Pages

Saturday, May 18, 2019

WATOTO WA MUME WANGU, WANATAKA NIACHWE, MAMA YAO ARUDIWE

Nilikuwa na uhusiano na baba mmoja huku kondoa ambae ni mtu mzima sana kwangu, lakini kwakuwa mapenzi hayachagui umri, basi tulipendana sana, na nilipomuuliza kwa umri ule alionao aniweke wazi kama ameoa, alisema walishaachana na mkewe, ila anawatoto watatu mabinti wakubwa wawili wa umri kama wangu, na wakiume mmoja.

alinipeleka kwao mwanza, akanitambulisha kwao, na ni kweli kwamba waliachana na mkewe, basi tukaanza maisha ya pamoja, yeye ni mfanya biashara! Na mm nina grocery yangu. baada ya miaka miwili nikajaliwa kupata mtoto wa kiume, nilimwambia tumeshachunguzana vya kutosha, sasa tufunge ndoa tuishi kiharari, akakubali, wakati tuko kwenye maandalizi ya ndoa alipigiwa simu huko kwao, kwamba watoto wake wanataka kuja, mimi sikuwa na hofu yeyote, nilimkubalia waje tu!

Violet, toka hao watoto wamefika, ndani hatuna amani hata kidogo, tunaishi kama mtu na wake wenzie, mimi kawaida huwa sipendi kuongea ongea lakini watoto hawa wamefanya niongee, Ugomvi kila siku, na kuna siku nilikuwa nafua nguo zangu, mtoto wa mume wangu wa kiume anamiaka 27, akatoa nguo zake zote mimi nifue, nilikataa kwakweli, ukizingatia hakuwa mgonjwa kusema anahitaji msaada, wale wa kike hawataki kufanya kazi yeyote ile, kukicha tu, sitting room kuangalia CD, kupika nipike mimi, au msichana wangu wa kazi wao wanataka kula tu, mbaya zaidi wanasema umemng’oa mama yetu nawewe jiandae tutakutoa, wakati mimi nilikuta wameshaachana kabisa. Na hapa tunapokaa ni nyumba yangu mimi. Baba yao kanikuta nayo

Kingine Hawampendi mwanangu kabisa, kuna siku nilirudi toka kazini, nikakuta mtoto kavimba mdomo wote, hawezi kuongea, nikamuuliza mschana, imekuwaje, akasema Regina (mtoto wa mwsho)wa mume wangu alimsukuma toka mlangoni hadi chini, akaangukia tofali, mdomo ukachanika kwa chini, nililia sana, nilichukia, nikawafata walikuwa chumbani kwao, alichonijibu akasema mwanao mjeuri, nilimuuliza wewe binti mkubwa miaka 24 utagombana na mtoto wa miaka mine kweli? wakati naongea nao walinirukia walinipiga sana,

Wakat yanatokea haya mume angu alikuwa safari, nilimpigia simu aliporudi nikamueleza, aliwasema sana, ila mimi nilimwambia hawa watoto wameshakuwa wakubwa, miaka 24 na 27 na huyo mkubwa 30. Wajitegemee, kwanini wakae kwangu ? nilimshauri awape mtaji wakafanye biashara, watoto walichukuwa pesa, na kuondoka hawakuondoka, na wamesema hawatoki pale, hadi mimi niondoke aje mama yao, sina amani wala raha hata kidogo, nisaidieni mwenzenu.

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +