Tabia hii imeenea kwa wasichana na hata walioko kwenye ndoa.
↓↓↓
Baadhi ya wasichana hulinda bikra zao lakini akawa anatumika kwa nyuma kisha akija kuolewa mume anampata mke bado ni bikra nyuma kuwazi hatimae wakati wakuzaa kunamletea shida na ndio hujulikana wakati huo wa kuzaa pale mtu anapo piga pumzi zina kuja kwa nyuma badala ya mbele.
↓↓↓
Pia wanaume wengine huwataka wake zao unyumba kinyume na maumbile . Na pia haifai kuchezea tundu ya nyuma kwa kuingiza kidole . Japo tumeambiwa mke amtii mumewe lakini twaa ya kheri sio twaa ya maasi
↓↓↓
"Hakika utiifu ni katika wema". (Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy, na Abu Daawuud.)
↓↓↓
Na pia,
"Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba". (Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, An-Nasaaiy na Ahmad.)
↓↓↓
Imekatazwa mwanamume kumuingilia mkewe nyuma
↓↓↓
Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) ansema
↓↓↓
“(Waingilieni wake zenu kwa mtindo wa) Kwa mbele au (kwa mtindo wa) kwa nyuma lakini epukeni dubur (tupu ya nyuma) na (kuwaingilia wakati wako) kwenye hedhi.” (Tirmidhi)
↓↓↓
Allaah anasema:
↓↓↓
"Wakishatwaharika basi waendeeeni katika pale Alipokuamrisheni Allaah. Hakika Allaah Huwapenda wanaotubu na Huwapenda wanaojitakasa. Wake zenu ni konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo" (2: 222-223).
↓↓↓
Na kuziendea konde zenu mpendavyo, si sehemu ya nyuma, bali ni sehemu ambayo inapatikana uzazi na ndio ikafananishwa na konde/ shamba kwa sababu shamba hulimwa na kuota mazao ambayo kwayo hupatikana mavuno.
↓↓↓
♣Kwa hivyo, ni ubaya sana kwa mwanamume kumwendea mkewe kwa nyuma na athari yake ni kubwa kwani inampatia shida sana mwanamke wakati wa kuzaa na matatizo mengine. Pia inaleta madhara ya kiafya, inakwenda kinyume na maadili matukufu na hii ni tabia mbaya sana.
↓↓↓
♣ Hadiyth zifuatazo zenye makatazo ya kumuingilia mke nyuma :
↓↓↓
1. "Allaah Hatomtazama mwanamume mwenye kumuingilia mkewe kwa nyuma" (an-Nasaaiy na Ibn Hibbaan kwa Isnadi nzuri).
↓↓↓
2. ♣ "Amelaaniwa mwenye kumjia mwanamke kwa nyuma" (Ahmad, Abu Daawuud na Ibn 'Adiy).
↓↓↓
3. ♣ "Mwenye kumuingilia mwenye hedhi au mwanamke kwa nyuma au kumuendea mchawi na kumuamini kwa anayosema basi amekufuru kwa aliyoteremshiwa Muhammad" (Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah, na Isnadi yake ni Sahihi).
↓↓↓
4. ♣ "Twaawuus amesema: 'Ibn 'Abbaas aliulizwa kuhusu mtu anaye muingilia mkewe kwa nyuma'. Akasema: 'Huyu ananiuliza kuhusu ukafiri'" (an-Nasaa'iy).
Friday, May 24, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments