Pages

Sunday, May 19, 2019

SIMULIZI YA *SIN* SEHEMU YA 21........ ONLY 18+

ILIPOISHIA
Mlio wa simu ya Steve uka wafanya watazamane. Steve akaitazama namba hiyo ya afande Mweta ambaye ali mtaarifu juu ya uwepo wa Tomas hapo yumbani kwake. Kitita cha milioni kumi hakika kime mtamanisha sana Steve na kujikuta akivunja uaminifu wa urafiki wake na Tomas. Steve akaingia chumbani kwake na kuipokea simu hiyo.
“Ndio”
“Una uhakika huyo mtu yupo nyumbani kwako?”
“Ndio yupo hakikisheni kwamba muna wahi na muta…….”
Steve akajikuta akihamaki mara baada ya kumuona Tomas akiwa ameingia ndani humo pasipo hata kubisha hodi. Sura ya Tomas imejaa mikunjo itokanayo na hasira kwani kauli zote za Steve zina ashiria kwamba Steve ana wasiliana na askari.

ENDELEA
“Jamaa una zungumza na nani?”
Tomas aliuliza huku akiwa amefura kwa hasira. Steve kwa kubabaika, akajikuta akiponyokwa na simu hiyo na ikaanguka chini na kumfanya Tomas aweze kuona namba iliyo andikwa jina la Afande Mweta na bado ipo hewani.
“Ndugu yangu huu ndio mpango ulio kuwa una nishirikisha pale sebleni eheee…..?”
Tomas alizungumza huku akiendelea kumsogelea Steve aliye anza kurudi nyuma kwa kuogopa. Tomas kwa hasira akamvamia Steve na kumuangusha chini. Akaanza kumshindilia mangumi huku akiendelea kumlaumu ni kwa nini ana wasiliana na askari na ana vunja uaminifu wake. Katika kurupushani hizo za kupigana kwa bahati mbaya kichwa cha Steve kika gonga kwenye pembe ya kitanda ambayo ime chongoka na kusababisha eneo la nyuma la kichwa chake kutoboka na damu nyingi zikaanza kutoka.
“Tomas mwanangu una…..nii….u….a”
Steve alizungumza kwa shida huku akimuona malaika mtoa roho akija kwa kasi sana. Tomas akajikuta akisimama huku mikono yake ikiwa imejaa damu nyingi mikononi mwake. Woga ukaanza kumtawala, mwili mzima ukaanza kumtetemeka mithili ya mtoto anaye fokewa na mama wa kambo. Damu inayo endelea kusambaa hapo nchini, ikazidi kumuogopesha.
‘Ehee Mungu nimeua’
Tomas alizungumza huku asijue ni nini ana fanya. Akakurupuka na kutoka ndani humo. Moja kwa moja akaelekea chumbani kwake na kuchukua begi lake la nguo. Akalivaa na kurudi sebleni, mikono yake yenye damu, ikamfanya aanze kuangaza angaza kila sehemu. Akachukua kitambaa kilicho tandikia moja ya sofa, akaanza kujifuta mikono yake hiyo, ila kitambaa hicho hakikuweza kumaliza damu hizo. Akaingia kwa haraka bafuni na kunawa mikono yake kisha akatoka nje kabisa ya nyumba hiyo. Akatazama mtaa huo ambao tayari umesha anza pirika pirika za watu. Akaanza kutembea katika mtaa huo huku akitoa kofia yake kwenye begi lake la mgoni. Akaivaa kofia hiyo aliyo ishusha kidogo nusu ya uso wake na kuifanya sura yake isiweze kuonekana vizuri na watu.
Afande Mweta, kwa haraka akatoa taarifa kwa RPC Karata na kumueleza kuna simu ime pigwa na msamaria mwema akitoa taarifa juu ya kumuona Tomas. RPC Karata kwa haraka akagiza vijana wake kwenda katika mtaa ambao afande Mweta aliutaja. Wakafika nyumbani kwa Steve na kukuta mlango ukiwa umerudishiwa.
“Afande Mweta ndio hapa?”
RCO aliye ambatana nao aliuliza mara baada ya kushuka kwenye gari lao.
“Ndio hapa kabisa na huyu aliye piga simu ni rafiki yangu”
“Zungukeni nyumba na hakikisheni kwamba jambazi hatoki ndani humo. Askari kadhaa wakaizunguka nyumba ya Steve huku wengine wakiingia ndani. Wakakutana na kitambaa chenye damu kikiwa kime tupwa chini, kila askari aliye kiona kitambaa hicho, akaishika bunduki yake vizuri kuhakikisha kwamba ana kuwa makini kwa kila kitu kitakacho tokea ndani humo. Askari wawili wakaingia katika chumba cha Steve, wakastushwa sana mara baada ya kumuona Steve akiwa amelala chini na tayari amaesha fariki dunia.
“Mkuu kuna maiti huku chumbani”
Askari mmoja alitoa taarifa na kumfanya RCO na askari wengine kuingia ndani ya chumba hicho. Afande Mweta akajikuta akifumba macho mara baada ya kumshuhudia rafiki yake aliye toka kuzungumza naye muda mcheche ulio pita akiwa amefariki.
“Mkuu tumetafuta nyumba nzima na hatujaona mtu yoyote”
Mmmoja wa askari alimuambia RCO.
“Atakuwa hajafika mbali hakikisheni kwamba muna mtafuta kila kila sehemu na huyu mshenzi lazima ata patikana.”
RCO alizungumza kwa uchungu sana. Kwa kutumia simu yake ya upepeo akawasiliana na RPC pamoja na IGP na kuwaeleza juu ya mauaji aliyo yafanya Tomas jambo ambalo lilizidi kuwaongezea hasira askari hao na amri moja iliyo tolewa na IGP ni yasizidi masaa kumi na mbili tayari Tomas awe amsha patikana kwa maana jiji la Dar es Salaam ni dogo sana na muhalifu hawezi kutoweka kwa dakika chache hizo toka afanye mauaji.
***
Mlio wa simu inayo ita kwa wimbo wa taartibu ukamfanya Magreth kufumbua macho yake huku akiangaza angaza ni sehemu gani ambayo ame iweka simu yake. Akaichukua na kuitazama na kukuta ni nabii Sanga. Akajigeuza vizuri na kuiweka sikioni mwake.
“Halooo”
Magreth alizungumza kwa sauti ya usingizi iliyo jaa mahaba ndani yake.
“Mmmm…bado ume lala mpenzi wangu?”
“Ndio baby, vipi wewe?”
“Ahaa…Mimi nimesha amka muda mrefu sana. Hapa nina elekea kanisani, si unatambua leo ni siku ya maombezi”
“Yaa ni kweli”
“Vipi una kuja?”
“Mmmm bado sijashuka hata kitandani hivyo hata sijajua ratiba yangu itakuwaje leo?”
“Ahaa, fanya upate kifungua kinywa basi kisha uje kanisani”
“Mmmm kwa kweli leo sina hata upako wa kuja kwanisani. Isitoshe mke wako je akiniona ita kuwaje?”
“Hawezi kukuzuia wala kukufanya kitu chochote kwa maana hapo nilipo muacha nyumbani ni mgonjwa”
“Ana umwa na nini?”
“Vidonda vya tumbo vina msumbua tu”
Nabii Sanga aliongopea, ila ukweli ni kwamba kipigo alicho mpatia mke wake jana usiku ndio ugonjwa unao msumbua mwana mama huyo.
“Mpe pole yake. Kama utapata nafasi wewe njoo huku kwangu ukitoka kanisani”
“Sawa nitaangalia. Baadae mpenzi wangu kwa maana nimesha fika hapa kanisani”
“Haya nina kupenda”
“Ninakupenda pia Mage”
Nabii Sanga akakata simu. Magreth akajishauri kwa sekunde kadhaa kama ana weza kuendelea na usingizi wake au laa. Akaitazama saa katika simu yake na ina onyesha muda huo ni saa saba mchana.
“Eheee saa saba!!”
Magreth alihamaki huku akishuka kitandani mwake. Akaingia bafuni na kuoga haraka haraka na kurudi chumbani kwake.
‘Leo ina bidi nimpikie huyu mwanaume chakula kiruzi sana’
Magreth aliwaza huku akimfikiria Evans aliye muacha hospitalini. Akaandika vitu anavyo vihitaji kwenye kikaratasi, kisha akampigia simu Sheby na kumuagiza amnunulie vitu hivyo.
“Angalia nyama wasikuwekee nyenye mifupa fupa mingi”
“Sawa boss wangu”
“Usiniite boss bwana. Wewe niite sister Mage ina tosha”
“Poa poa sister”
“Nakuingizia pesa kwenye simu yako”
“Poa”
“Jina la usajili kwenye laini yako ni nani?”
“Shabani Shabani Madanga”
“Ehee haya”
“Mbona una guna”
“Nimelipenda hilo jinala Madanga”
“Yaaa ni bonge moja la chata”
“Hahaa haya bwana. Usichelewe kuvileta si unajua kwamba nina mgonjwa hospitalini hivyo nina paswa kuwahi kumpelekea chakula mchana huu.”
“Usijali sisteriiiiii”
Magreth mara baada ya kumaliza kuzungumza na Sheby akamtumia kiasi cha pesa kinacho tosha kununulia vitu hivyo pamoja na nauli yake. Akajifunga matenge mawili na kuelekea sebleni. Akawasta tv, habari ya kwanza kukutana nayo ni kuhusiana na kutafutwa kwa Tomas.
“Mmmmm kwani hakushikiliwa?”
Magreth alijiuliza huku akiongeza sauti ya luninga ili aweze kusikia vizuri habari hiyo ya mchana.
“Ohoo ametoroka!!”
Magreth alizidi kushangaa kwani mtu anaye zungumziwa hapo ana mfahamu na kujua maovu yake yote aliyo yafanya ikiwemo la mpango wa kuhitaji kumuua yeye mwenyewe.
***
“Mkuu kuna wageni wako”
Sekretari wa RPC karata alizungumza mara baada ya kuingia ofisini kwa mkuu wake huyo wa kazi.
“Wageni kutoka wapi?”
“Ikulu”
“Ikulu?”
RPC karata alizungumza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.
“Ndio”
“Waruhusu kuingia”
Askari huyo wa kike akapiga saluti kisha akatoka ndani humo. Baada ya dakika chache wakaingia wanaume wawili walio valia suti nyeusi pamoja na miwani nyeusi huku kwenye mifuko ya makoti yao ya suti wakiwa wamening’iniza vitambulisho vinavyo waonyesha wao ni walinzi wa raisi.
“Karibuni sana”
RPC Karata alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti chake.
“Tuna shukuru. Raisi yupo nje ana hitaji kuzungumza na wewe”
“Raisi yupo nje!!?”
RPC Karata alishangaa juu ya ujio wa gafla wa raisi.
“Ndio, ongozana nasi”
RPC Karata akajiweka sawa yunifomu zake hizo za uaskari kisha akaongozana na walinzi hao na kuwafanya askari wake kubaki wakiwa wameduwaa, wasijue ni wapi bosi wao anapo elekea. Wakatoka nje na kumfungulia mlango wa gari RPC Karata na kuingia ndani ya gari hilo aina ya Range rover lenye namba za usajili wa kawaida na si plate namba za ikulu. RPC karata akastuka sana kumkuta raisi Chinas Mtenzi akiwa katika gari hilo.
“Habari yako mkuu”
RPC Karata alisalimia huku akimpa mkono raisi. Raisi Mtenzi akamtazama RPC karata kwa sekunde kadhaa kisha akaupokea mkono huo.
“Ume choka kazi yako?”
Swali la raisi likaustua sana moyo wa RPC Karata.
“Aha…hapana mkuu”
“Sasa ni nini unacho kifanya?”
“Aha….mkuu bado ume niacha njia panda. Tafadhali naomba kidogo uni fafanulie nini una maanisha”
“Jukumu na lengo la mimi kukuweka kuwa RPC katika jiji hili la Dar es Salaam, nina maanishakwamba una weza kumuda heka heka zote za usalama wa jiji hili. Ila sivyo nilivyo tegemea, kweli dalali ana weze kutoroka kituo cha polisi na wala hamustuki na muna kazi yakutoa tu matangazo kwa atakaye fanikisha kukamatwa kwake basi atapewa milioni kumi. Ana kitu gani huyo mtu hadi jeshi la polisi litoe hizo milioni kumi?”
Raisi alizungumza kwa kufoka huku dereva na walinzi wake alio ambatana nao wakiwa wamesimama nje ya gari hilo huku milango ikiwa imefungwa.
“Aha…mkuu una jua….unajua kwamba…….”
“Ona unavyo babaika. Karata kumbuka mimi nilikupokea depo wewe, heshima na adamu yako nina ijua nikikuwa mkufunzi wako wa chuoa. Pia nafahamu hichi kituo kwa maana nilisha kuwa RPC hapa kabla ya kuingia kwenye siasa na sasa nimekuwa raisi. Au umelisahau hilo?”
“Sijalisahau mkuu”
“Sasa nini? Hawa askari wa chini hawawezi kufahamu underground way(njia za chini) katika kituo hichi, RPC pekee ndio anaye fahamu kwamba chini ya kituo hichi kuna njia za kupita. Je imekuwaje mahabusu akatoroka, ikiwa nje kuna ulinzi wa askari wasio pungua ishirini?”
RPC Karata akahisi haja ndogo kama ina kwenda kumtoka kwa woga.
“Ahaa mkuu ni kweli, ila sijajua kama siku hiyo mtuhumiwa alipo toroka ilikuwaje kuwaje kwa maana sikuwepo kazini”
“Ulikuwa wapi?”
“Nyumbani mkuu”
Raisi Mtenzi akamatazama RPC Karata usoni mwake kwa sekunde kadhaa na kutambua macho ya mfanyakazi wake huyo yana danganya na isitoshe ana mfahamu vizuri sana toka alipo kuwa chuoni CCP Moshi.
“Una nidanganya. Sasa kama ulimtoa kwa maslahi yako binafsi basi nahitaji umrudishe ndani ya masaa kumi na mbili awe ndani ya sero za jengo hilo. Lasivyo nitakufukuza kazi na utahukumiwa kijeshi jela na nina imani una tambua ni sheria gani ina muhukumu askari anaye saidiana na majambazi? Nilikuambia kweye utawala wangu sitaki jeshi la polisi lilege lega, ikiwa mimi nami nimepitia huko. Umenielewa?”
“Ndio muheshimiwa nime kuelewa”
“Na hizo milioni kumi munazo watangazia watu. Zitatoka mfukoni mwako na si katika jeshi la polisi, hatuwezi kupoteza pesa kizembe namna hiyo.”
“Sawa mkuu”
“Shuka kwenye gari langu”
RPC Karata akashuka kwenye gari raisi huku akiwa amechoka sana kwa woga na mkwara alio pigwa na raisi. Walinzi wa raisi pamoja na dereva wakingia kwenye gari hilo na kuondoka. Hakuna hata askari mwengine aliye weza kugundua kwamba raisi amefika katika ofisi zao. RPC Karata akalisindikiza kwa macho gari hilo jinsi linavyo toka getini hapo na kutokomea.
“Ehee Mungu wangu nafanya nini sasa?”
RPC karata alizungumza huku akianza kutembea kwa mwendo wa haraka kuelekea ofisini kwake. Akafungua droo yake na kutoa simu ndogo yenye namba inayo julikana na familia yake pamoja na nabii SANGA. Akampigia na simu ya nabii Sanga ikaanza kuita.
***
Nabii Sanga mara baada ya kumaliza kuzungumza na Magreth akashuka kwenye gari lake na moja kwa moja akaelekea ofisini kwake. Akajifungia kwa ndani na kuanza kusali huku akijiandaa kwa ajaili ya maombezi ya siku hiyo. Alipo maliza kusali, akaandaa mahubiri ya siku hiyo huku akilini mwake akiwazia penzi la Magreth ambalo lina zidi kumchanganya siku hadi siku. Simu yake ikaanza kuita, akaitazama kwa sekunde na kukuta ni namba ya RPC Karata. Akaiweka sikioni mwake na kuanza kuisikiliza.
“Habari yako kijana”
“Pumbavu wewe, habari yangu ya nini. Yaani nina juta sijui ni kwa nini nilifwata mawazo yako ya kipumbavu”
Sauti ya ukali ya RPC Karata ikamstua sana nabii Sanga na kujikuta akiitazama simu yake ili kuhakikisha kwamba huyo anaye mpigia ni RPC Karata au mtu mwengine kwa maana wana heshimiana sana na hajawahi hata siku moja kusikia neno la kejeli wala tusi kutoka kinywani mwa kijana huyo.
ITAENDELEA
Haya sasa, swala la Tomas raisi ameliingilia kati, masaa kumi na mbili aliyo tatoa kwa RPC Karata yatatosha kweli kwa wao kumtia nguvuni Tomas? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 22.

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +