Pages

Wednesday, May 22, 2019

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME ,, VYANZO VYAKE NA TIBA YAKE


JE UNATATIZO LA NGUVU ZA KIUME?>>> FAHAMU VYAKULA VINAVYO ONGEZA NGUVU ZA KIUME WAKATI WATENDO LA NDOA
 Tatizo  upungufu wa nguvu za kiume ni sugu na limekuwa  ni shida miongongi mwa wanaume wengi. japo kuwa kuna baadhi ya vijana/wanaume hawajitokezi hadharani ila wamekuwa  wakiuliza maswali mengi sana kwa siri. ikumbukwe kuwa ndoa nying zimevunjika na zingine kupoteza mahusiano ya karibu baina ya wapenzi na pia kuongezeka kwa tatizo la USALITI KATIKA MAPENZI.
   wengi wamekuwa wakijiuliza kuwa tatizo hili husababishwa na nini?hapa nitataja kwa ufupi:

kujichua mara kwa mara( punyeto)
kufanya mapenzi mara kwa mara na watu waliowazidi umri.
kutopata vyakula vyenye kuchochea hamu ya mapenzi na nyenye kuleta  nguvu mwilini.


AINA YA VYAKULA VINAVYOONGEZA UWEZO KATIKA TENDO LA NDOA:




Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:

PILIPILI
Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya mtu akawa na hisia kali za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema kwa wale wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.

PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.

NDIZI
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.


CHAZA NA PWEZA
Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.

POMEGRANATE
Ni aina fulani ya matunda mekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.

MVINYO MWEKUNDU
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo.

MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya njema.

VANILLA
Vanila husaidia kuamasha hamasa mwili.Mwisho wa aina hizi za vyakula ni TIKITI MAJI ambalo linatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +