Pages

Wednesday, May 22, 2019

Tatizo la Kukaa muda mrefu bila kufanya mapenzi ( kutombana)

Je, kuna madhara kama mtu akikaa muda mrefu bila kufanya mapenzi?
Ukweli ni kwamba hakuna madhara yoyote ya kiafya ukikaa muda mrefu bila kujamii ana. Hakuna madhara yatakayokutokea kwenye sehemu zako za siri au katika sehemu nyingine ya mwili wako. Mwanaume au mwanamke akianza kujamii ana baada ya kukaa muda mrefu, atapata raha na starehe.
Watu wengine wanasema kwamba kutofanya mapenzi kunasababisha kuwa na chunusi usoni au sehemu za siri, au hata kuchanganyikiwa kiakili. Siyo kweli kwamba hali hizi zinasababishwa kwa kutojamii ana, vyanzo vya hali hizi ni tofauti.
Uwe na uhakika kwamba kutojamii ana ni salama kabisa kwako na huwezi kupata madhara yoyote. Lakini kama tulivyosema awali, kujamii ana kunaweza kukaleta matatizo mengi kama mimba i isiyotarajiwa, magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizo ya VVU na UKIMWI.

Je, ni kweli kwamba mwanamke akikaa muda mrefu akiwa bikira ni shida sana kuvunja kizinda akijamiiana kwa mara ya kwanza?
Ile ngozi ndani ya uke i inabakia kuwa nyembamba na laini sana, hata mwanamke akiwa bikira katika umri mkubwa i inaweza kuchanika. Kwa hiyo hamna haja ya kuwa na wasiwasi wa kutoweza kuvunja kizinda ukisubiri muda mrefu kabla ya kujamii ana kwa mara ya kwanza.

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +