Wachumba wakiwa wamejawa na furaha. Picha/FOTOSEARCH
Kwa Muhtasari
Wataalamu wengi wa mapenzi wanakubaliana kwamba wachumba wanapotumia mbinu tofauti za kuburudishana kitandani, wanaridhishana na wanawake wanafikia kilele cha tendo la ndoa.
KUNA kitu kimoja tu ambacho Susan* anatamani maishani mwake. Sio pesa, sio gari wala si vipondozi, bali ni kupata burudani tosha la mapenzi.
Anasema maishani mwake, hajawahi kufikia kilele cha tendo ndoa hata mara moja.
“Sijawahi kufikia kilele cha tendo la ndoa. Kwangu shughuli ni shughuli tu. Ninavumilia tu kwa sababu nampenda mpenzi wangu kwa dhati,” asema Bi Susan na kuongeza kuwa wakati mwingine anachukia tendo hili ili asiache kwenye njia panda.
Ili kuhakikisha kwamba kamwe havujiki moyo wakati wa shughuli, wataalamu wanasema Susan anaweza kutumia mbinu za kisasa za kufanya mapenzi.
Wanasema imegunduliwa kwamba kwa kubadilisha staili za kula uroda wachumba wanaweza kuridhishana kikamilifu na kufikia kilele cha shughuli hii muhimu.
“Kwa kutumia staili tofauti za kulishana uroda wachumba huridhishana kikamilifu,” asema mwanasaikolojia Kathy David.
Wataalamu wengi wa mapenzi wanakubaliana kwamba wachumba wanapotumia mbinu tofauti za kuburudishana kitandani, wanaridhishana na wanawake wanafikia kilele cha tendo la ndoa.
Kulingana na mwanasaikolojia Bi David aliye pia mwandishi wa vitabu vya mapenzi wachumba wanaotumia ubunifu wakati wa burudani kitandani wanaridhishana vilivyo.
Bi David asema sio siri kwamba wanaume wengi wamekuwa wakiwapoteza wachumba wao kwa kukosa kuwaridhisha kitandani.
“ Ni kweli watu wengi na hasa wanaume wamekuwa wakiwapoteza wachumba wao wa kukosa kuwapagawisha wakati wa tendo la ndoa.
Hata hivyo wanaotumia ubunifu na kutumia staili tofauti huwa hawana tatizo lolote,” asema na kuongeza kuwa utaalamu wa kurushana roho ndio msingi wa ndoa na uchumba wowote ule.
Bi David asema wachumba wanapasa kuwa wakibadilisha mbinu ili kufanya penzi kunoga na kupatiana shibe la burudani.
Anasema ubunifu na staili tofauti za kurushana roho huongeza ladha tendo la ndoa.
“Unaweza kutia nakshi burudani faraghani kwa kutumia mitindo mbalimbali ya kula uroda inayoendelea kuvumbuliwa kila siku,”asema na kuongeza kuwa kizazi cha wakati huu hakiridhishwi na mitindo ya zamani wanayosema imepitwa na wakati.
“Hizi sio nyakati ambazo mwanamke alikuwa akilala chali na kusubiri mwanaume apande juu yake. Kila mmoja ana wajibu wa kuchangia kufanikisha tendo la ndoa,” asema.
Kulingana na Bi David mwanamke anaweza kumfanya mwanaume alipuke kwa raha kwa kuwa juu yake na kumwongoza akiwa nahodha wa mechi kitandani.
“Mwanamke anaweza kuchukua usukani na kuwa nahodha wa mechi na kumfanya mchumba wake kuridima kwa raha ya ajabu. Na kwa sababu nahodha uelewa na kufahamu mechi vilivyo, ushindi lazima upatikane,” asema.
Anaeleza kwamba wanawake wanaojua kuwaelekeza mwanamume wanapocheza rumba kitandani huwapagawisha kimapenzi.
“Muulize mchumba wako kinachomtia kichaa mnapolishana asali. Mwelekeze ipasavyo huku ukiwasiliana na hisia zako mnapoelea katika bahari ya mahaba ,” asema.
Wataalamu wa mahaba wanasema watu wengi hukosa kuwafikisha wachumba wao katika kilele cha mapenzi kwa kutojiwachilia wakati wa tendo la ndoa tatizo ambalo baadhi ya mitindo ya kisasa inalenga kutatua.
Kulingana na Bi Libby Keatinge mwanasailokojia mwenye uzoefu mkubwa wa maswala ya mapenzi, ni muhimu kujiwachilia ili kupata matokeo bora ya raha wakati wa kulishana tunda.
Anasema ulaji uroda hufanikiwa ipasavyo ikiwa kuna mawasiliano ya mwili na akili. Bi keatinge asema baadhi ya staili za kisasa za kufanya mapenzi zimenuiwa kuimarisha hali hiyo.
“Unaweza kubadilisha maisha yako ya mapenzi kwa kuchagua baadhi ya mbinu ambazo wataalamu wamevumbua ili kupamba burudani na mchumba wako.”asema.
Kwenye kitabu Discovering Erotic Sex, Bi Keatinge anaorodhesha baadhi ya mitindo iliyothibitishwa kukata kiu cha penzi cha wanaoitumia.
Anasema mitindo hiyo humpatia mwanamke fursa ya kutawala wakati wa kucheza goma kitandani na mpenzi wake. Hata hivyo mtaalamu huyu asema sio staili zote za kisasa zinawafanya vidosho kuwa rubani wa ndege ya mapenzi.
“Staili za kisasa zimebuniwa ili kuleta usawa na kuhakikisha kila mmoja ametawala uwanja kwa awamu tofauti. Itatengemea aina ya mtindo na eneo la kusakatia goma,” asema.
Kusimama
Wataalamu wanakubaliana kwamba mawasiliano ya kihisi, kimwili na kiakili ndio msingi wa kufanikisha tendo la ndoa.
“Mnaweza kufanya mapenzi mkisimama, mkiinama mkichuchumaa, kwenye bafu,sakafuni kwenye zulia, mezani kwenye kochi na hata ndani ya gari. Hizi zote ni staili na maeneo ya kufanyia mapenzi. Hata hivyo cha muhimu ni mawasiliano kati ya mwili, akili na hisia zako zitakazokupeleka katika kilele cha tendo lenyewe,” asema.
Bi David asema mazingira ya kusakatia mechi pia huchangia kufanikiwa kwa staili yoyote ya kufanya mapenzi. “ Ikiwa unatumia mbinu yoyote ya kufanya mapenzi katika mazingira yasiyofaa ni vigumu kufikia kilele cha mlima wa ashiki,” asema katika makala yake kwa jina 5 things men think about sex.
Kulingana na Bi Keatinge wachumba wanaweza kufufua maisha yao ya gono na kujenga upya tajiriba ya kutifua vumbi kitandani kwa kutafuta na kutumia staili zinazowafaa.
Hata hivyo anasema ni hatari kumlazimisha mchumba wako kutumia staili isiyompendeza akisema ni kama kusukuma gari ya moshi mlimani.
Bi Keatinge asema kumshinikiza mrembo kutumia staili asiyoitamani ni kumwongezea mateso na anaweza kukuchukia maisha yake yote.
“Wachumba wanafaa kukubaliana staili zinazowafaa kuburudishana. Ni makosa kumlazimisha kiosha roho wako kutumia staili asiyoitamani kwa sababu itamwongezea mateso,” asema jambo ambalo watu wengi wanakubaliana nalo.
Anasema wachumba hawafai kukubali chochote kiwe kikwazo katika juhudi za kusaka shibe la uroda. “ Kila mmoja anapasa kumhusisha mchumba wake katika kila hatua hadi amfikishe katika kilele cha mlima wa mahaba,” asema.
Friday, May 24, 2019
UMUHIMU WA KUFIKA KILELE KWA MWANAUME NA MWANAMKE WAKATI WA KUMEGA TUNDA
Posted by
NeverGoBack
on
1:18 PM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments