Nilijikuta nimesisimkwa mwili kwa swali lake. Nilipomuangalia, niliweza kugundua macho yake yalikua yanamaanisha juu ya umuhimu wa jibu langu kwa swali aliloniuliza.
“Nakupenda sana Haiba. Huo ndio ukweli ambao moyo wangu umeshindwa kuuficha.” niliongea maneno hayo na kumfanya Haiba aniangalie usoni kisha akainamisha kichwa chini kunionyesha stara aliyonayo.
“Sasa tutafanyaje na wewe una mwanamke mwengine?” Haiba aliniuliza swali hilo.
Wakati huo akili yangu ilikua imesharuka tayari.
Maana niliona kama mtoto kanikubali halafu mpenzi wangu anakuwa kikwazo wakati hata yeye alitokea kunikimbia kipindi ambacho sikua na kitu.
“maswala ya mzazi mwenzangu we niachie mimi Haiba. Ila kama upo tayari kuwa na mimi, basi lolote linaweza kutokea.” nilijikuta nimeongea hivyo na kumfanya Haiba achukue glasi yake ya kinywaji na kunywa fundo moja. Mimi juisi yangu niliitelekeza muda wote toka nimeletewa.
“una moyo mmoja Molito... Huwezi kupenda wawili.”
Haiba aliongea maneno yaliyonichoma kama pasi. Maana moyoni mwangu alikua amejaa yeye peke yake japo kiuhalisia tayari nilishafanya chaguo lingine.
“utajuaje kama mimi moyo wangu umekupenda wewe peke yako?... Kama unakubali kuwa na mimi nipo tayari niliyenaye sasa. Najua kwangu amefuata pesa na nitampatia za kutosha ili aendelee na maisha yake. Maana kipindi nilipokua nazisaka yeye alichoka na kunikimbia. Hivyo nimemrudia ili kumuhifadhi kwakua ni mama wa mtoto wangu. Si vyema ahangaike wakati mimi nipo. Au ningemuona ana danga huko mitaani wakati mimi ninao uwezo wa kumchukua ili tulee mtoto wetu kwa pamoja. Ila kama ujio wake unanizibia mimi nisiwe na wewe.... Basi mkataba wake utasitishwa mara moja kwa manufaa ya moyo wangu.” niliongea maneno hayo na kumfanya Haiba ajiinamie.
“Nisikilize Molito.... Naomba simuache. Kwa kipindi mlichokaa na kuzaa, huyo ni mkeo tayari. Kwakua dini yetu inaruhusu, mimi nitakua mke wa pili. Ila sio kwa sasa. Tupate muda kwanza wa kusomana na kuona kama tunweza kuwa pamoja.”
Haiba aliongea kitu ambacho hata sikukifikiria. Hakika nilijikuta nina tabasamu baada ya kugundua mwanamke nimpendaye kwa ridhaa yake yupo tayari kuolewa na mimi hata kwa ndoa ya pili. Hakika nilifarijika hadi nikasahau kama nina kesi inayo niandama na kuninyima uhuru wa kufanya mambo yangu.
“nimekuelewa Haiba. Na nashukuru wa kunipa kwako nafasi ya kuwa na wewe. Kuhusu kusubiri, nitasubiri tu. Maana nimeshasubiri sana bila hata dalili zozote za kujua kama nitaweza hata kukuona. Sembuse hivi sasa nimekuona na umenihakikishia kua upo tayari kuwa mke wangu?” niliongea na kuachia tabasamu.
Basi tulikaa kwa masaa mawili huku tukiongea mawili matatu. Ndipo nlipoangalia saa na kugundua kua kiza kilishaanza kuingia.
“naomba nikuage Haiba.. Naona muda sio rafiki.” niliongea maneno hayo na kumfanya Haiba aangalie saa. Alishtuka pia. Maana wakati tunaongea na kucheka hatukujua kua tumetumia muda mrefu sana toka tumefika pale.
“ngoja nikusindikize.”
Haiba aliongea maneo hayo na mimi nikanyanyuka. Alinisindikiza mpaka kwenye kituo cha treni na kuchukua usafiri huo.
Nilirudi nyumbani na kufika usiku wa saa mbili. Nilimkuta yule askari mpelelezi akipata chakula cha usiku. Niliungana naye kwenye meza ya chakula. Aliniangalia bila kunisemesha kitu zaidi ya kuitikia tu ile salamu.
Nilipoenda kulala. Nilimtumia Haiba ujumbe mfupi wa maandishi wa kumtakia usiku mwema. Hazikupia hata sekunde kumi naye akajibu ujumbe huo. Niliweka simu yangu pembeni na kulala mpaka jogoo la alfajiri liliponiamsha.
Niliangalia simu yangu, hakukua na ujumbe mwengine ulioingia. Niliamua kutuma salamu za asubuhi na kwenda kuswaki.
“Molito... Jiandae twende kituoni.” niligongewa mlango na yule askari mpelelezi nami nikatii.
Tulioka wote hadi kituoni. Nilikaa meza moja na wapelelezi wa kesi hiyo inayonikabili.
“Haiba ni nani hasa kwenye maisha yako?” niliuzwa swali hilo baada tu ya kusalimiana nao na kukaa nao kwa ajili ya mahujiano.
“ni msichana niliyependa toka nikiwa na umri mdogo kabisa.... Hadi sasa nampenda sana.” nilijibu hivyo na kuwafanya wapelelezi hao kuangaliana kisha wakaniangalia tena kwa pamoja.
“na upo huku Marekani kwa ajili yake?” niliulizwa swali lingine.
“Ndio.”
“unawafahamu rafiki zake wa kike wa huku Marekani?” nilikumbanana swali hilo na kunifanya nikatae kwa kutikisa kichwa.
“Ahsante kwa ushirikiano wako Molito. Unaruhusiwa kwenda popote endapo tu itakulazimu uende huko na Haiba.” nilipewa ruhusa hiyo iliyonishtua kidogo.
“kwanini wanamuhisi Haiba kuhusika? Au ni moja ya kazi yao kuhisi chochote chenye ukaribu na mimi?” Nilijiuliza mwenyewe na sikuweza kujipatia majibu.
Nilikiwa njiani narudi nyumbani. Nilipokea simu ya Haiba.
“habari Molito.”
“safi, niambie Haiba.”
“upo wapi muda huu?” Haiba aliniuliza baada ya kusikia honi kadhaa za magari.
“nipo njiani... Nazunguka zunguka tu kuangalia mji.” nilijibu na kumfanya Haiba acheke.
“mbona unanicheka jamani.”
“hata sikucheki... Ila umenishangaza ulivyosema unazunguka zunguka tu asubuhi hii bila kujua unaenda wapi na kufanya nini.” Haiba aliongea na kunifanya nitabsamu.
“haya mama.... Niambie?”
“unaweza kuja kwangu leo hii.... Maana jioni nina mtoko kidogo na rafiki zangu. Unaonaje ukija kunipa kampani?” Haiba aliuliza swali lililonifanya nitabasamu. Maana sikutaraji kama mrembo huyo angetamani kutoka na mimi siku moja.
“ondoa shaka. Ngoja niende kununua nguo kisha nije huko.” niliongea maneno hayo na kuagana na Haiba.
Nilirudi nyumbani na kuchukua pesa ambazo niliamini zitatosha kununua nguo, kulipia gharama zote ambazo tutatumia huko tuendapo. Kifupi nilichukua pesa nyingi sana. Kibongo bongo ilifika milioni moja na nusu.
Sikutaka kuumbuka na kuonekana shemeji michosho mbele ya rafiki zake. Japo kiupande wakipelelezi, Sikutakiwa kuacha ile camera ndogo ninayobandikiwa kwenye kishikizo cha kila shati nilivaalo. Na kidaka sauti nilichowekewa kwenye pembe za masikio yangu.
Nilitoka na kwenda dukani. Nilichukua nguo zilizonipendeza na kulipia. Kisha nikachukua treni hadi nyumbani kwa mtoto mzuri.
Haiba alinipokea kwa furaha na kunikumbatia. Aliniachia busu matata kwenye midomo yangu lililodumu kwa sekunde kumi na tano. Halikua busu kavu, waswahili tunaita denda.
Baada ya mapokezi hayo matata, nilikaribishwwa kwenye meza ya chakula. Maana muda niliofika ulikua muda muafaka kabisa wa kupata chakula cha mchana.
Lisaa limoja baadae waliingia rafiki zake Haiba. Wasichana wawili na wavulana wawili.
Wote walikua Wamarekani weusi.
Tulisalimiana na Haiba akachukua nafasi ya kunitambulisha rafiki zake.
“Molito.....yule msichana aliyevaa topu ya njano anaitwa Clara. Na yule pembeni yake ni mpenzi wake anaitwa Simon. Na yule aliyekaa kwenye kochi pale anaitwa Anna na mpenzi wake anaitwa James. Jamani wapendwa, huyu ndo mpenzi wangu. Anaitwa Molito.”
Nilisikia makofi mengi kutoka kwa rafiki zake.
Nilihisi kabisa walikua na kiu ya kutaka kunifahau kwakua rafiki yao alikua hana mpenzi kwa muda mrefu. Vinywaji vililetwa pale kwa ajili ya kuchangamsha kijiwe. Mimi niliendelea kunywa zangu juisi taratibu.
“Shemeji hunywi bia?” Anna aliniuliza.
“mimi situmii kilevi. Sema hua nainjoy kuona watu mkitumia...hivyo kuweni huru.” niliwatoa wasiwasi na wote wakaendelea kufurahi.
Kiiza kilipooingia. Tulitoka kwa pamoja huku Haiba akiwa ndio dereva wetu.
Tulienda kwenye Club moja ambayo ipo mbali kidogo na mji wa Philadelphia. Sikuweza hatakuuliza, zaidi nilikubali kupelekwa popote walipoamua twende siku hiyo.
Tulifika kwenye Club hiyo ilioandikwa 29th Century. Nilishangaa sana. Maana Club hiyo ilikua inatabiri karne ya mbele kabisa tofauti na hii tuliyopo.
Nilipoingia ndani, kweli walikua wanamaanisha kile walichoandika. Niliweza kuwaona wahudumu wa kiume na wakike wote wakiwa uchi kama sare zao za kazi.
Nilijitahidi kiona ni hali ya kawaida. Niliambatana na mpenzi wangu huku rafiki zake wakiwa bega kwa bega na sisi.
Tulifurahi na kucheza mziki. Nilimshuhudia Haiba akinywa pombe hadi kulewa kabisa na kuanzisha vurugu.
Ilibidi tutolewe ndani na mabaunsa wa Club hiyo na kurudi nyumbani. Mimi ndio nilikabidhiwa jukumu la kuwaendesha kwakua wote walikua hawajiwezi kutokana na pombe walizokuwa wanakunywa toka mchana wa siku hiyo.
Niliweka semu yangu ramani ili iweze kuniongoza. Hatimaye nilifika nyumbani kwa Haiba na kuwaamsha. Maana wote walikua wameshalala.
Kwakua Haiba nammudu, niliamua kumbeba mpenzi wangu hadi chumbani kwake na kumlaza. Wale wengine niliwaamsha wakokotane wenyewe mpaka sebuleni na kuwaacha hapo.
Nilikua huru kufanya chochote kwa Haiba. Maana nilikua naweza kumgusa popote na asiamke.
Nilitumia muda mrefu sana kumuangalia na kuutathmini ubunifu wa muumba katika kuufinyanga udongo wake. Hakika Haiba alikua anavutia sana.
Niliamua kulala pembeni yake mpaka asubuhi. Nikawa wa kwanza kuamka. Nilimuangalia Haiba aliyekua kwenye usingizi mzito. Nilitoka sebuleni na kuwaangalia rariki zake, niliona wakiwa wamelaliana hovyo. Nilisikitika na kwenda jikoni kuwaandalia supu.
Nilichemsha supu ya kutosha na kuwaamsha ili waweze kupata supu hiyo.
Nilisikia hodi ikibishwa. Nilinyanyuka ili niende kufungua mlango.
“usiende kufungua.”
Nilisikia sauti ya mmoja wa wale rafiki zake na kunifanya niwatazame. Wote kwa pamoja wakanyanyuka na kwenda kujificha.
Nilijikuta napatwa na maswali. Kwanini wanajificha? Ina maana kwenye nyumba hiyo hawaingii wageni? Au kwa lile tukio la kule club wanahisi huenda huyo mgeni ni askari.
Nilikuja kushtushwa na sauti ya Haiba ikiniomba na mimi niende kujificha. Nilifanya hivyo huku nikiwa sina amani ile niliyokua nayo wakati wote
Baada ya mtu aliyekua anagonga mlango kuchoka, aliamua kuondoka na sisi tukatoka mafichoni.
Niliwashuhudia wote wakitokwa na jasho jingi na pombe zote ziliwatoka nakuwa wazima kabisa.
Nilitamani kuuliza, ila niliamua kutulia tu kwakua nilikua nafahamu kila kitu kinachoendelea hapo kilikua kinafuatiliwa vizuri kabisa na askari walionipa kazi ya kupeleleza.
“Molito, naomba tuongee kidogo.”
Nilimsikia Haiba akiongea kwa sauti ya chini baada ya tukio hilo kupita na mimi nikiwatazama wao kwa zamu huku nikiwa na mashaka juu yao.
Sikubisha, nilimsogelea Haiba alipo na akanishika mkono na kwenda na mimi kwenye meza ya chakula.
“Molito, unanipenda kwa dhati?”
Haiba aliniuliza swali hilo na kunifanya nimtazame usoni.
“nimeshalijibu hilo swali tayari baada ya kuniuliza.... labda nirudie tu kusema ili upate kuridhika. kiukweli kabisa nakupenda sana Haiba na sijapatapo kupenda kama wewe kwenye huu mgongo wa ardhi.”nilijibu hivyo ili nipate kumsikia nini hasa lengo lange Haiba la kuniuliza swali lile tena kwa kuniomba tukae kikao kabisa.
“kama unanipenda kiasi hicho.... Naomba nisaidie.”
Haiba aliongea maneno hayo na kunishtua kidogo. Ila nilijitahidi kujikaza ili niweze kumsikia nimsaidie kitu gani hasa.
“nakusikiliza.... Kipi unachohitaji ambacho unaona fika naweza kukusaidia.” niliongea maneno hayo na kumtazama machoni.
“nahitaji msaada wako wa hali na mali ili niweze kuondoka nchi hii na kurudi nyumbani.” Haiba aliongea maneno hayo na kuzidi kunichanganya.
“niambie sasa kipi ambacho unahisi ni kikwazo. Huna pesa au huna pasi ya kusafiria?” niliuliza na kumfanya Haiba ashike kichwa na kujiinamia. Kisha aliuinua uso wake na kunitazama.
“maisha yangu yapo hatarini. Yalishaharibika hapo kabla ila kwa hivi sasa ndio nimezidi kuyaharibu. Ile amani niliyoitaka kwenye moyo wangu sijaipata,imezidi kutoweka.” Haiba aliongea maneno hayo na kuzidi kunichanganya ni kipi hasa kinachomfanya awe vile.
Rafiki zake walitusogelea hadi pale tulipo.
“Haiba, naona kwa sasa hali ni shwari..... Ila jitahidi sana usije ukatukosea.” aliongea mmoja wa wale wasichana na wangeni wakatupa ishara ya kutuaga.
“Ni vyema na wewe ukaondoka hivi sasa, nahitaji kubaki mwenyewe.” Haiba aliongea maneno hayo na kukatisha kile alichotaka kuniambia ili nimsaidie.
“Haiba sikuelewi... Ni kipi hasa unajaribu kunificha?” nilimuuliza swali hilo na kumfanya Haiba anitazame machoni.
“nimeleemewa na kilevi... Sijui niongeacho. Naomba nenda. Nitakutafuta siku ambayo nipo sawa ili tuweze kuongea kwa kirefu zaidi hili swala. Kwanza unatarajia kuondoka lini?” Haiba aliuliza swali hilo na muda huo huo ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yangu. Niliusoma kisha nikaufuta na kuirudisha simu yangu mezani.
Ujumbe ulikua unanielekeza nisema kua naondoka siku inayofuata.
“naondoka kesho na ndege ya jioni.” nilijibu kama nilivyoelekezwa.
“basi kesho asubuhi nitakuja. Nitakuelekeza ni wapi tuonane na ikibidi hiyo jioni tuondoke wote.” Haiba aliongea maneno hayo na kunifanya nijiongeze.
“nikate tiketi mbili kabisa eeh?” niliongea huku nikionesha wazi kulifurahia lile tukio la kuondoka wote.
“kumbe unapenda kuishi na mimi eeh?” Haiba aliuliza huku akitabasamu.
“sanaaa.” nillijibu na kumfanya Haiba asimame. Nami nilisimama na kupata kumbatio lililosindikizwa na busu laini mdomoni.
“nakupenda sana Molito... Naomba tu utambue hivyo. Na pindi tutakapofika tu nyumbani utakua huru kufanya kitu chochote kwenye mwili wangu.” Haiba aliongea maneno hayo kwa sauti yake chokozi aliyoitua sawia kwenye ngoma za masikio yangu.
Hakika nilifarijika. Nilitamani nipae nae tu ili tufike tu Tanzania nikale raha za maungo yake ya uzazi.
Haiba alijitanda ushungi na kunisindikiza hadi kwenye kituo cha Treni. Nami nilimuaga na safari ya kurudi nyumbani ikaanzia hapo.
Kiukweli Haiba alikua ananitia mashaka. Na vile nilivyokua nafuatiliwa ndio kabisa, nilijua fika lazima nitahitajika kumchunguza zaidi Haiba kwa kuhisiwa kuhusika na mauaji. Ila nilijipa imani huenda akawa ana kesi nyingine lakini sio hiyo. Maana uoga wa Haiba ulinipa tafsiri kua hawezi kua jasiri wa kuua hata panya.
Nilifika nyumbani na kukutana na mpelelezi wa kesi ya mauaji ya Farahani.
“pole sana na kazi ndugu Molito. Nakupa masaa matatu ya kupumzika, baada ya hapo Itabidi uje ofisini tuongee.”
Baada ya kupita masaa matatu, nilienda kituoni kama kawaida na kuwekwa mtu kati na watu waliokua wanachunguza kesi hiyo. Nilimuona mpaka Alice akiwa na kalamu yake ambayo inarekodi sauti.
“Molito.... Unaweza kutuambia unahisi kitu gani kinamsumbua Haiba wako?”
Niliulizwa swali hilo na mpelelezi ninaye kaa nae nyumba moja. Swali hilo sikulitegemea, ilinibidi niwatazame watu wote kwa zamu. Kisha nikagandisha macho yangu kwa sekunde kadhaa kwa mtu aliyeuliza swali hilo na kunifanya nimeze mate kwanza kabla sijamjibu.
“nahisi ni hofu kwa tendo alilolifanya Club na zile vurugu. Pia ana stress, nimmeona kabisa hahitaji mtu mwenye maisha yake japo kwa upande mwengine ametokea kunipenda baada ya kumuhadihia hadithi ya nyuma ambayo yeye haikumbuki. Hivyo nahisi ananihitaji angalau nimpeleke nyumbani kwao aweze kufuatilia mali za wazazi wake ambao wameshatangulia mbele za haki baada ya kufa kwenye ajali.”
Nilitoa maelezo hayo na muda huo huo simu yangu ikaita. Jina lilitokea la Haiba. Waliweka mitambo yao sawa na kila kila mmoja akaweka kifaa cha kusikiliza masikioni mwake. Kisha nikaamriwa kuipokea simu hiyo.
“Molito... Siwezi kulala bila ya uwepo wako. Naomba uje, najihisi upweke kwa masaa machache tu uliyoniacha mpenzi wangu.” Haiba aliongea kwa sauti ya kudeka.
Niliwatazama wapelelezi, nao wakanipa ruhusa ya kuendelea kuongea nae vyovyote vile ninavyohitaji.
“sasa mama, mpaka nikifika huko ni usiku sana. Halafu asubuhi nahiaji niwahi kufuatilia ile michongo yetu. Mimi naona ni bora usubiri kesho tu.” niliongea maneno hayo na kumfanya Haiba ashushe pumzi.
“Molito... Yaani hata sijielewi. Naona kama najitisha mwenyewe.” Haiba aliongea maneno hayo na kuwafanya wapelelezi wazidi kunikazia macho.
“tatizo lako hutaki kushea na mimi kile kinachokusumbua. Niambie kipi kinakutisha?” Niliuliza swali ambalo wapelelezi wote walitingisha kichwa kunipongeza kua nilikua nimeuliza swali zuri kwa Haiba.
“nitakueleza kila kitu kesho.... Naomba unihakikishie kama tunaweza kuondoka wote. Nimechoka kukaa Marekani mimi.” Haiba aliongea kwa sauti ya Kudeka.
“Nakuahidi sitakuacha.. Lazima tuondoke wote.” nami niliongea maneno hayo na Haiba akakata simu.
“mpaka hapo unataka kutuambia hujaelewa chochote Molito.... Au upo pamoja nae unataka tukuchangamshe kidogo?” niliulizwa swali hilo baada ya simu kukatwa.
“toka mwanzo nimekua mtiifu kwenu. Sijui chochote kuhusiana na Haiba nyuma ya pazia. Ni muda mrefu sana tumepotezana na kuonana tena kibahati tu huku Marekani. Nisubirini niende kukutana naye hiyo kesho kisha mtafahamu kila kitu.” nilijitetea baada ya kuona nataka kubadilishiwa kibao.
“tunakuamini... Ila tukuambie tu ukweli, wauaji wa mfanya biashara Farhani ni huyo mpenzi wako na rafiki zake. Hivyo wakati wewe unaenda kukutana na Haiba. Sisi tutaenda kuwakamata hao rafiki zake kisha wewe ndio utakamilisha ushahidi. Kesho asubuhi tutakuwezesha kupata tiketi mbili za ndege za kusafiri jioni kama ulivyomuahidi. Nina imani atakuamini na kusema kila kitu kumuhusu. Hivyo hakikisha hautukoseshi nafasi hii adimu itakayokuweka wewe huru.” Alice aliongea maneno hayo na wapelelezi wengine wakaitikia kuashiria kua hiyo ilikua kauli isiyo na pingamizi kwao.
Niliruhusiwa nirudi nyumbani. Lakini muda wote nilitakiwa kuwa na vifaa nilivyopewa kwa ajili ya usalama wangu na urahisi wao katika kufanya uchunguzi.
Niliamka asubuhi na mapema. Nilifanya mazoezi kidogo kisha nikaenda kuoga. Nilichukua simu yangu na kukuta ujumbe mfupi wa maandishi niliotumiwa nusu saa iliyopita.
“samahani mpenzi, nilikua nafanya mazoezi. Hivyo najiandaa kwenda kukata tiketi. Tuonane baada ya masaa matatu.” nilituma ujumbe huo na kumfanya ajibu haraka.
“usijali mpenzi, ila tambua tu kua nakutegemea sana wewe kuliko mtu yeyote yule kwa sasa. Naomba usiniangushe.”
“usijali.... Baadae mpenzi.” nilimaliza kuandika ujumbe huo na kuiweka simu angu mfukoni.
Nililetewa tiketi za ndege na baada ya muda nikampigia simu Haiba ili kumpa taarifa kua nimefanikiwa kupata tiketi.
“jamani!..... Nipo njiani nakuja. Baada ya dakika Arobaini na tano nitakua hapo”
Haiba aliongea huku akionesha wazi amejawa sana nafuraha.
Akiwa njiani, tulikua tunachati na kukubaliana tukutane palepale tu mahala tulipopazoea. Kwenye mgahawa.
Nilitangulia baada ya kuniambia ameshafika stendi.
Nilikaa hapo kwa muda wa dakika kumi ndipo na yeye akafika. Nilisimama kama kawaida yangu na kumkumbatia. Hakika hata yeye alinipokea kwa furaha sana.
“kwanza kabla ya yote... Nionyeshe tiketi zetu.” Haiba aliongea na kunifanya nizitoe zile tiketi na kumkabidhi.
Alifurahi na kunikumbatia kwa mara nyingine.
Moyo wangu ulifarijika sana kuona nipo karibu na msichana mrembo kama huyo. Nafsi yangu ilikataa kabisa kuamini kua Haiba ndiye muuaji wanayemtafuta. Maana sijaona maajabu yoyote aliyonayo kuanzia mahala anapoishi na vitu anavyovipenda.
Niliamini juhudi zao za kutafuta muuaji wa Farahani zitafeli kwa Haiba ndio maana natoa ushirikiano mpaka mwisho ili hata wakishindwa kumnasa Haiba wasinigande mimi tena. Maana sina watu wengine ambao nina ukaribu nao huko Marekani zaidi yake.
ITAENDELEA.....
Monday, April 22, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments