ILIPOISHIA
“Munafundishwa juu ya nini?”
“Muheshimiwa bora yaani umekuja, sisi wengine humu tumefungwa kwa kesi za kusingiziwa, ila tumekuja huku tunakutana na mateso makali kama haya”
“Yana muda gani?”
“Miezi mitatu sasa, kuna wezetu wachache kila siku usi……”
Mfungwa aliye kaa karibu na mfungwa huyu anaye zungumza akamuwahi mwenzake na kumfunga mdomo kwa nguvu. Mfungwa huyo aliye zibwa mdomo akampiga mwenzake kisukusuku cha kifua na kusababisha vurumai kuanza kutokea, kati ya wafungwa hao, jambo lililo tufanya mimi na Babyanka kuchanganyikiwa tukitafuta ni jinsi gani tunaweza kumuokoa raisi kutoka katikati ya watu hawa wanao onekana kujawa na hasira kali sana.
ENDELEA
Babyanka akapiga risasi mbili hewani na kuwafanya wafungwa wote kulala chini huku wakivifunika vichwa vyao.
“Muheshimiwa tuondoke”
Nilimuambia raisi huku nikihakikisha kwamba anakuwa salama muda wote, raisi akakubaliana na ombi langu kwa maana hali sio salama kabisa katika eneo hili. Tukampeleka raisi hadi kwenye ofisi tulizo kuwepo awali, huku mkuu wa gereza akiwawa kimya kabisa. Ukimya ukatawala ndani ya ofisi huku kila mtu akiwa kimya. Raisi akatoa simu yake ya mkononi, akaminya baadhi ya batani kisha akaiweka sikioni.
“Andaa jeshi kudhibiti sekta zote za ulinzi”
“Hakikisha kwamba, mkuu wa mkoa pamoja na kundi lake munawaweka chini ya ulinzi mkali”
“Pia nahitaji vijana watakao linda hili gereza kuanzia sasa hadi pale nitakapo toa tamko jengine”
Raisi akakata simu, huku akionekana kuwa na hasira kali sana, akamsogelea mkuu wa gereza akabandua vyota zilizopo begani mwake ikiashiria kwamba amevuliwa cheo.
“Mkamate bosi wako kamsweke ndani”
“Sawa muheshimiwa”
Kijana wa mkuu wa gereza akamchukua aliye kuwa mkuu wa greza huku akimpiga pingu na kuondoka naye katika eneo la ofisini. Raisi kwa ishara akamtuma mlinzi mmoja kwamba afwatile hadi mkuu huyo atakapo wekwa ndani.
“Tuondokeni”
Kazi yetu ni kufwata amri ya raisi, tukaongoza njia, huku mbele nikitanguli mimi, nyuma akifwata Babyanka pamoja na mlinzi mwengine ambaye hasi sasa hatujajuana majina kabisa kutukana na mihangaiko ya kazi yetu hii. Tukaingia kwenye magari na kuondoka katika eneo la gereza hadi tunafika barabarani, raisi hakuzungumza kwamba ni wapi tuelekee.
“Muheshimiwa mbunge yupo wapi?”
Swali la raisi, likanifanya kusimamisha gari kwa maana hata wazo la kumtazama mama na baba mkubwa ambao tuliingia nao hapo gerezani, lilinipotea kabisa.
“Mbona umesimamisha gari?”
“Sifahamu kwamba tumewaacha wapi muheshimiwa kwa maana tangu tuelekee kwenye uwanja wa wafungwa hatujawaona”
Raisi akatoa simu mfukoni mwake na kumpigia baba mkubwa Eddy, ila akaishusha simu hiyo kama sekunde kumi baada ya kuiweka sikioni. Akairudisha tena sikioni, akaishusha tena kwa muda mchache huo huo.
“Hapatikani?”
“Hapatikani?”
“Ndio”
“Ninakuomba nikawaangalie muheshimiwa”
Raisi akaka kimya kwa sekunde kadhaa akionekana kulifikiria ombi langu.
“Hapana tuendelee na safari, nimetuma vikosi vya jeshi vitakuja kuimarisha ulinzi katika eneo hili”
Sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea na safari ya kuelekea Tanga mjini, akilini mwangu muda wote nikawa ninamfikiria mama na baba mkubwa huku nikijiuliza wamepotelea ndani ya gereza hilo au laa, kwa maana vurugu za wafungwa wale ninaimani zimeweza kuwatisha. Simu ya muheshimiwa raisi ikaita. Akaipokea kwa haraka na kuiweka sikioni mwake.
“Mumefanikiwa?”
“Sasa washikilieni hadi niwakute”
Akakata simu na kunipa maelekezo nielekea kwenye mji wa Sahare.
“Spidi mia na ishirini”
“Sawa”
Nilimpa Babyanka amri ya kuongeza mwendo kasi wa gari zetu kwa maana tunahitaji kuweza kudfika katika eneo hilo la Sahare ndani ya dakika kumi. Barabara ziliweza kutawaliwa na trafiki ambao wanaimarisha ulinzi wa baba bara hiyo wakiamini raisi aliyopo katika uwanja wa Mkwakwani ni raisi kweli kumbe ni raisi feki. Kila trafki aliye simamisha gari letu aliishia kuisima namba ya gari, hatukupunguza wala kuhofia kitu chochote, huku mimi ndio nikiwa ninauongoza msafara huu. Tukafanikiwa kufika eneo la Sahare. Tukaelekezwa hadi sehemu ya tukio ambayo ninaifahamu kabisa, ni sehemu ya jumba ambalo lilikuwa linatumiwa na Meya kuhifadhia wapiganaji wa Al-Shabab.
“Tukashuka kwenye gari huku tukuwa makini, tukaingia kwenye jumba hili huku tukiwa makini sana, tukakutana na wanajeshi si chini ya kumi wakiwa na silaha za kivita, wakiwashikilia wapiganaji wote waliokuwa ndani ya jumba hili wapatao hamsini.
“Mumewashika vipi?”
“Walikuwa ndio wanajiandaa kugawanyika katika kwenda kuvamia mkutano wako”
“Mukiwahoji wana kitua ambacho wanakizungumza?”
“Hapana hakuna kitu ambacho wanakizungumza?”
“Silaha zao mulizo wakamata nazo zipo wapi?”
“Hipo huku”
Mkuu huyo wa oparesheni ya kimya kimya alizungumza na raisi, na kuanza kuongozana naye kwenda kumuonyesha silaha hizi sehemu zilipo, sisi tukafwata kwa nyuma. Tukakuta silaha nyingi pamoja na mabomu vikiwa vimetandazwa chini, huku kukiwa na wanajeshi wengine wapatao sita wakiwa wameimarisha ulinzi sehemu hiyo.
“Aisee hawa watu, dawa yao ni kufa kabisa”
“Muheshimiwa, si tungewarudisha kwao na wakahukumie huko?”
“Huko kwao wenyewe wanashindwa kuwahukumu, sasa nahitaji wote wafe mbele yangu”
Amri ya raisi, hakuna ambaye anaweza kuipinga zaidi ya kuitelekeza. Tukarudi katia sehemu walipo shikiliwa wapiganaji hao. Wakaamrishwa kupanga mistari miwili, wakafanya hivyo huku wengine wakiwa wanavuja damu, wakionekana kushushuwa kipondo kikali kutoka kwa wanajeshi hawa wanao onekana kuwa ni makombandoo.
Walipo maliza kupanga mstari, kila mwanajeshi, akaifunga bunduki yake kiwambo cha kuzuia risasi na hata kama wakipiga risasi mtu aliyeyopo nje ya jumba hili wala hatasikia chochote. Ikatolewa amri ya kijeshi ya kujiandaa, kisha ikatolewa amri ya kushambulia. Milili ya wapiganaji wa kikundi hichi cha Al-Shabab, wakaanza kudondoka mmoja baada ya mwengine huko wote wakiwa wametandikwa risasi zakichwa. Kwa mara yangu ya kwanza katika maisha yangu, ndio ninashuhudia maujia ya watu wengi kiasi hichi, japo jana usiku niliweza kufanya kazi ya kuwaua wapiganaji wengine ila hii ya leo inatisha sana.
“Maiti zao hakikisheni kwamba munazitupa baharini mbali, ambapo hakuna mtu anaye weza kuziona wala kujua ni kitu gani ambacho kimetokea”
“Sawa mkuu”
“Je kuna kingine ambacho kimetoke?”
“Kama ulivyo agiza mkuu wa mkoa tayari yupo chini ya ulinzi, anahojiwa kambini huko”
“Ok hakikisheni kwamba kila kitu kinakwenda kama vile nilivyo agiza”
“Sawa mkuu”
Tukaondoka na raisi namoja kwa moja tukaelekea katika uwanja wa Mkwakwani, ambao umejaa wananchi wengi watanga wakimsikiliza raisi feki akitoa hotuba aliyo iandaa raisi tuliye kuwa naye.
“Amefanya vizuri”
Raisi alizungumza huku akiwa ndani ya gari hapakuwa na mtu aliye weza kushuka. Simu ya raisi ikaita, akaipokea.
“Ndio muheshimiwa mbunge?”
“Mupo salama lakini?”
“Sawa”
Raisi akakata simua na kuirudisha simu yake mfukoni.
“Mama yupo salama”
“Shukrani muheshimiwa”
“Sasa safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza sasa, nitaondoka na vijana nilio kuja nao na nyinyi jichanganyikeni katika raisi huyu murudi naye kesho”
“Sawa mkuu”
“Nimesha mtumia picha zenu kwa hiyo atawatambua pasipo nyinyi kujitambulisha”
“Sawa mku”
Nikashuka kwenye gari na kumuacha kijana wa raisi akiingia kwenye upande wangu wa dereva, huku kijana mwengine akishuka kwenye gari la Babyanka na kuingingia kwenye gari nililo shuka mimi, huku na mimi nikielekea kwenye gari la Babyanka. Raisi na vijana wake wawili wakandoka na kutuacha mimi na Babyanka uwanjani hapa.
“Nina usingizi ile mbaya”
“Wewe una nafuu, mimi hapa nilikuwa ninaendesha gari huku nasinzia sinzia, afadhali sijamuendesha raisi”
“Daa tupate ata kamuda kakulala”
“Sasa hatujajua raisi huyu naye anaondoka hapa uwanjani saa ngapi”
“Ngoja nishuke nitafute ratiba yake.”
Nikashuka kwenye gari huku nikiwa makini, nikatazama walinzi wengine walio zagaa kila kona ya uwanja huu wakiimarisha ulinzi, huku walinzi wengine wakiwa hawafahamu kwamba raisi waliye kuwa naye sio raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kwani raisi mwenyewe alisha ondoka na huyu amevaa tu kinyago kinacho fanana na raisi wetu.
“Kaka habari”
“Safi”
Nikamuonyesha mlinzi huyu kitambulisho changu, akakisoma vizuri, kisha akanirudishia.
“Raisi akitoka hapa anaelekea wapi?”
“Anaeleka mkonge Hotel kupumzika usiku atapata chakula na wazee wa jiji hili”
“Ok asante”
“Ila mbona unauliza kama ni mgeni wa hii ratiba?”
“Hapana mimi muheshimiwa alipa kazi ambayo ndio nimeimaliza muda huu”
“Ahaa sawa”
Nikaachana na mlinzi huyu ambaye alianza kunitilia mashaka, nikaingia kwneye gari na kuufunga mlango.
“Anasemaje?”
“Akitoka hapa anelekea Mkonge hoteli”
“Twende tukatafute sehemu tulale aisee”
“Poa”
Babyanka akawasha gari, tukaondoka eneo hili la hotelini moja kwa moja tukaeleka kwenye hoteli ya Maua INN, kwa maana ndio sehemu ya pekee ambayo si raisi kwa watu kutustukia kwamba sisi ni walinzi wa raisi, japo hoteli hii ipo kaikati ya mji ila imetulia sana.
Tukafika katika eneo hili, tukasimamisha gari letu kwenye maegesho akaanza kushuka Babyanka akaingia ndani, akalipia chumba na moja kwa moja akelekea sehemu kilipo na kwa kupitia kifaa cha mawasiliano akaniambia ni chumba namba ngapi yupo, nikashuka kwenye gari na kufunga milango vizuri, moja kwa moja nikaelekea kwenye chumba hicho, wala sikumsalimia muhudumu wa hii hoteli aliye kaa mapokezi. Nikapandisha gadi gorofa ya nne na kuingai katika chumba alicho nieleza Babyanka. Nikamkuta akiwa amelala kitandani na nguo zake pamoja na viatu vyake huku bastola yeka ikiwa pembeni yake.
“Dany mskaji wangu hembu naomba ukanichukulie maji nina kiuu”
“Ahaa si upige simu?”
“Ahaa sitaki wahudumu kujua jua chumba tulichopo”
Kutokana sikuwa nimekaa sehemu yoyote nikageuza na kutoa chumba huku nikiufunga mlango wa chumba vizuri. Nikaanza kutembea kwenye kordo hii huku nikiwa makini kutazama nyuma na mbele. Mlango wa chumbani cha mbele ukafunguliwa, ikanibidi kupunguza mwendo wa kutembea, macho yakanitoka baada ya kumuona K2 na Lukas wamesimama mlangoni hapo huku wakipigana mabusu ya mdomoni, huku Lukas akiwa amejifunga taulo kiunoni na K2 akiwa amevalia suti yeusi, ila vifungo vya shati lake vikiwa havikajaa vizuri, kwa bahati mbaya, K2 akanitazama, kitu kilicho mstua sana hata Lukas naye alivyo niona akakimbilia ndani.
ITAENDELEA
Saturday, May 25, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments