Pages

Tuesday, May 21, 2019

NANI AJUAYE SINA HATIA?

WHO KNOWS I’M INNOCENT?
(NANI AJUAYE SINA HATIA?)

Imetungwa na
Mwandishi
Geofrey Malwa
Ili kukukumbusha kuwa hivyo ulivyo sasa ni kwa neema tu.


***

Nilikuwa chachu ya furaha kwa wazazi wangu.Mtoto pekee wa kiume waliyenaye mwenye adabu na heshima,walijivunia hilo.Mfano nilikuwa mimi wa kijana jinsi anavyotakiwa kuwa kati ya vijana wengi wa kizazi hiki,mwenye maadili na elimu ya juu.Niliwapenda sana wazazi wangu na walinipenda mara mbili kuliko nilivyowapenda mimi.

Kwenye maisha hakuna ajuaye kesho,ndio maana tunakumbushwa kusali kila wakati ili Mungu atuepushie balaa na mikosi ya dunia hii,
“mwanangu Mungu akutangulie,naamini utafanikiwa,”
“amina mama,ubaki salama,”
“enhee…tena usichelewe leo nakupikia ndizi na nyama,”
“kweli?”
“ndiyo,nakupenda sana mwanangu,mtoto mwenyewe mmoja kwanini usinenepe jamani.” Tulicheka kwa pamoja baada ya kujibizana hivyo na mama yangu.Kwa jina niliitwa Ivan,nilimaliza chuo kikuu na nilisomea uhasibu hivyo siku hiyo nliitwa kwa ajili kufanyiwa intavyuu.

Nliondoka nyumbani hapo na kufunga safari mpaka Ofisini nilikoitwa.Nilikuwa na furaha sana kwani nilijiamini kupita maelezo,niliwakuta wenzangu watatu.Basi tukawa tunaitwa majina mmoja mmoja,waliingia wenzangu watatu kwa zamu ambapo ilikuwa ukitoka kuna sehemu unaelekezwa ukasubirie majibu kujua ni nani amepita kwa ajili ya kazi.

Kabla sijaingia mimi,alikuja jamaa mmoja aliyeonekana kufahamiana na sekretari,aliposimama wakati akiongea na huyo sekretari,simu yake iliita,akaitoa kutoka mfukoni…kitendo cha kuitoa simu mfukoni alidondosha chini kitambaa fulani cheupe.Kwa ukarimu nilinyanyuka na kukiokota kisha nikamkabidhi,alikipokea na kunishukuru japo mkono wake huo alivalia gluvo vyeusi na ndio aliopokelea kitambaa hicho.Moja kwa moja alipitiliza mpaka kwa bosi kisha baada ya dakika kama tano alitoka na kumuaga Sekretari,aliniaga na mimi pia huku akiniangalia kwa macho fulani ambayo sikuyaelewa kwa muda huo yalimaanisha nini.
“ingia kaka,hakuna mtu tena.” Alisema Sekretari akimaanisha naweza kuingia.Nilijiweka sawa na kuingia ndani.
“shikamoo mkuu,” nilisalimia lakini sikuitikiwa
“mkuu!” nilimshtua tena kwani kichwa chake alikiinamisha kwenye meza
“nakusalimia mkuu!” nilirudia tena na kuona kama ni mkosi siku yangu ya intavyuu kumkuta bosi amelala.Ilinibidi nizunguke meza na kumgusa kichwani huku nikimwita,lakini cha kushangaza ile kumgusa kichwa alikwenda kama gogo,hakunishangaza yeye kuwa hivyo tu,zaidi nilishangazwa na kile kitambaa cheupe ambacho niliokiokota na kumpa yule jamaa pale kwa Sekretari,kiliwepo hapo mezani,tena kiligandamizwa na paji la uso la Bosi huyo,Niliogopa sana,kumgusa bosi kwenye mapigo ya moyo yalisimama,nikajua ameshafariki.Kwa mwendo wa haraka nilitembea ili nikamtaarifu Sekretari,kumbe naye Sekretari alikuwa akija kwa Bosi hivyo nilipofungua mlango ilibaki kidogo tugongane uso kwa uso,
“kaka vipi! Mbona kasi namna hiyo?”
“Bosi amekufa,”
“unasemaje? Kivipi?”
“mi sijui,nimemkuta hivyo!” Sekretari alipopiga jicho mezani kwa Bosi aliogopa na kupiga kelele kubwa sana.Watu wakajaa,kila mmoja alishangazwa na tukio lile…sikuwa na cha kujibu kwasababu macho yao yote yaliniangalia kama ndio mimi nimeua,sikuamini.Simu ilipopigwa polisi,haraka waliwasili.Nilishuhudia wakikichukua kile kitambaa kwa ajili ya uchunguzi zaidi ambacho nilimwokotea yule jamaa aliyekuwa akiongea na Sekretari.

Taarifa ilipomfikia mama kuwa nimewekwa lumande kwa ajili ya uchunguzi zaidi alipoteza maisha kwani alikuwa na presha.Baba alijikaza sana na kutoamini kilichotokea,kutoka sifa ya kuwa kijana mzuri mwenye maadili mpaka muuaji.Uchunguzi ulipokamilika,ilisemekana marehemualiuawa kwa sumu iliyopuliziwa kwenye kitambaa,na kitambaa kilichotumika kiligundulika kuwa na alama zangu za vidole,sikuwa na pa kutokea kwenye kesi hiyo.
“NANI AJUAYE SINA HATIA? Kutoka ndani ya moyo wangu nilijua sijamuua yule Bosi wa watu lakini nani atanisikiliza na kuamini hivyo?” nilijisemea moyoni huku mtu pekee aliyekuwa amesimama upande wangu ni baba yangu mzazi mzee Saimoni.Ni bora hata Ofisi ingekuwa na kamera ingejulikana aliyefanya tukio hilo.Nilihukumiwa Jela kifungo cha maisha,sikuwahi kuwaza hata siku moja kama ningeweza kufungwa jela tena kwa kosa la kutoa uhai wa mtu? Niliumia sana.

Unayesoma hii simulizi yangu muda huu,tambua kuwa maisha ni mafupi sana.Na sio kwamba wewe ukiwa sio mzinzi basi hutopata UKIMWI,usipokuwa mgomvi hutopigwa na watu,sio kwamba usipokuwa mwizi hutopewa kesi ya wizi,ona mimi niliyekuwa sio muuaji kuitwa muuaji na kuchukiwa na ndugu wa marehemu bila sababu ya kweli,mama yangu mzazi pi aalipoteza maisha kwa ajili ya tukio ambalo sikufanya! Mambo mengine unaepushiwa kwenye maisha si kwamba unampendeza sana Mungu bali ni kwa neema yake tu.Mshukuru Mungu kwa mahali ulipo sasa,nilichukia wakati nilipohukumiwa lakini sasa niko Jela na ninaamini Mungu alikuwa na mpango mzuri na maisha yangu na niko sehemu sahihi….

MWISHO.

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +