Pages

Thursday, April 25, 2019

Sababu na tiba ya Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa

Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamme linaweza kusababishwa na vitu vingi sana. Sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au kisaikolojia au za mchanganyiko wa vitu hivyo viwili. Hebu tuone baadhi ya vyanzo vya tatizo hili.

Matatizo ya mahusiano kati ya mwanamme na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya mapenzi. Jee, unapata raha na una amani katika mahusiano yako na mpenzi wako? Huna wasiwasiwo wote na mahusiano yenu? Haya ni maswali ya msingi ya kujiuliza.

Kama mahusiano yako na mpenzi wako yamekuwa ya miaka mingi sana, unaweza kuwa umemzoea mno mkeo kiasi kwamba ukaanza kukosa hamu ya kufanya naye tendo la ndoa. Hili nalo hutokea mara nyingi.

Kama kuna mambo yanasababisha tendo la ndoa lisifanyike kwa urahisi, ufanisi na kufurahia, hamu ya kufanya tendo hilo inaweza kupungua. Kwa mfano, kama mwanamme unawahi kufika kileleni au una matatizo ya jongoo wako kupanda mtungi, tendo zima la ndoa halitakuwa la kukufurahisha sana hivyo unaweza kupoteza hamu ya kulifanya. Hebu fikiria tunda linalokufurahisha sana ukilila, ukilikosa kwa siku kadhaa, utalikumbuka na kulitafuta lakini ambalo halikufurahishi sana ukilila hutalikumbuka na kulitafuta.

Mawazo Mengi Na Uchovu
Matatizo ya kikazi na hadhi yako kazini vyaweza kuchangia. Kama unabezwa sana kazini na kujiona hutimizi kazi yako ipasavyo au kama unachoka sana kazini unaweza pia kukosa hamu ya kufanya mapenzi urudipo nyumbani. Kukosa mpango mzuri wa shughuli zako za kila siku na kujaribu kulazimisha kufanya mapenzi katikati ya ratiba yako iliyojaa. Mahusiano ya kimapenzi yanataka yatengewe muda wake na unaotosha.

Msongo Wa Mawazo
Msongo wa mawazo (depression) unatofautiana na kukosa raha au kujisikia si mtu wa thamani kwa kipindi kifupi. Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa hali ya kuwa na mawazo makali ya muda mrefu ya kukukosesha raha kutokana na kujisikia si mtu wa thamani au kukosa starehe katika vitu ulivyozoea kuvifanya na kukufurahisha hapo zamani. Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako pamoja na matamanio yako ya kimapenzi.

Matumizi Ya Madawa Na Pombe
Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia huweza kuleta tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja na:

– madawa ya high blood pressure

– madawa ya kuondoa msongo wa mawazo

– madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone, kwa mfano, cimetidine, finasteride na cyproterone

– na mengineyo

Umri Kuwa Mkubwa
Homoni ya msingi sana kuhusiana na masuala ya mapenzi huitwa testosterone. Kwa mwanammme homoni hii hutolewa kwa kiwango kikubwa na korodani na kwa mwanamke hutolewa na ovari. Homoni ikipungua katika mwili wa binadamu, humfanya apoteze hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kiwango cha testosterone katika mwili wa mwanamme hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanamme anvyozidi kuwa na umri mkubwa. Kiwango cha testosterone kikishuka sana katika mwili wa mwanamme huyu humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.

Matatizo Katika Mfumo Wa Homoni
Tumeshaona kwamba upungufu wa homoni inayoitwa testosterone unasababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo mengine katika mfumo wa homoni huchangia tatizo hili. Kama thyroid haitoi homoni za kutosha, tatizo hili huweza kutokea ingawa mchango wa thyroid katika tatizo hili ni mdogo sana. Thyroid ni kiungo cha kuzalisha homoni kilichopo katika eneo la shingo.

Tatizo hili linaweza kutokea pale homoni zinapozalisha kitu kinachitwa prolactin kwa kiwango kikubwa mno na kukisambaza ndani ya mfumo wa damu. Hali hii kiutaalamu huitwa hyperprolactinaemia.

Matatizo Ya Kiafya
Matatizo ya kiafya ya muda mrefu husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo ya moyo ya muda mrefu, kuwa na kisukari kwa muda mrefu, kansa ya muda mrefu na hali ya kuwa na unene wa kuzidi kiwango ni baadhi tu ya matatizo yanayochangia tatizo hili.

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Tiba Za Tatizo La Kukosa Hamu Ya Kufanya Mapenzi Kwa Mwanamme

Sasa tutazame mambo ambayo unaweza kuyafanya kuongeza na kudumisha hamu ya kufanya tendo la ndoa. Tatizo hili halijapatiwa dawa za kwenye mahospitali isipokuwa pale unapogundulika kuwa una kiwango kidogo cha testosterone ambapo utaandikiwa namna ya kukiongeza kiwango chako. Fanya yafuatayo kuongeza hamu yako ya kufanya mapenzi.

1. Tafuta mchezo ambao unaweza kushiriki au fanya mazoezi kama vile ya kutembea au kukimbia. Kila siku ufanyapo mazoezi yako jaribu kila siku kufikia kiwango cha juu zaidi ya kile ulokwisha kifikia.

2. Inasaidia kufahamu kuwa ni asilimia 40 hadi 50 ya matendo ya ndoa mnayoyafanya yatawaridhisha wote wawili. Kukosa kumridhisha mwenzio iwe changamoto ya kukufanya ufanye utafiti na utundu wa kuboresha tendo mtakapokutana tena.

3. Kama nilivyodokeza hapo juu, jaribuni kwa pamoja kujadili jinsi ya kuboresha namana yenu ya kushiriki katika tendo la ndoa kila mmoja akieleza kile ambacho angependa afanyiwe. Inasaidia kusoma maandishi kutoka sehemu mbalimbali na kutazama mikanda mbalimbali.

4. Kufanya tendo kwa kushitukiza inapendeza wakati fulani. Lakini hili kidogo linaweza kuwa si zuri ukizingatia majukumu ya kila siku ya maisha ya sasa, si rahisi kupata muda wa kutosha wa kustarehe na mpenzi wako. Kuwa na mpango na ratiba ni bora zaidi na inasaidia kuleta hamu mtu anapokisubiri kitu kilichopangwa siku fulani na muda fulani – fikiria unaposubiri mechi kubwa ya timu yako. Mletee zawadi mpenzi wako, weka muziki mororo ulikuwa unaupenda siku zile, zimisha simu na hakikisha kuna mazingira ya utulivu na ukimya.

5. Hamu huongezeka inapoona kitu kipya. Ukienda na mwenzi wako kwenye sherehe nje ya nyumba yenu, utapata fursa ya kumwona mkeo kwa namna nyingine. Utaweza kuuona uzuri wake na yeye pia atakuona wewe kwa namna nyingine. Wote mtakumbuka vitu ambavyo kila mmoja wenu vilimvutia kwa mwenziwe.

6. Kama umejaribu haya yote na hukupata matokeo mazuri, jaribu kutumia chakula kinachosidia kuongeza hamu kama nilivyoelezea kwenye ukurasa wa “Mwanamke kukosa hamu ya kufanya mapenzi” na/au kutengeneza na kutumia viagra asilia kama nilivyoielezea hapa chini. Viagra asilia nadiriki kusema, imewasaidia wasomaji wangu wengi sana.

7. Kuna kampuni zinasambaza virutubisho mbalimbali vya mwili. Virutubisho hivi ukivitumia vinafanya kazi mara moja na kuponya kabisa tatizo hili. Kama umeshindwa kupata kampuni bora ya kukupatia virutubisho hivi, wasiliana nami muda wo wote kwa njia nilizoorodhesha hapa chini nipate kukusaidia.

Chakula Na Kukosa Hamu ya Mapenzi
tikitimaji huongeza nyege
Chakula tunachukula kina uhusiano mkubwa na hali zetu za kupenda au kutopenda kufanya mapenzi. Kiujumla chakula chenye virutubisho vya kuusaidia moyo na mishipa ya damu kufanya kazi zao vizuri vitakuweka kwenye hali ya kuwa na matamanio ya kufanya tendo la ndoa. Ukweli huu unahusisha pia chakula chenye madini ya zinc ambacho huongeza na kuboresha mbegu za mwanamme. Kuweza kujua chakula bora kwa kusaidia hamu ya mapenzi, soma ukurasa wa “Mwanamke Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa“.

Jinsi Ya Kutengenza Viagra Ya Asili
Pamoja na kuyafanya hayo, jaribu kuutengeneza na kuutumia mchanganyiko wa matunda kama inavyoonyeshwa kwenye video hii hapa chini. Mchanganyiko huu wa matunda umeonyesha kuwa na nguvu ya kuamsha ari ya kufanya tendo la ndoa. Tuuite mchanganyiko huu “Viagra Asilia” kwani unatengenezwa na vitu vya asili tu. Nitaonyesha video mbili ili uweze kuchagua ile utakayoona ni rahisi kwako kuifuata. Video ya kwanza inaonyesha jinsi ya kutengeneza viagra ya asili kwa kutumia mchanganyiko wa matunda ya aina nyingi. Tazama video hii hapa:

Kutengeneza Viagra asilia
Kama una tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na umejaribu njia hizo hapo juu bila kupata mafanikio ya kukuridhisha, unaweza kutuandikia ili upate maelezo zaidi na ushauri zaidi kwa kutumia njia yoyote kati ya hizi tulizoziorodhesha hapa chini. Tutafurahi sana kuwa nawe. Kama msomaji wetu ni mwanamke, pata elimu nzuri zaidi kwenye ukurasa mahsusi wa “Mwanamke Kukosa Hamu Ya Kufanya Mapenzi.”

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +