Pages

Thursday, April 25, 2019

CHEKA POLE POLE USIJE VUNJA MBAVU ZAKO


KICHEKESHO: Ajira ngumu!! Cheki hawa walivyoamua kujiajiri

AJIRA NGUMU!!
Jamaa mmoja alienda kuomba kazi Mbuga ya Wanyama, akaambiwa nafasi ya Kazi ipo ila hakuna Sokwe, "hivyo utajifanya Sokwe na tutakupa ngozi utavaa"
Jamaa siku ya kwanza akavaa, walipokuja watalii mambo yalienda vizuri, Siku iliyofuata Banda lake liliwekwa juu ya Banda la Simba, Jamaa ktk kuongeza mbwembwe akawa anarukaruka, kwa bahati mbaya si akaangukia ndani ya Banda la Simba, akawa anapiga kelele "Mama nakufaaa!"
Mara yule Simba akamwambia "Acha Ufala ww kelele za nini sasa, mimi mwenyewe Binadamu! rudi kwenye Banda lako kabla watalii hawajaja watatushtukia! chezea ajira ww"………!!
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘†πŸ»πŸ‘†πŸ»πŸ‘†πŸ»πŸ‘†πŸ»
πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Wabongo ni noma! Angalia huyu mbongo anachokifanya

Basi juzi kati hapa sehemu ndogo ya ukuta wa Ikulu ya Magogoni ilianguka!..
Wakapelekwa contractors watatu ili achaguliwe mmoja atakayejenga vzr na kwa bei nafuu!..
Wakwanza alikuwa MUHINDI, wa pili MCHINA na MBONGO!…

MUHINDI: "ntajenga kwa milioni 90!.., 40 za vifaa, 40 za mafundi na milioni 10 faida yangu"

MCHINA: "mi ntajenga kwa milioni 70!.., 30 za vifaa, 30 za mafundi na milioni 10 faida yangu"

MBONGO kuona vile akamvuta chemba msimamizi wa Magogoni!..
MBONGO: "mi ntajenga kwa milioni 270"

MSIMAMIZI WA MAGOGONI: "we una wazimu nn!.. yaani unathubutu kusema hivyo na unaona wenzako wametaja kiwango kidogo?!."

MBONGO: "milioni 100 zako, 100 zangu alafu hiyo milioni 70 tunaajiri yule mchina"

πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Jihadhari na wachapaji wa kadi za harusi, cheki kilichompata huyu

*Jihadharini* na wachapaji wa kadi za harusi. Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!
Mchapaji aliombwa aweke 1 Yohana 4:18 katika kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.

1 Yohana 4:18 panasema, "Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu…"

Lakini Yohana 4:18 tunasoma, "Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako."

πŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚_MKE MTARAJIWA AKAZIMIA HAPA, TUNAMPEPEA_

πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Eti hili nalo ni kweli kwa dada yako?

oya people hv kwa mfano Dada yako akisomea sheria ndo anaitwa sister in law? au
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Angalia sababu ya mwanamme kubadili jina na Kuitwa jina la kike, hii dunia ina mambo kweli

Rashidi alimpa ujauzito mwanafunzi, akashtakiwa.
Kumbe Rashidi ana bibi yake mtaalamu wa yale mambo yao ya Sumbawanga, akampachika Rashidi i jinsia ya kike.

Alipofika mahakamani kuhojiwa Rashidi akasema sijampa ujauzito kwa sababu mimi pia nina jinsia ya kike.
Kwa kuthibitisha Rashid wakaenda kumkagua basi akashinda kesi, kufika nyumbani Rashid akawakuta watu wamejaa wanalia, akauliza kulikoni?
Akaambiwa bibi yako amefariki. πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜°πŸ˜°πŸ˜°πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
Kwa sasa Rashid anaitwa LeilaπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

------------------------------------------------------------------------------------------------
Kilichonitokea leo baada ya kuona nungunungu

Baada ya kukaa mda mlefu sijamuona nungu'nungu leo nikakuna nae nikajisikia furaha sana,

nikaona bora niende nikamkumbatie !! kutokana na kukaa cku nyingi sijamuona!
Dah! Alichonifanyia nung nung sitokisahau !!!

πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +