Pages

Thursday, May 23, 2019

SIMULIZI YA *SIN* SEHEMU YA 26........ ONLY 18+

ILIPOISHIA
“Ume sema haikuwa nia yako kufanya ulicho kifanya? Ni nani aliyopo nyuma ya hili jambo?”
Swali la raisi Chinas Mtenzi likazidi kumfanya RPC Karata kuwa katika kipindi kigumu.
“Zungumza ili huyo aliye kushawishi wewe kufanya ulicho kifanya, abebe adhabu ambayo nilipanga kukupatia. Nitajie ni nani huyo”
RPC Karata akashusha pumzi huku akimfikiria nabii Sanga. Japo ni mzee anye muheshimu kwenye swala zima la kiimani, ila hana jinsi zaidi ya yeye kutetea kibarua chake.
“Ni nabii SANGA”
Raisi Chinas Mtenzi akatokawa na macho ya mshangao kwani naye siku zote amekuwa ni shabiki namba moja wa nabii huyo anaye ponya watu mbali mbali kwa maombi yake.

ENDELEA
“Sanga huyu wa kanisha la Heaven light ministry au Sanga yupi?”
Raisi Chinas Mtenzi aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.
“Ndio muheshimiwa”
“Yeye amehusika vipi katika swala la kumtoa muhalifu mikononi mwa polisi?”
“Kijana ambaye tulikuwa tume mshikilia, alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa nabii Sanga”
“Ohoo Mungu wangu!! Ehee ikawaje?”
“Sasa mke wake kutokana na kukolea kwenye penzi la kijana huyo wakapanga mpango wa kumteka nabii Sanga.”
Raisi Chinas Mtenzi akajikuta akifumba macho kwani haya anayo yasikia na familia hiyo anayo ifahamu ni mambo mawili tofauti kabisa.
“Walifanikiwa katika kumteka nabii Sanga ndio maana nabii Sanga alitekwa. Baada ya upelelezi tukafanikiwa kumfahamu muhisika ambaye ni Tomas, ila Tomas baada ya mimi kumbana kwa kuda mrefu alikiri kwamba mke wa nabii Sanga ndio aliye toa wazo la kutekwa kwa mume wake. Ili kulinda heshima ya familia hiyo ilibidi kumueleza nabii Sanga kila jambo kuhusiana na mke wake ili niwee kufahamu ni maamuzi gani ambayo ata amua, kama ni kumjumlisha mke wake katika hilo jambo au laa.”
RPC Karata alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi kwani hatima yake bado haifahamu kwa mzee huyo.
“Nabii Sanga aliomba mke wake asihusishwe kwenye hilo na baada ya hapo aliomba kukutana na Tomas na kweli nilifanikisha hilo. Baada ya hapo akaniomba niweze kumuaa.”
“Ni kweli niliweza kumtorosha Tomas kutoka pale kituoni kwa kutumia njia za chini ya ardhi. Nilipo kuwa nipo njiani kwenda kumuua, nabii Sanga akanipigia simu na kuniomba niweze kusitisha na ikiwezekana niweze kumuachia huru kijana huyo ila nimsisitize aweze kutoka nje ya nchi hii kabla ya kumuua”
“Ohoo Mungu wangu. Kwahiyo sasa hivi wewe una pokea oda kutoka kwa nabii Sanga na wala si kwa IGP au kwanagu?”
“Hapana mkuu, nimefanya makosa, ila tafadhali nina kuomba sana uweze kunisamehe katika hili”
Raisi Mtenzi akafumba macho yake kwa sekunde kadhaa huku akijaribu kuizuia hasira yake anayo hisi ita kipasua kifua chake kwa maumivu. Siku zote hapendi kuwa na wafanyakazi wazembe.
“Alikulipa kiasi gani?”
“Milioni ishirini mkuu”
“Unazo hizo pesa?”
“Ndio mkuu”
Raisi Mtenzi akatoa simu yake kwenye mfuko wa koti la suti na kumpigia mlinzi mkuu wa ikulu.
“Ndio muheshimiwa raisi”
“Nileteeni nabii Sanga, popote alipo hakikisheni kwamba muna mleta hapa”
“Sawa muheshimiwa”
“Muna lisaa moja la kukamilisha hilo”
Raisi Mtenzi akakata simu na kumtazama RPC Karata anaye mwagikwa na jasho japo katika chumba hicho kuna air condition.
“Nahitaji kumjua vizuri huyu nabii Sanga. Sijawahi kukutana naye uso kwa uso zaidi ya kumuona kwenye tv”
“Aha…ni mtu mwema?”
“Mtu mwema anaye toa rushwa na ili kulinda heshima ya familia yake na mke wake ambaye amefanya makosa ya kijinga. Unalitia hasara jeshi la polisi na bado una sema kwamba ni mtu mwema.”
Raisi Mtenzi alifoka sana huku akimkazia macho RPC Karata.
“Vijana wangu wataanza kumfwatilia nyendo zake. Endapo nita mkuta na kosa la tofauti na hili alilo fanya. Sinto muacha na hapa ndipo nitakapo kuwa nina shuhulika na watu wote walio fungua fungua makanisa yao wakijiita manabii wengine sijui kina nani sitaki ujinga mimi”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa ukali sana. Haikuwa kazi ngumu kumtafuta nabii Sanga kwa kutumia GPRS, wakafanikiwa kugundua kwamba yupo kigamboni. Vikaondoka vikosi vya walinzi kumi wa raisi huku wakiwa katika gari mbili na kuanaza kuelekea eneo la Kigamboni.
***
“Mume wangu nakuomba unisamehe, moyo wangu ulijawa na uchungu sana nilipo kuwa nina sikia jinsi mukiana mapenzi wewe na mke wako”
Magreth alizungumza kwa sauti laini huku akimshika shika nabii Sanga shingoni mwake.
“Hata kama nimefanya makosa ila si kuniambia maneno makali kiasi hicho”
“Nisamehe mpenzi wangu, ni kweli yule ni mke wako na mimi ni mwanamke wa nje na yule ana haki ya kila jambo”
“Hata wewe una haki ndio maana upo hapa. Nitaondoka kwenda huko Nigeria, nakuandikia cheki ya milioni hamsini, hakikisha una fungua biashara unayo ihitaji na nikirudi ndani ya mwenzi huo mmoja nahitaji kuikuta biashara ikiwa ime kuwa”
“Sawa mume wangu”
Nabii Sanga akatoa kitabu cha cheki katika mfuko wa koti lake la suti na kuandika kiasi hicho cha pesa na kumkabishi Magreth ikiwa ni moja ya msamaha wake kwa mwanamke huyo anaye mdatisha kimahaba.
“Una taka kuniambia kwamba sikuridhishi mpenzi wangu?”
“Hapana mume wangu, una nirishisha sana na unanikojolesha hadi kiu yangu ina katika”
“Hahaa nakupenda sana Magreth”
Nabii Sanga alizungumza huku akimbusu Magreth mdomoni mwake. Kengele ya getini ikawafanya waachiane.
“Nahisi watu wa kampuni ya kufunga kamera watakuwa wamesha fika. Vaa nguo ukawapokee”
Nabii Sanga alizungumza hukua akimtazama Magreth kwa macho yaliyo jaa mahaba. Magreth akashuka kitandani, akachukua matenge yake mawili na kujifunga.
“Mage”
“Eheee”
“Hivi una jua kwamba wewe ni mzuri sana”
“Kweli?”
“Haki ya Mungu vile, hembu njoo”
Magreth akamfwata nabii Sanga kitandani alipo kaa. Nabii akayatomasa makalio ya Magreth na kuyapiga vibao kidogo.
“Haya nenda kawafungulie mimi ngoja nijimwagie maji”
“Sawa mume wangu”
Magreth akatoka chumbani humo na moja kwa moja akaelekea getini kwake. Akafungua geti dogo, akastuka kidogo mara baada ya kuwaona wanaume wanne walio valia suti nyeusi wakiwa wamesimama nje ya geti hilo huku kukiwa na gari mbili nyeusi.
“Aha….karibuni”
“Tumemkuta nabii Sanga?”
“Ndio nyinyi ndio kampuni aliyo wapigia muje kufunga kamera?”
Magreth aliuliza kwa mashaka kwa maana wanaume hao wamevalia nguo ambazo si za ufundi kabisa.
“Tunahitaji kumuona”
“Karibuni”
Wanaume hao wanne wakaingia ndani huku wengine sita wakishuka kwenye magari hayo na kuimarisha ulinzi nje.
“Ngoja niwaitie”
Magreth alizungumza huku akielekea chumbani kwake na walinzi hao wa raisi wakatawanyika sebleni hapo ili kuhakikisha kwamab wana mpata nabii Sanga haraka iwezekanavyo.
“Baby baby”
Magreth alizungumza huku akiingia bafuni.
“Kuna nini?”
“Wamekuja wanaume wamevalia suti nyeusi. Hao ndio mafundi?”
“Wamevalia suti nyeusi?”
“Ndio”
“Mmmm mbona wale kampuni yao mavazi yao yana rangi za blue”
“Hembu maliza ukawaone na watu wenyewe wanaonekana wapo serious kwa maana hata salamu hawajanipa”
“Mmmm”
“Ndio hivyo mume wangu”
Nabii Sanga akaoga haraka haraka kisha akatoka bafuni hapo. Akavaa nguo zake na kutoka sebleni, akamkuta mwanaume mmoja tu aliye valia suti.
“Ninaitwa agent John kutoka secrety service. Tumekuja kukuchukua uelekee ikulu”
“Ikulu!!?”
“Ndio, tuna weza kuondoka pamoja”
“Kuna nini Ikulu?”
“Mzee hii ni oda ya raisi. Tume kuja kukusindikiza kukupeleka ikulu tu”
Nabii Sanga akamtazama Magreth aliye jawa na wasiwasi.
“Sikia watakapo kuja watu wa kufunga kamera hakikisha una wasimamia na hawafanyi tofauti na nilivyo waelekeza”
“Ume waelekezaje?”
“Wafunge kamera thelathini, wao wenyewe watajua ni wapi watafunga na malipo yote nitayafanya kwa njia ya simu”
“Sawa”
Nabii Sanga mara baada ya kumuachia Magreth maelekezo akatoka na wanaume hao wanne ambao watatu walikuw awamejificha sebleni hapo na kumuacha mwenzao mmoja. Nabii Sanga akashangaa wingi wa walinzi hawa wa raisi nyumbani kwa Magreth, akatamani kuwauliza wamejuaje kama yupo hapo, ila akakosa nafasi hiyo kwani watu wote wana onekana wapo serious na kazi yao iliyo waleta hapo.
***
Levina akakamilisha kumkatia Tomas tiketi katika shirika la ndege la South Africa Air ways. Ndege atakayo itumia Tomas, itaondoka nchini Tanzania saa mbili na nusu usiku. Levina akarudi nyumbani na kumkuta Tomas, akiwa sebeleni akitazama tv.
“Baby huwezi amini jamaa bado wana endelea kunitafuta”
“Na watakutafuta sana, hawato kupata ng’oo. Sasa nime fanikiwa kupata ndege ya saa mbili usiku. Muda wa kuripoti ni saa mbili kasoro”
“Sawa mke mpenzi wangu asante”
“Tomas nina hitaji kuzungumza na wewe kabla hujaondoka”
“Sawa mpenzi wangu, tuzungumze”
Levina akaka kwenye sofa linalo tazamana na sofa alilo kalia Tomas.
“Tomas una nipenda au una mihemko ya kutokana nilikusaidia?”
“Nina kupenda mpenzi wangu”
“Una niahidi nini kwenye maisha yako ya kwenda huko”
“Kipivipi?”
“Utakuwa na mwanamke mwengine au?”
“Siwezi kuwa na mwanmke mwengine”
“Tomas, sitaki niumie kama ulivyo niumiza pale awali, kumbuka maisha yako na usalama wako sasa hivi yapo mikononi mwangu. Ukienenda kinyume na mimi hata kama una ishi Afrika kusini, lazima askari watakukamata”
“Levina nisikilize mpenzi wangu”
Tomas alizungumza huku akimfwata Levina sehemu alipo kaa.
“Levina una tambua kwamba nina kupenda na sinto kwenda kinyume na penzi lako”
“Tomas, nyinyi wanaume ni waongo. Wewe nieleze tu ukweli kama uta nisaliti niweze kujiandaa kisaikolojia kuliko kuweka ahadi ambayo una jua uta ivunja”
“Sinto kusaliti mpenzi wangu. Haki ya Mungu wewe niamini”
“Sawa ni hayo tu ndio nilikuwa nina kuuliza kwa maana nchi hiyo ina maradhi mengi sana hasa ukimwi. Sasa usije ukaniletea magonjwa bure”
“Siwezi kufanya hivyo mpenzi wangu mimi nina kupenda sana”
Levina taratibu akaanza kuchokozi wa kimapenzi ambao taratibu ukamfanya Tomas kujibu uchokozi huo kimahaba na toka wakutane jana tayari wamesha kwenda mizunguko zaidi ya kumi katika nyakati tofauti tofauti.
***
Nabii Sanga akashuhudia geti kubwa la ikulu likifunguliwa. Gari hizo walizo panda zikaingia Ikulu na kusimamisha kwenye maegesho. Wakashuka kwenye gari hizo na nabii Sanga moja kwa moja akapelekwa hadi katika chumba cha kupumzikia.
“Muheshimiwa nabii Sanga yupo hapa”
Mlinzi aliye ingia katika chumba cha mahojiano alimuambia raisi Chinas Mtenzi mara baada ya kupokea ujumbe huo kutoka kwa kiongozi wa walinzi aliye kuwa amekabidhi kazi hiyo na raisi Chinas Mtenzi.
“Yupo wapi?”
“Wamemuweka katika chumba cha mapumziko”
“Chumba cha mapumziko!! Amekuwa nani yeye, hembu mleteni huko ajumuike na huyu mjinga mwenzake”
Mlinzi huyo akatoa agizo hilo kwa walinzi wengine na baada ya muda mfupi nabii Sanga akaletwa eneo hilo na kuingizwa katika chumba hicho. Nabii Sanga akastuka mara baada ya kumkuta RPC Karata akiwa amekaa kinyonge huku mikononi mwake akiwa amefungwa pingu na yunifomu zake zime jaa jasho.
“Karibu”
Raisi Chinas Mtenzi alizungumza huku akisimama. Raisi Mtenzi akavua koti la suti yake na kumkabidhi mlinzi wake aliye muingiza nabii Sanga.
“Mzee kaa hapo una nitumbulia nini macho”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akikunja mikono ya shati lake. Nabii Sanga kwa woga akaka kwenye kiti ambacho hakikuwa na mtu. Raisi Mtenzi akaviweka sawa viungo vyake huku akimkazia macho nabii Sanga.
“Nabii wewe ume tumwa na Mungu kweli kuja kueneza neno lake hapa duniani?”
Swali la raisi Mtenzi likamstua sana nabii Sanga, akahisi haja ndogo ina kwenda kumtoka.
“Ndi….io muheshimiwa raisi”
“Una uhakika?”
“Ndio muheshimiwa”
“Kama kweli Mungu ana kutumia wewe, imekuwaje ukamashawishi kijana wangu mtiifu kumuachia mtuhumiwa aliye shirikiana na mke wako katika kukuteka kwako na pia mtuhumiwa huyo amekuibia mke wako. Eheeee?”
Nabii Sanga akashindwa kabisa kuuzuia mkono wake, ambao taratibu umeeanza kulowanisha boksa yake huku ukilowanisha suruali yake na ukaanza kuchuruzika kwenye miguu yake na kumwagika chini na kuanza kusambaa taratibu kwenye sakafu ya chumba hicho.
kwa maombi yake.
ITAENDELEA
Haya sasa swali moja moja tu la muheshimiwa raisi Chinsi Mtenzi lime mwaga mkono nabii Sanga je ataweza kujibu maswali yanayo fwata.? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 27.

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +