Aliamka na kumsimamisha mzoa taka ambaye bado alikuwa hoi kwa ‘mzuka’ ingawa naye alishabanjua dafu lake moja, lakini bado alikuwa anataka tena…
“Simama basi.”
Mzoa taka alisimama…
“Vaa…”
Mzoa taka alivaa nguo zake, akaendelea kusimama…
“Chukua matakataka yako, mimi nakuja sasa hivi,” alisema mama Joy huku akienda ndani.
Mzoa taka alijishangaa kwa jinsi alivyobaki na harufu ya pafyumu ya mama Joy…
“Mmm…ananukia vizuri, sijui kajimwagia nini mwilini?”
Baada ya dakika mbili tu, mama Joy alirudi, akampa mzoa taka shilingi elfu hamsini, nyekundu tupu…
“Hizi ukanunue suruali nzuri, shati zuri, viatu, chup*** na kisha uoge uwe mzuri zaidi ya hapa, sawa kijana wangu?”
“Asante sana mama, sawa.”
Mzoa taka aliweka pesa mfukoni, akabeba furushi lake na kutoka.
Getini, mlinzi alimtupia jicho baya mzoa taka…
“Hivi wewe kijana, huko mitaani hakuna matakataka hadi uje hapa?”
“Sasa kwani yako?”
“Jibu swali wewe, acha ujeuri, nitakuwa sikufungulii…”
“Usifungue tuone kama nitakuwa siingii…”
“Utaingia kwa njia gani?”
“Pana nini hapo getini..?” mama Joy aliuliza kutokea mbali karibu na mlango mkubwa wa kuingilia ndani…
“Si huyu hapa,” alisema mzoa taka…
“Anasemaje?”
“Mama namtania tu huyu ni mtani wangu. Teh! Teeh! Teeeh!”
Mama Joy aliingia ndani. Mwili wote ulikuwa ukinuka jasho la mzoa taka. Mbaya zaidi alimchafua hadi nguo aliyovaa…
“Daaah! Yataka moyo kuwa na mpenzi kama huyu,” alisema moyoni mama Joy, mara honi ya gari mlangoni ikalia…
“Mh! Siyo mume wangu kweli huyo?”
“Na kama ni mume wangu si ajabu amemuona mzoa taka,” aliwaza mama Joy huku akikimbilia chumbani, akachukua taulo kisha akakimbilia bafuni ambako alioga kwanza.
Alipotoka alimkuta mumewe amekaa sebuleni. Mama Joy alitetemeka sana…
“Vi…pi mwenzetu?”
Baba Joy alimkazia macho mkewe bila kumjibu kitu halafu akaangalia kwenye tivii ambayo ilikuwa haijawashwa…
“Baba Joy.”
Baba Joy alimwangalia mkewe kama ishara ya ‘nakusikiliza ongea’. Lakini mama Joy alipoona hali ile, hakuongeza neno, alipitiliza chumbani…
“Mh! Hapa kuna ishu, lazima.”
Licha ya kujikausha kwa taulo lakini aliendelea kuhisi ananuka uchafu aliogusishwa na mzoa taka. Alivaa gauni simpo, akatoka hadi mlango mkubwa, akatumbukiza miguu kwenye sendozi, akaelekea getini…
“Mlinzi…”
“Naam mama…”
“Baba Joy alipoingia alisemaje?”
“Hajasema kitu, amepiga honi tu kisha akaingia.”
“Ulimwamkia?”
“Ndiyo mama.”
“Akaitikiaje?”
“Kha! Mama kwani wewe nikikuamkiaga huwa unaniitikiaje?”
“We mshe** nini? Nakuuliza swali na wewe unanijibu swali…”
“Alisema marhaba, nikamuuliza mbona umewahi kurudi? Akasema amechoka sana…”
“Mlinzi fungua geti haraka,” sauti ya baba Joy ilisikika kwa kishindo na vile ilikuwa nzito na nene ndiyo kabisa.
Baba Joy aliingia kwenye gari, likarudi ‘rivasi’ na kugeuza kisha likatoka ndani bila kuaga mtu. Mlinzi alifunga geti nyuma ya baba Joy…
“Mlinzi,” mama Joy aliita…
“Naam mama…”
“Hebu njoo huku ndani,” mama Joy alisema huku akianza kutembea. Alipofika sebuleni, alikaa mkao wa hasira.
Mlinzi aliingia…
“Nifunge mlango mama..?”
“Wa nini..?”
“Nilikuwa nauliza tu…”
“Hebu kaa hapo.”
Mlinzi naye alianza kutetemeka, alihisi kibarua kimeingia mdudu mbaya…
“We mlinzi si una namba ya mume wangu..?”
“Ndiyo…”
“Simu yako iko wapi?”
“Kule kwenye kibanda changu.”
“Nenda kailete haraka sana.”
Mlinzi alisimama na kutoka. Mama Joy aliwaza mengi kichwani mwake wakati anamsubiri mlinzi…
“Huyu lazima alimpigia simu mume wangu, akamwambia mzoa taka amekuja, maana jana si alisikia baba Joy alivyokuwa akikataza watu kuingia? Lakini yeye alisema hataki watu waingie usiku, sasa kwani saa hizi usiku?”
“Halafu ni kweli itakuwa yeye maana hawapatani tangu zamani. Hata leo yenyewe pale getini si walibalulana kidogo. Atakuwa yeye tu. Baba Joy alikuja akidhani atamkuta mzoa taka, bahati nzuri kashaondoka.”
Mara, mlinzi aliingia…
“Iko wapi?”
“Hii hapa.”
Mama Joy aliipokea simu hiyo na kusachi namba zilizopiga kwa siku hiyo, hakukuwa na namba zilizopiga wala kupigwa…
“We unan’tania siyo..?”
“Hata kidogo mama…”
“Ina maana hii simu yako hujapiga simu wala kupigiwa..?”
“Leo kuna wakati nilitoa laini. Kwa hiyo kuna uwezekano namba zote zilizopigwa na nilizopiga zimefutika zenyewe.”
Mama Joy alikubaliana na hilo, lakini alijua mlinzi alifanya hivyo makusudi. Yaani alipomwambia akachukue simu, mlinzi alipofika alitoa laini au alifuta namba zote ili kupoteza ushahidi kama alimpigia baba Joy…
“Haya nenda,” alisema mama Joy. Mlinzi alisimama, akaondoka bila kuaga.
Nyuma, mama Joy alianza kufikiria vitu vyake…
“Huyu mlinzi atakuwa adui wangu kwa mzoa taka. Kama anaweza kumpigia simu mume wangu kumwambia kuna mwanaume ameingia ni tatizo, tena kubwa sana.
“Kinachoonekana, baada ya mume wangu kurudi alimwambia ameshatoka ndiyo maana hata alipoingia ndani alifikia sebuleni. Tena mbaya sasa amekuta mi natoka kuoga, si ndiyo hatari zaidi?
“Sasa hapa nifanyeje? Maana kama kutokea limetokea. Nikisema nimchongee chochote kwa mume wangu atajua natengeneza bifu kwa sababu anatoa siri zangu na mzoa taka, dawa yake hapa moja tu…” alisema moyoni mama Joy kisha akabetua vidole, akasimama, akaingia ndani…
“Asumta,” alimwita mwanamke anayefanya kazi ndani ya nyumba yake…
“Abee…”
“Kaniitie mlinzi.”
Asumta alitoka nje hadi kwa mlinzi, tena kwenye kibanda chake…
“Fuko unaitwa na bosi wa kike.”
“He! Leo mama yangu umetoka nje, ajabu!”
“Unaitwa huko.”
Asumta na mlinzi huyo waliongozana hadi ndani, Asumta akawa anapita, mlinzi akabaki sebuleni…
“Asumta…”
“Abee bosi…”
“Endelea na kazi zako, mimi nina maongezi na Fuko…”
“Sawa bosi,” Asumta aliitika huku akiinamisha kichwa kama ishara ya utii.
Mama Joy alisimama, akamfuata mlinzi kwenye kochi alipokaa, akapiga magoti chini yake na kumshika mapajani…
“Niambie ukweli. Ulimpigia mume wangu simu kumwambia..?”
“Kumwambia nini?”
“Kwamba mzoa taka ameingia..?”
“Lini? Leo?”
“Leo ndiyo.”
“Hapana, sijampigia.”
“Fuko…”
“Naam mama…”
No comments:
Write comments