Pages

Monday, April 8, 2019

Wavuta bangi wa Colombia watoa mpya


Asubuhi ya leo huko nchini Colombia baada ya serikali kuidhinisha matumizi ya bangi kuwa halali +++ Wavutaji bangi wamepanda basi la gorofa wengine juu wengine chini….

Waliopanda chini wanawauliza wa juu huko speed ni ngapi maana huku ni 80.

Wajuu wakajibu huku mpaka sasa hatujui dereva bado hajaja…. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚


Kali ya mwaka iliyotokea Benki Baada ya wezi kuiba

πŸ‘‰HII NI KALI KULIKO ZOTE ULIZO
ZISOMA

- KUNA WIZI UMETOKEA BENKI
•Jambazi akasema "wote laleni chini pesa ni za
Serikali na Maisha ni ya kwenu", wote wakalala
chini (HII INAITWA DHANA …YA USHAWISHI) -
kubadilisha njia ya kawaida ya kufikiria)
• Kuna dada kwa woga akawa
amelala chini kimitego, Jambazi
akamwambia, "dada hebu kuwa
na adabu chukua kanga jifunike hili ni tukio la
ujambazi na sio la ubakaji” (HUU UNAITWA
WELEDI) -zingatia ulichofundishwa kufanya)
• Walipotoka kwenye wizi jambazi mdogo
ambaye ana shahada ya Uzamili ya biashara
akamwambia mwenzake, "tuzihesabu hizi
fedha.” Yule mkubwa akamcheka kwa dharau
na kumjibu, "wewe mjinga sana hizo hazina
haja ya kuhesabu saa mbili wata tutangazia
kwenye taarifa ya habari tumeiba kiasi gani.
(HUU UNAITWA UJUZI) - Siku hizi ujuzi ndio
bora kuliko vyeti)

• Baada ya majambazi kuondoka meneja
akamwambia mhasibu wa bank, " ujumlishie na
zile milioni 80 tulizo iba sisi.” (HUKU KUNAITWA
KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI -
kushabihiana na mazingira magumu kwa faida
binafsi.)
•Mhasibu akafurahi na kusema, "dah wizi
ukitokea kila mwezi itakuwa burudani
sana.” (HUKU KUNAITWA KUWA NA MAWAZO
CHANYA - Furaha ndio kitu cha muhimu zaidi)

• Meneja kafurahi sana kwa kuwa sasa
matatizo yake yametatuliwana wizi uliojitokeza.
(HUKU KUNAITWA KUTHUBUTU-shikilia nafasi
pale inapojitokeza hata kama ni hatari kiasi
gani.
Haya usiku wake taarifa ya habari ikatangaza
kuwa wizi mkubwa sana wa million 100
umetokea leo benki. Majambazi kuskia hivyo
wakaanza kuhesabu zile pesa lakini wakajikuta
na milioni 20 tu.

πŸ‘‰Yule jambazi mkubwa akashtuka na kusema,
"dah! yaani meneja kaiba mara nne zaidi yetu
bila kutumia msuli? Bora Umeneja kuliko
Ujambazi.” (HII INAITWA ELIMU NDIYO KILA
KITU) - ishike sana elimu ina nguvu kuliko
chochote.

KAMA UMEIPENDA SHARE

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚

 Alichofanya mke baada ya mme wake kupenda kumchunga sana

Siku ya kwanza
MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikie…..mke­ akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja

Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa brender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili

Siku sita baadae mume akaamua kurudi bila kumtaarifu mkewe alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui ameondoka na blender toka asubuhi

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚



 Hii sasa ni kali


*Siku izi kujuana kumezidi hata ukienda msibani kama hauna connection hauli msosi*πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +