Mama yetu aliposikia kuwa tumefauru mimi na kaka yangu John alifurahi sana japokuwa alikuwa akifikilia jinsi ya kupata pesa ambayo itatuwezesha sie kutupeleka shule mimi na mdogo wangu John, kwan baadaya msiba kutokea wanandugu upande wa mwanaume(baba) walitokea kututenga pindi msiba ulipokwisha,wanandugu walihitaji mali za baba japokuwa mama alipambana sana kuzibakisha zisichukuliwe ndio chanzo cha kutengwa na ndugu upande wa baba. Mama alifikilia sana huku akikosa majibu na ndipo alifikilia juu ya kuuza shamba moja angalau apate pesa chache ili walau mmoja wetu aende shule. Mama aliuza shamba hilo na alipata pesa kiasi ambacho hakikukidhi wote kwenda shule na ilitosha kwa kumlipia mtu mmoja tu kwenda shule. Basi mama ilimbidi amlipie ndugu yangu John ada ya shule kwa kile kiasi cha fedha kilichopatikana kipindi kile,basi kaka yangu John ilibidi aanze shule na mimi nilibaki nyumbani tukiangaikia pesa ili nami nianze masomo japokuwa nilikuwa nimeshachelewa. Pesa yangu ya ada ilikuwa ngumu sana kupatikana kwani mama alihangaika huku na huko lakin hakufanikiwa siku hiyo,mama alirudi nyumban akiwa mnyonge sana na aliponikaribia aliniangalia kwa jicho la huruma sana na kuingia ndani azikupita dakika alitoka na kigoda ndani na aliketi pembeni yangu na kuanza kulia.
Mama “Jamani mimi nina mkosi gani?”
Mama aliongea huku akinitazama na mimi machozi yalinilenga na nikamuuliza
Lisa “Kwanini mama wasema hivyo? Nini kimekupata huko?”
Mama “Lisa mwanangu nimehangaika sana kwaajili ya kupata pesa itakayokupeleka shule lakini sijafanikiwa,kwani kila ninapopita sipati msaada na wengine wanadiliki hata kunitusi kisa mimi ni mjane na wengine wananisema vibaya wapendavyo lakini sitochoka kwani haya yote ni kwaajili ya mimi na familia yangu na nitapambana hadi nitahakikisha wanangu mnapata elimu na ninauhakika mtanisaidia hapo baadae”
Mama alikwisha kuyasema hayo na mimi machozi yalikuwa yameshafika chini kwani alichokuwa akisema kilikuwa kinanihusu mimi na familia yetu kwa ujumla. Zilipita siku kadhaa huku mimi nikimsaidia mama kazi za nyumbani na kuangalia ili apate fedha ya kuniwezesha mimi kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza……………………..! Wakati huo kaka yangu John alikuwa akiendelea na masomo vizuri kwani ilipatikana fedha yake iliyomtoshereleza yeye mwenye. Nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumapili mida ya saa 6 mchana, alikuja mgeni na………………………!
FATILIA SEHEMU YA 3
Thursday, May 16, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments