakisema. 




Mpenzi nakusifia, uzuri wa malaika,
Urembo ulozidia, hakika umeumbika,
Nami ninajivunia, kwako wewe nimefika,
U pekee duniani.

Hakika we u mzuri, kwa sifa zenye kujaa,
Kama nyota alfajiri, maishani unang'aa,
Uzuriwo u dhahiri, hakuna anokataa,
U pekee duniani.

Unayo sauti tamu, nyoka kutoka pangoni,
Mejaa mashamshamu, utamu masikioni,
Huniletea wazimu, kusisimuwa moyoni,
U pekee duniani.

Una rangi asilia, yang'ara kama dhahabu,
Rangi iliyotulia, wengine yawapa gubu,
Sichoki kukusifia, wewe ndo wangu muhibu,
U pekee duniani.

Macho kama ya gololi, na mapole kama njiwa,
Sifa wazistahili, kwani umebarikiwa,
Leo nasema ukweli, wanifanya kunogewa,
U pekee duniani.



Mwendo wako wa kuringa, mrembo mwendo mwendole,
Moyo wangu waukonga, waujaza raha tele,
Nipo radhi kukuhonga, sikupate watu wale,
U pekee duniani.

Sifa zako zimezidi, wewe u nambari wani,
Wewe kwangu maridadi, mwingine simtamani,
Nakupa yangu ahadi, daima 'takuthamini,
U pekee duniani.

Wewe wanipa sababu, kufurahia mapenzi,
Wako ustaarabu, hakika nitakuenzi,
Kukutunza ni wajibu, udumu wetu upenzi,
U pekee duniani.




leo nataka kuzungumzia maneno ya mahaba, jamani tunajuwa ya kwamba ukiwa na mpenzi wako unafurahi zaidi pale japo muda fulani atakupa maneno matamu, na mazuri na yenye kuzidi kukupa moyo wa wewe kuzidi kutaka kuwa naye...



sasa kuna wapenzi wengine hata mimi nilishapitia mmoja wakati fulani, jamani wanaume na wanawake wenzangu hebu tujitahidi maneno kama mpenzi, honey, sweety, mkiwa mbele za watu kumuita mpenzi wako sio mbaya maana wengine haswa waliozaa utasikia baba fulani mara mama fulani inamaana baada ya kuzaa mpenzi, sweety, honey umeisha?????? tunawapenda sana watoto wetu lakini wao wananafasi yao na mwenza wako ananafasi yake...



kwenye sita kwa sita watu utawakuta kimya tu madai wanasikilizia uhondo, jamani kuna maneno pale ama mnaoneana aibu sasa kwangu raha mpenzi aongee aniambie anavyojisikia wapi niongeze, vipi nikae, wapi nimshike kwa sauti ya taratibu na yenye mapenzi tele....sijui wewe mwenzangu



sasa pakiwa kimya tu jamani na ndio kwa mfano kitanda ndio vileeee ukigeuka tu majirani mpaka watujuwa hizo kwinyo kwinyo kwinyo hapo kwenye mechi sindio balaa maana utakuwa usikilizii raha unakilaani kitanda tu hichi nacho mpaka watu wajuwe leo napewa.....



kama mnaona aibu kuongea basi kama chumbani kuna redio wekeni hata mziki wa taratibu kuwahamasisha zaidi, maana ule ndio utakaoongea kwa niaba...

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +