Pages

Saturday, May 18, 2019

SIMULIZI YA *SIN* SEHEMU YA 20........ ONLY 18+

ILIPOISHIA
Wakawasiliana na RPC pamoja na IGP na kutoa taarifa hiyo ya kupotea kwa Tomas. Agizo la IGP kwa vijana wake walipo chini yake akiwemo RPC Karata ni kuhakikisha kwamba wana toa taarifa kwenye vituo vya usafiri vyote Tanzania ikiwemo Bandari zote, Airport zote, Vituo vyote vya mabasi, dalalada na mipaka yote ya jiji la Dar es Salaam inayo ruhusu mtu kutoka nje ya Dar es Salaam kufungwa. Huku mipaka yote ya Tanzania kufungwa na ulinzi mkali sana ukazidi kuimarishwa katika maeneo hayo. Picha ya Tomas, ikaanza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na vituo vya televishion huku vituo vya redio vikipewa sifa za Tomas na kuzitangaza usiku huo huo, ili hata ikitokea mtu kumuona jambazi huyo aweze kutoa taarifa kwa askari. Zawadi ya milioni kumi ikatengwa na jeshi la polisi na kwa yoyote atakaye fanikisha kukamatwa kwake basi ata pewa zawadi hiyo.

ENDELEA
Defenders za Polisi, zikazidi kusambaa mitaani huku msako wa kumtafuta Tomas ukizidi kupamba moto. Hakuna aibu kubwa wanayo jisikia askari ni kumpoteza muhalifu tena katika makao makuu yao. Kwani kitendo hicho kitalitia dosari kubwa snaa jeshi la polisi mbele ya jamii wanayo ilinda.
Tomas baada ya kumaliza kuweka kila kitu chake ndani ya begi na kujianda. Akatoka sebleni, akazima taa za ndani humo huku akiwaza ni wapi aelekee. Mvua inayo endelea kunyesha nje na giza kidogo kuna mpa wasiwasi wa kutembeaa mtaani peke yake, kwani kwa sasa hana gari. Tomas akwasha tv yake, kitu kilicho mstua ni kukutana na picha yake inayo onyesha kwamba ana tafutwa na zawadi ya milioni kumi imetolewa kwa wananchi watakao fanikisha kukamatwa kwake.
“Ohoo Mungu wangu”
Tomas alihamaki huku akihaha. Akarudi chumbani kwake kwa haraka na kuchukua bagi lake la nguo na kulivaa mgongoni. Kiasi cha pesa pamoja na hati zote za kusafiria alizo nazo zipo ndani ya mfuko wa suruali yake ya jinzi aliyo ivaa. Akachukua simu yake ambayo kwa mara nyingi huwa haitumii na amesajilia laini hiyo kwa jina la rafiki yake. Tomas akarudi sebeli na kuzima tv. Akatoka nyumbani kwake hapo na kufunga geti, akaanza kutembea kwenye viwambaza vya giza giza huku akiwa makini sana kuhakikisha kwamba askari hawamkamati. Akafika karibu na eneo la nyumba ya rafiki yake aitwaye Steve. Akampigia na kwa bahati nzuri Steve akaipokea simu hiyo.
“Ni mimi”
Tomas alizungumza huku akiwa makini kuendelea kuanganza angaza eneo hilo alilo simama.
“Vipi hii ni namba yako Tom”
“Ndio kaka. Nipo karibu na kwako hapa nina hitaji msaada wako”
“Vipi kwema kaka?”
“Sio kwema sana. Naomba unisaidie kunifungulia”
“Poa acha niamke”
Tomas akakata simu na kutembea kwa ahraka hadi katika nyumba ya rafiki yake. Steve aka mfungulia rafiki yake huyo mlango na akaingia ndani.
“Vipi mbona na mabegi kaka usiku usiku huu, kuna tatizo gani?”
“Kaka kwana nashukuru kwa kunisaidia. Hapa nilipo mwenzako nina matatizo makubwa sana”
Steve akamtazama Tomas aliye lowana mwili mzima, kisha aka tazama saa yake ya ukutani na ina muonyesha ni saa tisa usiku.
“Ngoja nikuletee taulo, ujikaushe kaushe maji kaka”
Steve alizungumza huku akiingia chumbani kwake, akarudi sebeleni akiwa na taulo. Akampatia Tomas na akaanza kujifuta mwili mzima.
“Ehee kaka saa tisa hii na namba mpya kanisa ume tumia. Hembu niambie ni nini kinacho endelea?”
“Kaka yule mama amenisababishia matatizo makubwa sana”
“Mrs Sanga?”
“Ndio mwanangu?”
“Matatizo gani ndugu yangu”
Tomas akaanza kumuadithia rafiki yake jambo moja baada ya jengine. Ila jambo la kuingiliwa kinyume na maumbile alilo fanyiwa na nabii Sanga alilificha na kuifanya iwe siri yake.
“Daa kaka pole sana. Sasa una ondokaje Dar na Tanzania kwa ujumla?”
“Yaani ndugu yangu hapa hata sieweli. Nahisi kuchanganyikiwa”
“Wewe ni ndugu yangu na tumesaidia kwenye mambo mengi sana. Kaa hapa kwangu kwa usiku huu hadi kuki pambazuka basi tuta kuwa tume pata njia ya kukutoa nje ya Dar na pia utatoka nje ya nchi hii”
“Sawa ndugu yangu nina shukuru sana kwa msaada wako”
“Usijali kaka. Chumba cha wageni kipo wazi una weza kukaribia”
Steve alizungumza huku akimuonyesha Tomas chumba hicho na akaingia ndani humo huku Steve naye akiingia chumbani kwake na kuendelea kulala.
***
Hadi kuna pambazuka alfajiri, mrs Sanga bado yupo bafuni na an alia kwa uchugu sana. Kipigo alicho kipata kime mvimbisha baadhi ya maeneo katika mwili wake. Taratibu akanyanyuka huku akichechemea, akarudi chumbani kwake na kumkuta mume wake akiwa ame lala usingizi fofofo kitandani. Mrs Sanga taratibu akavua nguo zake na kubaki kama alivyo zaliwa. Akasimama mbele ya kioo kikubwa kilichopo ndani humo na kutazama majeraha aliyo yapata kisha taratibu akapanda kitandani huku akiendelea kutafakari ukatili alio ufanya mume wake usiku.
“Baba Julieth”
Mrs Sanga aliita kwa sauti ya upole huku akimgusa begani mume wake.
“Nini?”
“Tuna weza kuzungumza?”
Nabii Sanga akageuka kwa haraka na kumtazama mke wake. Akakutana na sura ya mke wake iliyo vimba vimba kutokana na makofi aliyo kuwa akimtandika.
“Mume wangu nakuomba unisamehe, nakuahidi kwamba nitakuwa nawe bega kwa bega katika kila jambo”
“Ni hivyo au kuna kingine unacho kihitaji kukizungumza?”
“Jambo jengine nina kuomba usinisaliti ukifanya hivyo nami nita kuadhibu kwa namna ambayo nina itambua mimi mwenyewe na kitu kingine sihitaji kumuona yule Magreth kanisani kwetu”
“Una zungumza hivyo wewe kama nani?”
“Kama mke wako. Umeniadhibu kihaki kwa maana nime fanya makosa. Sikulaumu kwa kunifanya hivi ila na wewe nakuomba uachane na yule mwanamke”
“Una ushahidi kwamba mimi na yeye tuna mahusiano?”
“Tomas aliniambia kila jambo”
“Yaani ukitaka nikuvunje vunje tena. Tamka hilo jina la Tomas mbele yangu. Umenielewa wewe”
“Sinto litamka tena ila nilicho kizungumza ni ukweli, simtaki Magreth kanisani kwangu”
Mrs Sanga alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Poa acha nilale nime choka”
“Nashukuru kwa kunielewa”
Nabii Sanga akanifunika shuka huku akigeuka na kumpa mke wake mngo. Mrs Sanga kwa jinsi alivyo jeruhiwa hakuweza hata kujilaza mwili zakwa zaidi ya kukaa kitako kitandani kwa maana kipigo alicho kipata ni kizito sana
‘Ehee Mungu nitengeneze niwe mpya kwenye haya maisha’
Mrs Sanga alizungumza huku machozi yakiendelea kumbubujika usoni mwake.
***
“Hei”
Evans alimuita Magreth aliye lala pembeni yake kwa sauti ya chini.
“Beee”
“Amka kume pambazuka”
“Kume kucha?”
Magreth aliuliza huku akiwa amejawa na mstuko. Akasimama na kuchugulia dirishani, mwanga wa jua ulio tawala eneo hilo ukamfanya amkumbuke Sheby aliye kuja naye jana usiku.
“Evans nina kuja”
Magreth alizungumza huku akichukua wallet yake na kutoka ndani humo. Akaelekea eneo la maegesho ya magari na kumkuta Sheby akiwa amelala ndani ya gari lake. Taratibu aka gonga kioo cha gari hilo na kumfanya Sheby kukurupuka, taratibu Sheby akashusha kioo.
“Mbona ume kurupuka, ulikuwa una ota ndoto ya kukimbizwa na simba nini?”
“Yaani wee acha bora hata ningeota hivyo. Ila nilicho kiota si kizuri kabisa”
“Pole mwaya kwa kukuacha hapa usiku wote peke yako”
“Usijali, nilifwata agizo lako la kuhakikisha kwamba nina kusubiria”
“Sasa ngoja nimalize kumuangalia mgonjwa wangu kisha nitatoka tuondoke”
“Sawa”
Magreth kwa haraka akarudi katuka chumba alicho lazwa Evans. Akamkuta daktari akifungua jeraha la Evans kwa ajili ya kulisafisha.
“Ahaa samahani dada una weza kusubiria nje nimalize hii kazi”
“Sawa dokta je kidonda cha mgonjwa kine endeleaje?”
“Samahani dada yangu. Sinto weza kukujibu hadi niimalizie hii kazi.”
“Sawa. Evans tuta onana baadae nina rudi nyumbani kubadili nguo”
“Sawa Mage”
Magreth akatoka ndani humo na moja kwa moja akaelekea alipo muacha Sheby na akaingia ndani ya gari na safari ya kurudi nyumbani kwake Kigamboni ikaanza.
“Mbona ume tumia muda mwingi sana hospitali, mgonjwa alikuwa katika hali mbaya sana au?”
“Ndio ila nashukuru Mungu asubuhi hii madaktari wameweza kumaliza upasuaji”
“Ahaaa pole sana”
“Vipi mke wako ana hali gani na ujauzito wake?”
“Ana endelea vizuri”
“Hivi ana shuhulika na nini?”
“Yeye?”
“Ndio yeye”
“Yupo nyumbani tu.”
“Basi akifanikiwa kujifungua basi nita muomba katika biashara yangu ambayo nitakwenda kuianzisha. Unajua kwa sasa wana wake tuna takiwa tupambane ili tuweze kuwasaidia waume zetu. Ikitokea kwa bahati mbaya japo hatuombei, wewe ume tokewa duniani, una hisi uta muacheje hapa duniani na mtoto mdogo?”
“Mmm hilo ulilo lizungumza ni kweli”
“Ndio kama ulikuwa na imani potofu ya kuto mruhusu kufanya kazi, basi ifute hiyo imani yako”
“Nimekuelewa sister”
Wakafika nyumbani kwa Magreth. Magreth akamlipoa Sheby laki na nusu.
“Sheby jumamosi njoo unifundishe kuendesha gari langu”
“Kweli dada?”
“Ndio jitahidi una tenga hata masaa mawili, nita kulipa”
“Sawa dada yangu”
“Ila Sheby hakikisha kwamba humleti au kumuambia mtu yoyote wa mtaani kwetu kuhusiana na hapa nina ishi”
“Usijali sister sinto muambia mtu yoyote”
“Haya asubuhi njema”
“Nawe pia dada”
Sheby akaondoka na Magreth akafunga geti lake na moja kwa moja akaingia ndani kwake. Akapitiliza hadi bafuni, akaoga na kupanda kitandani kwa ajili ya kuumalizia usingizi na uchovu wa mitanange aliyo pitia jana usiku.
***
Hadi kuna pambazuka Tomas hakuweza kupata usingizi. Habari ya kutafutwa kwake hakika ina mpa mashaka na wasiwasi mkubwa sana. Tomas akaamka kitandani kwake na kuelekea sebleni, akawasha luninga na kuanza kufwatilia kila kinacho endelea juu ya kutafutwa kwake.
Steve aka kurupuka kitandani kwake huku akiwa amejawa na mawazo ya uwepo wa rafiki yake ndani kwake. Akaingia kwenye mtandao wa Instergram na kuona ofa ya milioni kumi iliyo tolewa na askari. Akakaa kitako kitandani huku akiwa ana waza ni kitu gani ambacho ana weza kukifanya.
‘Milioni kumi ni nyingi sana kwa hali ya sasa lazima niipate.’
Steve alizungumza huku akiitafuta namba ya simu ya afande Mweta. Akamtumia meseji afande huyo na kumueleza kwamba mtuhumiwa wanaye mtafuta yupo nyumbani kwake. Steve alipo hakikisha kwamba meseji hiyo imemfikia mlengwa, akatoka chumbani kwake na kumkuta Tomas akiwa amekaa sebleni.
“Kaka umesha amka?”
Steve alimuuliza Tomas aliye kaa kimashaka sebleni hapo.
“Yaa kaka”
Steve akatupia macho yake kwenye luninga na kuona picha ya Tomas pamoja na dau la pesa lililo tangazwa na jeshi la polisi.
“Kaka hivi ni kosa gani kubwa ulilo lifanya hadi kutafutwa hadi kwa kuwekewa dau la milioni kumi?”
“Yaani kosa ni kama lile nililo kuaambia la kumteka nabii Sanga na mbaya zaidi wazo alilitoa mume wake”
“Sawa kaka, hapa hakuna muda wa kujutia. Nina mpango ambao nina imani kwamba uta kusaidia kutoka nje ya jiji la Dar es Salaama na Tanzanai kwa ujumla.”
Steve alizungumza kwa lengo la kuzidi kumpotezea Tomas muda huku akisubiria majibu kutoka kwa afande Mweta aliye mtumia ujumbe mfupi wa meseji.
“Mpango gani?”
“Hatuwezi kutumia airport. Inabidi tutumie usafiri wa malaori ambayo yana kwenda nchini Afrika kusini”
“Ndugu yangu kwa kutumia malori si itakuwa ni rahisi sana kukamatwa?”
“Hapana hapa tuta taufuta lori la mizigo ambalo moja kwa moja uta ingia ndani ya mizigo husika na nina imani una weza kufika salama nje ya Tanzania na huko mbeleni uta endelea na safari yako kama kawaida ndugu yangu”
Mlio wa simu ya Steve uka wafanya watazamane. Steve akaitazama namba hiyo ya afande Mweta ambaye ali mtaarifu juu ya uwepo wa Tomas hapo yumbani kwake. Kitita cha milioni kumi hakika kime mtamanisha sana Steve na kujikuta akivunja uaminifu wa urafiki wake na Tomas. Steve akaingia chumbani kwake na kuipokea simu hiyo.
“Ndio”
“Una uhakika huyo mtu yupo nyumbani kwako?”
“Ndio yupo hakikisheni kwamba muna wahi na muta…….”
Steve akajikuta akihamaki mara baada ya kumuona Tomas akiwa ameingia ndani humo pasipo hata kubisha hodi. Sura ya Tomas imejaa mikunjo itokanayo na hasira kwani kauli zote za Steve zina ashiria kwamba Steve ana wasiliana na askari.
ITAENDELEA
Haya sasa, Tomas ametambua usaliti wa rafiki yake ni nin atafanya ikiwa ana tafutwa jiji zina la Dar Es Salaam na Tanzania nzima kwa ujumla? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 21.

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +