Pages

Thursday, May 16, 2019

INGIZA DUDU YOTE NDANI BABY SEHEMU YA TANO

"wewe si kidume ngoja nikuoneshe uanaume sasa"alisema baba, akazidi kunitisha,hata mama sikumuona eneo hilo najua angenitetea ila hayupo.
Baba baada ya kufunga mlango na kujiridhisha tayari aliukaza vyema mkanda mkononi kisha akanifata sasa huku amefura kwa hasira.
"nisamehe baba utaniumiza nisamehe."nilitamka kwa kunyenyekea lakini ikawa bure kabisa haikuwa sababu ya yeye kuacha kunipiga.

"wewe si ushakuwa leo nakufundisha adabu."alisema kabla hajamaliza tayari alinirarua mkanda ulionipata mgongoni.

"nisamehe baba sitarudia tena."nilizidi kumuomba msamaha huku nikijikaza na maumivu ya mkanda alionitandika wa mgongo. hakunisikia nilichoongea tena ndio mikanda ilinishukia dabo dabo hata kuizuia nilishindwa.

"baba sasa nakuomba msamaha hunisikii wanipiga tu kwani mimi gogo sisikii maumivu."nilitamka bila haya wala soni za uso na kuto kujali kama ni baba nilifananisha na vijana wenzangu ila yote ni kutokana na jinsi alivyokuwa akinirarua bila huruma.

"unasemaje gao unanikazia sio haya tupigane wewe si kidume."alisema baba, na kuweka mkanda chini hapo.
Na mimi akili zangu za kijinga na jazba niliokuwa nayo eti nikakunja ngumi kitendo kilichopelekea baba anitandike mtama ulionipeleka moja kwa moja chini na kuangukia ule ule mgongo.

"aiiii mama."nilipiga kelele,baada ua kuanguka chini kama mzigo tena kwenye marumaru pale sebuleni.
"amka amka kidume."alisema baba hapo hata nguvu sina za kuamka, alijipa nafasi ya ushindi na kuchukuamkanda wake aliouzungusha kama mwanzo kisha akaanzaa kunitandika mara mbili mbili bila huruma maumivu niliyoyapata hayaelezeki hata kuyasimulia yananitoa machozi ama kweli ukubwa dawa mkubwa ni mkubwa tu.
baba alitandika mikanda bila huruma, aliponiachia nikajikokota hadi mlangoni kwangu.

"nakuchukia baba, nakuchukia sanaa utaona wewe."nilimtishia baba na kusahau mtu mzima hatishiwi nyau.

"unasemajee.?"aliuliza kisha akageuka kunifata hapo nikaingia ndani kwa fujo na kufunga mlango na funguo kabisa.

"wewe gao fungua kichaa wewe nakwambiaje nitakunyoosha wewe nitaomba likizo mwezi mzima kwa ajiri yako tu wewe."alisema baba akiwa mlangoni kwangu.

"achana na mimi si uende kumnyoosha mchepuko wako asikuchune sana sana,mpaka uninyooshe mimi.,"nilipata ujasiri wa kuongea maneno ambayo sijayafikiria yote ni kutokana na kuwa ndani yeye nje.

"unasema wewe.?"aliuliza,hapo nikakaa kimya sikujibu kitu nilizidi kuugulia maumivu ya kupigwa mikanda kadhaa.

Aliniumiza nyakutosha hata mwili nao kila mahali umevimba ni alama za mikanda kila nikijitazama machozi yananitoka hali iliyopelekea nijifunike shuka hakika nilijiwekea kisasi kwa baba tayari nilimchukia kiasi kwamba hata kumsikia naona izrael kanijia. nikiwa nimetulia kichwa kimejaa msongo wa mawazo sambamba na hasira.

"gao mwanangu gao baba kakufanya nini"ni sauti ya mama ilioita mlangoni kwangu, akimaanisha hajui kilichotokea kabisa, nikahifunua shuka kisha nikafungua sauti ya sabufa mpaka mwisho hata wasemavyo nje sisikii na usiku ule niliwawekea watu mziki wa bure kutokana sabufa lililopo chumbani kwangu kuwa na sauti kali nilioifananisha na sauti za spika kubwa,sikuona tabu kujisurubu ngoma za masikio nilichojua ni kupunguza mawazo.
Akili zangu zikanituma nichungulie dirishani hapo bila kutegemea naona kikundi cha watu wavulana kwa wasichana wakicheza mziki niliofungulia ndani.
Nilijichekea mwenyewe japo ninahasira kisha nikaanza kufungasha nguo zangu kwenye begi aliloninunuliaga mama kipindi nilichokuwa naenda dodoma kwa mjomba ambapo alininunulia la kuhifadhia nguo.
niliweka nguo zangu baada ya kuziweka zote hata chafu pia nilishindilia nikiwa na wazo la kutoroka nyumbani nikajitafutie maisha yangu mwenyewe japo ni usiku nilifikiria nikalale hata chini ya sakafu yote ni kutengana huyu baba nisiempenda.
Tayari nilijiandaa na kuzima mziki,kitendo kilicho wakera jamaa wa njee.

"aaaah dj vp weka mambo hayo tukeshe sio"niligundua ni wavuta bange na wanywa gongo hivyo sikuwajali.

Nikasogea hadi mlangoni nikafinya kitasa kikafunguka hapo nikatoka na begi langu haraka haraka nikiwahi mlango wa kutokea nje nilifinya kitasa cha nje ila kabla sijatoka.

"haya wewe mtoto unaenda wapi usiku huu."ni sauti ya mama iliyonistua sana.

"mbona unataka kuniua na presha mwanangu unataka kwenda wapi sasa.?"alizidi kunitandika maswali mama ambayo sikuyajibu nilikuwa nikiugulia maumivu ya mikanda.

"mama nakuamba niache niondoke zangu mimi siwezi ishi na baba hapa nitamtilia sumu au nitamchoma kisu akiwa amelala bure bora niende tafadhali."nilisema bila woga kwa kujiamini na ujasiri huku nimetuna hasira zimenijaa hata macho yalikuwa yakidondokwa na machozi.

"unasemaje mwanangu yani wewe unaweza kuua kakufunza nani tabia hizo za kishetani mlaani ibirisi mwanangu maneno gani hayo umuue baba yako."alisema mama kwa busara ambazo hazikuwa kitu kwangu,niliona ni ngonjera tulizokuwa tukiimba mashuleni kipindi cha mahafari.
Nikiwa nimesimama na mama pale mlangoni kashika begi nisiondoke, baba akatokea tena anatoka kuoga.

"anataka kwenda wapi huyo jambazi"aliniita jambazi jina lililoniuma hadi kutaka kumfata ila mama akanizuia.

"wewe unamwitaje mwanangu jambazi embu nenda ndani huko.

"mama niachie niondoke sitaweza kukaa humu mimi nitamwaga damu ya mtu."nilizidi kutishia tu.

"nyoooookooo labda ukamwage damu ya vikuku vya mama yako ila sio mimi."alisema baba hapo nikamponyoka mama na kukimbilia kabatini nilitoka na umma baada ya kutafuta kisu na kukosa nilitaka kumchoma nao akanizuia kwa kunishika.

"niachie niachie."nililalamika.

"we mtoto huna akili unaweza shindana na mimi."alikasilisha zaidi na maneno yake, nikagundua 'NAZI HAISHINDANI NA JIWE'nilijipa ununda tu ila baba simuwezi.

"jamani mwanangu unanini wewe kutaka kupigana na baba yako,embu mwachie mwanangu,"alisema mama huku akisikitika kisha akanipeleka chumbani kwangu.

"twende ukalale kesho nakupeleka kwa shangazi yako sawa"aliniambia mama ila nikaona tabu hata kumjibu akanifikisha ndani kisha akatoka na kufunga mlango kwa nje nilibaki na hasira mfanowe hakuna nilimlaumu mungu kuchelewa kuniumba hadi kuwa mdogo kuonelewa, maswali yangu hayakuwa na wakuyajibu nilichoona nikujitupa kitandani na hasira zangu, kimya kilitawala hadi naja kusikia mlango ukikongwa nikagundua kumekucha nilinyanyuka kwa tabu kwenda mlangoni nikakutana na mama.

"jiandae nikupeleke sawa."alisema mama hata sikumsalimia, hasira hazikuisha.
Nililiendea bafu na kujiandaa haraka siku hiyo ya ijumaa, nilipokuwa tayari mama akawasiliana na shangazi kisha tukatoka.

Nje hakukuwa na mtu hata mama imma sikumuona nimuage,nilipita kimya kimya na mama ila nilikuwa na lengo la kumtembelea mama imma siku nikipata nafasi.
Mama alinipakiza kwenye bajaji na begi langu kutokana na kwa shangazi sio mbali na shule ninako somea kwa dada ndio mbali hivyo alimlipa kabisa dereva na safari kuanza umbali mfupi tu nilifika hadi mlango kwa shangazi, nikashuka na kupokewa begi likaingizwa ndani,nilianza kuithaminisha nyumba kwa uzuri wake kila kitu kipo nilipapenda sana mandhali yake nikaingia ndani.

"karibu mwanangu gao jisikie upo nyumbani hapa ni kwenu."

"sawa shangazi nashukuru sana"nilijibu hapo nikajua sio mswahili hafagilii shikamoo.

Alizidi kunikaribisha pale kama vile ni mama yangu mzazi,nilichokumbuka mule alikuwa akiishi na wasichana watupu wakuwepo wanae wawili waliokwenda shule wanarudi pamoja na mfanyakazi wa ndani na mtoto wa mume wake. nilikumbuka mama aliniambiaga siku moja kumbu kumbu hiyo haikufutika kichwani mwangu. tukiwa tumekaa kwenye makochi nadhifu yaliyopendeza kwa mtindo wake yalivyotengenezwa na upambwaji pale sitting room kulipo wekwa runinga kuu kuu ya ukutani set za sabufa, meza ya kioo, maua mbali mbali na masofa ya kila aina.

"Ester ester."aliita shangazi.

"abeeh dada."

"njoo."alimwambia aje hapo ester akaja,Ukisema ester ester kweli kuanzia umbo lake mpaka jina lake ni dhahiri vilifanana nilimmezea mate alipokuja ila nikajipa ustaarabu 'NJIWA WA KWAKO MANATI YA NINI"ndio maneno yaionikaa akilini wakati huo.

"umemuona huyu ni kaka yako anaitwa gao,heshima iwepo."

"sawa dada."aliitika kwa kuinama chini.

"muamkie sasa."akiendelea kusona shangazi, ila nikamwambia ache niligundua anatania alafu ester ananidhamu ya woga alikuwa anataka kuniamkia.

"haya katuletee juisi ya embe ya baridi"akiagiza shangazi hapo ester akiwa anaondoka nikawa natazama alivyoumbika na ufupi wake pamoja na unene ndio kabisa hata nyuma alifungasha,Nilimtazama hadi akakata kona.

"nambie mwanangu habari za huko"

"salama shangazi za hapa je mnaendeleaje"tuliendelea kuongea ester akaleta juisi tulipiga story huku tukimeza mafunda ya juisi.

"hivi shangazi yule anaeishi na mama ni baba yangu."nilimtandika swali ambalo hakutegemea kama nitamuuliza alipata mshangao shangazi.

"haah kwanini umeuliza.?"

"nataka kujua tu."

"gao hiyo ni siri ya muda mrefu sana tumekufichia wewe embu achana nayo nitakuambia."alikatisha maneno haraka na kumuita ester aliekuja.

"nenda kamuoneshe chumba mwenzio."

"sawa dada."aliitika hapo sikuwa na pingamizi, nikaamka kishingo upande tu na kumfata ester kunipeleka huko.
Nilikuwa nyuma ester mbele niliehisi akinifanyia makusudu kwa utembeaji wake hadi tunafika chumbani dushelele linaleta shida.......
ITAENDELEAAAA..

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +