Pages

Thursday, May 23, 2019

Vichekesho nane vya nguvu. Enjoy...

Mwizi wa atm

Jamaa aliibiwa kadi yake ya benk akaulizwa kama ameripoti polisi akajibu "sijaripoti bado, mwizi mwenyewe hamfikii matumizi kama mke wangu.

Cheka kidogo 

Njia rahisi kusahau matatizo yako (japo kwa muda mfupi) vaa viatu vinavyokubana.

Mlizi mbio mbio 

Tulikuwa bar moja jana mlinzi kaingia spidi, akamwambia jamaa mmoja aliyekaa kaunta, Mlinzi: Mzee gari lako limeibiwa Mzee: Umemtambua aliyeiba? Mlinzi: Hapana lakini nimeandika namba za gari hizi hapa.

13, 13... 

Jamaa alikuwa anapita nje ya wodi ya vichaa akasikia mtu anasema, 13, 13, 13, 13, 13, 13,..... akaamua kuchungulia kwenye kitundu alichokiona ajue kuna nini, ile kuchungulia tu akamwagiwa mchanga wa machoni, sauti ikabadili ikaanza 14,14,14,14,14......

WATAALAM

Jamaa alikuwa anaumwa sana, mkewe akamwita daktari, alipofika akamkuta jamaa kafumba macho; 
Dokta: Huyu mbona amekwisha kufa? 
Jamaa: Sijafa bwana 
Mke: Hebu nyamaza bwana acha kubishana na wataalamu.

Ya leo mgonjwa 

Dokta alipotembelea wodi ya mgonjwa wake aliyepata ajali. Mgonjwa akiwa amening'inizwa mikono juu akauliza "dokta ntaweza kweli kupiga kinanda nkitoka hospitali?" 
Dokta: Bila shaka utaweza, wewe ni mpiga kinanda mzuri enh? 
Mgonjwa: Hapana sijawahi kabisa bado.

4WD 

Mwanaume alimnunulia pete ya almasi mkewe, rafiki akauliza "si ulisema anapenda gari yenye four wheel drive, mbona umenunua pete?" Mume akajibu "unadhani wapi ntapata rav4 feki?"

Ajali ilivyotokea 

Trafiki polisi akihoji palipotokea ajali "ahaa! Sasa naanza elewa embu nielezee jinsi ajali ilivyotokea wewe ukiwa kama dereva mhusika." Dereva akajibu "hata sikumbuki nlifumba macho"

Faini ya kukojoa 

Polisi alimdaka jamaa anakojoa pembezoni mwa ukuta. 
Polisi: Wewe unajua panakatazwa kukojoa hapa? 
Jamaa: Sasa nimebanwa nifanyaje? 
Polisi: Faini yake elfu tano. 
Jamaa akatoa noti ya elfu 10. 
Polisi: Sasa chenji tunaipataje? 
Jamaa: Tafuta chenji unipe changu. 
Polisi: Basi kojoa tena...

Mume anaenda kazini 

Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang'ang'ania kuwa anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong'oneza mkewe aliyekuwa usingizini; "Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana" Mke: Si ndio nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kazini...

Hasira za mtoto 

Baba na mtoto: 
Baba: Mwanangu ukiwa na hasira unafanya nini? 
Mtoto: Naenda chooni. 
Baba: Chooni? Kufanya nini? 
Mtoto: Kusafisha. 
Baba: Halafu ndio hasira zinaisha? 
Mtoto: Ndio. Nasafisha choo kwa mswaki wako.

Mgonjwa na Dokta 

Mgonjwa: Dokta nimekuja nahisi ninaumwa Malaria na kifua. 
Dokta: Sasa ushajua unaumwa nini hapa umefuata nini kwangu? 
Mgonjwa: Sasa si nimekuja kwa dokta. 
Dokta: Wanaojua kuwa wanaumwa kama wewe wanapitiliza maabara.

Pilau la bachela 

Bachela mmoja aliyekua akiishi kwa muda mrefu peke yake kwenye nyumba aliyopanga siku moja alitaka kupika pilau kwa mara ya kwanza. Sasa asijue nini kinachobadilisha rangi ya wali kuwa rangi ya brown, yeye akapika kama kawaida (wali) kisha wakati wa kula akavaa miwani yenye rangi ambayo ukiuangalia wali unauona kama pilau wakati anakula.

Mwizi na chizi 

Mwizi kaiba TV na kuanza kukimbia nayo, kumbe ile nyumba mlikuwa na chizi, akaanza kumkimbiza yule mwizi. Kila mwizi akiongeza mbio chizi nae huyo, mwishowe mwizi akasalimu amri na kusimama, yule chizi akamsogelea na kumwambia.. Daah umesahau remote hii hapa mwizi kafleti.

Chemsha bongo 


Baba akimuuliza chemsha bongo mwanae anayesoma shule ya chekechea "haya niambie kitu gani hakiwezi kuliwa wakati wa breakfast?" Mtoto akajibu "hiyo mbona rahisi baba, si lunch na dinner"

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +