Pages

Monday, April 22, 2019

SIMULIZI YA *SIN* SEHEMU YA 09 ........ ONLY 18+

ILIPOISHIA
“U…u…m….e…sema U…me….me..mkamata nani?”
Mrs Sanga alizungumza kwa kubabaika.
“Mtekaji wa mume wako.”
RCP akampa ishara kijana wake mmojaa kuweka bahasha ya rangi ya kaki, aliyo ishika mezani hapo.
“Fungua”
Mrs Sanga taratibu huku akitetemeka akaichukua bahasha hiyo. Akachungulia ndani ya bahasha hiyo na kukuta lundo la picha. Taratibu akazitoa picha hizo, Mrs Sanga alipo inaona sura ya Tomas akishuka kwenye gari lake, akahisi mwili mzima ukiishiwa nguvu, ubaridi mkali ukamtawala na kujikuta akiziangusha picha hizo na kuwafanya askari wote kumshangaa.

ENDELEA
“Vipi mama mama mbona una wasiwasi?”
RPC alimuuliza Mrs Sanga huku akimtazama usoni mwake.
“Huyo kijana ndio….ndio yule aliye chukua pesa zangu”
“Yaa tuliweza kuweka mtego ambao umefanikiwa na hivi sasa kijana huyo yupo nasi na tuna kwenda naye kwenye oparesheni ambayo, Mungu aingize mkono wake ili tuweze kufanikiwa”
“Amen”
“Basi vijana wagu wanatendelea kuwepo hapa kwako. Mimi ngoja nikaendelee na majukumu ya kikazi na endapo kutakua na mabadiliko ya aina yoyote katika oparesheni hii basi nitakuja kukuambia”
“Sawa afande”
Mrs Sanga alijikaza tu kuzungumza ila mapigo yake ya moyo hayapo sawa kabisa. RPC akaondoka na vijana wake baadhi pamoja picha hizo. Mrs Sanga akakikimbilia chumbani kwake huku mwili mzima ukimvuja jasho kutokana na wasiwasi mkubwa alio upata.
“Ehhee MUNGU nini hichi tena jamani. Ooohoo jamani Tomas wangu”
Mrs Sanga aliendelea kulalama huku akitafuta bibilia yake ilipo. Akanaaza kusali maombi ambayo sidhani kama mwenyezi Mungu ana weza kuyapokea kwa haraka.
***
“Hembu simamisheni gari”
Rama D alizungumza na kumfanya Selemani D kusimamisha gari hilo.
“Kuna nini kaka?”
“Roho yangu nina iona imekuwa nzito gafla”
“Kwa nini?”
“Sijui kuna nini, alafu mshakiji hadi sasa hajatokea na nikimcheki hewani hapatikani”
“Kuna ishu imempata nini?”
“Sijajua, hembu turudini kambini tukachukue kila kilicho chetu na tuondoke”
“Poa poa”
Selemani D akawasha gari hilo na kuondoka kwa kasi huku wakiwahi kurudi porini. Wakafika katika kambi yao, wakaanza kukusanya kila kilicho chao ili kutokomea wanapo pajua wao wenyewe. Walipo hakikisha kwamba wamebeba kila kilicho chao wakaigia kwenye magari yao manne huku kila mmoja akiendesha gari lake moja na kuondoka msituni hapo na kuianza safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro.
Hadi polisi wanafika katika msitu huo na kuanza kuifanya oparesheni ya kuwasaka majambazi hao, taayari walisha chelewa. Wakakuta nyumba zilizo tengenezwa kwa mbao zikiwa tupu kabisa na ndani ya nyumba hizo kukiwa hakuna mtu wa aina yoyote.
“Wewe ni wapi walipo kwenda wezako?”
Askari mmoja alizungumza huku akiwa amemuekea bastola ya kichwa Tomas anaye endelea kutetemeka kwa woga.
“Ni hapa hapa tu”
“Wapo wapi sasa, au umewapa taarifa ya kuondoka?”
“Hapana, sikuweza kuwapa taarifa yoyote ile”
“Mkuu kuna aina nne za alama za matairi ya magari zimeondoka eneo hili”
Askari mmoja mwenye taaluma kubwa ya upelelei alizungumza huku akimuliaka kwa toshi alama za matairi za magari yalioyo ondoka hapo.
“Wanaonekana hawapo mbali”
“Ndio”
“Sasa tuanzeni kufwatilia alama hizo za magari. Hakikisheni kwamba muna wasiliana na askari wa Kabuku, Chalinze, Segera. Kote hakikisheni kwamba kuna pigwa patroo ya maana.”
Mkuu wa kikosi hicho alizungumza na askari wote wakarudi ndani ya magari yao na kuianza safari ya kufwatilia alama hizo za magari. Ubaya ni ni kwamba barabara aliyo pita Rama D na wadogo zake ni barabara ya yenye tope kiasi na ndio maana askari wameweza kufahamu kirahisi juu ya muelekeo wao.
Katika barabara nzima ya kutoka Chalinze hadi Segera, askari wame weka road block katika vituo zaidi ya mia moja. Hali ambayo imepelekea msongamano mkubwa sana wa magari makubwa yanayo fanya safari zake za usiku.
“Ni nini kinacho endelea?”
Rama D alizungumza huku akipungumza mwendo kasi wa gari lake na kuwafanya wadogo zake wanao mfwata kwa nyuma nao kupunguza mieondo ya magari yao. Rama D akatoa simu ya upepo(Redio call) na kuwapigia wadogo zake.
“Kuna ukaguzi wa magari unao endelea”
“Tuna fanyaje kaka?”
“Tupangeni foleni na tuwe makini ila hakikisheni kwamba silaha zenu muna ziweka tayari na endapo ikitokea kuna mjinga yoyote atazingua. Hakuna kufanya makosa”
“Poa”
Wakapanga foleni Yuma ya lori kubwa la mizigo. Jinsi foleni hiyo inavyo sogea ndivyo jinsi nao wanavyo kisogelea kituo cha kukaguliwa.
Taarifa ya ni aina gani za magari ambazo alama za matairi zake zilikutwa msituni zikaanza kusambazwa kwa njia ya whatsapp kwa kila polisi aliyopo katika vizuizi vya barabarani. Gari ya kwanza ni Ford Ranger, gari ya pili ni Range Rover,gari ya tatu ni Benz Compresa na gari ya nne ni Toyota Harrier. Umakini wa askari ukazidi kupamba moto na kuachana kabisa na malori makubwa na kuanza kutilia umakini kwenye gari ndogo.
“Tumeziona gari za majambazi zipo kwenye foleni hapa kwenye road block D20 Over.”
Askari alizungumza kwa kupitia simu yake ya upepo na kuwapata taarifa wezake wote waliomo kwenye hiyo oparesheni ya kuhakikisha kwamba wana wakamata majambazi walio mteka nabii Sanga.
“Hakikisheni kamba muna wazuia muwezavyo sisi tupo njiani tuna kuja”
Mkuu wa kikosi cha polisi kilicho toka makao makuu ya askari Dar es Salaam alizungumza kwa simu yake hiyo ya upepo na kuwafanya madereva wa gari hizo nne kuaongeza mwendo ili kuwahi eneo la tukio.
“Sawa mkuu”
Askari walipo katika road block D20 wakaendelea kuwahoji maswali madereva wa malori yaliyopo katika eneo hilo ili kuwaweka majambazi walipo nyuma ya malori hayo kuzidi kuchelewa, ili msaada uzidi kuwepo.
“Mbona wana tuchelewesha hawa?”
Selemani alizungumza huku gari lake likiwa ndio la mwisho kabisa kutoka nyuma.
“Tuweni wapole”
Rama D aliwasisitiza wadogo zake huku bastola yake ikiwa mkononi mwake.
“Au tuvunje vizuizi vyao?”
“Acheni ujinga. Mukivunja munahisi nini kitatokea?”
“Tunaliamsha dude na tunasepa”
“Nimesema tulieni. Mimi ndio mtoa amri wa mwisho sawa”
Rama D alizungumza kwa ukali kidogo mara ya kuona wadogo zake wana leta upinzani wa kubishana katika swala hilo. Selemani D, kwa kupitia site mirrow akaanza kuona gari zaidi ya nne zinazo fanana zikishuka kwenye kilima kilichopo nyuma yao kwa kasi sana zikija eneo walipo wapo.
“Waskaji huu nimtego. Tuondokeni”
Selemeni alizungumza huku akiwasha gari lake. Hakujali kama kuna kizuizi mbele yao, akaanza kuondoka kwa kasi sana huku ndugu zake wakimfwata kwa nyuma na kusababisha kuanza kwa mapambano makali sana kati yao na askari walipo kwenye kizuizi hicho.
***
“Niandalie maji nikaoge”
Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Sawa ila vyoo vyetu ni vya passport”
“Una manisha nini?”
“Ni vile vyoo ambavyo havijazibwa kwa juu”
“Duu sasa kama hakijazibwa kwa juu si nitaonekana?”
“Ndio utaonekana, ila kwa sasa ni usiku hakuna mtu ambaye atakuona”
“Hapana, sinto oga”
Nabii Sanga alizungumza huku akinawa mkono wake wa kulia mara tu baada ya kumaliza kula chipsi hizo.
“Ila nimepata wazo”
“Wazo gani?”
“Mimi nikienda kuoga. Nawe uoge humu ndani kuna dishi kubwa ambalo una weza kuingia na kuoga bila ya tatizo”
Nabii Sanga akamtazama Magreth kwa sekunde kadha kisha akatabasamu.
“Hembu nilione hilo dishi”
Magreth akainama na akalitoa dishi hilo chini ya kitanda chake. Nabii Sanga akalitazama kwa sekunde dishi hilo na kurishika kwamba ana weza kabisa kutosha ndani ya dishi hilo.
“Leo inabidi nirudi utotoni”
“Hahaa ndio hivyo”
“Haya niwekee maji nijimwagie”
Magreth akandaa kila kitu kwa ajili ya nabii Sanga kuoga, kisha yeye akachukua tenge lake na kindoo cha cha bafuni chenye maji na kuelekea katika choo cha nje ili aoge. Nabii Sanga akavua taulo hilo pamoja na boksa kisha akaingia ndani ya dishi hilo na kuanza kuchota maji katika ndoo ya pembeni na kujimwagia mwili wake. Dakika saba zikamtosha nabii Sanga kuoga. Akatoka ndani ya dishi hili, akajifuta maji mwili mzima na kujifunga taulo hilo. Magreth mara ya kutoka bafuni, akagonga mlango wa chumba chake na babii Sanga akafungua.
“Tayari”
“Ndio una weza ingia”
Magreth akaingia huku akiwa amejifunga tenge hilo, lililo mfanya nabii Sanga kupagawa. Magreth akabeba dishi hilo na kutoka nalo nje. Akamwaga maji na kurudi ndani na kuliingiza mvunguni. Nabii Sanga uvumilivu ukamshinda kabisa, akatamani amshike Magreth japo kalio ila woga na wasiwasi vika mjaa.
“Baba wewe utalala kitandani mimi nitalala hapa chini”
Magreth alizungumza huku akitandika tenge jengine chini ya sakafu hiyo.
“Ahaa…tuna weza kusali”
“Ndio baba, tena nilikuwa nime jisahau kabisa.”
“Sawa njoo ukae hapa kitandani”
Magreth bila ya wasiwasi akakaa kitandani. Hakuwa na wazo kabisa kwamba uumbaji wa mwili wake umesha vuruga kichwa cha nabii Sanga. Hata hayo maombi anayo kwenda kuyaomba hakuna hata moja ambalo litamfikia Mungu, kwani shetani wa ngono tayari amesha tawala mwili wake.
‘Hapana leo siwezi kumuacha’
Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Lete mikono yako, tusali”
Nabii Sanga alizungumza huku akiishika mikono ya Magreth. Ukaribu walio sogeleana ukazidi kumuweka nabii Sanga kwenye wakati mgumu sana. Jogoo wake tayari alisha simama kiasi cha kulifanya taulo alilo jifunga kiunoni kumchoresha jogoo huyo kisawa sawa.
Mageth mapigo ya moyo yakaanza kumuenda kasi mara baada ya kuona eneo la mbele la nabii Sanga likiwa limetuna kisawa sawa. Akatamani kuiachanisha mikono yake na mikono ya nabii Sanga ila akashindwa kwani tayari nabii huyo alisha anza kusali kwa suati ya chini chini.
‘Hawezi kunifanya jambo baya’
Magreth alijipa moyo huku naye akiyafumba macho hayo kuungana na nabii Sanga katika maombi hayo.
***
“Wanakimbia, ongeza mwendo ongeaza mwendo”
Mkuu wa kikosi cha askari wanao toka makao makuu, alimuimiza dereva wa gari lake na akazidi kuongeza mwendo. Askari walipo katika road block D20 hawakuwea kuwazuia Rama D na wadogo zake kwani tayari wamesha gonga kizuizi chao na kuzidi kutokomea. Gari hizo za polisi nazo zikapita kwa kasi katika kizuizi hicho na kuwafanya askari wa kizuizi hicho nao kuingia kwenye Defender zao na kuanza kujumuika katika kufukuziana huko.
Makimbizano hayo ya magari kwa haraka haraka unaweza kuyafananisha na mafukuzano ya magari yanayo patikana katika filamu za Fast and Furios. Seleman D ambaye ndio anaendesha Range Rover akazidi kuwaacha wezake kwani gari lake hilo lina uwezo mkubwa sana katika kukimbia. Rama D naye ni wa pili kwani mwendo kasi wa Ford Ranger sio wa mchezo mchezo. Mkuu wa askari askashusha kioo cha upande wake na akajitokeza kwenye dirisha huku mkononi mwake akiwa ameishika bunduki aina ya AK47. Akaanza kulishambulia gari Toyota Harrier iliyo mbele yao. Mashambulizi ya risasi zake hayakwenda bure kwani risasi kadhaa zilipiga katika tairi za nyuma za gari hili lililopo kwenye mwendo wa kasi sana. Gari hilo linalo endeshwa na Rashid D, likapasuka tairi za nyuma na kupelekea kupaa hewani huku likipoteza muelekeo wake, likaanguka chini na kuanza kubingirika na kuelekea pembezoni mwa barabara.
“Rashid amepata ajali”
Abdalah D anaye endesha Benz Compresa alizungumza hukua kishuhudia gari la kaka yake huyo likibingirita pembezoni mwa barabara.
“Hakuna kurudi nyuma”
Rama D alizungumza huku akizidisha mwendo wa gari lake. Askari wa gari mbili za mbele wakalipita gari hilo la majambazi lililo pata ajali. Gari mbili za askari wa nyuma zikazimama na askari wakashuka na bunduki zao. Wakaanza kulisogelea gari hilo huku wakiwa makini sana. Askari wenye Defender zao mbili nao wakafika eneo hilo.
“Piteni piteni”
Askari moja aliwapa amri askari hao mbao hawakushuka kwenye gari zao na wakaendelea kuzifukuzia gari za majambazi. Rashid D, mwenye hali mbaya sana ya majeraha aliyo yapata kutokana na ajali hiyo, taratibu akafungua mkanda wa gari hilo huku akijikaza sana. Kitendo cha kutoka kwenye gari hilo lililo pinduka na matairi yapo juu, akakutana na askari wanne walio shika bunduki wakimsubiri kwa hamu atoke ndani ya gari hilo.
“Hana haja ya kuishi”
Mmoja wa askari alizungumza huku akiikoki bunduki yake. Akaachia risasi nne zilizo tua kifuani mwa Rashid D na akapoteza uhai hapo hapo. Askari wawili wakaingia kwenye gari lao na kuondoka huku askari wawili wakibaki kwenye eneo hilo kuhakikisha wana tafuta vitu ambavyo vita wasaidia kwenye upelelezi woa.
Milio ya risasi iliyo sikika kupitia simu zao za upepe, zikawafanya Rashid na wadogo zake kuumia sana mioyoni mwao. Kwani wamesha mpoteza ndugu yao mmoja.
“Hei nisikilizeni”
Rama D alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Rashida hatupo naye tena duniani. Ila tunatakiwa kufanya kitu juu ya hawa washenzi walio muua ndugu yetu. Hatuwezi kuwa kunguru na kukimbia zaidi. Tunatakiwa kupambana nao na kama ni kufa basi tufe kishujaa zaidi”
Rama D alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka kwa hasira.
“Tunafanya nini kaka?”
Selemani D aliuliza.
“Tufunge barabara”
“Poa”
Wakaanza kupunguza mwendo. Selemani aliyopo mbele na gari lake aina ya Range Rover akaligeuza kwa utaalamu mkubwa na kuifunga barabara. Rama D naye akampisha mdogo wake Abdalah D kumpita kisha naye akalisimamisha gari lake na kuifunga barabara na kuwafanya askari wanao wafwata nao kupunguza mwendo wa magari yao kwani hawajui ni kitu gani kilicho pelekea majambazi hao kujiamini sana na kufunga barabara hiyo.
***
“Amen”
Nabii Sanga alimaliza Sala yake na kufumbua macho. Macho yake yakakutana na macho ya Magreth. Wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha Magreth akaiachanisha mikono yake na mikono ya nabii Sanga.
“Nikutakie usiku mwema baba”
“Nawe pia mwanangu, ila ni vibaya kwa mtoto wa kike kulala chini huku mimi mwanaume niliye komaa nikilala kitandani. Huo utakuwa ni unyanyasaji mkubwa sana na nina weza nisipate usingizi kabisa mwanangu. Ninacho kuomba ni wewe uweze kulala kitandani na mimi uniache nilalale chini”
“Hapana baba wewe ni mgeni haina shinda. Wewe lala tu kitandani”
Magreth alizungumza huku akisimama, ila kwa bahati mbaya kitando cha nabii Sanga kumzuia katika kusimama kwake, kukapelekea tenge lake kulegea kishikizo alicho kuwa amekichomeka kifuani mwake na kupelekea tenge hilo kuanguka chini na kumfanya Magreth abaki kama alivyo zaliwa na kumfanya nabii Sanga ashuhudie uumbaji wa Mungu alio kuwa akiutamani kuuona siku zote mubashara.
ITAENDELEA
Haya sasa, Rama D na wadogo zake wameamua kujitoa muhanga je watafanikiwa kuwazuia askari hao? Nabii Sanga naye ana karibia kuokota dodo chini ya mpapai je atafanikiwa? Nini kitatokea? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 10.

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +